Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

ahsante sana Mzizimkavu hadithi inazidi kufurahisha tunaisubiri kwa hamu Alhamis.
 
Vitu kama hizi za kurndelea mara part II mara Part III sizipendiiii si kwa vibaya lakini MziziMkavu maliza story mara moja bana.Kama nakukwaza Im deeply sorry

We D. Amsi za kwako, sijakusikia ukikoment kumbe upo, haya ngoja mzizi mkavu hauchimbwi dawa aendelee.
hadithi inatia huzuni sn.
 
mzizi hivi upo seriaz au??tuandikie bwana watu tule raha....maana hii inanoga kwelix2....
 
Unanichosha MziziMkavu maana nachukia kusubiri hapa nasubr na kule queen of gorilla nasubr kwa nn usifanye hv wakati kule tunasubr huku unaendelea na wakati huku tunasubr kule unaendelea plz,
 
Last edited by a moderator:
MAMA YANGU ADUI YANGU - 19-

ILIPOISHIA;
“MWAIJA za kazi?”
“Nzuri shemeji, shikamoo.”
“Marahaba, sasa wewe wasiwasi wako nini?” aliniuliza swali bila kunitazama.
“Wasiwasi! Wa nini?”
“Naona umeshaanza kuniogopa, nimekueleza lile ni ombi wala haliingiliani na mambo mengine.”
“Nikuogope kivipi?” sikumuelewa.
“Najua huniamini na kuona natumia turufu ya kukusaidia ili niweze kufanikisha mambo yangu. Lakini sivyo hivyo sina nia mbaya na wewe. Ningeweza kumpa mtu yeyote fedha niliyonayo lakini naamini kwako haitapotea.”
“Uliyosema nimekuelewa lakini sikuwa na maana hiyo. Nilikuwa na mazungumzo kidogo na da Suzy, nikaona nitakuchelewesha.”
“Niliyeamua kukuleta kazini na kukurudisha ni mimi wala sikulazimishwa na mtu.”
“Sawa, lakini kunipitia si adhabu, kama kuna dharura lazima tuambiane.”
“Nimekuelewa, ila nilipata wasiwasi, jana kuzungumza leo upatwe na dharura.”
“Walaa, wasiwasi wako siku zote wanadamu si wapangaji bali kila kitu hupanga wenyewe.”
“Ni kweli, vipi mzigo uliuona?”
“Ooh! Samahani kwa kuchelewa kushukuru, asante sana shemeji yangu,” nilijikuta nikiona aibu ya kuchelewa kutanguliza shukurani mapema.
“Usihofu ni kawaida, nia yangu siku moja uishi maisha kulingana na heshima yako.”
SASA ENDELEA...

