Mama mwenye nyumba ananitaka

Mama mwenye nyumba ananitaka

Inaonyesha huheshimu ndoa yako na wala haumuheshimu mkeo kabisa, kuna mahali umesema kuwa tatizo ni mumewe tu tena kwa sababu mnaheshimiana. Hii ina maana ya kuwa wewe huna kikwazo, haujafungwa na kitu chochote, ndio kusema kama angekua sio mke wa mtu hata huu UZi usingeandika, ungetafuna tu maana mkeo si kikwazo katika hilo.
Kitu kingine nimegundua kaka unapenda sana mteremko ( kitonga) maana suala la mama kukusamehe pesa ya umeme umeliandika ukiwa unatabasamu.
Kumbuka ya kuwa unachojaribu kufanya kwa mke wa mwenzako na wako anaweza kufanyiwa hivyo hivyo. Pia katika suala kama hilo kabla ya kuangalia huyo mwanamke ameolewa au hajaolewa kwanza angalia wewe mwenyewe umeoa au haujaoa. Jifunze kuheshimu ndoa yako kwanza.
Nakusihi achana na huo mpango, tabia ya kuchepuka tu sio nzr lakini mbaya zaidi wewe unataka kuchepuka na mke wa mtu na kama haitoshi huyo mwanamke unakaa nae nyumba moja.
Uanaume una dhana pana kaka, sio tu kufungua fungua zipu kwa kila mwanamke.
Fikiria kuhusu mkeo, fikiria kuhusu heshima yako, fikiria kuhusu heshima ya ndoa yenu na zaidi fikiria kuhusu heshima iliyopo kati yako na baba mwenye nyumba.
Ukiona maji yamefika shingoni hama nyimba.
Hapo utakua umefanya maamuzi ya kiume.
Maneno ya kiume na yenye heshima kubwa yanafaa kuandikwa kwenye kuta ya dhahabu halfu uweke nyumban kwako wewe mwiz....
 
Umesema MAMA, yaani ni kama mama yako. Ogopa hii dhambi cheif em achana na kile kiroho kinachokwambie 'Sijui nimtafune tu'.
 
Dogo maisha magumu watu wanastress za maisha angalia zisije kukuishia wewe? Sio ujanja kula mke wa mtu ndugu yangu achana na hayo mawazo maana yanaweza kubadilisha historia ya maisha yako ghafla.
 
aisee, isije ikawa ndiye wewe kijana mpangaji wangu hapa kwangu. ngoja nianze kuwafuatilia. nakushauri uhame haraka kijana maana nikikukamata....
Ahahah
mkuu unaishi sehemu gani?
 
Yaani wewe una mukhofu mume wake tu? Hukhofu mungu? Humukhofii mkeo pia?
 
Wakuu
Hapa nilipopanga naona nimepata jaribu kubwa
Siku za hivi karibuni mama mwenye nyumba hapa amekuwa akinionesha dalili za wazi kabisa za kuhitaji huduma yangu licha ya yeye kuwa na muwe wake nami pia nina mke wangu

Baadhi ya viashiria nilivyovibaini mpaka sasa, kwanza ananitumia meseji zenye mitego sana yaani ata haziendani na umri wake...tunapokuwa nyumbani hapa unakuta tunapishana ananikonyeza

Zaidi hapa ndio nimeamini kabisa huyu mama ananitaka kwa namna yoyote ile leo hii, alikua anakusanya pesa Tsh 15000 kwaajili ya umeme lakini kaniambia kwa awamu hii ananilipia yeye, nami nikasema sawa na ninashukuru sana

wakuu hii dhambi naiona kabsa ila hofu ni huyo mme wake maana tunaheshimiana saaaana! Akijua sijui itakuaje, hapa naona uzalendo unakaribia kunishinda
hapa nahisi kapotea maana mi kwa tabia zangu za kitambo siwaachagi hawa, naona ananifuatilia saaana, soon mtaona manyoya wakuu

Nimeona tu niwape taarifa!
Nawasilisha
tutaona manyoya baada ya wewe kuliwa na mumewe.
 
Back
Top Bottom