Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

Kuna vitu ambavyo maishani bora mtu usiyajue ... mhh.. sidhani kama mama amina anaweza kumweleza kama mganga kweli kweli
 
ILIPOISHIA:
Naye nilimdanganya sababu ile ilitokana na kukumbuka hali iliyonitokea nyuma.
Alinisihi nisiwaze vitu vilivyopita kwa vile ananitunza kama mboni ya jicho lake. Nilimuhakikishia hali ile haitajitokeza tena, maneno yangu yalimfariji sana mume wangu na kurudisha tabasamu lililopotea baada ya kuwa na wasiwasi wa tatizo langu kuwa kalisababisha yeye.
Nilijitahidi kuwa katika hali ya kawaida ili niweze kuwatoa wasiwasi wote na kunipa nafasi ya kuweza kwenda kwa mama Amina. Siku zilikatika nikiwa katika hali ya kawaida.
Baada ya wote kuamini nipo sawa nilifunga safari hadi kwa mama Amina kutaka kupata ukweli. Aliponiona alifurahi kuniona nikiwa katika afya njema huku mwili wangu ukiwa umerudi kama zamani.
SASA ENDELEA...

Kwa vile nilikuta watu wengi wakisubiri huduma nami nilikaa kusubiri. Baada ya muda niliitwa ndani, niliingia na kwenda kukaa kwenye mkeka.
“Mwaija naona leo mdogo wangu umenitembelea, vipi familia yako?”
“Namshukuru Mungu haijambo.”
“Una habari gani?”
“Mama Amina naomba msaada wako ambao ni muhimu kuliko kitu chochote.”
“Msaada gani?”
“Kuna jambo umekuwa ukinificha kwa nini usinieleze ili nimjue mbaya wangu?”
“Mwaija, mbaya wako wa nini, tatizo limekwisha unataka kuchimbua nini?”
“Mama Amina ukweli nimeujua lakini nataka msaada wako ili yasijetokea tena.”
“Ukweli gani?”
Nilimweleza yote niliyoelezwa na Beka kuhusu mama ambayo yalikuwa na ukweli asilimia kubwa. Maelezo yangu yalimshangaza sana mama Amina ambaye aliamini pengine nilichokisema nisingekijua.
Baada ya kushusha pumzi ndefu mama Amina alisema:
“Unayosema ni kweli lakini hakukuwa na umuhimu wa kukueleza kwa vile mbaya wako alijisalimisha na kuzivunja nguvu zake, hivyo hakuwa na madhara tena.”
“Lakini aliyefanya vile ni mama yangu?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.
“Ndiyo, lakini sasa hivi hana ubaya wowote baada ya kukubali kuzivunja nguvu zake za kishirikina.”
“Hizo nguvu zake zimevunjwa wapi?”
“Hapahapa kwangu.”
“Ilikuwaje mpaka akakubali zikavunjwa hizo nguvu zake?”
“Baada ya tatizo lako kupelekwa kwa mtaalamu wake ambaye kama angeweza kulitatua tatizo la mke wa bwana uliyekuwa naye basi siri hii ingeendelea kuitafuna familia yenu.
“Lakini Mungu naye ana mambo yake, baada ya kushindikana na wewe kuzidiwa sana na kuletwa kwangu. Hakuwa na jinsi ilibidi ajivue nguo ili kuokoa maisha yako.
Kabla ya kuanza kukuhudumia nilipoangalia niliyaona madudu yake. Kutokana na matatizo yako kuwa ya muda mrefu nisingeweza kukutibu juujuu bila kuanza kung’oa mzizi. Hakukuwa na njia nyingine ya kuvunja nguvu za mama ili niweze kukupata vizuri.
“Ilikuwa kazi kubwa, lakini kutokana na hali yako ilivyokuwa na kumuhakikishia utapona alikubali. Basi nikavunja nguzo zote alizokuwa nazo na kumsafisha kisha nikawaosha na dada zako wote.”
“Mama alisema alifanya vile kwa ajili gani?”
“Basi tu alipenda kushiriki mambo ya kishirikina ambayo sitakueleza kwa vile si sehemu yake zaidi ya kukueleza yanayokuhusu.
“Ukiingia katika mchezo ule uchelewi kujiunga kwenye chama cha waharibifu, si wachawi bali wanaozunguka kwa waganga kuharibu maisha ya watu kama kuwaharibia watu kwenye kazi au kuharibu ujauzito wa mtu kwa wivu tu wa kijinga.”
“Ina maana kuna watu wengine wanaendelea na mchezo ule aliokuwa nao mama?”
“Ndiyo, tena baada ya kujitoa watamsumbua sana. Juzi tu nimemtoa kitu kizito walichomtupia washirika wake kwa sababu ya kujitoa kwenye chama chao.”
“Mmh! Kwa hiyo sasa hivi mama ajihusishi na mchezo huo?”
“Umegundua mabadiliko gani kwenye familia yako ambayo siku za nyuma hayakuwepo?”
“Kuna tofauti kubwa sana, sasa hivi mama swala tano.”
“Basi shukuru Mungu mama yako amerudi kwenye mstari sahihi.”
“Nakubaliana na wewe kuwa kuna mambo mengi yamebadilika kwa sasa, dada wa kati sasa hivi anafanya kazi tofauti na zamani kwani alikuwa mtu wa starehe na kushinda nyumbani tu. Kingine nimeambiwa na mama kuwa dada mkubwa amepata mchumba.”
“Tatizo lilikuwa kwenye vifungo lakini baada ya kuvifungua na kuondolewa nuksi kila mmoja mambo yake yamemnyookea na dada yako anayetaka kuolewa ni mjamzito kwa sasa.”
“Usiniambie!” nilishtuka kusikia vile.
“Kila kitu sasa hivi tambarare mengine yakija itakuwa ni kudra ya Mungu si mkono wa mtu.”
“Nashukuru kwa maelezo yako pia nashukuru kwa kumuokoa mama yetu toka kwenye kundi baya.”
“Ndiyo kazi yetu kuona tunatumia fani yetu kutengeneza si kuharibu. Kuna kitu kimoja kinamuumiza mama yako kuhusiana na aliyoyafanya kwa kweli kinamkosesha raha, nimejitahidi sana kumtuliza.
“Mama yenu anajua hamjui chochote na hataki mjue alifanya nini. Nina imani akijua umefahamu ataumia mara mbili.”
“Nataka kumweleza mama ukweli japokuwa sina ujasiri huo.”
Itaendelea wiki ijayo.
 
[h=1]Mama Yangu Adui Yangu - 44-[/h]ILIPOISHIA:

Naona hadithi imefika patamu sasa. Hatimaye mama amezidiwa 'kankani' na kuamua kuitema mikoba ya ulozi.
 
[h=1]Mama Yangu Adui Yangu - 45-[/h]ILIPOISHIA:
"Tatizo lilikuwa kwenye vifungo lakini baada kuvifungua na kuondolewa nuksi kila mmoja mambo yake yamenyokea na dada yako anayetaka kuolewa ni mjamzito kwa sasa."
"Usiniambie!" nilishtuka kusikia vile.
"Kila kitu sasa kiko tambalale mengine yakija itakuwa ni kudra za Mungu si mkono wa mtu."
"Nashukuru kwa maelezo yako pia, nashukuru kwa kumuokoa mama yetu kutoka kwenye kundi baya."
"Ndiyo kazi yetu kuona tunatumia fani yetu kutengeneza si kuharibu. Kuna kitu kimoja kinamuumiza mama yako kuhusiana na aliyoyafanya, kwa kweli kinamkosesha raha nimejitahidi sana kumtuliza.
"Mama yenu anajua hujui chochote na hataki mjue alifanya nini. Nina imani akijua umefahamu ataumia mara mbili."
"Nataka kumweleza mama ukweli japokuwa sina ujasiri huo."
SASA ENDELEA...

"Nakushauri ungeachana nayo kwa vile umeelewa nawe umekuwa tayari kumsamehe."
"Sawa, nimemsamehe mama kwa vile nampenda sana."
Baada ya maelezo ya mama Amina nilirudi nyumbani kwangu nikiwa kidogo na afadhali baada kuutua mzigo mzito ulionisumbua lakini nilijiuliza kwa nini nisimueleze ili ajue alichotufanyia wanaye.
Kutokana na maelezo ya mama Amina jinsi mama yangu anavyoumizwa na matendo yake nilishindwa kumweleza na kuamua kumsamehe kwa vile tayari alikuwa amerudi kwa mola wake.
Siyo siri nilikuwa nampenda mama yangu sana kwa malezi yake. Nilishtuka sana kusikia ndiye aliyekuwa adui yangu mkubwa.
Lakini nilifarijika baada ya kujirudi na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaye tunaishi katika mstari mzuri baada ya kupotea.
***
Siku zilikatika nikiwa na siri yangu moyoni huku nilijitahidi kuyasahau yote yaliyotokea.
Nilijikuta nikimpenda zaidi mama yangu pamoja na yote aliyonitendea. Kila nilipokumbuka yaliyonitokea, nilijifungia ndani na kulia huku nikizidi kumuomba Mungu amsamehe mama yangu.
Niliwaza sana kuhusu siri ile kuwaambia dada zangu, bado nafsi ilinisuta kwani niliamini kuwaeleza wasiyoyajua ni sawa na kumvua nguo mama yangu.
Mama alibadilika sana baada ya kuanza kuswali na kuachana na pombe, alikuwa mpole na mtu mwenye mawazo mengi sana kila alipokuwa peke yake.
Dada zangu walishangazwa na hali ya mama kurudi katika ibada, kuacha pombe na tabia zote mbaya.
Alikuwa mkali kwa mambo machafu na kuwaeleza waige mfano wangu wa kuolewa na si kuzini ovyo.
CD za taarabu alizipiga marufuku nyumbani na kuifanya nyumba kupoa huku majirani wakishangazwa na hali hiyo kwani sauti za muziki siku za nyuma zilikuwa juu na kuwakera.
Pia, mabadiliko ya mama yaliwashangaza na kuifanya nyumba yetu irudishe heshima ya wakati wa uhai wa marehemu baba.
Taarifa zilizotoka kwa dada zangu zilisema mama amebadilika sana hakai tena sebuleni kama zamani muda mwingi alikuwa akishinda ndani kwa ajili ya kuswali, muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake na alipotoka alionesha kuvimba macho akionesha alikuwa akilia.
Japokuwa mabadiliko yale yalikuwa mazuri, lakini hali ya mama ya kukosa raha na kushinda chumbani peke yake hata sisi wanawe ilitunyima raha.
Wasiwasi wangu ulikuwa labda mama anateseka na aliyotufanyia. Niliingiwa na wasiwasi wa kumpoteza mama kwa kuhofia kwamba angeweza kufa kwa kihoro.
Maana aligeuka na kuwa kama mgonjwa, alianza kupungua kila siku mpaka kupelekea kuugua vidonda vya tumbo. Hali ile ilitufanya tukutane kutaka kujua kipi kimemsibu mama yetu japokuwa niliamini aliyoyafanya ni sehemu ya maumivu ya majuto.
Kila tulipomuuliza mama kuhusu matatizo yake aliishia kulia, nilikuwa na wasiwasi wa kuwaeleza dada zangu tatizo la mama na jinsi lilivyotokea.
Niliamini mtu wa kutusaidia kipindi kile alikuwa ni mama Amina. Niliamua kwenda kwake na kumuomba ushauri kuhusu tatizo la mama.
Alinieleza tatizo la mama yetu linatokana na kuumizwa na vitendo alivyotufanyia wanawe.
"Mama yenu anashindwa kuwaeleza ukweli tatizo hilo kwa kuhofia kwamba mnaweza kumtenga na kumfanya afe kwa kihoro. Nilimhakikishia hakuna tatizo litakalotokea bila kumueleza kama wewe unajua kila kitu."
"Sasa tufanyeje? Maana hali ya mama ni mbaya. Mimi nimemsamehe leo na kesho kiama, nina imani hata dada zangu pia watamsamehe."
"Mwaija najua sasa hivi moyo wako umetulia, mfuate mama yako na umueleze unayoyajua kuhusu yeye na kuonesha umemsamehe ili kuondoa donge moyoni mwake."
"Mmh! Nitaweza, nina wasiwasi mama yangu anaweza kulia mbele yangu. Nampenda sana mama yangu na naumia na hali yake pia nitaumia zaidi akilia," nilishindwa kuzizuia hisia zangu.
"Sasa tutafanya nini?"
"Mama Amina kaa na mama na umweleze yote kisha tukutanishe wote, nina imani una nafasi ya kurejesha furaha ndani ya familia yetu. Siyo siri sisi wote kwa sasa hatuna raha."
"Nitafanya hivyo, wewe nenda kesho nitakuja."
"Mama Amina wewe ndiye tegemeo langu la mwisho kwa mama yetu."
"Shaka ondoa mdogo wangu, mama yetu atarudi katika hali yake ya kawaida maadamu mmeamua kulimaliza."
Niliachana na mama Amina na kurudi nyumbani. Sikuwa na furaha kwa kusubiri simu ya mama Amina kuhusu mama amepokeaje alichomueleza.
Siku iliyofuata nilikuwepo nyumbani lakini mawazo yangu yalikuwa mbali sana. Nilisubiri simu ya mama Amina kwa shauku kubwa. Nikiwa namalizia kumuosha mtoto simu iliita, mapigo ya moyo yalinibadilika ghafla, nilimuacha mtoto kwenye beseni na kuikimbilia simu sikutaka kumtuma msichana wa kazi aifuate niliona kama angechelewa.
Lakini haikuwa ya mama Amina, nilijikuta nikichukia. Baada ya kuzungumza nilirudi kumalizia kumuosha mtoto. Kabla sijaanza kumuosha iliita tena. Nilimtuma msichana wa kazi.
"Niletee," hamu yote iliniisha.
Alipokuwa ameishika nilimuuliza nani, akaniambia mama Amina. Nilimwacha mtoto na kuwahi kama itakatika na salio sikuwa nalo.
"Haloo," nilipokea huku mapigo ya moyo yakiwa juu.
"Vipi mbona unahema?"
"Mwenzangu, hata sijielewi mama kanichanganya sana, vipi umeishafika nyumbani?"
"Ndipo ninapoongelea."
"Umeishazungumza na mama?"
"Ndiyo."
"Amesemaje?"
"We upo wapi?"
‘Nyumbani."
"Njoo basi mara moja."
Nilishindwa kuendelea kumuosha mtoto nilimfuta na mimi kubadili nguo bila kuoga na kuondoka. Nilipofika barabarani nilikodi teksi kwenda Tandika kwa mama.
Bahati nzuri kipindi kile hakukuwa na foleni kubwa barabarani kama sasa. Gari lilikwenda mpaka njia panda ya Mandela na Tazara Vetenari ilikata kulia.
Nilifuata barabara ya Vetenari kabla sijafika maghorofa ya Tazara nilishangaa dereva kusimamisha gari pembeni karibu na kituo kidogo cha polisi.
"Vipi mbona unasimama?"Nilimuuliza dereva.
Kuna gari nyuma limeonesha ishara ya taa tusimame sijui ana shida gani.
"Sawa," nilitulia sikushughulika naye nilijua ni watu wake.
Baada ya muda nililiona gari la mzee Sambi likisimama mbele yetu. Nilishtuka mpaka mapigo ya moyo yakanienda mbio. Baada ya gari kusimama alishuka mzee Sambi na kuja kwenye gari letu.
Alipofika alitoa miwani yake na kusema kwa kushtuka:
"Ni wewe Mwaija?"
"Ndiye mimi, ulijua nitakufa?"
"Sivyo Mwaija ni historia ndefu."
"Ya kunitaka kuniua na kunidhurumu mali yangu?"
"Mwaija naomba tukae pembeni tuzungumze."
"Katu sitazungumza na wewe muuaji," nilimjibu kwa hasira.
"Usiniite hivyo Mwaija nipe nafasi unisikilize."
"Ili?"
"Utajua sababu ya mimi kuondoka ghafla."
"Nikijua itanisaidia nini, nilikufuata kukuliza?"

Itaendelea Jumapili....
 
Hii story mbona haiendelei tena tangu wakati ule hapa mimi nilishafika hebu endelea ama tupe link ya mahali ilipo maana ni story nzuri sana, fiction lakini ina reflect hali halisi ya maisha yetu jamani. kudos
 
hii hadithi ni nzuri lakini sehemu zingine hazipo ningependa kuipata yote, na hii habari ya mzee sambi itaendelea lini? hongera tena, pia sijaon sehemu inayoeleze nini hasa kilitokea mpaka kufika kwa bi amina
 
Duh Naona jamaa anajua kuipaisha hii stori...Naona Mzee Sambi kaja ibukia mbele tena...Haya mpaka tuione mwisho🙂
 
[h=1]MAMA YANGU ADUI YANGU - 46-[/h]
ILIPOISHIA:
Baada ya muda nililiona gari la mzee Sambi likisimama mbele yetu. Nilishtuka mpaka mapigo ya moyo yakanienda mbio. Baada ya gari kusimama alishuka mzee Sambi na kuja kwenye gari letu.
Alipofika alitoa miwani yake na kusema kwa kushtuka:
"Ni wewe Mwaija?"
"Ndiye miye, ulidhani nitakufa?"
"Sivyo Mwaija ni historia ndefu."
"Ya kunitaka kuniua na kunidhuruma mali yangu?"
"Mwaija naomba tukae pembeni tuzungumze."
"Katu sitazungumza na wewe muuaji," nilimjibu kwa hasira.
"Usiniite hivyo Mwaija nipe nafasi unisikilize."
"Ili?"
"Utajua sababu ya mimi kuondoka ghafla."
"Nikijua itanisaidia nini, nilikufuata kukuliza?"
SASA ENDELEA...

"Ha! Mwaija umeolewa?" mzee Sambi alishtuka baada ya kuiona pete ya ndoa kutokana na kurusha mikono yangu wakati nilipokuwa nikiongea.
"Ulifikiri siolewi?" nilimjibu kwa nyodo.
"Na huyo mtoto ni wako?" alizidi kushtuka kila dakika.
"Ndiyo, uliambiwa mi ni mgumba?" nilimjibu kwa nyodo.
"Mwaija angekuwa wangu huyo, mama yako anahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga uhusiano wetu."
"Aliyetaka kuniua ni mama yangu au mkeo?"
Muda wote dereva wa teksi alikuwa akitushangaa kwa jinsi tulivyokuwa tukitupiana maneno.
"Huwezi kunielewa naomba basi uje kwenye gari langu tuzungumze."
"Mlinikosa kuniua hamtanipata tena, ulimtuma mkeo aniue ili mchukue nyumba. Sawa, mmechukua vyote hivyo, lakini sijawafuata kuwaulizia kitu chochote."
"Mwaija nyumba bado ni yako."
"Usinichefue, kukusikiliza usinifanye mjinga, uliniambia nini kuhusu mkeo na matokeo yake kimetokea nini? Kwa taarifa yako najua kila kitu katika ile nyumba."
Nilimweleza yote tangu siku nilipokwenda na kumkuta na mkewe wakiwaonesha wapangaji nyumba. Nilimuona akishangaa kama kaona meli barabarani.
"Basi naomba tuzungumze Mwaija ili unielewe nipo radhi kukupa chochote ili tuondoe tofauti zetu."
"Naomba hayo tuachane nayo, endelea na maisha yako na mkeo mchawi. Acheni kuwaroga watoto wa watu kwani mnawaharibia mambo yao."
"Mwaija maneno gani hayo?"
"Tuachane na hayo, naomba uendelee na safari yako."
"Sasa?"
"Kuhusu nini?"
"Nipe hata dakika tano."
"Nimeitwa nyumbani mama anaumwa naomba uniache niwahi."
"Naomba namba yako ya simu."
"Siwezi kukupa, mume wangu ana wivu sana."
"Sasa ita.."
"Dereva hebu tuwahi safari yetu."
Dereva aliondoa gari na kumuacha mzee Sambi akiwa amesimama barabarani. Dereva hakuniuliza mpaka tulipofika kwenye kona ya Maguruwe.
"Dada vipi?"
"Achana naye," nilimijibu kwa mkato.
Nilijikuta nikiwa mtu mwenye hasira baada ya kuachana na mzee Sambi mpaka machozi yalinitoka huku kifua kikinijaa kwa hasira. Nilifika nyumbani na kumlipa dereva kisha niliingia ndani.
Nilipokelewa na mama na ndugu zangu pamoja na mama Amina.
"Karibu mama yangu," mama Amina alinitania kutokana na kumwita mwanangu jina lake kama shukurani kwake kwa kuwa sehemu ya kupatikana kwa mwanangu.
"Asante, shikamoo."
"Marahaba mama yangu."
"Shikamoo mama," nilimgeukia mama.
"Marahaba, za nyumbani?"
Mama yangu aliitikia kwa unyonge, hali ile ilizidi kuniumiza moyoni.
"Nzuri mama, shikamooni dada zangu."
"Marahaba mama Husna," waliitika wote.
Nilikwenda kukaa pembeni ya mama na kumpa mjukuu wake, alimpokea na hapohapo nikagundua mama alikuwa akitokwa na machozi.
Baada ya kuketi mama Amina alifungua kikao kile cha kifamilia.
"Jamani nina imani mtashangaa kuuona uwepo wangu hapa kwenu kwa muda huu," alianza kuzungumza mama Amina.
"Walaa," tulijikuta tukijibu kwa pamoja.
"Basi leo sikuja kama mlivyonizoea, kuna jambo zito limenileta ambalo nina imani hamlijui lakini mama yenu anataka mlijue kabla mauti hayajamchukua.
"Nina imani hivi karibuni mmeona mabadiliko ya hali ya mama yenu?"
"Ni kweli," tulijibu kwa pamoja.
"Nina imani hali hii imewashtua sana na kukosa jibu, ni kweli?"
"Kweli," dada alijibu.
"Nina imani mi si msemaji ila mzungumzaji mkubwa ni mama yenu ataeleza kinachomtesa moyoni mwake."
"Hakuna tatizo," dada mkubwa alijibu.
"Kabla sijamkaribisha mama yenu naomba kuwauliza."
"Uliza tu," tulimkubalia.
"Je, mnampenda mama yenu?"
"Zaidi ya sana."
"Kama amewakosea mpo tayari kumsamehe?"
"Leo mpaka kesho kiama," tulijibu wote kwa vile tulikuwa tukimpenda sana mama yetu.
Nini kiliendelea? Usikose kusoma Alkhamisi ijayo.
 
Mkuu Hadithi/simulizi hii ni nzuri sana. Please Mzizi Mkavu. Ongeza speed ya kutumbukiza story. I imefhukua muda mwingi sana.
 
There are currently 20 users browsing this thread. (4 members and 16 guests)
Eberhard, Home First, Akthoo, kimyazo
 
Back
Top Bottom