Mama yake Zitto avamiwa

Mama yake Zitto avamiwa

thanx kamanda,mweleze zemarcopolo,bungeni,m23 kuwa waje na vichwa vyao akili ndogo waendelee kupata posho lumumba bidae ktk thrid live updates:mkutano wa chadema mbeya..wataharisha mwaka huu hawa magamba
usisahau mafilifili na sumu
 
Zitto, mchezo wako huo siku moja utakuja mpoteza umependa and still ukakosa unacho kitaka (Urais) nahisi hi move ni mwendelezo wa kutengeneza ushahidi kwa Lakatare na CDM kwa ujumla, sometimes mue mnamkumbuka na Mungu kwamba nae pia yupo, mtakuja umbuliwa vibaya, shauri yenu!
 
CCM na usalama wa taifa wandhani Zito ni uchochoro wa kupitia kufanikishia mpango wao wa kuisambaratisha CHADEMA hawajui kuwa Zito alijiunga na CHADEMA akiwa na umri wa miaka 16! Hivyo hajui chama kingine zaidi ya hicho kilichomkuza. Wao wanadhani wanaweza kumfanyia usanii hovyohovyo akasaliti na kusambaratisha chama kilichomlea, walie tu. Bali mimi nimjuavyo Zito ana akili nyingi na anajua kuwatumia CCM na usalama wa taifa kwa manufaa MAPANA ya CHADEMA na ataendelea kuwatumia kwa kadri ya ujinga wao na wakiishi kwa matumaini siku moja watamtumia, KATU hawawezi nawashauri watafute uchochoro mwingine, vinginevyo subirini kunyolewa 2015

mkuu mbona comment yako haiendani na hali halisi na ukweli wa tukio lenyewe??? wewe unawalaumu ccm na usalama wa taifa wakati aliyetendewa tukio amekwambia amemfahamu kada wa chadema, au ungesoma tena hiyo habari uielewe
 
Mtanzania na propaganda
wamesema mama yake Zitto alimwona kada wa chadema na anamfahamu yale
yale ya baba yake Mtela Mwampamba, mtu amuonye tu Shida binti Salum ana
heshima kwenye jamii asijiingize kwenye propaganda za kusaidia usaliti
wa mwanane wa masalia, mama tulia kula vya mwanao pole pole dhambi ya
uongo ni mauti , sasa hili dili litakufa kama lilivyokufa la video, pole
mama habari ya leo ni liwale

kama dkt ulimboka alimtambua yule afisa wa usalama, unafkiri mama zitto kumtambua kada wa cdm haiwezekani mkuu? au unataka tu kuamini unachopenda kuamini?
 
Mmh tumeanza kuyatambua hadi majambazi kwa itikadi za kisiasa eeeh Mungu tuepushe Usalama wa Taifa wanatupeleka kubaya.

ninyi ndio mnaopanga mauwaji na mateso ya raia huko gizani kisha mnawahi kupotosha kwenye vyombo vya habari...kitendo cha kukamatwa na video mkipanga mauwaji kisha mkaanza kuwalaumu wana usalama ni ushahidi tosha..kama haitoshi mama yake zitto amemtambua kada wa chadema lakini pia akampigia kaimu mkuu wa usalama wa chama bwana sabula akamjibu anapatia wapi fedha anayotumia kumfanyia kampeni za urais na uenyekiti mwanaye zitto.. hebu kabla hujaandika kaa chini tafakari kwanza ndipo uone namna gani ujipendekeze kwa mabwana zako.
 
Jamani acheni meno na kucha za mama ZITTO....... malizaneni wenyewe wazazi wetu mtuachie

Siamini kama watu wanaweza kuamini CDM inaweza kufanya tukio hili kwa mama yake Zitto wkt tuna changamoto nyingi zinakikabili chama. Unadhani CHADEMA ni wajinga ama hawajui mbinu za namna hii zitaharibu chama.....imepandikizwa hii kuna matu anatafuta revenge.....lakini bahati nzuri kila kinachofanyika gizani sikuzote kinawekwa hadharani. Mungu tamuumbua mnafiki. Tunasubiri mengineyo zaidi kutokana na taarifa ya polisi wa gazeti la mtanzania
 
mmmmh.....imepikwa hii. Kila njia kwa sasa zinatafutwa kuvuruga Chama, kuna lengo linapotezwa hapa, Chezea ZZK wewe. Nasubiri mchezo huu tuone utafikia wapi
kuunganisha dots huwa kazi ngumu sana, unatumia resorces nyingi mno na on the process kuna wengine lazima wawe mbuzi wa kafara.
 
Duhh kutambua majambazi kwa itikadi ya vyama hizi sasa ni siasa za maji taka, huyu mama kuvamiwa inawezekana kama vile ambavyo angevamiwa mtu yeyete yule, lakini kitendo cha kutaka laptop, flash na simu kuna jambo hapo, tunasubiri wahusika watuambie huyo mama ana nyaraka gani muhimu kwa cdm mpaka zitafutwe kwa silaha za moto? Vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa ni muendelezo wa siasa za kuchafuana.
 
Huu ni mwendelezo wa Mwigulu wa kuwatumia akina Ludo wengine ili aweze kupata cd nyingine ya kuitoa kama ushahidi mahakamani na mbinguni.
 
Hili gazeti la Mtanzania Jumatano huwa lina matatizo gani maana lazima waandike propaganda chafu dhidi ya Chadema
Mkuu, hii ni kazi ya charles Mulinda, alikuwa mwandishi wa tanzania daima na kazi zake ni hizi za kuchafua watu, miaka ya nyuma alimuwinda samwel sitta mpaka mzee wa watu ikabidi atishie kwenda mahakamani
 
Muhalifu anaweza kuwa CHADEMA, Muhalifu anaweza kuwa CCM , muhalifu anaweza kuwa CCK au chama chochote kile.Mhalifu anaweza kuwa muislam mkristo au mpagani,anaweza kuwa mpare, mzaramo au mnyakyusa, anaweza kuwa mrefu au mrefu mwanaume au mwanamke.Zote hizi ni hali za kibinadamu ambazo hazina uhusiano wa kisayansi na uhalifu; hivyo basi muhalifu atabakia kuwa muhalifu tu bila kujali hali mojawapo atakayojikuta akiwapo miongoni mwa hizo hapo juu.Cha msingi muhalifu anatakiwa kushughulikiwa kama muhalifu na si vinginevyo. Zaidi ya hapo itakuwa ni mnyukano wa makundi maslahi unaofanywa na makundi ya watu fulani flani unaoongozwa kwa hila kali kupitia kwa muhalifu husika.
 
hivi kama mtu alishatishiwa kuuawa kwa sumu,ikapangwa auliwe kwa ajali,ikapangwa afukuzwe kwenye chama lakini umaarufu wake ukawatisha,namba yake ikatolewa hadhalani,sasa wamegeukia kwa mama yake hawa watu wanatupeleka wapi?
 
mtanzaniiaaaaaaaaaaa! gazeti la kuchochea uhasama na siasa chafu za kutaka kuua upinzani.. acheni njaaa kali.... "serukamba"
 
Back
Top Bottom