Mama Salma atoa vifaa vya uvuvi Lindi

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
2,000
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete aetoa misaada mbalimbali ya vifaa vya uvuvi kwa kikundi cha ujasiriamali cha uvuvi kinachoitwa Mwambao Fishing Group kilichopo Wilayani Humo. Mama Salma amefanya zoezi hilo Alasiri ya leo katika eneo la kivukoni ambapo ndipo Kikundi hiko kilipoweka masikani yake.

Mama Salma alitoa misaada hiyo zikiwemo nyavu, maboya, matanga na mashine za boti kwa kikundi hicho akiongozana na Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali ambao wamo mkoni humo kuhudhuria maazimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo kitaifa yalifanyika Mkoani Lindi.


Mama salma aliwataka wavuvi hao kufanya kazi kwa UMOJA na kushirikiana akiwakumbusha kauli mbiu ya Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi ya "UMOJA NA USHINDI" na kuwaambia kuwa mafanikio yao yatatokana na kujituma kwao na hivyo kukuza kipato chao na kuwa mfano kwa wavuvi wengine. Mama salma alisema "Nawasihi kujituma kwa bidii kwani hiko ndicho kitu pekee kitakachowasaidia kuendeleza kikundi chenu hiki, tumieni uwezo wenu, fikra zenu na nguvu zenu zote zielekezeni katika kukijenga na kukiimarisha kikundi chenu ili kiweze kuwa ni kikundi cha mfano kwa watu wengine, kitoe msukumo kwa wavuvi na wajasiriali wengine lakini pia kiwe ni tegemeo na matumaini kwa jamii."


Mama Salma yuko mkoani Lindi kwa Ziara ya siku Tano ambapo ameongozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete.
attachment.php
attachment.php


attachment.php
 

Attachments

 • PB290247.JPG
  PB290247.JPG
  3.2 MB · Views: 375
 • PB290230.JPG
  PB290230.JPG
  3.1 MB · Views: 338
 • PB290259.JPG
  PB290259.JPG
  3.1 MB · Views: 312

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Nahisi harufu ya rushwa hapa. Baba rais mama mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa, watoto mashemeji na kila mtu. Kweli huu ni usultani wa Jakaya Kikwete.
 

Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,173
2,000
hivi kuwa mjumbe wa chama tawala tayari ni kiongozi wa taifa tena mkubwa mpaka unafuatana na mawaziri wa serikali???
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,753
2,000
Yule Mbunge wa Lindi mjini - CUF (sijui anaitwa nani tena) akae mkao wa kula. Jimbo analichukua mama hivyo! Kwa kuwa ni vyama tofauti mama atapita kwa kishindo hatua zote. Mh. Mbunge anza kutafuta kazi nyingine, jimbo limerudi magamba hilo; na CUF mlivyopoteza mvuto, kazi unayo.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,753
2,000
Yule Mbunge wa Lindi mjini - CUF (sijui anaitwa nani tena) akae mkao wa kula. Jimbo analichukua mama hivyo! Kwa kuwa ni vyama tofauti mama atapita kwa kishindo hatua zote kama ambavyo amepita bila kupingwa kwenye chaguzi zao hivi karibuni.

Mh. Mbunge anza kutafuta kazi nyingine, jimbo limerudi magamba hilo; na CUF mlivyopoteza mvuto, kazi unayo. Kuna ile NGO yako ya watu wenye ulemavu wa ngozi, elekeza zaidi nguvu huko; ushauri wa bure huu.

Hii thread ilipaswa kusomeka "Mke wa Rais Kugombea Ubunge Lindi". Dalili zote zinaonesha hivyo.
 

timbilimu

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
4,840
2,000
Yule Mbunge wa Lindi mjini - CUF (sijui anaitwa nani tena) akae mkao wa kula. Jimbo analichukua mama hivyo! Kwa kuwa ni vyama tofauti mama atapita kwa kishindo hatua zote. Mh. Mbunge anza kutafuta kazi nyingine, jimbo limerudi magamba hilo; na CUF mlivyopoteza mvuto, kazi unayo.

Mama sasa anaelekea Mjengoni!
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
Nataka kujua kama Mke wa Raisi anapokea Mshahara, na kama anapokea ni kwa kazi gani? na kama hapokei hizo pesa za kununua hivyo vifaa zimetokea wapi?

Ufalume unarudi katika Bara la Africa, ila tofauti na ufalume wa zamani wa sasa ni kuwarisisha wanawake ni staili ya BRITAIN
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
Mama sasa anaelekea Mjengoni!

Hakika huyu mama kama si sasa hivi basi ni baada ya miaka michache ijayo huyu mama atakuja kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi , ameisha jifunza kutoka kwa yule mama wa kule Argentina alie mrithi mme wake
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,753
2,000
Mama sasa anaelekea Mjengoni!

Ha ha ha ha ha! Kama yule mrembo Cristina Fernández de Kirchner; mumewe alikuwa Rais wa Argentina na yeye ni Rais wa taifa hilo kwa sasa. Huyu Kirchner (mama) ni kichwa hakuna mfano na anapendwa na watu wake balaa. Hawakumwonea "gere" eti kwa kuwa mumewe naye alikuwa mkuu wa nchi; uzuri mama ana-deliver ile mbaya. Ni bahati mbaya 2010 alikumbwa na msiba wa mumewe kipenzi.

Haya, tunasubiri kumwona "kichwa wetu" Mama Salma. Kazi kwako mama.
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
1,225
Mama Salma sijui ni mke wa rais wa Tanzania au ni mke wa rais wa Lindi? Kila leo, yeye na WAMA yake, wanapeleka misaada sehemu moja tu - Lindi? Vipi sehemu nyingine za Tanzania? Na kama mke wa rais anaelekeza jicho lake sehemu moja tu, sehemu aliyozaliwa, ni vipi akipewa madaraka zaidi? Si atahamisha kila kitu kielekee Lindi?
 

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
649
500
Mama Salma sijui ni mke wa rais wa Tanzania au ni mke wa rais wa Lindi? Kila leo, yeye na WAMA yake, wanapeleka misaada sehemu moja tu - Lindi? Vipi sehemu nyingine za Tanzania? Na kama mke wa rais anaelekeza jicho lake sehemu moja tu, sehemu aliyozaliwa, ni vipi akipewa madaraka zaidi? Si atahamisha kila kitu kielekee Lindi?
Akiwa kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama akiiwakilisha LINDI MJINI ulitegemea yale anayoyafanya kama MNEC wa LINDI aje ayafanye arusha..?
 

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
2,000
Mama Salma sijui ni mke wa rais wa Tanzania au ni mke wa rais wa Lindi? Kila leo, yeye na WAMA yake, wanapeleka misaada sehemu moja tu - Lindi? Vipi sehemu nyingine za Tanzania? Na kama mke wa rais anaelekeza jicho lake sehemu moja tu, sehemu aliyozaliwa, ni vipi akipewa madaraka zaidi? Si atahamisha kila kitu kielekee Lindi?

Ukweni mkuu!
 

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
2,000
Ukweni mkuu!

Hivi ni lini watu wanaweza kujadili with free mind mambo ya msingi yahusuyo jamii yao, kwa mitazamo ya aina hii jamii yetu inaweza kuchelewa sana kupata maendeleo. Tushiriki pamoja na tuunge mkono juhudi zenye kulenga kuendeleza watu wetu, hilo ni la msingi na bora zaidi.
 

swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
0
kwa taarifa nilizonazo huyu mama atagombea ubunge 2015 na anajua kuwa lazima ataupata na wakati huo huo membe atakuwa rais na yeye atateuliwa kuwa waziri wa mambo ya chi za nje na 2025 agombee u president
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom