Mama mkwe amegeuka kero kwenye ndoa yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama mkwe amegeuka kero kwenye ndoa yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SUNGURA MPOLE, Dec 14, 2011.

 1. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama ananifanyia visa vingi sana na kwakweli najiskia hasira sn na kisa cha kunifanyia yote hayo ni MIMI KUKATAA KUACHA KAZI NA KUMUACHA MUME WANGU MJINI KWENDA KUKAA NAYE KIJIJINI MACHAME KAMA ALIVYOKUA ANATAKA YEYE, kwakweli amekua mtu wa visa anafanya mambo kwa makusudi hlf anasema simpendi, mf: siku 1 aliniambia atakuja kwangu jumamosi hlf kwa makusudi akaja ijumaa bila kunijulisha na mimi nilikua kazini mschana kaenda kwao kuzika akakuta geti limefungwa badala anipigie simu akaanza kulia na kuwapigia wifi zangu kuwaambia kw nimemfungia yn sa 10 jioni ndo baba mkwe anapata taarifa toka kwa mabint zake na kunijulisha huku akisikitishwa na kitendo alichofanya mkewe. YN NI MENGI SN ANANIFANYIA MPAKA NAONA KERO SIJUI NIFANYAJE?? NIFANYAJE WAPENDWA??
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Pole Sungura Mpole
   
 3. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu! Mie sijui mambo ya ndoa hasa namna ya kuishi na wakwe(coz sijaamua kuwa mwanachama), ngoja wenye uzoefu waje kukushauri,
   
 4. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ASANTE NYANI NGABU nisaidie nifanye nini?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole mpendwa tafuta namna ya kuishi na mama mkwe,kaa kitako mweleze ugumu wa maisha ulivyo kama utaacha kazi faida na hasara ,labda atakuelewa
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hebu kuwa mwanamke acha kuwa kasichana
  hivi umeweza kupata cheti cha fomu 4 utashindwa ishi na mama mkwe wa kijijini
  nyie kizazi cha dot com mna mambo.

  Anyway, mkalishe muongee tofauti zenu sababu huyo ndo mama wa mumuo na mumeo anampenda kama wewe unavyompenda mama yako

  kulia haisaidii, mwisho wa siku hujaolewa na ukoo umeolewa na mumeo learn to make tough decisions when necessary
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Behave like a woman not a girl
  kila mtu atakuheshimu including mama mkwe

   
 8. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mlie bati tu akiona hubabaiki naye atakupotezea,ukimjibu ataona amepata victim wa kumchezea hizo mind games..........................usionyeshe kukasirika wala kufurahi akija mpokee kwa ukarimu baada ya muda wa kuwa 'ignored' mwenyewe ataacha kukuchokoza.
   
 9. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  pole wenye wanakuja.
   
 10. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ASANTE KWA USHAURI kweli nilishakaa na mama nikamweleza kuwa sitaweza kuacha kazi nikakaenaye kijiji si tuu kutokana na ugumu wa maisha bali pia kuishi mbali na mume kutachangia uwezekano wa kuleteana ukimwi, mama hanielewi ndo kwanza kila siku akaanza kulalamika anaumwa leo kichwa,kesho tumbo, keshokutwa maskio analalamika hana mtu wa kumwangalia basi nikamwambia aje mjini tukae naye ili tumpeleke na hosp. Kubwa AKAKATAA AKASEMA HAWEZI KUMUACHA MUMEWAKE PEKE YAKE, analalamika kila kukicha yn!
   
 11. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  pole dear
  mumeo kwa hili anasemaje?
  ongea nao kwa pamoja ili kuweka mambo sawa
  inawezekana anashirikiana na mamake kutaka wewe kurudi kijijini
   
 12. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SWALA LA KUENDA KIJIJI NILILIKATAA MAPEMA KABISA NA MUME ALINIUNGA MKONO lkn jins siku zinavyoenda mbele mume anabadilika ktkn na maneno anayoambiwa na mama yk na dada zake!
   
