Mama mkwe jamani msaada!

Mama mkwe jamani msaada!

Enyi wadada na wamama wa kileo,tufunge tumwombe Mungu atusaidie tuje kuwa mama wakwe wema wenye upendo wa kweli sio wa kinafiki.Naandika tu lakini nilishamwachia Mungu afanye anavyopenda yeye ila sasa ninazidi kuumizwa.

Hivi kina dada wa humu niambieni,wewe ukiwa na mimba huwa unamwambia mama mkwe? Yamenikuta sikusema ila hua naenda kusalimia wakwe zangu na tumbo wanaliona,sasa mama anasema why sijamwambia maana ndio nimejishaua tunaongea nae kwenye simu yuko mkoani nikajidai nimechoka ila this week ndio naweza kutua mzigo mama,looooh!!! najuta anashangaa kwani wewe ni mjamzito?mbona hujawahi kuniambia!

Niko mama sasa si hua unaniona jamani,anasema nilipaswa nimwambie. Mwenzenu hata mama yangu hua simwambii ananionaga tu tumbo hilo.

Ninachoshangaa ni mimba ya pili ya kwanza pia sikusema waliniona tu.Naumiaje sasa changanyia sipendwi na mama mkwe !Nimelia tu mwenyewe nimefuta machozi nimezama JF kujifariji!

Msiniponde maana mume ndo kashaniponda anasema nijitakia kulia kwani wewe ni mgeni na mama mkwe wako!wali sikuambii nyamaza na kilichokufanya umpigie ni nini?kaondoka akirudi namnunia live!!

Msimtukane mume wangu,nitaumia zaidi,sorry kwa mipaka.

PLEASE PRAY FOR MAMA WAKWE WOTE NA SISI PIA TUWE NA UPENDO WA KWELI!!inafsi ninaupendo sana na wakwe zangu,ni basi tu mama huwa ananikwaza sana.

Dada, hebu twende taratibu maana umeongea mengi hapa. Tuanze na "blue". Dada usiangalie upande mmoja tu wa mama mkwe, hebu angalia na upande wako je, umejiombea na unajiona una tabia ambazo hazimuudhi mama mkwe? Kumekuwa na tabia ya wanawake wengi kujijengea imani kuwa mamamkwe ni mbaya tu siku zote. Hawafikirii kuwa naye ni binadamu ana mapungufu yake na anatakiwa apate upendo sawa na ule wewe unaoutamani kutoka kwake.

"green" Dada ulipokuwa na mimba hukumwambia mama yako mzazi? Kwa nini usimtreat mamamkwe kama mama yako mzazi? Mama Mkwe wako angefurahi kama ungemshirikisha una mimba, yeye kama mama angeweza kuwa huru kuongea na wewe kuhusu mimba na kupanga mipango mbalimbali kabla ya mtoto hajazaliwa; hii haijalishi eti alikuwa anaona tumbo, kwa hiyo ulitaka yeye aanze kuongea na wewe kuhusu mimba yako kwa kuwa ameona tumbo?? kwa kutokumwambia ulimfanya afunge mdomo na ajisogeze pembeni maana hukutaka kumshirikisha kama ambavyo ungemshirikisha mama yako. Kumbe hii ni mara ya pili na hujajifunza tu kosa lako? Inaonekana hauko karibu hata na mama yako mzazi, pole ila ni vizuri hasa kwa kipindi cha mimba mama yako/mamamkwe ukawasogeza karibu.

Huna sababu ya kulia; jisogeze kwa mama zako. HAKUNA KAMA MAMA. jifunze katika hili tofauti na hivyo utajihesabu unachukiwa na mamamkwe na kuishia kulia kwa makosa yao uliyoyatengeneza mwenyewe. Bila shaka sijakuponda ila nimekwambia ukweli. ZINDUKA jijengee maisha na familia ya amani kwa mikono yako
 
pole mwaya. kama na wewe unamjua mkweo achana na kujikomba. ukishusha kitu muache mwanae aseme mama tumejaaliwa mtoto. ukimuona kaja mkenulie meno (mtori si ananunua mwanae, wewe inakuuma nini?)

Na umri wote huu, kumbe bado kuna vitu kibao vya kunishangaza.....

Hivi unamwambia mama mkwe habari za ya mimba ili iweje?? Yeye ni mtaalamu wa magonjwa ya akina mama kwamba atakuwa ndo consultant wako??

Wenye mimba wana raha na amani, kwa nini kijihangaisha na watu wengine??

Watu inabidi wajue kuwa ndoa ni ya watu wazima, labda kama wanataka kuendelea kudekezwa na wazazi!!

Babu DC!!!
 
Dada, hebu twende taratibu maana umeongea mengi hapa. Tuanze na "blue". Dada usiangalie upande mmoja tu wa mama mkwe, hebu angalia na upande wako je, umejiombea na unajiona una tabia ambazo hazimuudhi mama mkwe? Kumekuwa na tabia ya wanawake wengi kujijengea imani kuwa mamamkwe ni mbaya tu siku zote. Hawafikirii kuwa naye ni binadamu ana mapungufu yake na anatakiwa apate upendo sawa na ule wewe unaoutamani kutoka kwake.

"green" Dada ulipokuwa na mimba hukumwambia mama yako mzazi? Kwa nini usimtreat mamamkwe kama mama yako mzazi? Mama Mkwe wako angefurahi kama ungemshirikisha una mimba, yeye kama mama angeweza kuwa huru kuongea na wewe kuhusu mimba na kupanga mipango mbalimbali kabla ya mtoto hajazaliwa; hii haijalishi eti alikuwa anaona tumbo, kwa hiyo ulitaka yeye aanze kuongea na wewe kuhusu mimba yako kwa kuwa ameona tumbo?? kwa kutokumwambia ulimfanya afunge mdomo na ajisogeze pembeni maana hukutaka kumshirikisha kama ambavyo ungemshirikisha mama yako. Kumbe hii ni mara ya pili na hujajifunza tu kosa lako? Inaonekana hauko karibu hata na mama yako mzazi, pole ila ni vizuri hasa kwa kipindi cha mimba mama yako/mamamkwe ukawasogeza karibu.

Huna sababu ya kulia; jisogeze kwa mama zako. HAKUNA KAMA MAMA. jifunze katika hili tofauti na hivyo utajihesabu unachukiwa na mamamkwe na kuishia kulia kwa makosa yao uliyoyatengeneza mwenyewe. Bila shaka sijakuponda ila nimekwambia ukweli. ZINDUKA jijengee maisha na familia ya amani kwa mikono yako

Hapa ujumbe ni upi??

Sijaelewa kwa kweli...

Babu DC!!
 
Kwa mila zetu sio kitu cha kumwabia mtu wanaona tu tumbo likikua. hata ma mzazi akiona atafurahi lakini hatademand why u havent told her. tofauti na wenzetu wa magharibi ya wiki 2 itapigiwa ngoma hadi siku ta kujifungua atasema. wiki 2!!!!!. kwa hiyo ulivyofanya sioni tatizo.
 
yeye alinyamaza ila akajisemelesha. sijui alitaka mama mkwe amuuguze?
ndo hayo ya mamaz' gal, mimba itasimuliwa hadi style iliyoingilia mweeh!

afu weeh babu umenitapeli. ile issue aisee, nna mpango wa kujitwika mimba ya mapacha hapa ntakuacha ubungo, ohooo!
Na umri wote huu, kumbe bado kuna vitu kibao vya kunishangaza.....

Hivi unamwambia mama mkwe habari za ya mimba ili iweje?? Yeye ni mtaalamu wa magonjwa ya akina mama kwamba atakuwa ndo consultant wako??

Wenye mimba wana raha na amani, kwa nini kijihangaisha na watu wengine??

Watu inabidi wajue kuwa ndoa ni ya watu wazima, labda kama wanataka kuendelea kudekezwa na wazazi!!

Babu DC!!!
 
Bora kujinyamazia mpaka wajionee wenyewe maana kuna watu wana midomo inanuka laana hata kama ni ndugu zako so to me you are very right kaa kimya mpaka ajionee mwenyewe na kama yupo mbali mpatie taarifa za kujifungua na sio taarifa za mimba
 
Waambie bibie, wanaweza kufikiri ni tumbo la bia tu wakaona haya kukwambia ufanye mazoezi kulipunguza.

Kwani kuna ubaya gani kuwaambia?

Kama unaamua kuwa na mawasiliano nao kuwa na mawasiliano kikwelikweli, waambie.

Kama unawapotezea vile vile unawapotezea kijumlajumla, hata simu hawasikii mpaka junior anafanya birthday yake ya kwanza, wasije wakamdondoshea kichwa bure kwa gubu.

Imeandikwa hata "bwana" hawapendi wavuguvugu.
 
Na umri wote huu, kumbe bado kuna vitu kibao vya kunishangaza.....

Hivi unamwambia mama mkwe habari za ya mimba ili iweje?? Yeye ni mtaalamu wa magonjwa ya akina mama kwamba atakuwa ndo consultant wako??

Wenye mimba wana raha na amani, kwa nini kijihangaisha na watu wengine??

Watu inabidi wajue kuwa ndoa ni ya watu wazima, labda kama wanataka kuendelea kudekezwa na wazazi!!

Babu DC!!!

labda huyo mama ni mkunga au daktari!
 
yeye alinyamaza ila akajisemelesha. sijui alitaka mama mkwe amuuguze?
ndo hayo ya mamaz' gal, mimba itasimuliwa hadi style iliyoingilia mweeh!

afu weeh babu umenitapeli. ile issue aisee, nna mpango wa kujitwika mimba ya mapacha hapa ntakuacha ubungo, ohooo!

