mpenda siri
Member
- Dec 30, 2015
- 79
- 40
Habari wana JF,
Kuna binti nimekaa nae kwenye uhusiano kuanzia mwaka januari 2014, bila kufanya mapenzi mpaka nilifunga nae ndoa mwanzoni mwa 2015, akidai yupo bikra na hajawahi kujihusisha na mapenzi japo ni mzuri na watu wanamtamani sana, kweli ni mzuri na ana figure namba nane, hata wazazi wangu waliponikataza ndoa sikuwaelewa, ukizingatia anatoka nchi jirani kwa yule rais mrefu kupita wote hapa mashariki, aliniambia ametendwa na jamaa hivyo amekubali kuwa na mimi na nisimsababishie maumivu ya kutendwa kama zamani, nikamwelewa na nikaanza kumtunza kila mwisho wa mwezi nampa visenti na mawasiliano yakawa kwa simu kwani yeye alikuwa mkoani.
Nikatoa mahari na kuchukua jumla tena kwa ndoa ya kanisani mapema mwaka 2015 nilimpenda sana ila she took me for granted, yaani alinichukulia poa, akawa na dharau siku tatu tu baada ya honeymoon akaonyesha makucha, matusi kwake ni kawaida kwan jibu lolote linalomjia bila kulichuja, nikaja kufumania meseji ya mapenzi kamtumia jamaa yake.." i still have feelings on you" kila mara anaomba ruhusa kwenda kwao hata kama ukimzuia lazima ataondoka na kurudi anavyojisikia ila habari ya kwenda kwa wakwe zake yaani kwetu alipo olewa anazua sababu zisizo za msingi na kupiga kalenda, sms za whatsapp mpaka usiku ukimwuliza anazua ugomvi na kuweka password kwenye simu yake, kutwa nzima ni kulala anadai anaumwa na kazi hafanyi, kwani nilipomwoa alikuwa anasubiri post ya ualimu.
Baada ya post kutoka alichaguliwa mkoa wa jirani, nikamwambia tufanye process ili apate uhamisho kuja mimi nilipo ila aligoma na kudai serikalini mpaka ipite miaka miwili ndo upate uhamisho, nilimwambia kuna watu wanafanya magumashi na wanahama hata kabla ya kuanza kazi nipo tayari kuhonga ili aje nilipo lakini aligoma na kutaka mimi nihame kumfata, nikaona isiwe shida ngoja nitafute hela tupange nyumba nzima huko alipopangiwa kazi lakini mimi niwe naenda mara moja moja kwani ni mbali na kazini kwangu na nilihofia kuharibu kazi yangu, wakati huo anaishi guest house kwani aliripoti kazini hakuwa na pakufikia.
Siku moja nilienda kufanya suprise ili nijue sababu ya tabia kuzidi kuwa mbaya na kukata mawasiliano mpaka nimtafute, labda kuna watu wanatumia mali zangu, nilichokikuta huko ni maajabu, sikumkuta pale guest nilipomwacha hayupo kama siku ya tatu, nikampigia simu akasema yupo guest nilipomwacha, wakati si kweli, nikamwambia ukweli kwamba mimi nipo pale guest na yeye aseme alipo, akasema alihamia karibu na shuleni, hivyo niende, kwenda mpaka shuleni hayupo, nikaongea na mwalimu mkuu kama alimpa nyumba hapo akasema hajampa nyumba kwani zilikuwa chache.
Akaja pale shuleni amesindikizwa na mwalimu wa kiume ambae anaishi nyumba za jirani na pale shuleni, baada ya utambulisho kuwa yule aliyemsindikiza ni mwalimu mwenzake anaeishi jirani na pale shuleni tulimuaga mwalimu mkuu na kuondoka kurudi pale guest alipofikia mwanzoni, njiani nikamwuliza sababu ya yeye kuhama bila taarifa na kukaa kimya muda wote huo, akawa anadai alipata walimu wenzake wa kike walioajiriwa pamoja na kupanga chumba jirani na shule hivyo kuepuka gharama za guest house na wanaume wasumbufu pale kijijini, niliamua kumsamehe na maisha yakasonga. Nikampa hela ya kupanga nyumba nzima ili atoke kule kwa waalimu wenzake. Likabaki suala la kuhamia tu kwani alipewa ufunguo na kufanya usafi.
Walipofunga shule alirudi kwangu na tukapanga kupata mtoto kwani niliwaza nikimpiga mimba atatulia na mawenge yote yatamwisha, kweli mara baada ya mwezi mmoja akanasa mimba tukaenda hospital na kuconfirm, sasa ndio akazidisha timbwili mara visa vya hapa na pale, kukasirika bila sababu nk. nikajua hivi ni visa vya mimba changa hivyo natakiwa kumvumilia, akaanza kuninyima papuchi na usumbufu mwingi, mara anaficha vitu vyangu vya gharama kama simu, hati za viwanja, akazidisha mpaka ikawa kero nikiwasha taa ya chumbani kubadili nguo ni ugomvi kwake anataka akae gizani, akahama chumba na kwenda kulala na mdogo wake.
Baada ya vigisuvigisu vingi nakuona hali ya mahusiano hairekebishiki niliongea na mama yake ili amkanye bila mafanikio, badala yake mama yake akaja kumchukua kwangu na kuomba aende akamuuguze kwani alikuwa anatapika sana na mara kwa mara alidai anaumwa kichwa, nilitafakari sana nikaona nisimkatalie mama ni bora aende kwao kidogo akauguzwe kwani akijanifia ndani nitaonekana ndio chanzo pia kupunguza malumbano na ugomvi kila siku, nikakubali waende nae ila nikaweka kikao kidogo na mama mkwe na kumwambia matatizo yote ya mwanae, mke wangu alikuja juu km moto wa kifuu na kunishambulia kwamba na mtesa na kumnyanyasa vitu ambavyo sio kweli hata kimoja, hivyo akasema tuachane na leo ndio mwisho wa ndoa yetu, aliongea kwa sauti ya juu na kufanya majirani wajae kuona sinema ya bure, baada ya kusema uongo wake nikaondoka na kwenda kulala chumbani yeye akagoma kuja na kwenda kulala chumba kingine na mdogo wake wa kike.
Kesho yake wakaondoka kwangu yeye na mama ndipo alikata mawasiliano na mimi kwenye simu kwani alini block hakupatikana na sms yake ya mwisho ni kwamba nimtumie hela kwenye m-pesa ya matunzo ya mimba na yeye hana shida ya kuongea na mimi na hanitaki tena, nikimtumia sms hajibu, baada ya wiki moja nikaenda kumsalimu kule kwao, niliambulia matusi ya nguoni, mbele ya mama na wadogo zake na kufukuzwa juu kwamba nisije nikapeleka kwato zangu pale kwao, nikaonda na kurudi baada ya wiki mbili hali ilikuwa mbaya zaidi kwani hata ndani hakutoka kuja kunisalimu mpaka naondoka pale kwao, nilijaribu kwenda pale kwao zaidi ya mara nne pamoja na kuongea na wazazi wake, wakasema nisubiri ajifungue kwani ni matatizo ujauzito tu.
Wazazi wangu walikwenda kule kwao kumjulia hali na kutaka kuweka mambo sawa, mama mkwe alikuwa busy na hakuwa pokea vizuri wazazi wangu kwa kutoa udhuru kwamba anakwenda kitchen party ya jirani na binti aligoma kutoka ndani kuwaona ila baba yake alimshawishi sana ndio akaja kuwaona wazazi wangu na kuwaambia anitaki tena na hayupo tayari kurudi kwangu, wazazi wakamsihi sana lakini hakuwasikia, nilivyopata mrejesho wa safari ya wazazi wangu, nikasema kama ndoa basi, imekwisha na sioni sababu ya kutuma hela kwa mtu ambae hanitaki tena wala hataki mawasiliano.
Mwishoni mwa mwaka 2015 yaani tarehe 31.12.2015 saa tano usiku, mke wangu akatuma sms kwamba anaomba msamaha kabla ya kuingia 2016 nikamwambia hakuna shida nimekusamehe, akaendelea kunisihi sana nimsamehe na anataka kurudi kwangu , nikamwambia akae kwao mpaka ajifungue na suala la kurudi kwangu kwa sasa asirifikirie kwani nimegundua ana mapenzi kwa mnyalu mwenzie hivyo asilazimishe kurudi kwangu wakati hisia zake zipo kwa mtu mwingine kama ni matunzo ya mtoto mimi nitakuwa natoa na ushirikiano wowote atakaohitaji ila suala la kurudiana anipe muda nifikirie kwa kina kabla sijamrudisha akafanya makosa makubwa zaidi ya mwaka jana.
Anadai ni shetani ndio amesababisha na yeye yuko tayari kuwa na mimi kwani ndoa yetu ni ya kikristo hivyo hawezi kutoka nje ya ndoa au kuzaa na mtu mwingine kwani ina effect kubwa sana kwenye maisha ya malezi ya watoto, ni mrudie kwani mimi nimekuwa kwa baba na mama hivyo nimhurumie mwanangu ambae anatarajia kujifungua mwezi huu wa kwanza. amejiliza sana kwangu na kujutia makosa yote aliyofanya, nimemuhurumia
Binafsi nampenda sana ila siko tayari kuwa nae kwa sasa kwani nimepata aibu kubwa kwetu kwasababu yake na pia hizi dharau alizo zionyesha kwangu mpaka majirani wananicheka na ndugu zangu hawataki hata kumsikia. wakati tunaanza kuishi nilimpa matunzo yote vizuri hata kwenye tendo la ndoa nipo vizuri sana kwani nikichepuka nje wanaomba poo, na sikuwa mchepukaji ila ilinibidi nianze kupunguza mawazo na stress za hii ndoa.
Nishaurini nimrudie mke wangu? Au niwe nampa matunzo ya mtoto na kumwacha aolewe kwingine na mimi nifanyeje ili nimsahau na kujipanga vizuri kwa mwaka huu 2016!
Nawasilisha kwenu wadau.
NB; Weka mchango wako wa mawazo hata matusi napokea kwani mimi sio wa kwanza kutukanwa humu JF.
Karibuni kwa ushauri.

Last edited by a moderator: