Tigga Mumba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 746
- 474
Nawasalimia wana JF.
Nashukuru sana kwa kunipa ushauri kipindi kile nina matatizo na mchumba wangu. Nafurahi kuwa ushauri ulisaidia na nilishawafahamisha kuwa tunaelekea mipango ya ndoa.
Kitu kipya kimetokea ambacho kwa bahati mbaya sikuwashirikisha.,,, MAMA MKWE!!!!
Kwanza nianze kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya mchumba wangu alifiwa na wazazi wake wote wawili, amelelewa kipindi fulani na upande wa mama yake(mama mkubwa) na kipindi kirefu zaidi mpaka sasa na upande wa baba yake(baba mkubwa).
Huyu baba na mama(walezi wake) walijaaliwa watoto mabinti watatu. Baba ni mtu msomi sana, muelewa very diplomatic. Mama navyosikia katika ujana wake alikuwa mtu wa magumashi sana, mtu wa kujirusha. Mama ni mama wa nyumbani
Nitaenda specific kwa mama. Huyu mama ni MLEVI. Akinywa bia 2 tu hapakaliki. Anafanya vituko na fujo inafikia hatua mpaka baba anakasirika lakini mara nyingi sana huwa anamtuliza mkewe(ikiwezekana kumpigia magoti asifanye fujo).
Wale mabinti wa hao wazazi wote walisoma shule nzuri(Academy) na mchumba wangu alisoma shule za kawaida(kayumbas). Kwa bahati nzuri binti alijitahidi kusoma na kufaulu na wale wenzake kasoro mkubwa hawakufanya vizuri na ninaweza kuwa term as failures.
Sasa basi kipindi nafahamiana na mchumba wangu, binti mmoja wapo wa hiyo familia alitokea kunipenda. Mimi sikuwa na hisia zozote kwake so nothing happened.
Imetokea kuwa tangia nitangaze uchumba na issues za mahari na ndoa huyu mama amekuwa anaongea ovyo sana kwa watu wengine. Amekuwa na wivu kupindukia kwa mchumba wangu, kila akiongea na mimi(huyo mama) kazi ni kusema mabaya ya mchumba wangu, mara ana jeuri, mvivu, hajui kupika, etc etc.
Imefikia hatua huyu mama ameongea, "ngoja tuone sasa kama ndoa itafungwa". Kusema ukweli mimi simuelewi. Lengo lake haswa ni nini?
Mchumba wangu nimekaa nae muda mrefu, namjua weaknesses zake na strengths zake. Na bahati zaidi yeye ndiye alinifundisha/ananifundisha kupika. Mengine tunarekebishana.
Je huyu mama hawezi kuwa setback ya harusi yangu? Nifanyeje? Nimpotezee kabisa au niwe mnafiki?