Mama Samia ameanza kunishawishi

Mama Samia ameanza kunishawishi

Tatizo la vyama kutoshirikiana ili kuwa na sauti moja dhidi ya maccm ni njaa. Kumbuka Zitto na chama chake ACT Wazalendo mara baada ya uchaguzi walifanya news conference pamoja na Chadema kuonyesha msimamo wao mmoja kupinga yote yaliyotokea kuhusu uchaguzi wa 2020.

Pia Zitto na chama chake walikusanya ushahidi wa kutosha kuhusu vipigo na mauaji mbali mbali kule Zenj na kusambaza ushahidi huo katika taasisi mbali mbali duniani ikiwemo UN, ICC na haki za binadamu. Hata kabla taasisi hizo hazijatia neno ACT wakachangamkia FURSA ya Serikali ya mseto kule Zenj kwa kupewa umakamu wa Urais na nafasi chache za Mawaziri.

Hilo ni tatizo kubwa ambalo maccm wanalitumia kuvigawa chama visiwe na sauti moja. Somo kutoshiriki uchaguzi limeeleweka kwa Chadema lakini hivi vyama vyenye njaa navyo vitasusia uchaguzi?

Kwa maoni yangu watahongwa pesa/vyeo ili washiriki na hivyo kuonyesha uchaguzi huo ni wa vyama vingi. Imagine participation kwenye uchaguzi ni 20% tu ya eligible voters sijui kama katiba hii ya sasa inasema chochote kuhusu percentange ya eligible voters wanaotakiwa kushiriki kwenye uchaguzi ili President elect awe halali kuongoza nchi.

I’ve advocated for boycotting elections under the current conditions since 2005.

2025 voter participation ikiwa ndogo zaidi ni jambo zuri.

Vyama vyote vya upinzani vilipaswa kutokushiriki chaguzi zote tokea 1995..
 
Nimegundua kuwa viongozi wanaotoka kwenye dini ambazo waumini wanajumika kusali kila siku wana hekima sana na ni waungwana kuliko sisi tunaosubiri Jumamosi na Jumapili. Mwenyezi Mungu azidi kumpa hekima na busara mama yetu.

Halafu CCM wasirudie tena kosa la kuwapa uongozi wa juu Illegal Immigrants!
Nakubaliana nawe, ukiangalia kipindi cha uongozi hawa wenzetu wanapokua madarakani kunakua na ahueni fulani hivi
 
Usisahau kahaidi kupandisha mishahara ya watumishi....kwa hili tutampamba hadi achoke
 
Bunge lipo live

Waangalie Mashehe wa uhamsho duh!

Anatumbua kwa haki bila kuonea mtu.

Waliofanya uhuni wanashughulikiwa sio kwa kukomolewa Bali ni kwa mjibu wa sheria zilizopo.

Anafuata sheria katika kufanya maamuzi.

Achanganyi siasa na utendaji.

Sijaona kikao cha ccm kikifanyika Ikulu

Bodaboda na bajaji walinyanyaswa sana na police leo kawabeba kwenye faini kutoka elfu 30 mpaka elfu 10.

Morogoro kwenye soko la manispaa kamwagiza mkuu wa mkoa wapunguze kodi kutoka laki 1 mpaka elf 30 ili machinga wapewe vibanda kwa bei rahisi.

Hii pia itafanyika nchi nzima vibanda na maduka yanayomilikiwa na halimashauri yapunguze kodi ili hata watu wa kawaida waweze kumiliki biashara ndani ya masoko.

Leo nimekuwa kariakoo, Kariakoo imerudi kwenye ubora wake.

Leo nimekuwa bandarini, Bandarini meli za kutosha kwa sasa.

Biashara imeanza kurudi na kuchanganya

Mama apewe sapoti ya kutosha ana kitu cha ziada anaweza kutupa hata katiba.
Mkuu hata wafanyakazi haki zao zimeanza kutatuliwa mfano upandaji wa madaraja
 
Ujambazi? Uzembe? Udini? Kuahirishwa mechi simba na yanga? Umeme Tanesco,Upigaji bandarini? Kutoibuliwa miradi mipya? Kufunguliwa masheikh kutainua uchumi wa nchi? Rubbish!
Binafsi nilikuwa mmoja wa waliokuwa wanaipinga sana awamu ya tano na Rais wake Magufuli ila baada ya kutafakari na kujionea hali halisi ilivyo sasa Ninakiri kwamba nilifanya makosa makubwa sana, Ninaomba nisamehewe.Magufuli alikuwa ni nabii aliyepata kuishi ili kuonyesha njia sahihi na miongozo tunayopaswa kuiishi.Leo utumbuaji umekuwa kawaida pale uzembe unapodhihirika zamani haya hayakuwezekana.Kazi alizofanyia Tanzania ni kubwa sana tangu akiwa waziri.Ni kweli alivyosema kuwa amejitolea uhai wake kwa ajili ya Tanzania na sote tumeshuhudia lawama nyingi alizobebeshwa yote hayo yalikuwa ni kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwa Tanzania.Magufuli ameitendea haki Tanzania katika nyanja zote, Uchumi,Elimu,Afya,Miundombinu muhimu amani na usalama wa taifa.Kwakweli ni mengi sana aliyoyafanya hayatoshi kuelezea hapa.Ila itoshe tu kusema tumeona ukuu wa Mungu kupitia mtu huyu aliyetumwa kuonyesha njia.Bwana ametoa,Bwana ametwaa.Jina lake lihimidiwe! Amen
 
Back
Top Bottom