NILIJIKUTA nikipata kigugumizi cha kumpa jibu kuwa nimekubali, nilitaka mwenyewe kwanza aniulize kuliko kukurupuka.
Kwa vile tulikuwa tumekaribia maeneo ya nyumbani, nilishangaa siku ile kusimamisha gari mbali kidogo na nyumbani na kunigeukia kisha aliniita jina langu.
“Mwaija?”
“Abee.”
“Vipi, nina imani umepata muda wa kufikiria.”
“Nini?” nilijifanya sijui.
“Au basi,” shemeji naye alipindisha swali lake.
“Shemeji,” nilimwita huku nikimtazama usoni.
“Naam.”
”Wewe na dada mpoje?” nilimtupia swali.
“Kwa nini unauliza hivyo?”
“Jibu swali si sikuuliza swali.”
“Mwaija mbona hilo tuliisha lizungumza toka jana?”
“Sina maana ya unayofikiria ila jibu nililokuuliza.”
“Tulikuwa wapenzi.”
” Mlikuwa wapenzi, sasa hivi?”
“Si wapenzi tena.”
“Hilo halinihusu.”
“Ulikuwa unasemaje?”
“Nina imani tabia za dada unazijua vizuri?”
“Tabia zipi?”
“Za kutokuwa na mwanaume mmoja.”
“Ndiyo.”
“Nina imani katika starehe zenu kuna kipindi hamkutumia kinga?”
“Sina kumbukumbu hiyo, lakini sijawahi kukutana naye bila kinga.”
“Basi kupata uhakika tukapime.”
“Ili?”
“We si unataka kuzaa na mimi.”
“Mwaija mi nipo sawa mbona!”
“Sijakataa, ila muhimu tukapime, hata mimi najijua nipo sawa. Lakini kwa uhakika zaidi tukapime pamoja,” nilimwambia nami nipo tayari ili kumtoa hofu.
“Mmh! Sawa.”
“Mbona kama nakulazimisha?”
“Walaa nipo tayari.”
“Kwa hiyo tutakwenda lini?” nilimuuliza kumsikiliza.
“Siku yoyote utakayotaka.”
“Kesho ukinipitia wakati wa kutoka kazini.”
“Hakuna tatizo, Mwaija ila leo nitakushushia hapa sifiki kwenu.”
Ajabu siku ile mzee Sambi hakutaka kufika nyumbani kitu kilichonishtua sana.
“Vipi mbona leo hufiki nyumbani?”
“Sitakiwi.”
“Na nani?”
“Na dada yako.”
“Utakiwi una maanisha nini?”
“Dada yako hataki nifike kwenu.”
“Kwa sababu gani?”
“Anasema yeye si mke wangu hivyo anahitaji uhuru.”
“Mmh! Sasa itakuwaje?”
“Kila kitu nimekihamishia kwako.”
“Tokea lini umekatazwa na dada kufika nyumbani?”
“Leo inatimia wiki?”
“Wiki! Muongo!”
“Kweli kabisa.”
“Mbona kila siku ulikuwa ukifika nyumbani?”
“Sababu nilikuwa nakurudisha nyumbani pia nilizungumza na mama na dada yako mdogo.”
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Basi tena, kama utakuwa tayari kuwa na mimi sitafika tena kwenu, tutajua tukutane wapi?”
“Tukutane wapi ili iweje?” nilishindwa kumuelewa tukutane ili iwe nini.
“Si kama unavyofikiri, nia kubwa kukutana baada ya kazi na kuzungumza kisha anarudi nyumbani kwenu.”
“Makubaliano yetu mpaka unipatie tulivyokubaliana pia kwenda kupima, sasa habari hiyo inakuwaje?” pamoja na kuonesha dalili za kukubali lakini sikutaka kujirahisi.
“Kupima tunakwenda kesho, kwa vile nimekuahidi lazima nitafute kiwanja nikununulie na kuanzisha ujenzi.”
“Mmh! Hiyo si itakuwa kazi ya mwaka mzima?”
“Hapana ni ya miezi miwili, nilichokuwa nasubiri jibu lako tu.”
“Mi nimekubali.”
“Basi kila kitu niachie mimi, ungependa wiki hii uanze kuendesha gari lako?”
“Hapana nimalizie kwanza nyumba.”
“Basi Mwaija ndani ya miezi miwili utakuwa ndani ya nyumba yako.”
“Basi nikuache uwahi nyumbani.”
Niliagana na mzee Sambi aliyenipa elfu hamsini ya kupandia bajaj japokuwa nyumbani hapakuwa mbali. Sikutaka kukodi bajaj nilichepua kwa mguu hadi nyumbani.
Nilipofika dada alishtuka na kuniuliza.
“Vipi shemeji yako ndiyo kasusa?”
“Kwani vipi?”
“Achana naye kapewa lifti anataka kupiga mpaka honi.”
“Una maana gani?”
“Kumpa penzi mara moja kanigeuza mkewe, ooh! Nataka kukuoa ooh, nataka kuzaa na wewe nani kamwambia mi kiwanda cha kutotolea watoto?”
“Lakini dada, yule jamaa ana fedha zake kwa nini usimkubalie.”
“Mwaija nawe msichana kama mimi hujapungukiwa kitu. We si mtu wa kuolewa, mkubalie.”
“Dada nikimkubalia si utakasirika.”
“Mwaija nikasirike ili iweje?”
“Si tutakuwa tumechangia mwanaume mmoja.”
“Angekuwa mume wangu hapo kidogo afadhali, lakini mpita njia, wee kama katuma maombi mkubalie maisha yenyewe yapo wapi,” dada alisema kama alikuwa akijua nini kinaendelea.
“Mmh! Basi acha nikapumzike.”
“Haya mdogo wangu, kama katia timu kazi kwako hela zinamuwasha.”
“Dada baadaye basi.”
“Haya mdogo wangu.”
Niliagana na dada na kwenda chumbani kwangu kubadili nguo ili niende nikaoge. Baada ya kuoga na kula nilijilaza chali kama kawaida yangu mikono niliweka kichwani. Nilijikuta nikipata wazo la kumweleza dada kuwa mzee Sambi ananitaka kimapenzi.
Niliamini kutokana na maneno yake hawezi kushtuka, lakini kwa upande wangu niliona ni mapema sana kumwambia jambo lile ambalo bado lili--kuwa halijakamilika. Nilijiuliza nini hatima ya maisha yangu kama nitakuwa na mzee Sambi mwanaume mwenye mke.

Itaendelea ..
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 20-

ILIPOISHIA:
Niliamini kutokana na maneno yake hawezi kushtuka lakini kwa upande wangu niliona ni mapema sana kumwambia jambo lile ambalo bado lilikuwa halijakamilika. Nilijiuliza nini hatima ya maisha yangu kama nitakuwa na mzee Sambi, mwanaume mwenye mke.
SASA ENDELEA...

Niliamua kufanya kwanza siri mpaka kila kitu kitakapokuwa wazi, kwa vile nilikuwa nimechoka na kazi usingizi haukuchelewa kunichukua.
***

Siku ya pili, baada ya muda wa kazi mzee Sambi alinipitia kutokana na makubaliano yetu ya kwenda kuangalia afya zetu, alipofika tu nilimueleza tuliyokubaliana jana yake. Naye hakuwa na pingamizi, alikubali twende tukapime.
Tulikwenda kwenye hospitali moja iliyopo Keko Maduka Mawili. Kama kawaida, tulifika na kupokelewa na dada mmoja aliyekuwa mapokezi.
Baada kuandika kadi, alituelekeza kwa daktari, chumba kilichokuwa mbele kidogo. Tulielekea moja kwa moja kwa vile muda ule hakukuwa na wagonjwa wengi, wengi walionekana wamekuja kupata huduma ya sindano za saa.
Baada ya kuingia ndani ya chumba cha daktari tulipokelewa na kaka mmoja mtanashati.
“Karibuni.”
“Asante,” tulijibu kwa pamoja.
“Ndiyo niwasaidie nini?”
“Tunataka kuangalia afya zetu.”
“Kuangalia kivipi?”
“Kupima Virusi vya Ukimwi.”
“Mmh!” daktari aliguna kidogo na kututazama wote kwa zamu kisha aliuliza.
“Mpo vipi?”
“Ni marafiki.”
“Wa kimapenzi?”
“Ndiyo,” alijibu mzee Sambi.
“Mna muda gani katika uhusiano wenu?”
“Mwezi sasa,” alijibu mzee Sambi.
“Sasa katika huo mwezi mlipokutana mlitumia kinga?”
“Hatujawahi kukutana, tumekuja hapa kupima ili tujue afya zetu kabla ya kuanza uhusiano rasmi.”
“Kwa mfano mmoja akikutwa na tatizo mtafanyaje?”
“Kwa upande wangu hakuna kitakachopungua kwa vile nina mapenzi ya dhati na mpenzi wangu,” alijibu mzee Sambi huku akiushika mkono wangu na kuupapasa.
“Na dada yangu kama utamkuta mzee ana matatizo?”
“Kwa upande wangu naamini mapenzi ndiyo yataishia hapa.”
“Kwa nini?”
“Kumbuka mi bado msichana mdogo nahitaji kuwa na familia halafu leo mwenzangu awe hivyo unafikiri raha ya ndoa ipo wapi?”
“Lakini kuna njia ya kuweza kupata mtoto bila tatizo.”
“Hiyo njia ndiyo siitaki kabisa kwa vile haipo salama asilimia mia moja.”
“Mzee umemsikia mama?” daktari alimuuliza mzee Sambi huku akimtazama.
“Kwangu hakuna tatizo, ikiwa hivyo namruhusu aamue chochote anachotaka lakini kama tatizo litakuwa kwake bado nitaendelea kumpenda na kumpa huduma zote muhimu kama nilivyomuahidi.”
“Sawa, basi nitawapa karatasi mtaingia chumba cha kwanza mkono wa kushoto mkapime damu.”
“Hakuna tatizo.”
Daktari aliinama na kuandika karatasi ya vipimo na kutupa, tulizipokea na kufuata maelekezo. Tulitoka na kuingia chumba cha pili, kwa upande wangu sikuwa na wasiwasi kwa vile sikuwa na tabia ya kurukaruka, pia hata mtalaka wangu naye hakuwa na tabia mbaya japokuwa sikuwa nashinda naye muda wote tulipokuwa pamoja.
Mzee Sambi naye hakuonesha wasiwasi wowote, baada ya kuingia chumba cha maabara tulikaribishwa kwenye kiti. Tulikaa na kumpa vyeti vyetu, baada ya kusoma alichukua vifaa na kutuchukua damu mmoja mmoja. Baada ya kumaliza zoezi lile alituomba tukakae sehemu ya mapumziko kusubiri majibu yetu.
Tulitoka hadi kwenye makochi na kukaa kusubiri majibu, muda wote tulikuwa kimya, hakuna aliyeanzisha mazungumzo. Baada ya robo saa tuliitwa kwa daktari, nilijua majibu yameishatoka.
Tuliingia kwa daktari na kukaa kimya kusubiri majibu yetu.
Baada ya kukaa kwenye viti, ndani ya chumba kukiwa kimya, daktari alikuwa akipitia karatasi ya majibu yetu. Muda ule niliutumia kumsoma anachokisoma kwa kumuangalia usoni kwake nikiamini atakachokisoma kitaonekana kwenye uso wake.
Nilimuona akisoma akiwa ametuliza macho, muda wote aliosoma karatasi ya kwanza alikuwa ametuliza macho. Aliiweka pembeni na kuchukua nyingine ambayo ndiyo iliyokuwa na jina langu. Aliisoma taratibu kama ya kwanza lakini kuna kipindi niliona kama amekodoa macho. Baadaye aliyarudisha katika hali ya kawaida.
Aliichukua karatasi ya kwanza na kuisoma upya na kuirudia yangu harakaharaka kisha alitutazama. Macho yake yalionesha kuna kitu amekiona kwenye karatasi, sikujua yangu au ya mzee Sambi.
Alikohoa kidogo na kutuita majina yetu kupitia kwenye vyeti vyetu.
“Mwaija.”
“Abee.”
“Mzee Sambi.”
“Naam.”
“Majibu yenu yametoka, sasa sijui niyatoe kwa kila mmoja au kwa wote pamoja?”
“Kwa wote, sababu ya kuja pamoja kila mtu anataka kujua afya ya mwenzake.”
“Vizuri, je, mpo tayari kupokea majibu yenu?”
“Daktari acha mbwembwe we tupe majibu tujue tunasuka au tunanyoa,”

Itaendelea katika Alkhamisi ijayo...
 
Jamani Mzizi Mkavu alhamisi mBona mBali

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii forum
 
hadithi nzuri sana, hapo kwa majibu hapo mmmmmm isijekuwa Mwaija kaukwaa, kipindi anamwamini mume wake kumbe mume alikuwa na wapenzi zaidi yake.
 
duuuhh
umeachia sehemu mbaya kweli.lol
Hata mi nawashwa yaani nataka kujua majibu lolest.
 
Eti MziziMkavu unatumia laptop,tab au simu maana natamani nikuibie ili nimalizie hizi stori,yaani ulipoachia ungekuwa karibu haya nanyamaza sasa
 
Last edited by a moderator:
MAMA YANGU ADUI YANGU - 21-

ILIPOISHIA
“Mwaija.”
“Abee.”
“Mzee Sambi.”
“Naam.”
“Majibu yenu yametoka, sasa sijui niyatoe kwa kila mmoja au kwa wote?”
“Kwa wote, sababu ya kuja pamoja kila mtu anataka kujua afya ya mwenzake.”
“Vizuri, je, mpo tayari kupokea majibu yenu?”
“Daktari acha mbwembwe we tupe jibu tujue tunasuka au tunanyoa,” mzee Sambi ilibidi amweleze daktari aliyeonekana jambo dogo anataka kulikuza kitu ambacho humuongezea mtu hofu moyoni.
SASA ENDELEA...

“Sawa nimekuelewa mzee, majibu yenu yapo kama ifuatavyo wote wawili kwa vipimo vya awali vinaonesha mpo sawa.”
“Una maanisha?” nilimsikia lakini sikumuelewa.
“Damu yenu wote inaonesha ipo safi.”
“Ooh! Alhamdulilah,” japokuwa nilikuwa na uhakika na afya yangu lakini nilimshukuru Mungu kwa vile sikuwa na uhakika wa uaminifu kwa mtalaka mwenzangu kwa asilimia mia moja.
Lakini upande wa mzee Sambi yeye alikuwa yupo katika hali ya kawaida zaidi ya kutabasamu na kuninyanyua na kunikumbatia kwa furaha.
“Hongera mpenzi wangu.”
“Asante.”
“Jamani kama nilivyosema vipimo vya awali ndivyo vinavyoonesha mpo salama.”
“Ina maana kuna majibu mengine?” nilijikuta nikiuliza kwa sauti huku nikijitoa kifuani kwa mzee Sambi.
“Hapana ila mnatakiwa msikutane bila kinga mpaka mchukue vipimo vya pili ambavyo ni baada ya miezi mitatu.”
“Kwa upande wangu sihitaji kurudia kwani nina zaidi ya miaka miwili, simjui mwanaume.”
”Mmh! Hongera.”
“Hata mimi nilikuwa najijua nipo salama, lakini ili kuzidi kumtoa hofu nitafikisha miezi mitatu nitapima tena ndipo tuanze uhusiano rasmi,” mzee Sambi alinitoa hofu.
“Basi mi niwapeni hongera kwa kutunza afya zenu, majibu yasiwape kiburi bali yaongeze uaminifu katika uhusiano wenu,” daktari alituasa.
“Asante daktari.”
Baada ya kuchukua majibu na kupata nasaha za daktari tuliondoka kurudi nyumbani. Njiani moyo wangu ulijikuta ukijaa furaha na kuanza kumuamini mzee Sambi ambaye tokea mwanzo alionesha nia njema kwangu.
***
Mzee Sambi aliendelea kunipeleka na kunirudisha nyumbani kwa mtindo wa kuniacha njiani na kunipa fedha ya teksi. Wiki mbili baadaye alinijulisha kiwanja kimepatikana na mwisho wa wiki alinipeleka kwenda kukiona.
Kiwanja kilikuwa kizuri sana kilichokuwa maeneo ya Boko, hakikuwa mbali na Barabara ya Bagamoyo. Kilikuwa kikubwa cha kutosha kujenga nyumba kubwa na kubakia eneo la kupumzikia.
Kwa kweli siku ile kwa mara ya kwanza nilifurahi sana na kumkumbatia mzee Sambi kwa furaha ya kweli toka moyoni.
“Asante mpenzi wangu.”
“Huu ni mwanzo tu, nataka uamini sipo na wewe kukupotezea muda wako bali kuhakikisha nayabadili maisha yako.”
“Asante mpenzi naanza kuamini.”
“Utaamini siku moja, najuta kuchelewa kukufahamu mapema.”
“Hayo achana nayo tugange yaliyopo nayajayo.”
“Basi mpenzi tukirudi kwenye gari nitakuonesha ramani ya nyumba yako inatakiwa kuwa vipi?”
“Ramani yake ipo wapi?” nilijikuta nimepata kimuhemuhe mtoto wa kike.
“Ipo kwenye gari.”
“Twende nikaione,” mtoto wa kike shauku ikanipanda.
“Utaiona tu wala usiwe na wasi.”
“Lakini mpenzi huku mbali sana na mji?”
“Si utakuwa na usafiri wako ili kukurahisishia kwenda popote bila tatizo.”
“Mmh! Hapo sawa.”
Baada ya kuzunguka eneo la uwanja wangu tulirudi kwenye gari. Kabla ya kuondoka alinionesha ramani ya nyumba yangu pia picha ya nyumba iliyokuwa imeishajengwa ambayo ilionekana nzuri pembeni kukiwa na gari la kifahari na bustani nzuri.
“Basi nyumba yako ikiisha itakuwa kama hivi.”
“Muongo!” nilishtuka kuambiwa nyumba kama ile nzuri itakuwa yangu.
“Ikiwa tofauti na hii picha ikatae.”
“Na hili gari la kifahari lililopo pembeni ya nyumba nitakuwa nalo?”
“Lazima kila kitu kiwe kama kinavyoonekana kwenye picha.”
“Wawooo! Jamani asante mpenzi wangu.”
“Hizi ni rasharasha tu, mambo mazuri yanakuja.”
Tulitoka kwenye kiwanja changu na kunirudisha nyumbani, kama kawaida aliniteremshia mbali na nyumbani. Nilipofika nilijikuta kila dakika nikitabasamu baada ya kukumbuka picha ya jumba la kifahari nililooneshwa na mpenzi wangu na kunihakikishia nyumba yangu ndivyo itakavyokuwa.
Nilijikuta nikiyaona maisha yangu yakibadilika na kunifanya niwe mtu mbele za watu. Nilikumbuka baadhi ya wanawake waliokuwa wakija kazini na kuwatetemekea kwa vile walikuwa na magari au wake wa watu wenye fedha nami nilijua tayari nimewafikia. Moyo uliniuma baada ya kujua sina haki ya asilimia mia moja hata nikiwa naye. Nilijiuliza kwa upendo alionionesha angekuwa wangu peke yangu sijui ingekuwaje! Naamini ningekuwa juu zaidi ya mawingu.
Siku iliyofuata ilikuwa Jumatatu, nilikwenda kazini kama kawaida. Da Suzy aliniuliza mchakato wangu na mzee Sambi. Nilimweleza yote sikumficha hata moja.
“Unaona mdogo wangu ulitaka kuupiga teke mfuko wa fedha!”
“Lakini kumbuka si wangu wa kufa na kuzikana, Lakini ndiyo hivyo cha kuazima hakisitiri ------.”
“Mdogo wangu usifikirie visivyo kuhusu, ridhika na unachokipata. Amekuahidi mambo mengi na moja ameanza kulitekeleza. Ningekuwa ndiyo mimi mbona ningemzalia mtoto kwa vile mmepima na kuzijua afya zenu.”
“Mmh! Sawa, huwezi kuamini nimeanza kumpenda hata bila kujijua.”
“Chezea faranga wewe?” Dada Suzy alitania.
“Walaa, si kwa ajili hiyo bali ameonesha upendo wa dhati kwangu, ni mtu mwenye huruma, mkweli pia mwenye nia njema kwangu.”
“Basi mdogo wangu usiipoteze nafasi hiyo.”
“Dada sasa hivi mimi na mzee Sambi kama chanda na pete.”
“Hongera mdogo wangu, la muhimu mzalie mtoto ndicho kilio chake.”
“Atampata tu muda si mrefu tukianza kujirusha.”
“Ina maana hujampa?” Dada Suzy alishtuka kusikia siku zote hizo sikuwa nimempa mwili wangu mzee Sambi.
“Dada sikutaka kuwa naye kibiashara bali kujua hatima ya maisha yangu.”
“Kweli mdogo wangu una msimamo.”
Tuliendelea na kazi, jioni kama kawaida mpenzi wangu alinipitia na kunirudisha nyumbani. Gari lilipofika makutano ya Barabara ya Chang’ombe na Nyerere nilishangaa kuona likinyooka kufuata Barabara ya Nyerere badala ya kukata kushoto.
Sikutaka kumuuliza kwa kujua labda ameamua kupitia Barabara ya Mandela na kuingilia barabara ya kuelekea maghorofa ya Tazara. Lakini tulipofika njia panda ya Nyerere na Mandela alikata kulia badala ya kushoto kitu kilichonishtua.
Vilevile sikuhoji nilitaka nione mwisho wake utakuwa vipi. Gari lilielekea Buguruni, lakini tuliongoza hadi Tabata Dampo. Tulipinda kulia kufuata barabara ya kuelekea Tabata.
Tulipofika Bima alikata kulia kuelekea Tabata Kimanga nami nilikuwa kimya nimetulia nione ananipeleka wapi. Tulipofika Savana alikata kulia na kusimamisha gari nje ya nyumba moja yenye geti, akateremka na kufungua geti.
Aliporudi kwenye gari nilimuuliza.
“Mpenzi wewe si una mke?”

Mzee Sambi atajibu nini? Pale alipompeleka ni wapi? Kuyajua yote tukutane Jumamosi ijayo.......
 
Back
Top Bottom