Yaani kazi tunayo....may be ndiyo process ya kuondoa tongo tongo kwenye macho...

Sikuwahi kumwona Bibi akimtangazia mtu kuwa kimenasa au anataraji boy au girl...

Ila issue bado tunachora master plan....muda ukifika tutakutumia details kwa courier.......usiwe na shaka kabisa!!

Babu DC!!
 
labda huyo mama ni mkunga au daktari!

Kama ni mkunga si angesubiri uchungu uanze??

May be, kosa la huyu mama ni tabia ya kujiongelesha ongelesha hata mambo ambayo si lazima mtu useme...

Ila nimeshangaa mtu ambaye kaona kitumbo hukooooooo....bado anataka breaking news!!

Hii dunia kwa vituko, haitakaa ifirisike kamwe....lol!!

Babu DC!!
 
Dada, hebu twende taratibu maana umeongea mengi hapa. Tuanze na "blue". Dada usiangalie upande mmoja tu wa mama mkwe, hebu angalia na upande wako je, umejiombea na unajiona una tabia ambazo hazimuudhi mama mkwe? Kumekuwa na tabia ya wanawake wengi kujijengea imani kuwa mamamkwe ni mbaya tu siku zote. Hawafikirii kuwa naye ni binadamu ana mapungufu yake na anatakiwa apate upendo sawa na ule wewe unaoutamani kutoka kwake.

"green" Dada ulipokuwa na mimba hukumwambia mama yako mzazi? Kwa nini usimtreat mamamkwe kama mama yako mzazi? Mama Mkwe wako angefurahi kama ungemshirikisha una mimba, yeye kama mama angeweza kuwa huru kuongea na wewe kuhusu mimba na kupanga mipango mbalimbali kabla ya mtoto hajazaliwa; hii haijalishi eti alikuwa anaona tumbo, kwa hiyo ulitaka yeye aanze kuongea na wewe kuhusu mimba yako kwa kuwa ameona tumbo?? kwa kutokumwambia ulimfanya afunge mdomo na ajisogeze pembeni maana hukutaka kumshirikisha kama ambavyo ungemshirikisha mama yako. Kumbe hii ni mara ya pili na hujajifunza tu kosa lako? Inaonekana hauko karibu hata na mama yako mzazi, pole ila ni vizuri hasa kwa kipindi cha mimba mama yako/mamamkwe ukawasogeza karibu.

Huna sababu ya kulia; jisogeze kwa mama zako. HAKUNA KAMA MAMA. jifunze katika hili tofauti na hivyo utajihesabu unachukiwa na mamamkwe na kuishia kulia kwa makosa yao uliyoyatengeneza mwenyewe. Bila shaka sijakuponda ila nimekwambia ukweli. ZINDUKA jijengee maisha na familia ya amani kwa mikono yako

Kwa kweli na Mungu ananiona,nampenda mama mkwe wangu na ninmheshimu sana,mimi ni mvumilivu sana sana,na nimwelewa mno na ninapenda kukoselewa,ni mwepesi kuomba msamaha na huwa sirudii kosa haswa nikionywa,ni mama tu na ninamjua ni mtat.Dada mi huwa naona aibu kusema nina mimba,ndio maana huwa naenda kuliko kusema,ndio udhaifu nilionao katika hilo,hata mama mzazi huwa simwambii anaona,atanitania tania,basi najua ameshajua.Pia mimba ya kwanza angeniambia hili lisingetokea ningesema mapema kweli yani, ok nimejifunza dada,sitarudia tena kosa hilo,ingawa ninaona watoto wawili wananitosha,nitaenda kuomba msamaha,yani mi nilikuwa naona si sawa kumwambia mama ninamimba.Asante mwaya.
 
Mi naona unadeka tuu hapa,kipi cha kukuliza hapo???
 
yeye alinyamaza ila akajisemelesha. sijui alitaka mama mkwe amuuguze?
ndo hayo ya mamaz' gal, mimba itasimuliwa hadi style iliyoingilia mweeh!

afu weeh babu umenitapeli. ile issue aisee, nna mpango wa kujitwika mimba ya mapacha hapa ntakuacha ubungo, ohooo!

Nilitaka ajue nategeme hivi karibuni!msaada mbona hata jirahi anakulea tu uzazi,wala sina wasiwasi kwa hilo!Thanks ndugu!!
 
relax sweeetie!
relaaax !
sio isssue kuuubwa kiiiihvyo!
usiniumizie mamdogo bure !
relaaax!
sawa?
na hubbie akija wala usinune!
kwanza mara ya mwisho umeongeza njia lini?(nizoee tu ndo akili yangu ilivyo nikiwa naongea pwenti):wink:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom