Mama Samia ameanza kunishawishi

Mama Samia ameanza kunishawishi

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,729
Reaction score
58,992
Bunge lipo live

Waangalie Mashehe wa uhamsho duh!

Anatumbua kwa haki bila kuonea mtu.

Waliofanya uhuni wanashughulikiwa sio kwa kukomolewa Bali ni kwa mjibu wa sheria zilizopo.

Anafuata sheria katika kufanya maamuzi.

Achanganyi siasa na utendaji.

Sijaona kikao cha ccm kikifanyika Ikulu

Bodaboda na bajaji walinyanyaswa sana na police leo kawabeba kwenye faini kutoka elfu 30 mpaka elfu 10.

Morogoro kwenye soko la manispaa kamwagiza mkuu wa mkoa wapunguze kodi kutoka laki 1 mpaka elf 30 ili machinga wapewe vibanda kwa bei rahisi.

Hii pia itafanyika nchi nzima vibanda na maduka yanayomilikiwa na halimashauri yapunguze kodi ili hata watu wa kawaida waweze kumiliki biashara ndani ya masoko.

Leo nimekuwa kariakoo, Kariakoo imerudi kwenye ubora wake.

Leo nimekuwa bandarini, Bandarini meli za kutosha kwa sasa.

Biashara imeanza kurudi na kuchanganya

Mama apewe sapoti ya kutosha ana kitu cha ziada anaweza kutupa hata katiba.
 
Sijaona kikao cha ccm kikifanyika Ikulu
Miezi 3 tu madarakani…..mpaka 2025 na 2030, safari bado ni ndefu sana!

Kuna waliodai Samia halindwi na askari wenye mabunduki makubwa waliovaa magwanda ya kijeshi, siku chache tu baada ya kuapishwa!

Hii picha hapa chini ni ya wiki chache zilizopita…

E48692D4-54D9-445E-8386-DA85D5D963B9.png
 
Miezi 3 tu madarakani…..mpaka 2025 na 2030, safari bado ni ndefu sana!

Kuna waliodai Samia halindwi na askari wenye mabunduki makubwa waliovaa magwanda ya kijeshi, siku chache tu baada ya kuapishwa!

Hii picha hapa chini ni ya wiki chache zilizopita…

View attachment 1821928
Hao maaskari amewekewa na Mabeyo.

Ukishaambiwa kwenye suala la ulinzi wako uwekewe hao walinzi, hakuna namna angekataa.

Halafu siku hizi haonekani sana kwenye media kama enzi za Magu, possibly na yeye alikuwa anaagizwa tu mpaka anachoka.
 
Miezi 3 tu madarakani…..mpaka 2025 na 2030, safari bado ni ndefu sana!..
Nyani Rais kulindwa namna hiyo ni jambo la kawaida sana, Out of 60mil people, yeye pekee ndiye anawaongoza, maniac yeyote anaweza kutokea katika hao mil 60 na akafanya lolote na ikalisababishia taifa siyo tu hasara bali na aibu pia. Nafikiri tumpime kwa uongozi wake zaidi kuliko ni wangapi wanamlinda, nipo tayari kurekebishwa Bro
 
Naam!

Lakini ilikuwa nongwa Magufuli kulindwa na hao hao jamaa wanaomlinda Samia sasa hivi!

Au wewe hukuwepo pindi Magufuli ananangwa kwa ulinzi aliokuwa nao?
 
Nitashangaa sana Chadema na vyama vingine ikiwa vitaweka wagombea tena 2025, Itakuwa ni unafiki mkubwa sana kwa vyama hivyo

Ikiwa Raisi tuliyenaye leo ndio haswaa anapendwa na si tu viongozi wa Chadema bali na wanachama wote wa chama hiki cha wanafiki duniani

Raisi wetu songa mbele!!
 
Naam!

Lakini ilikuwa nongwa Magufuli kulindwa na hao hao jamaa wanaomlinda Samia sasa hivi!

Au wewe hukuwepo pindi Magufuli ananangwa kwa ulinzi aliokuwa nao?
Hahaha, nilikuwepo Mkuu! Siasa kweli ni mchezo mchafu, na kuna lile gari lina antennas za kutosha, Magu alikuwa analitumia na watu walichonga kwelikweli, mother naye kaanza kulitumia! Nafikiri ndiyo maana kuna bachelor, masters na phd ya sayansi ya siasa, ni kitu kigumu kweli kweli!
 
Kazi iendelee means tuendelee kujaza matumbo yao na hela zetu mpaka yapasuke. Nashauri wewe uwe mbunge, akili yako ni Kama kuku!
 
Back
Top Bottom