Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Umedate na wangapi?
Ukute hata wa5 hawafiki ila mnakuja waingiza wachagga wote kwenye hizo tabia .

This is not fair.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Mbona povu Sana, that's how I see it and that's my experience,mambo ya Umedate na wangap na it's not fair so what. Usiforce tufanane kama we unaamin otherwise it's all good too. It's the truth of your reality so sio issue Sana.
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Pole ,mchaga mwenzangu
 
Pole sana dada angu jipe moyo utashinda
Ila sisi wamakua tuna maumivu makubwa na wachaga Tena makubwaaaaaaaaa
 
As long as jamaa hatajatetereka, endeleeni na mchakato wenu, lakini kamwe usije kuonesha chuki ya waziwazi kwa mamako mkwe.
 
Mbona povu Sana, that's how I see it and that's my experience,mambo ya Umedate na wangap na it's not fair so what. Usiforce tufanane kama we unaamin otherwise it's all good too. It's the truth of your reality so sio issue Sana.
Aisee,hilo swali wewe umeliona povu?
Ungelijibu tu boss.

Pengine uliangukia kwa wachaga wasumbufu lakini sidhani kama wachaga wote ni wasumbufu.
 
Habari zenu wapendwa?

Mwenzenu na matatizo sielewi nichukue uamuzi gani naombeni mnishauri wapendwa, nilianza mahusiano na mkaka wa kimakuwa toka 2016 kiukweli ananipenda sana na Mimi nampenda na Mungu ametujalia mwaka Jana mwezi wa 12 kapeleka mahari kwetu akanivalisha na Pete ya uchumba.

Baada ya hapo wakualiana na wazazi harusi iwe mwezi wa 4 mwaka huu Ila baada ya muda mama yake akamwambia naomba harusi mfanye mwezi wa 7 nataka nijipange sherehe iwe kubwa tukamkubalia kupeleka hadi wa 7 Ila Cha kushangaza juzi kipindi wamekaa kwenye kikao Cha kuandaa kamati ya harusi mama mtu akasema harusi isogezwe tena iwe mwezi wa 10

Baada ya mwanae kumbana mama yake kuwa kwanini kila cku unapeleka mbele akamwambia sitaki uowe mwanamke wa kichaga ndomana nafanya hivi, kiukweli mwanae alichukia sana kuskia hiyo kauli akanipa mrejesho kuwa mama yake hataki anioe kisa mimi mchaga Ila kwakuwa nakupenda tumeshirikiana mambo mengi siwezi kukuacha tutafunga ndoa mwezi wa 8 bila hata ndugu zake kuwepo atasimamia shoo mwenyewe bila msaada wa ndugu zake nikamwitikia sawa

Ila hapa nawaza usikute huu uamuzi ameuchukua sababu ya hasira nahisi Kama akitulia atanibadilikia asikilize ndugu zake aniache na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nimetoka naye mbali kanipotezea muda na hivi kapeleka hadi mahari kwetu watu wanasubiri harusi.

Kama akinibadilikia sijui hii aibu tutaibebaje na familia yangu, nimechanganyikiwa mpaka nawaza sijui nimbebe tu mimba ili azidi kuwa na msimamo aogope kupoteza mke na mtoto!,

Ila nakosa jibu huyu mama simuelewi kwanini ananifanyia hivi Kama alikuwa hataki niolewe na mwanae kwanini hakumzuia kipindi anapeleka mahari wakamsapoti apeleke, kinachoniumiza ni aibu kwetu mahari imeenda alafu ikitokea tukiachana kisa mama yake aibu itakuwa kubwa Bora hata angekuwa hajapeleka mahari.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyaje kulishinda hili jaribu lililopo mbele yangu, Ndugu zangu Bado sijawambia Kama Kuna huu mgogoro maana hata sijui watalipokeaje nachanganyikiwa Mimi jamani
Mimi mtoto wangu akisema tu anamchumba mchaga na ataitaj kumuona tamkubalia ila lazima nimtoe kwenye usimamiz wa Mali zangu zote mana wachaga nawajua
 
Dada..hebu achana na huyo mwanaume. Utachukiwa na ukoo mzima na hutakuwa na furaha. Usiingie kwenye ndoa kama wazazi wa mwanaume wamekukataa.
Lkn maamuzi ni yako..
 
Hapana mama ndoana tatizo na Mimi niliwaza mwanzo mama wewe Ila Kuna wakati waligombana sana kisa hili swala na Mimi nilimsikia mama mwenyewe simu ilikuwa na sauti na sahivi mtoto wake naye kachanganyikiwa haelewi afanyaje Mimi ndo inanibidi tena nimtie moyo
Sepa wewe...unajitafutia matatizo
 
Acha tu ni aibu najiuliza kwanini aliacha mahari ipelekwe ingekuwa haijapelekwa pengne ningepata ujasiri wa kumuacha Ila wazazi wangu ni watu wa heshima sana hili swala litawachanganya sana pia itakuwa aibu ambayo haijawahi tokea kwetu ndomana nachanganyikiwa
Ni afadhali kupata aibu ya mara moja kuliko maisha unayotaka kwenda kuishi. Waelekeze wazazi wako hali halisi wakushauri.
Kumbuka ndoa ni yako si ya mtu mwingine.
.
.
Ingekuwa mimi ni wewe ningekubali matokeo. Jiamini.. utapata mume mwingine na utajishangaa kwanini ulikuwa ukimng'ang'ania huyu mtoto wa mama
 
Kama mama mkwe akupendi usiolewe hutakaa kwa Amani kwenye iyo ndoa subiri kwanza na uwaambie wazazi wako ukweli watakua Cha kufanya Tena usije kubeba mimba ukadhani mwanaume ndo hatokuacha mwanzoni mwanaume atakua benet na wewe ila itafika mahali atakua upande wa mamaake tu lazima mama na mtoto wana bond
 
Pole sana dada , Kama anayekukataa ni mtu mmoja ( mama) ,mi nafikiri sio sana , Kama ingekuwa familia nzima hapo ndio ingekuwa tatizo , kwa hiyo olewa Tu bibie, kila la heri
 
Miss Chuga mdogo angu;
1. Ni wanaume wachache sana ambao wanaweza wakaamua kwenda kinyume na wazazi wao, especially mama zao. Wanawake tukipenda huwa tunaforce kivyovyote huko nyumbani hadi mchumba atakubaliwa, wakibisha sana tunabeba mimba au tunahamia kwa mwanaume bila ndoa, maisha yanasonga. Ila hawa wenzetu, atakaloliamua mama mkwe mara nyingi ndiyo linakuwa final say. Usijiaminishe sana kwamba mchumba wako ana msimamo sana na hautobadilika. Nina rafiki angu Mmachame yalimkuta kama yako, mwisho wa siku mchumba akamwambia mimi siwezi kuendelea na mipango ya ndoa bila wazazi wangu. Ila Mungu sio wakwe, alikuja akaolewa zake na mtu mwingine na yupo anadunda na ndoa yake. (Hopefully wa kwako atapambana hadi mwisho)

2. Kamwe usije ukaungana na mtoto wa mama mkwe kwenda kinyume na mama mkwe; huo utakuwa ni ugomvi wa maisha, na ikiwezekana ugomvi utaendelea hadi kwa watoto wako (ya Hamissa na Mama Diamond). Yes kuna muda wazazi wanazingua, but still tunahitaji baraka zao, hata kama watazitoa kinafki na kuja kujumuika nanyi kwenye sherehe yenu. Usikubali kufunga ndoa na huyo mchumba wako kama wazazi wake hawajaridhia. Yeye anachotakiwa kufanya ni kuwalainisha na kuwaelewesha huko nyumbani kwao hadi waje wakubali. Usishindane na mama mkwe; kesho watapatana na kijana wake ila wewe ndiyo utabaki kuwa adui yake.

Naweza kukuelewa unajisikiaje, aibu unayoiwazia, kuchekwa na kuchambwa na wananzengo, bado muda wako na upendo ulioinvest kwenye hayo mahusiano, labda unaona na umri umeshaenda aisee inaumiza sana. Lakini pamoja na yote hayo, ikitokea imeshindikana kufunga hiyo ndoa; lia mshukuru Mungu kwa yote. Na usije ukakaa unajilaumu sijui ukaharibu maisha yako kisa umeachwa; hujafanya kosa lolote la kukufanya uachike: wewe kuzaliwa mchaga sio kosa wala sio dhambi na huwezi kubadili kabila lako ili kuwaridhisha wakwe. Kuvunjika kwa uchumba sio mwisho wa maisha

Imagine ukiforce hiyo ndoa, utaishi maisha ya aina gani na wakwe zako? Usije ukajidanganya kwamba labda mtaishi mbali na wakwe zako so ni sawa tu; mdogo angu hao ndugu mtawahitaji tu, na watoto wako watawahitaji hao ndugu wa baba zao pia.

Na usijidanganye kubeba mimba, kwa sababu unaweza kubaki single mom, ndoa isifungwe na hata huyo mtoto wako wasiwe na habari naye. Acha mambo yaende naturally, muache mchumba wako apambane hadi kieleweke. Ikishindikana basi mama, wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kuvunja uchumba, na wakati mwingine ni bora kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa. Familia nyingine unaenda kujipa mateso tu.

Muombe Mungu, mapenzi yake yatimizwe kwenye huo uchumba wenu. Litakalotokea lolote, kubaliana nalo then mshukuru Mungu. Yeye anakuwazia mema siku zote, na anaijua kesho yako.

Na nyie wanaume muulizage mapema kwa mama zenu, wawaambie hawataki muoe kabila gani: sio unakaa na mtoto wa mtu miaka 5 afu ndiyo mama mkwe anakuja "sitaki mchaga sijui mnani". Afu alivyokosa huruma eti aliruhusu kabisa utolewe mahari. Mungu amsamehe, hiyo mbegu isije ikamea kwa mabinti zake.

Ukiona linakuchanganya sana, washirikishe ndugu zako. Usije ukadondoka kwa presha bure. Mungu na akutetee

Mimi ni mmoja wa mashabiki wako hapa jf wewe Heaven Sent! Napenda sana uandishi wako na maoni yako kwenye mijadala serious kama hii!

Unajua kunaweza kukawa na utofauti mkubwa sana wa kitu mtu anacho andika humu na anacho kiishi lakini trust me wewe ni mmoja ya watu ambao mimi hutafuta maoni yao kwenye mijadala serious kama hii na huwa naishia kuunga mkono tuu kwakweli kwakuwa huwa una maliza kila kitu!

Umemsaidia sana huyu dada kama atakuwa serious kukusoma
Wengi hapa watamdanganya mapenzi ni ya wawili lakini wewe umemwambia ukweli mchungu sana ni lazima aujue lakini baadae atashukuru!

Kama huyo binti hatokuelewa kwenye uliyo yaandika basi......

Ubarikiwe sana...
 
Bora umejua mapema na huyu mkaka aoe kwengine, huyo mama angekusumbua sana kwenye ndoa yako na inavyonekana huyo mwanaume anamsikiliza mama yake zaidi,bora umejua mbichi na mbivu mapema, ndoa yako ingekua ngumu sana

Hakuna mwanaume hapa Tanzania asiyemsikiliza Mama yake hayupo hYupo hayupo
 
Wow, this means a lot to me.

Ujue bana mama mkwe akishaweka kimgomo; bila neema ya Mungu hamtoboi. Laini ni mtihani pia kwa kijana, imagine anataka aoe akiwa na baraka za wazazi wake, afu mzazi anagoma kukupa baraka zake hata kishingo upande tu. Utaendelea na ndoa bila wazazi? Mungu atuepushie

Mimi ni mmoja wa mashabiki wako hapa jf wewe Heaven Sent! Napenda sana uandishi wako na maoni yako kwenye mijadala serious kama hii!

Unajua kunaweza kukawa na utofauti mkubwa sana wa kitu mtu anacho andika humu na anacho kiishi lakini trust me wewe ni mmoja ya watu ambao mimi hutafuta maoni yao kwenye mijadala serious kama hii na huwa naishia kuunga mkono tuu kwakweli kwakuwa huwa una maliza kila kitu!

Umemsaidia sana huyu dada kama atakuwa serious kukusoma
Wengi hapa watamdanganya mapenzi ni ya wawili lakini wewe umemwambia ukweli mchungu sana ni lazima aujue lakini baadae atashukuru!

Kama huyo binti hatokuelewa kwenye uliyo yaandika basi......

Ubarikiwe sana...
 
Hata mimi toka nasoma naanza kujitambua niliambiwa na mama angu mwanangu usije ukaja kuoa mchaga .hii kauli hadi leo mama ananisihi nisioe mchaga juzi tu hapa aliniambia tena...hata mie nimeyaona haya wachaga wanayoambiwa ..hili kabila wengi wapo upande pesa kuliko utu
 
hii kauli wameambiwa wabongo wengi tu, japo wengine indirect ila siku zote usipotaka kuoa kabila fulani iwe kwa kuambiwa au kwa kutokutaka mwenyewe, basi epuka kuingia katika mahusiano nao, wengine walianza kwa lengo la kutafuna tu( kama jinsi tunavyoishi mjini) ila wakajikuta wananogewa na hatimae wakaoa. . . usithubutu kudate na mtu kwa minajili ya kuonja tu, watu hutofautiana sana
 
Hili kabila kuna watu walifanya matatizo na kuwapa sifa vizazi vyao kwa kweli demu wa kichaga hata wachaga wenyewe baadhi wanatengana hawapendani wanaangalia huyu anatokea wapi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom