BABA JUICE
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 426
- 54
ndugu wanajamii huku kijijini napata shida kweli....jana jirani yangu mama preta kaja, juzi alikuja mama alfani ananiuliza kama bado nawasiliana na mwanae aliepo mjini?nikamjibu mama siku hizi mwanao kabadili namba na hapatikani hewani nikamwambia mama usiohofu habari zake nitamfikishia jamii forum kwani hata na jina siku hizi kabadili anaitwa money maker, kwani mama tatizo nini jioni yote hii? mwanangu aliniahidi atatuma pesa kwa m-pesa hadi leo mwezi wa pili umepita hajatuma kitu.....basi mama chukua hii elfu tano itakusaidia kwa wiki moja.ndugu wanajamii mama zetu ni wake zetu na wadogo zetu ni watoto zetu...tusiwasahau kwa starehe za huko mjini tutume japo kidogo kiweze kuwakimu huku vijijini kwani huku hali ni ngumu.....tusijisifu kuwa tunawasaidia wazee wetu wakati hatufanyi hivyo.....kwako kidogo kwake nyingi...tuma chochote....alfani na preta pesa zangu mnilipe.