Mama mkwe hataki kunirudishia mwanangu, nifanyeje?

Mama mkwe hataki kunirudishia mwanangu, nifanyeje?

Rafiki Mr. Kyaka Mtoto HUWA AGOMBANIWI. Jua atakufa tena kifo cha ghafla. Fuatilia..... Acha akae kwa anayemng'ang'ania. Subiri akikua atakuja. Take my words. FREE ADVICE.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ulilofanya ni ujinga!
Unajua unaweza kushtakiwa kwa child abduction hata kama mtoto ni wako?
Mtoto ni wa mama hadi afikishe miaka 18 ndio unaweza kuclaim OWNERSHIP.
As for kubaki naye au kumregesha, ningekushauri umregeshe hili kuwaonyesha kwamba you keep your word.
Mtoto kama anasoma usimwuusishe katika masuala yako na mkeo. Huenda yakawa na effect kwa self-esteem yake.

QUIZ. Uko tayari kuwa single parent?
mimi ndie ninaemsomesha mkuu hiyo shule aliyopo kwasasa na mm pia ndo naweza kuamua ni shule ipi nimpeleke kwahiyo sioni sababu ya wao kuzuia mtoto nisimtafutie shule yenye elimu bora zaidi
 
Wew si umeambiwa uende? Shida iko wap? Nenda mwenyew ukamchukue mwanao.

sikuambiwa kwenda kabla na ndo maana sikufanya hivo na isitoshe niliiagiza akamchukue mtoto ni ndugu yake na ukweni wa zaman wote wanamtambua huyo aliyetumwa
 
Wewe ndo una matatizo
watu wanakutunzia mwanao hata kwenda tu kuwaona shida
unatuma watu kwani huyo mbuzi?

nenda ukasikie wanataka kukuambia nini..
watu wazima wakikuita ujue kuna kitu
mimi huwa nakwenda huko mara kwa mara na mtoto huwa namhudumia km kawaida ingawa nilikuwa na muda km miez km mitatu sijakwenda kutokana na kubanwa na majukum ya kikaz na pia niko mbali
 
Wew si umeambiwa uende? Shida iko wap? Nenda mwenyew ukamchukue mwanao.
ndio mkuu hakukuwa na ugomvi kabisa na isitoshe mtoto alikuwa anakuja matembez ya kawaida ya wk end kiltichonishtua ni kuanza kumzuia hata asije kuniona tu na wakati hata huduma za mtoto huwa natoa bila kuonana nao mara nyingine
 
Unatumia nguvu nyingi kumchukua mwanao.
Situmii nguvu mkuu ila mimi nilitaka mtoto nimuweke kwenye mazingira ambayo ni huru ili kila mzazi amuone bila masharti maana naona mm nazuiwa kuwa na mwanangu pindi ninapomuhitaji wakati mm ndo nawajibika kwa kila kitu
 
Rafiki Mr. Kyaka Mtoto HUWA AGOMBANIWI. Jua atakufa tena kifo cha ghafla. Fuatilia..... Acha akae kwa anayemng'ang'ania. Subiri akikua atakuja. Take my words. FREE ADVICE.
Kifo kipo kwa kila mtu hizo ni iman tu ndugu yangu,hakuna anaemgombania mtoto ila natafuta kumuweka mazingira ya kuonana na wazaz wote bila upande mmoja kujiona wao ndo wana mamlaka zaid
 
Last edited by a moderator:
Ingekuwa busara zaidi ungekuja kuomba ushauri humu wakati wa hujaamua kumuiba mtoto japokuwa ni wako. Kingine katika hali ya kawaida ulitakiwa uende mwenyewe moja kwa moja kumchukua mtoto kwa bibi yake na si kumwagiza mtu hata kama ingekuwa mimi ningemnyima huyo uliyemwagiza.

JITAHIDI KUJENGA UHUSIANO MWEMA NA FAMILIA YA WAKWEO WA ZAMANI, WAHESHIMU HATA KAMA UMEACHANA NA MTOTO WAO; KWA MAANA ITAKULAZIMU KUOMBA MSAMAHA KWA KUMKWAPUA MJUKUU WAO BILA IDHINI YAO VINGINEVYO UTAKAA NAE KUANZIA SASA NA UHUSIANO WAKO NA WAKWEO WA ZAMANI UTAKUWA MBAYA ZAIDI.
Uhusiano uliopo kati yangu na wao ni mwanetu sasa kama hawataki mi niwe karibu na mtoto mojakwamoja uhusiano wetu na wao hauwez kuwa mzur
 
Wakwezo huwaheshimu hivyo,je huyo mkeo ilikuwaje?
Kwa kawaida heshima huwa inakuwepo pindi na wewe unapoheshimiwa kama ukitokea upande mmoja hauheshimu upande mwingine hapo ndo tatizo linapoanzia, katika mahusiano lazima pande zote ziheshimiane mkuu
 
Situmii nguvu mkuu ila mimi nilitaka mtoto nimuweke kwenye mazingira ambayo ni huru ili kila mzazi amuone bila masharti maana naona mm nazuiwa kuwa na mwanangu pindi ninapomuhitaji wakati mm ndo nawajibika kwa kila kitu

Mwache mtoto kwa bibi yake malezi si rahisi ka ufikiriavyo mwishowe umu affect kisaikolojia bure kuanza kulelewa na watu asio wazoea
 
Hapo kama kudharaulika ushadhaurika sana kama kuombewa mabaya uliombewa sana, kama mbwai mbwai tumepitia huko komaa na mtoto wako usimrudishe mama mkwe hana adabu. Kwnn mkubaliane then atengue makubaliano yenu hapo ndipo ninaposema ulishadhaurika sana...
 
