Mama mkwe hataki kunirudishia mwanangu, nifanyeje?

Mama mkwe hataki kunirudishia mwanangu, nifanyeje?

mr kyaka

Senior Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
193
Reaction score
53
Niliachana na mke wangu mwaka jana kwa sababu zisizozuilika . Tumezaa mtoto mmoja wa kike ambaye kwa sasa ana miaka saba. Baada ya kuachana na mke wangu nilimuomba mama mkwe mwanangu abaki nae mpaka January mwakan ndo nitamchukua rasmi, lakini cha kushangaza kila nikimwambia mama mkwe suala la kumchukua mwanangu anakuwa hanyooshi maelezo,. Mara anasema ashauriane kwanza na babu yake, mara mtoto huku anasoma n. k. yaan kwa ufup tu anakuwa na vijisababu vingi vingi.

Juzi nilimpigia mama mkwe simu kuwa nina hamu na mwanangu, kwa hiyo Jumamosi nitamtuma ndugu yangu akamchukue, mama mkwe akakubali. Leo nikamtuma ndugu yangu akamchukue, kufika pale mama mkwe akamwambia hawezi kumpa mpaka mimi mwenyewe niende. Kumbukeni juzI nilishampigia mama mkwe simu na nikamwambia mpaka mtu atakayeenda kumchukua akasema sawa.

Kwa kweli nilipata hasira sana kwanini nina hamu ya kumuona mwanangu halafu mama mkwe anaweka ugumu!? Nimempigia simu kumuuliza kwanni amekataa na mtoto amesema hadi ampe taarifa babu yake maana hayupo amekwenda msibani. Baada ya kuona ananizungusha sana na nilimpa taarifa mapema nimeamua niende shuleni kwa mtoto nikamchukua kisha nikawapa taarifa wasimtafute mtoto mimi ndo nimemchukua.

Nilipanga aje anisalimie tu na kesho nimrudishe, sasa je kesho nimrudishe kama nilivyopanga au nisimrudishe tena? January nilipanga kumchukua jumla, sasa nahisi kama nikimrudisha tunaweza kuanza kuzungushana tena na nitakapomhitaji tena wanaweza kumficha au kumtorosha.

Naombeni ushauri tafadhali..
 
sasa shida yako mtoto wako keshafik kwako unatak umrudishe ten wp? baki naye mkuu
 
Wew si umeambiwa uende? Shida iko wap? Nenda mwenyew ukamchukue mwanao.
 
Wewe ndo una matatizo
watu wanakutunzia mwanao hata kwenda tu kuwaona shida
unatuma watu kwani huyo mbuzi?

nenda ukasikie wanataka kukuambia nini..
watu wazima wakikuita ujue kuna kitu
 
Ingekuwa busara zaidi ungekuja kuomba ushauri humu wakati wa hujaamua kumuiba mtoto japokuwa ni wako. Kingine katika hali ya kawaida ulitakiwa uende mwenyewe moja kwa moja kumchukua mtoto kwa bibi yake na si kumwagiza mtu hata kama ingekuwa mimi ningemnyima huyo uliyemwagiza.

JITAHIDI KUJENGA UHUSIANO MWEMA NA FAMILIA YA WAKWEO WA ZAMANI, WAHESHIMU HATA KAMA UMEACHANA NA MTOTO WAO; KWA MAANA ITAKULAZIMU KUOMBA MSAMAHA KWA KUMKWAPUA MJUKUU WAO BILA IDHINI YAO VINGINEVYO UTAKAA NAE KUANZIA SASA NA UHUSIANO WAKO NA WAKWEO WA ZAMANI UTAKUWA MBAYA ZAIDI.
 
Shida ako si mtoto? Ushamchukua umrudishe wa nini tena? Au unaenjoy kuzungushana na huyo mkweo
 
Kwanini wewe hutaki kwenda, wewe si ndiye uliyeomba akusaidie kumtunza mwanao
 
Ustaarabu ungekwenda kuonana na Mama mkwe na kumpa asante baada ya hapo unamweleza unachohitaji sidhani kama mngezungushana kama ilivyo sasa. Hata kama mtoto yupo kwako sasa nenda onana na mkweo
 
Walikubali kumlea mwanao, leo unaenda kum'beba kuhuni tu. Kwanza pia unamchanganya mtoto kisaikolojia. Mtoto ana haki pia za kuwaaga babu, bibi, ndugu na marafiki zake. Unazingua Chief.
 
Wewe ndo una matatizo
watu wanakutunzia mwanao hata kwenda tu kuwaona shida
unatuma watu kwani huyo mbuzi?

nenda ukasikie wanataka kukuambia nini..
watu wazima wakikuita ujue kuna kitu
I dont have a like button.
Vijana wa siku hizi tuna tabu kweli. Jamaa anamuagizia mtoto
 
Wewe ndo una matatizo
watu wanakutunzia mwanao hata kwenda tu kuwaona shida
unatuma watu kwani huyo mbuzi?

nenda ukasikie wanataka kukuambia nini..
watu wazima wakikuita ujue kuna kitu

Majibu yote yapo hapa.
Kwa kuongezea hata kama mama mkwe anahudumia mtoto si unajua kuna baba mkwe? Hivi anawasiliana nae kuhusiana na mtoto au ndio dharau???
 
Kwa ulilofanya ni ujinga!
Unajua unaweza kushtakiwa kwa child abduction hata kama mtoto ni wako?
Mtoto ni wa mama hadi afikishe miaka 18 ndio unaweza kuclaim OWNERSHIP.
As for kubaki naye au kumregesha, ningekushauri umregeshe hili kuwaonyesha kwamba you keep your word.
Mtoto kama anasoma usimwuusishe katika masuala yako na mkeo. Huenda yakawa na effect kwa self-esteem yake.

QUIZ. Uko tayari kuwa single parent?
 
duuh mtoto anathaman kubwa..unajisikia raha ukiwa karibu nae..!!
 
Mkuu naanza kupata wasi wasi kuwa utakuwa usha
likoroga huko former ukweni sasa hutaki hata waione
sura yako.
Mlinde mtoto dhidi ya madhara ya kisaikolojia yanayoweza kuja
mpata kutokana na uamuzi wako.
 
Iinawezekana mtoto sio wako umepigwa bambi kapime DNA
 
Punguza ghadhab.

Wewe si ulimchukulia mwanae? Na yeye kakuchukulia mwanao.

Bila - Bila.
 
Niliachana na mke wangu mwaka jana kwa sababu zisizozuilika . Tumezaa mtoto mmoja wa kike ambaye kwa sasa ana miaka saba. Baada ya kuachana na mke wangu nilimuomba mama mkwe mwanangu abaki nae mpaka January mwakan ndo nitamchukua rasmi, lakini cha kushangaza kila nikimwambia mama mkwe suala la kumchukua mwanangu anakuwa hanyooshi maelezo,. Mara anasema ashauriane kwanza na babu yake, mara mtoto huku anasoma n. k. yaan kwa ufup tu anakuwa na vijisababu vingi vingi.

Juzi nilimpigia mama mkwe simu kuwa nina hamu na mwanangu, kwa hiyo Jumamosi nitamtuma ndugu yangu akamchukue, mama mkwe akakubali. Leo nikamtuma ndugu yangu akamchukue, kufika pale mama mkwe akamwambia hawezi kumpa mpaka mimi mwenyewe niende. Kumbukeni juzI nilishampigia mama mkwe simu na nikamwambia mpaka mtu atakayeenda kumchukua akasema sawa.

Kwa kweli nilipata hasira sana kwanini nina hamu ya kumuona mwanangu halafu mama mkwe anaweka ugumu!? Nimempigia simu kumuuliza kwanni amekataa na mtoto amesema hadi ampe taarifa babu yake maana hayupo amekwenda msibani. Baada ya kuona ananizungusha sana na nilimpa taarifa mapema nimeamua niende shuleni kwa mtoto nikamchukua kisha nikawapa taarifa wasimtafute mtoto mimi ndo nimemchukua.

Nilipanga aje anisalimie tu na kesho nimrudishe, sasa je kesho nimrudishe kama nilivyopanga au nisimrudishe tena? January nilipanga kumchukua jumla, sasa nahisi kama nikimrudisha tunaweza kuanza kuzungushana tena na nitakapomhitaji tena wanaweza kumficha au kumtorosha.

Naombeni ushauri tafadhali..

Yaan kitendo cha kuachana na mkeo umeonyesha udhaifu Mkubwa sana hutaweza kumlea huyo mtoto Wa kike wakwe zako wameliona hilo. Inaonyesha unatamani kukaa na mtoto wako ila kulea huwezi kwa ufupi mrudie mkeo mmalize tofauti zenu mtoto wako atakua salama
 
mi naona unakwepa majukumu, ulipanga kumchukua january!! haya umemchukua leo si tatizo ! vipi unataka umrudishe tena au unavyompigia ma mkwe unapata raha labda atakuambia msameheane mrudiane ebooo
 
Back
Top Bottom