Mama Tibaijuka, Flora Mbasha &Co.-Mtashinda tu!

Hapa wamejaa wapuuzi wengi, mashabiki mandazi wasiozidi buku(1000) kwenye nchi yenye watu milion 45 na ukiwaendekeza wayaongeayo unaweza kudhani ndio ukweli na hali halisi nchini kote. Kumbe ni wapuuzi watupu wasiokuwa na shughuli za kueleweka na zaidizaidi ni watu waliojawa na stress za kuchapika na maisha.

Nawasoma(ga) jinsi wanavyofarijiana na ku-share ujinga wao mwishowe naishia kucheka tu.

hao hao wapuuzi ndo wanafanya damage kubwa sana kuliko unavyodhani,wanapokua hapa wanaweka threads after threads after threads hatimae wana achieve malengo yao,kwani ni watanzania wachache sana wanaothink clitically na daima wataamini kila linalosemwa na hata hao wapuuzi kama hamna counterpart
 
Pamoja na ukweli kwamba wanaotajwa kuhusika na haya mambo ya Escrow ni wengi ktk Serikali ya raisi Kikwete, lkn ni mmoja tu ndio amekuwa akishambuliwa kila siku kwa kejeli na saa saa nyingine mpaka matusi naye ni Mama Tibaijuka, na ukiangalia sana utaona ya kwamba hakuna sababu nyingine yoyote ya maana zaidi ya ubaguzi dhidi ya Wanawake - Mfumo Dume!

Kama ilivyokuwa kwa Mwanamuziki Flora Mbasha ambapo watu walimshambulia bila hata kujua ukweli, Jamii nzima ikageuka kuwa hakimu na kumhukumu mama Mbasha na kumkingia kifua Mumewe, walimlaumu mama Mbasha kwa kila baya lililoikumba ndoa yao!

Sijasikia Jaji Werema, Chenge,waziri Muhongo au hata Raisi Kikwete mwenyewe wakishambuliwa kwa kiasi ambacho mama Tibaijuka amekuwa akishambuliwa! Hii ndiyo sababu inayonifanya niamini anashambuliwa kwa kuwa ni Mwanamke!
Hakuna jamii Dunia Hii inayodharau Mwanamke kama hii yetu, na iko kila mahali nchini mwetu!

Najua Mama Tibaijuka analijua hili na ametoka mbali, amepitia na kuyashinda mengi hata hili nalo pia atalishinda!

Shame labda akaloge
 
Atulie aache kukwepesakwepesa, wamrime mbere na nyuma !!!!!!!!

Huyu mama amenichekesha sana ile siku Ya press conference " eti wamekuja wengi walidhan anajiuzulu .. Eti kujuzulu sio fasion
Sasa prof mzima hayo ni maneno gan?
 
bright maana yake nini? maana wewe ndiyo umekazana kumtetea! mtumishi wa wa umma anapewa tshs 1.6b/- na mfanyabiashara zisizo na maelezo yanayoeleweka halafu mnasema anasakamwa kwa vile ni mwanamke! how silly? na bado anitisha press conference na kusema hatajiuzulu kwa sababu rais kikwete ana imani naye!! really? wewe unajua maana ya kutakatisha pesa chafu au upo upo tu kama dodoki?

bright maana yake mtu mwenye akili,unaposema eti tiba kapewa bilion1.6 na mfanyabiashara sasa kumbe ulitaka upewe wewe?
unasema hazina maelezo yeyote,maelezo ni kwamba zimetolewa kwa shule zake,sasa maelezo yapi tena unayotaka?.
unasema tibaijuka ametakatisha pesa,shurti sasa utwambie kwanini unadai hizo pesa zilikua chafu
 
wewe ni mbabaishaji tu! hujui kuwa ili pesa ya deal kwenye a/c ya serikali haiwezi kutoka bila mlolongo wa wahusika? na unajua mlolongo wa deal hiyo jinsi lilivyochezwa? au una tetea tu kwa sababu umeshiba makombo?

mlolongo lazima uwe na connection na ishu husika,sasa kwanini waziri wa ardhi na isiwe waziri wa fedha ama gavana wa benki?
 
Ningemuona wa maana sana huyu mama kama sehemu ya hela alizokwapua angezipeleka jimboni mwake kuhudumia wananchi wanaoteseka kwa kukosa maji, wanafunzi mashuleni na si kupeleka kwenye shule yake binafsi ambayo ina kila kitu kinachotakiwa kuwa nacho shule ya kimataifa. Bukoba matokeo ya darasa la saba ni mabaya na asilimia kubwa ya shule zilizoboronga ni za muleba jimboni kwa tibaijuka. Inatia hasira kusema mabilioni hayo ni mchango, huyu bob ruge hana ndugu wa kuwapa hizo zote hadi akupe wewe ukaboresha shule yako. Mwisho fuata nyayo za Chenge, Ngleja na wengine wamepiga hela lakini wako kimya tofauti na wewe kila kukicha unataka utoe ufafanuzi, utaweza wapi mama.
 
Huyu mama anashambuliwa shauri ya kidodomo chake angetulia watu wasingeendelea lakini muwasho wake umemponza ns si vinginevyo

Hajazoea wizi kaingia kwa magamba wamemuambukiza,kinachoendelea hivi sasa ni nafsi inamsuta
 
Back
Top Bottom