Mwache mtoto kwa bibi yake malezi si rahisi ka ufikiriavyo mwishowe umu affect kisaikolojia bure kuanza kulelewa na watu asio wazoea
malezi sio suala la mazoea dada km ni tusingekuwa tunapeleka watoto shule za bwen kwa hofu ya kumbadilishia mazingira!kinachotakiwa katika malezi ni kumfanya mtoto aelewe lipi baya na lipi jema ninapolifanya pia kumuonyesha upendo km mzaz au mlezi pia kumkosoa pale anapotenda kinyume
 
hivi unaomba ushauri au vipi? mbona unapewa ushauri mzuri lakini naona tena kama unawabishia washauri!
anywei, majibu na final say unayowewe ukiona umeamua vyema sawa.
kwa sisi wengine usifanye kosa linalofanana na hilo. from my experience
 
Wewe ndo una matatizo
watu wanakutunzia mwanao hata kwenda tu kuwaona shida
unatuma watu kwani huyo mbuzi?

nenda ukasikie wanataka kukuambia nini..
watu wazima wakikuita ujue kuna kitu

Safi sana , kama ana akili atasikia. Mama Mkwe akuleleemtoto hata kumsalimia , hata service unaishia kupiga simu kuwa mtotoatachukuliwa kama parcel. Anaonyesha hata adabu kwa wakubwa ni ndogo.

Mimi ningemshauri amrudishe mtoto kwanza kuepuka kumpa mtotomatatizo ya kisaikolojia kwa kumuhamisha ghafla. Pili mtoto anatakiwa aandaliwekidogo kidogo kiakili kuwa karibu atarudi kwa baba siyo kumchukua vaaaap. TAtu na la msingi ni yeye kufanya frequentvisit kwa mama mkwe kama tendo la shukrani na kumuona huyo mtoto anaendeleaje.Jamani kuna vitu vya kutuma watu ila sio mambo ya kifamilia hata kama upomkoani? Huwezi kutenga masaa machache kwenda kumuona mtoto? Tena ukifika ukaombe msamaha mkubwa huwezikuwakosea heshima watu wazima kama hivi.
 
Niliachana na mke wangu mwaka jana kwa sababu zisizozuilika . Tumezaa mtoto mmoja wa kike ambaye kwa sasa ana miaka saba. Baada ya kuachana na mke wangu nilimuomba mama mkwe mwanangu abaki nae mpaka January mwakan ndo nitamchukua rasmi, lakini cha kushangaza kila nikimwambia mama mkwe suala la kumchukua mwanangu anakuwa hanyooshi maelezo,. Mara anasema ashauriane kwanza na babu yake, mara mtoto huku anasoma n. k. yaan kwa ufup tu anakuwa na vijisababu vingi vingi.

Juzi nilimpigia mama mkwe simu kuwa nina hamu na mwanangu, kwa hiyo Jumamosi nitamtuma ndugu yangu akamchukue, mama mkwe akakubali. Leo nikamtuma ndugu yangu akamchukue, kufika pale mama mkwe akamwambia hawezi kumpa mpaka mimi mwenyewe niende. Kumbukeni juzI nilishampigia mama mkwe simu na nikamwambia mpaka mtu atakayeenda kumchukua akasema sawa.

Kwa kweli nilipata hasira sana kwanini nina hamu ya kumuona mwanangu halafu mama mkwe anaweka ugumu!? Nimempigia simu kumuuliza kwanni amekataa na mtoto amesema hadi ampe taarifa babu yake maana hayupo amekwenda msibani. Baada ya kuona ananizungusha sana na nilimpa taarifa mapema nimeamua niende shuleni kwa mtoto nikamchukua kisha nikawapa taarifa wasimtafute mtoto mimi ndo nimemchukua.

Nilipanga aje anisalimie tu na kesho nimrudishe, sasa je kesho nimrudishe kama nilivyopanga au nisimrudishe tena? January nilipanga kumchukua jumla, sasa nahisi kama nikimrudisha tunaweza kuanza kuzungushana tena na nitakapomhitaji tena wanaweza kumficha au kumtorosha.

Naombeni ushauri tafadhali..
Kiugwana ungekwenda mwenyewe ukasalimia ukamchukua mwanao wasinge kunyima hata kama walikua wamepanga kukunyima lakini kitendo cha wewe kutokea ingesaidia sana, naomba niulize huyo ni mtoto wa kike naamini kua wewe unafanya kazi huyo mtoto atakaa nanani? ningekua mimi nadhani chamsingi nikuhakikisha mtoto anapata malezi bora na jaribu kutumia mda wako mwingi kua na mtoto wako uongeze mawasiliano na mtoto mda ukifika utamchukua,na hata kama unafikiria Bording school mtoto ni mdogo sana .huo niushauri tuu maamuzi ni yako......
 
Kifo kipo kwa kila mtu hizo ni iman tu ndugu yangu,hakuna anaemgombania mtoto ila natafuta kumuweka mazingira ya kuonana na wazaz wote bila upande mmoja kujiona wao ndo wana mamlaka zaid
Kama uliyataka hayo ungemvumilia mama yake.
 
Back
Top Bottom