Mama Mjane amlilia Rais Magufuli mbele ya Waziri wa Sheria

Habari mbona nusu nusu mngemtaja maama na shida yake mpk amefika kwa huyo mtu
Huyu mama anakesi ya mirathi ya mume wake, sasa mawakili wake wanasaidiana na wanaotaka kumdhulumu ili asipate haki yake, kahangaika kwa mawaziri wa sheria IGP na DPP lkin bado anaona mapichapicha tu
 
Huyu mama kwa jicho la pili asee katoa funzo kubwa sana.kwamba..kila unachokitaka maisha ni kinawezekana haijalishi vizingiti vingapi unakutana navyo...mama kasema hivi kati ya vitu vingine"Niko tayari kufungwa ama kupata haki yangu natoa machozi yangu Mbele yako Mh raisi"na hakuishia kujitetea mwenyewe bali kawatetea na wamama wote wanaonyanyasika out there,she nearly made me cry,nilimkumbuka mwanangu na mkewangu!!
 
Halafu Igp Mangu hajui hata kujieleza walishazoea kuwashurutisha tu watuhumiwa kwa vipigo kumbe na yeye ni mweupe kabisa katika kujieleza kaulizwa tu swali na rais Igp una taarifa na hii kesi? Akaanza kujiumauma tu maelezo hata hanyooshi ya ni blaa blaa kama kawaida ya mapolisi
 
kama nilivyoeleza hapo juu sasa nimeanza kumuelewa magufuli baada ya kuichana makavu live muhilmili wa mahakama kwa kukithiri kwa rushwa,upindishaji wa kesi,kutotoa haki stahiki kwa wenye haki kwa kua eti tu hawana hela za kuhonga.baada ya kumaliza kuichana mahakama ndipo mama mmojo alipojitokeza na kutaka kutoa malalamiko yake kwa rais ndipo wana usalama walipojitahidi kumzui na hata kumnyang'anya documents zake alizokua kabeba ili asiende kwa rais ndipo mama wa watu alipoangua kilio ambacho hata mimi kimeniliza na baada ya anko magu kumuona alimuonea huruma na kuwaambia wanausalama wamuachie aende kwa rais kutoa malalamiko yake kwa kweli aliongea kwa uchungu huku machoz yakimtoka kwa kudhulumiwa miradhi yake ndipo magufuli akamuweka kiti moto IGP na kuwatupia lawama mawakili na sasa mama kapewa ulinzi wa polisi na suala lake lishughulikiwe haraka iwezekanavyo
 
Tukio hilo limeibeba shughuli ya leo
Nandilo likalouza magazeti ya kesho, mwanzo niliwaona wanausalama wakimtoa mbio mbio yule mama, polisi + usalama wa taifa walijazana kumsomba mama wa watu. Lakini baada ya muda kido, nilimuona mh Mwakyembe akimueleza rais kuhusu huyo mama, kisha mh Rais akatoa maamuzi ya yule mama aachiwe na asogee mbele ili amsikilize. Mama akaelezea shida yake , huku akiangusha kilio, na alimwambia mh rais kuwa alikuwa tayari kwa lolote kwa siku ya leo, ( yaani alijipanga kufikisha kilio chake kwa rais, hata kama ataonekana ni mchochezi na polisi wataamua kumfunga kwa kosa hilo la uchochezi , alisema yupo tayari).

Lakini Mungu amemsaidia zoezi lake limefanyika kwa amani, kilio chake kimemfikia Mh. Rais, na rais alimpa muda kidogo IGP atoe maelezo kama analifahamu hilo tatizo la huyo mama. IGP alitoa maelezo vizuri jinsi anavyolifahamu tatizo la huyo mama, mh raisi alitoa maagizo kwa idara husika, walifanyie kazi hilo tatizo, na haki itendeke na mama apewe haki yake. Pia mhe Rais alitoa maagizo kwa IGP ahakikishe mama anapewa ulinzi, ikiwezekana apewe polisi mmjo wa kumlinda, maana mama alishatumiwa sms za vitisho na hao wabaya wake.

Yeye aliwataja kama drug dealer (wauza unga, kwahiyo alimuomba rais ampe ulinzi kwa kitendo chake cha kuweza kuonana na rais na kumueleza kinachoendelea.

Pia mama aliambiwa achukuwe namba ya Jaji kiongozi, ili awe anawasiliana naye moja kwa moja. Katika kupeana taarifa kwa kinachoendelea.

Mm binafsi nimempongeza huyu mama, kwa ujasili aliokuwa nao.
Aliweza kuonana na viongozi wengi sana, katika kufikisha kilo chake.
Lakini huko kote hakufanikiwa, naye akaona katika tukio la sherehe za mahakama ndiyo sehemu husika kwa kufikisha kilo chake.

Pia nampongeza mhe Rais Dkt. John P. Magufuli , kwa kutoa amri ya yule mama achiwe aseme shida yake, na pia kutoa maamuzi yenye hekima,.

Mungu amsaidie apate haki yake.

Sent from my GT-I9195 using JamiiForums mobile app
 
Ccm na serikali yake police na mahakama wote majambazi.nimeona kule michuxi insta kuna video.police ccm na wengine wanaoegemea ccm kuficha uchao Mungu anaendelea kuwaumbua.


swissme
 
Huwa sielewi wajane wanataka hata hukumu z mahakama zisifuatwe na wao tu ndio wapewe wanazodai haki.....ukute mchakato umepita mahakama zote na imeonekana hawastahili wao kupata wanacholilia!!! Sasa kisa ni wajane wanalia lia hovyo! Ukisikiliza hapo utaona kesi imeenda mahakamani na ameshindwa lakinii........analial alia
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mama mmoja ambaye ni mjane amefika mbele ya Rais kulilia haki yake, hakika kuna uwezekano hili suala linaenda na mtu


Kesi ya msingi hasa ni mirathi, hili jambo limekuwa likifanyika sana kwa watu wa hali ya chini.

 
Mkuu tuwekee na video. What i can say ni kwamba rushwa imetawala sana, huku mtaani kwetu mtu kaziba njia na mahakamani kashinda kesi, hivi hata logic kidogo tu hawatumii jamani!
 
Number ya simu imechukuliwa.......mama kataja issue ya madawa ya kulevya.....that really trickled Mr.President's attention.....
Nadhani madawa ndo yamepelekea kupewa ulinzi
Kwa maana ametoa Mwanga na soon watakamatwa
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mama mmoja ambaye ni mjane amefika mbele ya Rais kulilia haki yake, hakika kuna uwezekano hili suala linaenda na mtu


Kesi ya msingi hasa ni mirathi, hili jambo limekuwa likifanyika sana kwa watu wa hali ya chini.


Haya ndio mambo ambayo Magufuli angetumia nguvu zake zote kupambana nayo. Badala ya kupambana na wapinzani.
 
Mama anayosema kama ni kwa kweli amenihuzunisha sana,kama kuna mizengwe ya hivi huko mahakamani wangapi wanateseka? chombo kinacho simamia haki kinashindwa kutoa haki kwa sababu ya watu kucheza michezo michafu kwa kutumia pesa so sad ila Mungu yupo.
 

Kuna Tatizo Hapo Wengi Tunalikosa Kuliona, Siku Hizi Kumekuwa Na Viofisi Vingi Vya Wanasheria Wa Vichochoroni Wanatumia Sana Vibaya Taaluma Yao Kusababisha Migogoro Kwenye Kesi Za Mirathi Na Mwisho Wa Siku Ni Wao Ndiyo Wanaofaidika.

Wanakuwa Kimbelembele Sana Na Mali Za Urithi Ziuzwe Wakati Wakijua Wao Ndiyo Wanaofaidi Kwenye Hayo Mauzo Na Kuwaacha Warithi Wakipata Shida.

Wanashiriakana Na Mahakimu Wa Mahakama Hizi Ndogo Ndogo Za Wilaya Ili Kudhulumu Mali Za Watu, Wameona Pesa Za Mihuri Hazitoshi Sasa Wanatumia Mbinu MPya Ya Kujitajirisha Kwewnye Kesi Mirathi.

Na Hizi Mahakama Za Wilaya Zina Mahakimu Wa Ovyo Sana, Mahakama Imekuwa Kama Magenge Ya Wahuni Taratibu, Kanuni Na Weledi Havipo Kabisa

Nilienda Kusikiliza Kesi Moja Ya Mirathi Unaona Kabisa Kuna Kitu Kati Ya Hakimu Na Mwanasheria Uchwara

Mwanasheria Anatoa Tu Tuhuma Bila Ushahidi Na Hakimu Anaandika Tu Akiulizwa Ushahidi Wa Anayoyasema Anasema Ni Mtuhumiwa Ndiyo Anatakiwa Kudhibitisha Na Hakimu Anakubali Tu Kijinga Kijinga
 
Back
Top Bottom