 13. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hana lolote huyo anataka kuongeza nyumba ndogo lol,usikubali kurudi kijijini..huyo mama mkwe wako hampatani kuanzia sasa hivi ukienda kwake ndio atakunyanyasa zaidi...kwanza mjini kulivyo kutamu weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee????!!!!!!!
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Mtafutieni Housegirl ndio amtunze, kama issue ni kuumwa!r
   
 15. K

  Kampini Senior Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umewaacha wazazi wako na kuunganika na mumeo ambaye pia amewaacha wazazi wake.Hapo mwenye tatizo ni mumeo maana yeye ndo anatakiwa kumpa mama yake somo. Vituko vya huyo mama vione kama kelele za mwenye nyumba kwa mpangaji au zile za chura kwa ng'ombe.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  bora wewe mama mkwe, wengine unakuta ni mzazi analalamika wala hajali
  as long as anatimiza wajibu wake kwa wazazi

  uko too spoiled

   
 17. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mume wako ni mtoto wa mwisho?level ya elimu ya huyo mamamkwe?eti mama mkwe ni mmachame au wakuja,kwa sababu wamama wachache sana wa kimachame wana muda wa kuwarudisha wali nyumbani sana sana atakuambia mwali kitenge sina,ila subiri akija dada Ashadii atakushauri vizuri,aliwahi andika thread juu ya hili
   
 18. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Jamani huyo mama mkwe si anawatoto wakike mwambie aendenao kijijini wakamlea wewe haupo hapo kwenda kumlea kijijini au uliwambia wewe nesi.

  Yeye mbona anaona kama anaibiwa mumewe kijijini,inawezekana wewe huonyeshi msimamo wako wanapokuambia ongea kwa kumaanisha.Wewe mwaache alalamike ataacha ila tu fanya wajibu wako kama mkamwana.
   
 19. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mimi nina mama mkwe poa sana. Lakini tokana na experience ya mama wakwe wa ndugu zangu kuna kitu nime learn. Nna dada yangu ni mpole saaana; mama mkwe na wifi zake walikuwa wanamwendesha hakuna maelezo mpaka mumewe anaingilia kati.

  Dada yangu wa pili ni very strict na principled; mama mkwe wake pia ni mkorofi kwa wakwe wengine lakini si kwa huyu dadangu. Yani hata mawifi zake ambao wanamzidi umri wanamheshimu sana kwani yuko serious; mpaka wake wenzake wanamuuliza wewe mbona wanakuogopa?

  Kuhitimisha ni kuwa; sisi wanawake tunalea huu upuuzi. From day one tuache kujikomba ukweni. Wanawake wengi sana wanashindwa kuwa themselves when it comes to wakwe na which make those wakwe take advantage of that. Dawa ni kujiamini from day one kuwa huwezi vumilia nonsense, uone kama mtu atakupeleka puta. As long as mmeo alikuoa kwa pendo na si kulazimishwa he will be by your side.

  Mi nshaona hata kwa mawifi wake wa kaka zangu wana mapenzi yalopitiliza kwetu ambayo ni full of acting si real. Lets be ourselves. KUna watu wakishajua unawaogopa wanakukalia kichwani.

  Mimi sina ushoga na mawifi (wa mama mkubwa wa mume wangu since they are all men in his family) wala mama mkwe, I just repsect them na hii imefanya tusigombane na nashangaa wanawaambia watu am the best wife wakinilinganisha na mke wa shemeji yangu ambaye kutwa anawapa mazawadi tena kwa kujinyima.
   
 20. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Mama mkwe hawezi kuja mjini kwa sababu HAWEZI KUMWACHA MUME WAKE ila wewe anataka UMWACHE MME WAKO, UACHE KAZI uende kumtuza mama mkwe! Hivi kuna mama mkwe bila ndoa? Anataka kuwatenganisha na mme wako, je mkitengana uhusiano wako na yeye si umekwisha? Bila ndoa hakuna wifi, shem, baba wala mama mkwe! Pili, kuacha kazi hata kwa sababu ya mume ni jambo la hatari, sembuse kuacha kazi kwa ajili ya mama mkwe! Nahisi huyo mama mkwe wako anataka uache kazi ukose pa kuegemea ili akudhibiti vizuri. Kama walivyokushauri wengine, kuwa jasiri. Matatizo yakizidi usiogope kmwambia mmeo muachane, kwa sababu mmeo amekosa msimamo na kumruhusu mama yake kutawala ndoa yenu. Najua mme unampenda na uamuzi wa kuondoka ni mgumu lakini hiyo ni njia nzuri ya kututia adabu wanaume tusiotumia akili zetu. Atakuja tu kwako kama kondoo aliyenyeshewa:'mke wangu nimefikiria sana, naona tulikukosea, wewe usimjali mama, niangalie mimi kama mmeo. Tusahau ya nyuma turudiane'. Akija hivyo hapo ndio wakati wa wewe kuweka guidelines ili ndoa yako isichezewe tena.
   
Loading...