Mama mkwe amegeuka kero kwenye ndoa yangu

ASANTE NYANI NGABU nisaidie nifanye nini?

Naamini hilo liko ndani ya uwezo wa mumeo, (wifi zako au baba mkwe ikiwa wanaelewa kiini cha hayo yote). Mumeo ni mtu muhimu ktk kukata mzizi wa fitna hii, ikiwa si muoga wa kumkabili mamake.
Jadili na mumeo, akisimama kama mume kikweli kweli, hiyo ni vita ndogo sana, ni kama kuzima mshumaa, hata mtoto mdogo anaweza!
 
Muhimu kwako ni kujua mtazamo wa mumeo, kama na yeye anaungana
na mama yake nafikiri ni muhimu na wewe sasa kuwa mjeuri, mkali na kuonyesha
dharau ya wazi s'times upole wako ndo unakufanya akuonee. Ukiona hicho kitu
kinaendelea na mumeo anaunga mkono anza kumuwekea sukari kwenye mboga,
chumvi kwenye chai siku nyingine hata upupu kwenye maji bila shaka utakuwa
umetibu tatizo. DAWA YA MOTO NI MOTO.
 
Nafikiri ni wakati sasa tuwe na ujasiri wa kuwaface watu wanaotuletea kero kama hizo kujua tatizo ni nini na wapi unakosea badala ya kuishia kulalamika. Umeshafuga matatizo mengi kiasi kwamba hujui uanzie wapi. Sio mbaya, jaribu kuanza kumweka karibu mkweo.. Mchukulie kama mama yako mzazi na tafuta siku mtoke pamoja na huko unaweza kumwomba msamaha na kuongea nae vizuri akwambie wapi unamkosea. Usishindane na mama mzaa chema. Sawa binti?
 
Nafikiri ni wakati sasa tuwe na ujasiri wa kuwaface watu wanaotuletea kero kama hizo kujua tatizo ni nini na wapi unakosea badala ya kuishia kulalamika. Umeshafuga matatizo mengi kiasi kwamba hujui uanzie wapi. Sio mbaya, jaribu kuanza kumweka karibu mkweo.. Mchukulie kama mama yako mzazi na tafuta siku mtoke pamoja na huko unaweza kumwomba msamaha na kuongea nae vizuri akwambie wapi unamkosea. Usishindane na mama mzaa chema. Sawa binti?

Umeolewa? Hivi ulishabahatika kupatwa na visa vya mama mkwe?
 
huyo mama mkwe hana watoto wa kike?kama wapo kwa nini wasiache kazi wakaenda kumlea?

wewe na mumeo mna watoto? ukienda kijijini wanao atawatunza nani?

mama mkwe hana wakwe wengine? na wao wataenda kumtunza?
kama mnamisuguano/manyanyaso ya aina yoyoyte na mama mkwe wako, ukathubutu kuacha kazi uwe golikipa huko kijijini dada utaisoma namba.........

damu nzito kuliko maji,mumeo anaweza kusikiliza maneno ya ndg zake lakini mwisho wa siku ukwel hujitenga maana wanaume huwa hukwepa kukabiliana na matatizo yanayotokea baina ya mke na ndugu zake ila unatakiwa kuwa strong, uwe na msimamo, na uushikilie, ujenge nyumba yako.

Imeanikwa: MWANAUME ATAIACHA NYUMBA YA BABA YAKE NA KUAMBATANA NA MKEWE NAO WATAKUWA MWILI MMOJA.. sasa inakuwaje umuache mumeo uambatane na mama mkwe?

kaka mama mkwe yupo kijijini peke yake, tafuteni utaratibu wa kumtunza huko, lakini si kuacha kazi

huyo mama mkwe wako ni muharibifu tu, si yuko na mumewe? baba mkwe nae ana msimamo gani?

 
hebu subiri, sina hakika kama nimeelewa viizuri. Yaani umuache mumeo mjini alafu wewe uende Machame? Hivi kumbe hizi mambo bado zipo uchagani? Huwa zinaboa ile mbaya.. yani unaolewa halafu unakaa na wakwe, mumeo atakuja desemba kwa desemba. Usikubali kuacha kazi, wala kwenda huko, tumia busara kutatua hili. Wewe uliliolewa ili uishi na mumeo na si ukaishi na wakwe...!
 
jaman uyu mama mkwe ana mabinty wa kike wakamlee mama yao jaman
speak it out dia wangu kuna wamama wakwe nouma wasumbuf kama nn kwa watoto wa wenzao
mamii mpe msimamo wako kbs kuwa hauendi bs.
 
kwahiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe nao watakua kitu kimoja ,mwanzo 2:24 hiyo ndio ndoa,hujaoelewa kukaishi mbali na mumeo.
Pia nakushauri usije ukathubutu kuacha kazi nina mfano hai wa maisha yangu be a strong woman,baba angu alikua tajiri mkubwa ktk mji wetu ikawa alimshawishi mama aache kazi yake ya ualimu kwakua atakua anamlipa mshahara mara mbili yake.Namshukuru Mungu mama alikata wakagombana sana bt maisha yakaendelea mpk Mungu alivompenda baba zaidi.ndugu walichukua mali zoteeeee hadi kiti cha jikon isingekua mshahara wa mama mdogo wa ualimu leo hii tungekua kijijini hatuna mbele wala nyuma.
Tatu ndoa ni ya watu wawili kamwe usikubali mtu wa tatu kufanya ivunjike kumbuka mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe
 
ASANTE KWA USHAURI kweli nilishakaa na mama nikamweleza kuwa sitaweza kuacha kazi nikakaenaye kijiji si tuu kutokana na ugumu wa maisha bali pia kuishi mbali na mume kutachangia uwezekano wa kuleteana ukimwi, mama hanielewi ndo kwanza kila siku akaanza kulalamika anaumwa leo kichwa,kesho tumbo, keshokutwa maskio analalamika hana mtu wa kumwangalia basi nikamwambia aje mjini tukae naye ili tumpeleke na hosp. Kubwa AKAKATAA AKASEMA HAWEZI KUMUACHA MUMEWAKE PEKE YAKE, analalamika kila kukicha yn!

Sasa kama yeye hawezi kumuacha mumewe kwann akushauri wewe uhamie kijijn umwache mumeo mjini? Na je mumeo anasemaje kuhusu hilo swali?
 
Yanawakuta wengi na yakuja kwa dizaini mbalimbali. MVUMILIE.
 
Sahihi kabisa, wa kuongea naye ni mmeo na si mama mkwe, mweleze kinaga ubaga yale mama mkwe anakutendea na amweleze mama yake, pia mmeo akiweza amweleze baba yake (baba mkwe) kwa ninavyojua baba mkwe anaweza kuelewa zaidi na akayamaliza na mkewe amabye ni mama mkwe wako. Akumbuke umeolewa na mwanae na kama mmekubaliana na mwanae hana namna ya kulezimisha mambo, Pole ataelewa tu lakini.
Umewaacha wazazi wako na kuunganika na mumeo ambaye pia amewaacha wazazi wake.Hapo mwenye tatizo ni mumeo maana yeye ndo anatakiwa kumpa mama yake somo. Vituko vya huyo mama vione kama kelele za mwenye nyumba kwa mpangaji au zile za chura kwa ng'ombe.
 
Pole sana mwaya,
Sijawahi kupambana na mambo ya hv coz bado sijauaga usingle,
Ila kwa uelewa wangu mdogo hili linahitaji busara itumike,
Jishushe kwa mama mkwe wakati wa kuongea naye angalau aweze kusikia msimamo wako,
Ni km yeye alivyo hataki kumwacha mumewe na kuja kuishi nanyie huku mjini,
Kwa kushirikiana na mmeo naamini mnaweza badilisha hiyo hali ya hewa.
 
Huyu mama ananifanyia visa vingi sana na kwakweli najiskia hasira sn na kisa cha kunifanyia yote hayo ni MIMI KUKATAA KUACHA KAZI NA KUMUACHA MUME WANGU MJINI KWENDA KUKAA NAYE KIJIJINI MACHAME KAMA ALIVYOKUA ANATAKA YEYE, kwakweli amekua mtu wa visa anafanya mambo kwa makusudi hlf anasema simpendi, mf: siku 1 aliniambia atakuja kwangu jumamosi hlf kwa makusudi akaja ijumaa bila kunijulisha na mimi nilikua kazini mschana kaenda kwao kuzika akakuta geti limefungwa badala anipigie simu akaanza kulia na kuwapigia wifi zangu kuwaambia kw nimemfungia yn sa 10 jioni ndo baba mkwe anapata taarifa toka kwa mabint zake na kunijulisha huku akisikitishwa na kitendo alichofanya mkewe. YN NI MENGI SN ANANIFANYIA MPAKA NAONA KERO SIJUI NIFANYAJE?? NIFANYAJE WAPENDWA??

Vipi kuhusu baba mkwe? inaonekana yeye una mahusiano naye mazuri. isije ikawa mama anaumia maana wazee wa kichaga wana tabia ya kula wake wa watoto wao! hapo vipi, umepona kuliwa na baba mkwe? lazima kuna sababu ya mama mkwe kukuchukia, ichunguze kisha rekebisha mambo.
 
Dah Sungura Mpole sana!!Nnachoweza kukushauri kwanza hata iweje kaz usiache please hata iweje usiache,kaz ndo itakutetea hata mme na wakwe watakapokutosa!!Kuhusu huyo mamamkwe hebu ongea na mmeo kwanza akuuleze waz waz yeye anaonaje kuhusu mambo ambayo mama yake anafanya,ujue kabsa kama yuko upande wako au vp, lakin kama baba mkwe ni mwelewa pia mshirikishe. Ila kijijin usiende ng'o hiyo ndoa gan bila tendo la ndoa maana mtakuwa mbali na mmeo, afterall wewe ni mke sio mlez wa mama mkwe kwann sasa ukakae mbali na mmeo?usikubal kabsa na Mungu atakutetea mwaya
 
Huyu mama ananifanyia visa vingi sana na kwakweli najiskia hasira sn na kisa cha kunifanyia yote hayo ni MIMI KUKATAA KUACHA KAZI NA KUMUACHA MUME WANGU MJINI KWENDA KUKAA NAYE KIJIJINI MACHAME KAMA ALIVYOKUA ANATAKA YEYE, kwakweli amekua mtu wa visa anafanya mambo kwa makusudi hlf anasema simpendi, mf: siku 1 aliniambia atakuja kwangu jumamosi hlf kwa makusudi akaja ijumaa bila kunijulisha na mimi nilikua kazini mschana kaenda kwao kuzika akakuta geti limefungwa badala anipigie simu akaanza kulia na kuwapigia wifi zangu kuwaambia kw nimemfungia yn sa 10 jioni ndo baba mkwe anapata taarifa toka kwa mabint zake na kunijulisha huku akisikitishwa na kitendo alichofanya mkewe. YN NI MENGI SN ANANIFANYIA MPAKA NAONA KERO SIJUI NIFANYAJE?? NIFANYAJE WAPENDWA??

vitu vingine mnaviendekeza wenyewe, Kwan amekuoa yeye mpaka ukakae nae, ukikaa naye, muulize kama atakuwa anakupa na chakula cha sasa tisa usiku,
 
Kuna baadhi ya watu kila asubuhi akiamka inabidi apigwe viboko 10 na kabla ya kwenda kulala viboko 10 ili
kukumbushana majukumu ya kiutu uzima.Wewe na mume wako mnahitaji adhabu hii kila siku,upuuzi kabisa.

Wewe na mume wako mtakua na matatizo makubwa kuliko huyo mama mkwe wako.
Hivi inaingia akilini mama mkwe anakuambia uache kazi uende kukaa nae kijijini?Halafu mume wako atakaa na nani?
Na mume wako ana msimamo gani juu ya hilo,yeye yupo tayari uache kazi uende kijijini kukaa na wazazi wake?
Halafu unatuambia ,ulimwambia aje mjini ili apate na huduma ya afya,akakujibu hawezi kumuacha mumewe aje
kukaa nanyi?

Kama yeye hawezi kumuacha mumewe na kuja kukaa nanyi,wewe ndo umuache mume wako atie?Basi wewe mume
wako mbuzi?

Ushauri ukiona hivyo,basi wewe wamekudharau sana,wanataka uende kijijini uwe maid wa mama,na huyu mume wako
ana mtu atamuweka ndani ukishaondoka,ndo maana hujatushirikisha mawazo ya mume wako huenda nae anataka uende kijijini.
Vinginevyo wewe mwanamke kuwa na msimamo ,tena mwambie huyo mama kama hataki kuja kukaa nanyi mjini,basi akae
kijijini atulie zake na mume wake,upuuzi mtupu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom