Mama ntakupenda daima

Jagood

JF-Expert Member
Aug 15, 2016
2,141
2,390
8998d4e1e748d155b2668b41e71f5eef.jpg
 
Hasa wa vijijini sio wa mjini kazi kufuatilia tamthilia sijui za kikorea wengine wanafuliwa hadi kufuli na housegirl. Kuna mama jirani yangu ananikera sana huyo hii sifa haistahili hata tone.
 
Huyu mama ukimuangalia kwa makini lazima upatwe na huruma.Aliko toka si salama kwa maana jinsi alivyo ondoka na mtoto pasipo kuifunga mbeleko vizuri (japo inawezekana mtoto msumbufu hataki kubaki na mtu mwingine) au ana kimbilia sokoni (mfuko mweusi mkononi),kibaya zaidi baiskeli yake haina breki na ni mfupi hawezi kukanyaga chini wakati wa kusimama.Itabidi aruke huku amemshikilia mtoto maana mbeleko imefunguka."Uko wapi baba ? Mama anateseka peke yake?" Pumzika huko uliko mama andjul,umepita kwenye magumu kwa ajili yangu.Amen
 
Ukifika hapa,elimu zetu, ajira zetu, starehe zetu na vyote tuvipendavyo havina thaman. Mama, ulioga mkojo wangu, ukajipaka kamasi zangu, ulikesha kuniangalia kama niko salama, mchana kila ulichofanya hakikukamilika bila kuchunguza usalama wangu. MUNGU PEKEE A AWEZA KUKULIPA, LKN MIMI SIWEZI. Mwanamke popote ulipo pokea heshima zangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom