Mama Regina Lowassa: Kwa hili UMENIGUSA SANA!

Ushabiki wa siasa pembeni lakini huyu mama ana mvuto sana na tayari anaonekana kama first lady tayari. Hii ni leo akiwa Kahama na mumewe. Mimi ni Msukuma na nayajua madhila ya vikongwe hawa anaoongea nao.
Wengi wanahisi kuwa jamii imewatenga na wanaishi kwa hofu ya kuuawa kwa tuhuma za uchawi.

Japo najua kuwa pengine mumewe hatashinda na kuwa rais lakini kwa hili tu amenivutia sana.
Asante mama Lowassa kwa hili.
Umetonesha milizamu za macho yangu na Mungu Akubariki whether ukiwa first lady ama la!

Natamani angeendelea na hii huduma bila kujali ni raia wa kawaida sio first lady.

Changamoto za wanasiasa wetu wanayaona Sana matatizo ya wananchi wakiwa kwenye nyakati za uchaguzi pekee
 
Yeye na mumewe walikutana chuoni wakati wanasoma usanii; lazima walikuwa wanafunzi wazuri pia maana hizi perfomances zao nimezivulia kofia.

Mama ajawahi kuchangia ata senti ya msaada na utajiri wao wote mara tu anajali matatizo ya akina mama.
You said it all!
 
21 December 2013
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akishiriki kuhudumia chakula watoto wenye ulemavu--katika Kituo cha Huduma ya Walemavu kinachomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha kilichopo Monduli wakati alipokwenda kushiriki nao Ibada ya X-Mass pamoja na kuzungumza na kula nao chakula cha mchana
Kwa Sasa anajitolea wapi au hapendi camera?
 
Back
Top Bottom