hebu subiri, sina hakika kama nimeelewa viizuri. Yaani umuache mumeo mjini alafu wewe uende Machame? Hivi kumbe hizi mambo bado zipo uchagani? Huwa zinaboa ile mbaya.. yani unaolewa halafu unakaa na wakwe, mumeo atakuja desemba kwa desemba. Usikubali kuacha kazi, wala kwenda huko, tumia busara kutatua hili. Wewe uliliolewa ili uishi na mumeo na si ukaishi na wakwe...!
Hapo mwenye kuokoa hilo jahazi ni mume wako, kwa nini anakosa msimamo??
cha ajabu mama mkwe anaishi na mumewe ila anataka binti wa watu amuache mumewe akakae na wakwe. wanawake jamani mnapokua na wakwe zenu msiwafanyie hayo loh
Hii tabia kwa wachaga ilikuwepo toka enzi, but nimeshangaa sana kumbe hadi leo hii inaendelea. You can imagine: yeye na uzee wake hataki kumwacha wa Ubavu wake, halafu anataka mwali wake (ndoa ndo kwanza imenoga) amwache mumewe, haiingii akilini kabisaaaa.
Huyu mama ananifanyia visa vingi sana na kwakweli najiskia hasira sn na kisa cha kunifanyia yote hayo ni MIMI KUKATAA KUACHA KAZI NA KUMUACHA MUME WANGU MJINI KWENDA KUKAA NAYE KIJIJINI MACHAME KAMA ALIVYOKUA ANATAKA YEYE, kwakweli amekua mtu wa visa anafanya mambo kwa makusudi hlf anasema simpendi, mf: siku 1 aliniambia atakuja kwangu jumamosi hlf kwa makusudi akaja ijumaa bila kunijulisha na mimi nilikua kazini mschana kaenda kwao kuzika akakuta geti limefungwa badala anipigie simu akaanza kulia na kuwapigia wifi zangu kuwaambia kw nimemfungia yn sa 10 jioni ndo baba mkwe anapata taarifa toka kwa mabint zake na kunijulisha huku akisikitishwa na kitendo alichofanya mkewe. YN NI MENGI SN ANANIFANYIA MPAKA NAONA KERO SIJUI NIFANYAJE?? NIFANYAJE WAPENDWA??
Kama yeye awezi kumuacha mume wake ambaye ameshakula chumvi nyingi,vipi wewe ambaye bado wote damu zenu zinachemka? Mpotezee huyo mama hana nia nzuri na ndoa yako,anataka kukualibia kwa Mr wako ili akuache,kwani utakapo enda kukaa naye kule kijijini,atafikisha ripoti mbovu kwa mumeo,kama uhamini wewe subutu kwenda naye huko kijijini,yatakayo kukuta utanitafuta. Chakufanya we shika 50 zako ila usimzalau wala kumtusi,kwa lolote atakalokufanyia we mpotezee tu na unatakiwa uonyeshe msimamo wako na huo msimamo mumeo aujue.ASANTE KWA USHAURI kweli nilishakaa na mama nikamweleza kuwa sitaweza kuacha kazi nikakaenaye kijiji si tuu kutokana na ugumu wa maisha bali pia kuishi mbali na mume kutachangia uwezekano wa kuleteana ukimwi, mama hanielewi ndo kwanza kila siku akaanza kulalamika anaumwa leo kichwa,kesho tumbo, keshokutwa maskio analalamika hana mtu wa kumwangalia basi nikamwambia aje mjini tukae naye ili tumpeleke na hosp. Kubwa AKAKATAA AKASEMA HAWEZI KUMUACHA MUMEWAKE PEKE YAKE, analalamika kila kukicha yn!
Pole ndugu! Mie sijui mambo ya ndoa hasa namna ya kuishi na wakwe(coz sijaamua kuwa mwanachama), ngoja wenye uzoefu waje kukushauri,
Hapo mwenye kuokoa hilo jahazi ni mume wako, kwa nini anakosa msimamo??
mwanzo mume wangu alikua na msimama lkn mama yake akaanza kumlalamikia kuwa alimzaa na kumlea kwa shida sana na baba yake alimtelekeza akahangaika kumlea mwenyewe na anamtoto wakiume 1 tu (mumewangu)alitegemea akioa mkwewe(mimi) nitaenda kukaa naye, mwanae akaanza kubadilika na kuanza kunishawishi nihamie kijiji nikamwambia twendewote akasema hatoenda niende mimi nami kwa ustaarabu nikamwambia sitoenda basi mara kwa mara anakua na maneno ya kunilaumu tu mpaka naona ndoa chunguHuyo anataka akufanye ushitakiwe na dhamira na ujione mkosaji,mpuuze halafu jaribu kuongea na mwanae(mumeo)ili amkanye tabia yake hiyo!
mwanzo mume wangu alikua na msimama lkn mama yake akaanza kumlalamikia kuwa alimzaa na kumlea kwa shida sana na baba yake alimtelekeza akahangaika kumlea mwenyewe na anamtoto wakiume 1 tu (mumewangu)alitegemea akioa mkwewe(mimi) nitaenda kukaa naye, mwanae akaanza kubadilika na kuanza kunishawishi nihamie kijiji nikamwambia twendewote akasema hatoenda niende mimi nami kwa ustaarabu nikamwambia sitoenda basi mara kwa mara anakua na maneno ya kunilaumu tu mpaka naona ndoa chungu
mwanzo mume wangu alikua na msimama lkn mama yake akaanza kumlalamikia kuwa alimzaa na kumlea kwa shida sana na baba yake alimtelekeza akahangaika kumlea mwenyewe na anamtoto wakiume 1 tu (mumewangu)alitegemea akioa mkwewe(mimi) nitaenda kukaa naye, mwanae akaanza kubadilika na kuanza kunishawishi nihamie kijiji nikamwambia twendewote akasema hatoenda niende mimi nami kwa ustaarabu nikamwambia sitoenda basi mara kwa mara anakua na maneno ya kunilaumu tu mpaka naona ndoa chungu