Mama yangu adui yangu

Mama yangu adui yangu

Nadhani haujaruka story ila nahisi umeruka Namba, sijui kama right maana natumia simu
 
Kwanza pole kwa mkasa ukiokukuta ila wazungu wanasema kwamba"True love never ask why!!" Kama kweli umempenda na upo tayari kuishi nae chukua uamuzi mgumu! Ila my advice 2u, never hate ur mum! Prey 4her and one day she will know that is wrong, plz and plz again dont hate ur mama bwana,!
 
Tena sana 2... Bahati ya kupata wachumba...Sababu sijui ni uzuri... Tabia... Au ni hao kalumanzira!

Mwaija ni dezaini ya watoto ki pwani (waweza ita wa kiswahili). Mtoto wa kike aliyefundwa na akafundika. Anajijuwa na kujitambua. Anajua dhana na thamani yake kama mtoto wa kike. Anajua kujibeba wakati wowote awapo peke yake au pale awapo na mwenza (mume). Anajua nini maana ya kuwa na mwenza (partner). Vilevile anajua nini maana ya kujikita (kuji-commit) katika mahusiano ya ki unyumba pasipo kugawanya (diversify) attension yake kwa mume. Yaani ile ku stay focus- one man one woman.

Ni msichana mvumilivu na mwenye subira. Hana hulka ya kiburi wa ukisirani kama wasichana wengi wa kizazi cha leo. Si unaona hata wanaume wanapomtaka kuomba undugu (read ndoa) huzungumza nao kwa staha pasipo kuwabehua au kuwajibu kwa majibu ya kejeli kuwa wao sio wa daraja au saizi yake🙂.

Na hii ndio imemfanya awe chachu ya wanaume kumpangia foleni si ya kutaka kum date bali kuoa moja kwa moja bila kutaka mjadala. Na pia Mwaija haamini katika kudate (au kutoka na wanaume kula uroda tu) bali yeye muumini wa ndoa tu, kama hakuna wakuji commit wacha ikae🙂. Hivyo wanaume humfuata wakiwa wameshakata shauri kuoa kwa kumjua thamani ya sampuli ya mwanamke wa aina na daraja lake. Na hii ndio imemtofautisha yeye na dada zake japokuwa naweza kusema wote wamekuzwa chuo kimoja lakini wale wale hawakufudhu na wamebaki wakishindwa kukidhi viwango vya kuwa wake.

Tatizo moja kubwa ni kuwa ametoka kwenye familia yenye Mama mshirikina na mlozi. Ni Mama alikuwa kama kuku anayedhuru kifaranga chake mwenyewe. Ki ukweli ni kwamba kuna akina mama wengi sana wenye ku practice mambo haya katika jamii yetu ya ki Tanzania. Yapo na ni mambo ya kweli na yanazungumzwa kila siku mitaani na ndugu na hata majirani juu ya familia flani flani.

Mwisho, Mwaija ni mseto uliotimia barabara wenye kila aina ya viungo. Naamanisha kuwa ya si mambo ya mtoto wa kike aliyekuwa na sifa moja pasipo nyingine.

Haya tuendeleeni na hadithi yetu.....
 
Lol, ulivyompamba? ngoja nikamwite huyo mwaija aje ajionee hizi sifa mwenyewe
Mwaija ni dezaini ya
watoto ki pwani (waweza ita wa kiswahili). Mtoto wa kike aliyefundwa na
akafundika. Anajijuwa na kujitambua. Anajua dhana na thamani yake kama
mtoto wa kike. Anajua kujibeba wakati wowote awapo peke yake au pale
awapo na mwenza (mume). Anajua nini maana ya kuwa na mwenza (partner).
Vilevile anajua nini maana ya kujikita (kuji-commit) katika mahusiano ya
ki unyumba pasipo kugawanya (diversify) attension yake kwa mume. Yaani
ile ku stay focus- one man one woman.

Ni msichana mvumilivu na mwenye subira. Hana hulka ya kiburi wa
ukisirani kama wasichana wengi wa kizazi cha leo. Si unaona hata wanaume
wanapomtaka kuomba undugu (read ndoa) huzungumza nao kwa staha pasipo
kuwabehua au kuwajibu kwa majibu ya kejeli kuwa wao sio wa daraja au
saizi yake🙂.

Na hii ndio imemfanya awe chachu ya wanaume kumpangia foleni si ya
kutaka kum date bali kuoa moja kwa moja bila kutaka mjadala. Na pia
Mwaija haamini katika kudate (au kutoka na wanaume kula uroda tu) bali
yeye muumini wa ndoa tu, kama hakuna wakuji commit wacha ikae🙂. Hivyo
wanaume humfuata wakiwa wameshakata shauri kuoa kwa kumjua thamani ya
sampuli ya mwanamke wa aina na daraja lake. Na hii ndio imemtofautisha
yeye na dada zake japokuwa naweza kusema wote wamekuzwa chuo kimoja
lakini wale wale hawakufudhu na wamebaki wakishindwa kukidhi viwango vya
kuwa wake.

Tatizo moja kubwa ni kuwa ametoka kwenye familia yenye Mama mshirikina
na mlozi. Ni Mama alikuwa kama kuku anayedhuru kifaranga chake mwenyewe.
Ki ukweli ni kwamba kuna akina mama wengi sana wenye ku practice mambo
haya katika jamii yetu ya ki Tanzania. Yapo na ni mambo ya kweli na
yanazungumzwa kila siku mitaani na ndugu na hata majirani juu ya
familia flani flani.

Mwisho, Mwaija ni mseto uliotimia barabara wenye kila aina ya viungo.
Naamanisha kuwa ya si mambo ya mtoto wa kike aliyekuwa na sifa moja
pasipo nyingine.

Haya tuendeleeni na hadithi yetu.....
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 42-

ILIPOISHIA:
“Si nilikuuliza nani anataka kukubakiza jina huniambii ikabakia siri yako na familia yako huku ukitaka kunigombanisha na mama yangu.”
“Samahani naomba tutafute sehemu nzuri tuzungumze vizuri.”
SASA ENDELEA...

“Leo ndiyo unaweza kumsema?” nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho.
“Kama mpaka leo hujui tatizo lazima nikueleze huenda likaiokoa ndoa yako ya sasa.”
Kauli ile ilinifanya niwe na hamu ya kumsikiliza. Tulisogea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na kutafuta meza ya pembeni.
Baada ya kukaa tuliagiza vinywaji, nilitulia kumsikiliza Beka mtalaka wangu, bwana na mwanaume wa usichana wangu ambaye alionekana maisha si mabaya.
“Mwaija najua unaweza kunichukia na kuniona adui yako kutokana na kushindwa kusema ukweli. Lakini nilifanya hivyo kulinda amani iliyo ndani ya familia yenu.
“Nina imani mama yako unampenda sana na unamuamini kwa kila kitu.”
“Ndiyo.”
“Ni vigumu kuamini mama yako ndiye aliyekuwa adui yako namba moja.”
“Etiii!?” nilishtuka kusikia vile.
“Ndiyo maana sikutaka kuyasema hayo kipindi kile kwa vile tungeweza kupotea wote kabla siri haijatoka nje.”
“Una maana gani?” sikumuelewa alimaanisha nini.
“Mwaija nina imani unanijua vizuri kuliko mtu yeyote.”
“Ndiyo.”
“Na maisha yangu unayajua vizuri?”
“Ndiyo.”
“Baada ya ndoa yetu kupigwa mizengwe na wewe kusimama kidete, mwisho tulifanikiwa kuoana. Namshukuru Mungu baada ya ndoa maisha yalikuwa mazuri sana, mpaka tukanunua kiwanja na kuanza ujenzi.”
“Ni kweli.”
“Tatizo lilianza baada ya kubeba ujauzito, uongo kweli?”
“Ni kweli.”
“Na ujauzito wako ulitoka katika mazingira ya utatanishi?”
“Ni kweli kabisa.”
“Na baada ya hapo ndipo mikosi na mabalaa yalipoanza mpaka nikakosa hata kazi na wewe ni shahidi ulifuata fedha kwenu.”
“Ndiyo.”
“Kwa kweli sikujua chochote kuhusiana na matatizo yale kwa kuamini ni mipango ya Mungu. Lakini nilishikwa mkono na rafiki yangu aliyeshangazwa na anguko langu la ghafla na kunipeleka kwa mtaalamu, Handeni, Tanga.
“Nilipofika huko niliyoyasikia kwanza sikuamini, niliamini mganga ni muongo. Alinieleza mambo mengi kuhusiana na matatizo yangu mpaka ya ndani ya familia yako.”
“Eeh!” nilishtuka kusikia vile.
“Eeh! Ndiyo, alisema chanzo ni mama yenu ndiye aliyefanya mambo ya kishirikina kwa kukutega mlangoni, uliporuka ujauzito ukatoka kisha akaanza kuniwangia mpaka mambo yangu yakawa hayaeleweki.
“Alikwenda kwenye kiwanja na kuifunga nyumba yetu iliyokuwa kwenye hali nzuri ili tusiendelee huku akifunga riziki kila kona. Baada ya kuona pamoja na hali ya maisha kuwa mbaya lakini hutaki kuachana na mimi, alianza kuitafuta roho yangu kuhakikisha ananitenganisha na wewe.
“Ilionesha hata kama ningekueleza usingekubali kitu ambacho kingefanya nipoteze maisha kwa vile alikuwa na nafasi ya kuja kwetu angenimaliza kwa urahisi.
“Japokuwa maneno ya mganga yalikuwa yakifanana na kweli, bado sikukubaliana naye kwa kuamini kauli ile ni ya uchonganishi ambayo ndiyo chanzo cha vitabu vya dini kuikataa ramli.
“Ukweli kuamini moja kwa moja nilishindwa wala kukueleza jambo zito kama hilo ambalo lazima lingeleta mpasuko. Nilimueleza mganga jinsi mama mkwe alivyonisaidia mpaka hata kupata nauli ya kwenda kule.
“Alinieleza kama siwezi kukueleza basi niachane na wewe. Ilikuwa vigumu kukubali kuachana na wewe mke wangu kipenzi ambaye naamini mpaka nakufa sitapata mwingine kama wewe.
“Mwaija hata sijui kwa nini nilichukua uamuzi huo heri ningesema mapema kwa jinsi ulivyokuwa ukinipenda ungeweza kunisikiliza lakini wasiwasi wangu ndiyo ulionifanya nilie kila siku kukukumbuka mke wangu mpenzi.
“Basi mganga alinieleza nichague moja katika ya matatu. Nikueleze ubaya wa mama yako, kama nikishindwa nikuache huku nikikueleza kila kitu anajua mama yako na kama ungemwambia angeujua ubaya wake au vyote vikishindikana nikubali kufa.”
Maneno ya Beka yalinisisimua mwili na kuanza kuamini yote aliyosema hasa baada ya mama Amina kukataa kunitajia mbaya wangu. Niliendelea kumsikiliza mtalaka wangu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi.
“Kwa kweli bado sikuwa tayari lakini alinichambulia moja baada ya lingine kama ameniumba yeye, hata sababu ya dada zako kuachika na kutokuwa na wazo la kuolewa tena. Kama mtu akitokea anataka kuoa basi hugeuka ugomvi na kumfukuza kama mbwa.”
Maneno yale yalikuwa na ukweli kwa sababu dada alimfukuza mzee Sambi baada ya kutaka kumuoa.
“Basi alinipa mtihani mmoja ili kuhakikisha anachosema ni kweli, aliniambia angenipa kitu ambacho ningekuja nacho kwenu. Mama yako angeniona angeanguka.
Alinieleza baada ya tukio lile nilitakiwa nikuache na kuondoka haraka kwani kama ningeendelea kuwepo kwenu mama yako angekufa.”
“Ni kwa nini?” niliuliza mkono shavuni.


Fuatilia wiki ijayo alkhamisi........
 
MAMA YANGU ADUI YANGU - 43-

ILIPOISHIA:
"MAMA yako angeniona na kitu hicho angeanguka, ndiyo maana nilitakiwa nikuache na kuondoka haraka. Kama ningeendelea kuwepo kwenu, mama yako angekufa."
"Ni kwa nini?" niliuliza mkono wangu ukiwa shavuni.
SASA ENDELEA...


"Kwa sababu ya ubaya wake," alisema.
"Unafikiri kwa nini amekuwa na tabia hiyo?" nilimuuliza swali ambalo nilitakiwa nilijibu mimi mwenyewe.
"Ni roho mbaya na kupenda kushiriki mambo ya kishirikina yamemfanya apende kucheza michezo ya kichawi."
"Enhee, nini kiliendelea?"
"Kwanza nilikataa na kuamua kuachana na wazo hilo. Baada ya kubahatika kupata kazi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Tanga.
"Nilifanya kazi kule kwa muda huku nikiwa na wazo la kutafuta njia mbadala tofauti na maelezo ya mganga.
"Lakini mganga alinieleza kama sijipendi nifanye kinyume na alivyonieleza. Baada ya kufanya kazi kwa muda nilipata nafasi ya kurudi nyumbani.
"Kabla ya kuja Dar nilirudi kwa mtaalamu ambaye alinieleza nifanye kama alivyonielekeza na kuniambia mambo nitakayoyakuta siku nitakayokuja kwenu na hali itakayojitokeza.
"Niliporudi Dar sikukaa, nilikuja kwenu na kila nilichoelezwa na mganga kilitokea ikiwa ni pamoja na mama yako kuanguka alipokuwa amekaa baada ya kushtuka aliponiona.
"Kwa kweli tukio lile lilinifanya nichukue uamuzi mgumu wa kukupa talaka na kukuacha na fumbo kuhusiana na talaka yako.
"Niliamini mama yako angekueleza lakini hakukueleza, nilipoondoka sikutaka kujua habari za nyuma. Leo unaponiona nina siku mbili na kesho naondoka kurudi nilipo, kwa yaliyonitokea nimejikuta sipendi tena kukaa katika jiji hili."
Mpaka Beka anamaliza kunieleza chanzo cha talaka yangu, macho yake yalikuwa yamejaa machozi. Si yeye tu, hata mimi muda wote nilikuwa nikilia huku nikitumia mtandio wangu wa kichwani kujifuta machozi.
Nilijitahidi kuzungumza japokuwa moyo wangu ulikuwa kama amechubuliwa katika kovu lililoanza kupona na maumivu yake yakawa mara mbili.
"Beka nakubaliana na wewe kwa asilimia mia kuwa, mama yangu anahusika lakini bado hukutakiwa kuutesa moyo wangu kwa maswali yasiyo na majibu.
"Najua pengine mimi ndiye niliyesababisha kwa kutoa siri ya kipato chetu kwa mama ila kwa vile ni mkeo ulitakiwa kuniweka wazi. Siamini kama kuna mwanadamu anaweza kuua bali kwa idhini ya Mungu.
"Hata kwenye riziki binadamu anaweza kuichelewesha si kuizuia kabisa.
"Beka ungekuwa wazi ningejua nifanye nini, pengine ukimya wako umenifanya nichungulie kaburi au ningezikwa ningali hai."
"Kwa nini?" Beka aliuliza macho yakiwa yamemtoka pima.
Nilimueleza yote yaliyotokea baada ya kunipa talaka, maisha niliyoishi na kufikia kuugua ugonjwa wa ajabu.
"Dah! Pole sana Mwaija, nina imani hata huyo bwana kuondoka kwake inawezekana mama yako amechangia."
"Inawezekana," nilimkubalia.
"Lazima ujiulize kwa nini mtu akukimbie wakati wa matatizo?" aliniuliza.
"Beka nashukuru kwa maelezo yako ambayo naamini yamechelewa kunifikia, nina imani leo hii tungekuwa pamoja."
"Ni kweli lakini sina wa kumlaumu bali wasiwasi wa nafsi yangu."
"Beka naomba nikapumzike kwa vile sijisikii vizuri, pia mwanangu nimemwacha muda mrefu."
"Ha! Mwaija una mtoto?" Beka alishtuka.
"Beka uliambiwa mi mgumba?"
"Mmh! Sawa," Beka alishusha pumzi nzito na kuinamisha kichwa.
"Beka naomba niondoke, kwani hali yangu siielewi nahisi mapigo ya moyo yananienda kasi," niliongea kwa shida kidogo.
"Hakuna tabu Mwaija kwa vile nina gari nitakupeleka."
"Hapana Beka, nitakodi teksi au nitamwita mume wangu anifuate."
"Kwa nini usumbuke nitakupeleka mara moja, kwa hali hii siwezi kukuacha peke yako."
"Hakuna tatizo."
Ilibidi nikubali kwa vile sikuelewa baada ya muda hali yangu ingeendeleaje. Kila nilivyofikiria nilikosa jibu na kujikuta moyo ukiniuma kama unataka kutoka na kuachana na mwili wangu.
Beka alinipeleka mpaka kwangu kwani hata nguvu za kutembea sikuwanazo. Nashukuru nilifika nyumbani salama na kuagana na Beka huku tukipeana namba za simu kwa ajili ya kuendelea kusalimiana kama marafiki si wapenzi tena.
Nilipofika ndani hali ilizidi kuwa mbaya, kila nilipoyakumbuka mambo yote yaliyokuwa yamejificha nyuma ya pazia.
"Kumbe mama yangu ndiye adui yangu!" nilijiambia mwenyewe moyoni.
Kichwa kiliniuma na mapigo ya moyo yalinienda kasi, nilimwambia msichana wa kazi amjulishe mume wangu kwa vile hata uwezo wa kupiga simu sikuwa nao.
Mume wangu baada ya kupewa taarifa alifika mara moja na kunikimbiza hospitalini. Niliambiwa kuwa presha ilikuwa juu sana na kuwafanya madaktari kupata kazi ya kuishusha.
Walifanikiwa baada ya saa mbili ndipo nilipata usingizi mpaka asubuhi. Taarifa zilimfikia mama, naye akawa wa kwanza kufika hospitalini na kufuatiwa na dada zangu.
Siri ya matatizo yangu sikumueleza mume wangu, alijua ni matatizo ya kawaida japokuwa hali ile haikuwahi kunitokea tangu aliponioa. Mama naye alishangaa na kutaka kujua presha ile ilisababishwa na nini.
Nilishindwa kumueleza ukweli, nilisingizia imetokea ghafla japokuwa mama alikataa katakata maelezo yangu.
"Hapana Mwaija, kwa maelezo aliyonipa mumeo nahisi kuna kitu mnanificha.Hebu niambie mama nini kimekusibu? Madaktari wamesema presha ile ingeweza kukupofua macho au kukufanya upooze mwili."
"Hata sijui nimejisikia tu mwili ukikosa nguvu na kumpigia simu mume wangu ambaye alinieleta hapa," bado niliificha siri ile.
"Mwaija mi' mtu mzima maisha ya ndoa nayajua, kama kuna kitu mumeo amekuudhi niambie ili tujue tufanye nini, sitaki yatokee ya mzee Sambi."
"Haki ya Mungu, kuhusu mume wangu utamuonea. Ananitunza kama malkia, hajawahi hata kunikemea tangu anioe na ananipenda kwa mapenzi ya dhati."
"Sasa tatizo ni nini?"
"Mama ni hali umenitokea tu, hata sielewi, pengine ni mawazo ya kutaka kuzikwa ningali hai, kila nikikumbuka moyo unanipaa," nilitengeneza uongo uliomfanya mama aamini.
"Lakini mwanangu mambo hayo si yameshaisha? Sasa hivi una ndoa yako nzuri, pia una mtoto, hebu achana na mambo hayo ili kuondoa kuishi kwa wasiwasi."
"Sawa mama nimekuelewa nitajitahidi kusahau."
"Itabidi ufanyiwe na kisomo."
"Hakuna tatizo."
Kila alilokuwa akilifanya mama na kutoa maneno yenye faraja, yaliufanya moyo wangu uzidi kuwa njia panda kwa kutoamini kama mbaya ni yeye.
Niliamini lile lilikuwa fumbo zito ambalo alilifahamu mama Amina peke yake, yeye ndiye aliyekuwa na majibu ya maswali yangu. Nilipanga nikitoka hospitali na kutulia, nimfungie safari ili akanieleze ukweli, nilikuwa radhi kumpa kiasi chochote atakachokitaka ili tu anieleze ukweli.
Baada ya hali yangu kuwa nzuri niliruhusiwa na kurudi nyumbani. Mume wangu naye alitaka kujua sababu ya tatizo lile kama alikuwa amelisababisha yeye. Naye nilimdanganya sababu ile ilitokana na kukumbuka hali iliyonitokea siku za nyuma.
Alinisihi nisiwaze vitu vilivyopita kwa vile ananitunza kama mboni ya jicho lake. Nilimhakikishia hali ile haitajitokeza tena, maneno yangu yalimfariji mume wangu na kurudisha tabasamu lililopotea baada ya kuwa na wasiwasi wa tatizo langu.
Nilijitahidi kuwa katika hali ya kawaida ili niweze kuwatoa wasiwasi wote na kunipa nafasi ya kuweza kwenda kwa mama Amina. Siku zilikatika nikiwa katika hali ya kawaida.
Baada ya wote kuamini kuwa nilikuwa sawa, nilifunga safari hadi kwa mama Amina ili kujua ukweli.
Aliponiona nikiwa katika afya njema na mwili wangu ukiwa umerudi kama zamani, alifurahi sana.


ITAENDELEA TENA JUMAPILI IJAYO...
 
Back
Top Bottom