Mama wa rafiki yangu ananitaka kimapenzi

BEDUI Jr

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
2,041
2,836
Habari wana JF,

Kama kichwa cha Habari hapo juu kinavyosema. Nina rafiki yangu kiumri tunafanana japo sio rafiki kihivyo, pia tulikua majirani lakini kwa sasa nimehama kwa kero za Mama yake kunitaka kimapenzi. Huyo rafiki yangu ndio mwanawe wa kwanza, jumla huyo mama ana watoto wa 3.

Sikumoja aliniita nimuungie WhatsAapp, Facebook na Twitter. Baada ya hilo zoezi kumaliza akaomba na namba zangu kisha akaniuliza nikupigie saa ngapi? Nikamwambia muda wowote. Nikaondoka zangu, usiku akanituma sms kaniuliza
"Umelala?"
"Ndiyo"
"Na nani?"
"Peke yangu"

Akaguna "Mhhhhh siamini", nikajifanya simsikii kama mtandao unasumbua hivi nikakata simu nikalala. Akaendelea kunisumbua; kuna siku kanitumia SMS akaniambia leo naenda kuoga choo cha nje wewe njoo moja kwa moja sifungi mlango nauegesha tu. Sikwenda. Siku ya pili akaninunia baadaye akaniita akaniuliza, "Vipi message yangu?" nikamdanganya simu niliweka chaji sikuwa nayo, akasema sawa.

Nikaamua kuhama na namba ya simu nikabadili kumkwepa. Sasa kapata tena namba zangu ila hajui ninapokaa. Akinipigia ananiita mpenzi wangu na anataka aje kwangu, na keshamuaga mumewe anataka kwenda Mbagala kwa dada yake kumbe anataka aje kwangu alale siku tatu.

Nifanyeje nijinasue na huu mtego? But mwanawe anapajua kwangu.
 
Sasa mkuu, mama wa rafiki vumilia tu ngono sio lazima sana sehemu ambayo sio sahihi...ila ukaanzaje kwenda kumuunganishia facebook na whatsap na mshikaji wako yupo, kuanzia hapo ungemjibu haujui hayo mambo...we mwisho wa kuona ni karibu sana???

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom