Mama Mjane amlilia Rais Magufuli mbele ya Waziri wa Sheria

LH XiV

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
346
350
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mama mmoja ambaye ni mjane amefika mbele ya Rais kulilia haki yake, hakika kuna uwezekano hili suala linaenda na mtu

Kesi ya msingi hasa ni mirathi, hili jambo limekuwa likifanyika sana kwa watu wa hali ya chini.

Hii kesi inapande mbili ukimsikiliza IGP alivoulizwa na Mkuu wa Nchi, kwanza marehemu anamke zaid ya mmoja, pili kesi imeshughulikiwa na mawaziri zaid ya wawili na bado kesi ipo mahakamani.

Kwa mujibu wa mama kesi imefanyiwa judgements za aina mbili mama kapewa yake na hao nduguze pia, hii maana yake nini ?
 
Kuwa mjane siyo justification ya taratibu kupindwa ili kutoa favour...ila kwa mihemko ya kisiasa sishangai yakachukuliwa maamuzi ya kushangaza!
Hakika hiyo sio justification lakini katika uhalisia akina mama wengi wamekuwa wakipoteza sana haki zao kwa njia kama ya huyu mama, wakili ku play doubelroles upande wa mashtaka na upande wa utetezi
 
Kuwa mjane siyo justification ya taratibu kupindwa ili kutoa favour...ila kwa mihemko ya kisiasa sishangai yakachukuliwa maamuzi ya kushangaza!
Utaratibu upi zaidi ya kutetea haki za wanyonge, hii nchi watu wamedhulumiwa sana haki zao...Na vyombo vya kutoa haki vikihusika kwa asilimia kubwa .

Nampongeza sana mama kwa kujitoa mhanga, amewakilishwa kilio cha wengi.
 
Tukio limewavutia wengi waliokuwepo hapo kwenye ukumbi + tuliokuwa tunaangalia mubashara via Azamtv.
 
Huyu mama ni jasiri sana. Na ukiangalia kafanya kila juhudi kuweza kupata haki yake. Kitendo cha leo kufika mbele ya Rais ni ujasiri wa hali ya juu sana.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
mjane.jpg


DAR ES SALAAM: Mjane mmoja (kwenye picha kushoto), mkazi wa Mkoa wa Tanga ameibuka kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kumwaga machozi mbele ya Rais John Magufuli wakati akitoa malalamiko yake kuhusu kudhulumiwa kwa haki yake ya mirathi baada ya kifo cha mumewe.


Akilia kwa uchungu, mjane huyo amesema kuwa, kesi yake ilitolewa hukumu ambapo nakala ya hukumu aliyopewa yeye ni tofauti na aliyopewa mdaiwa.

Aidha mama huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa malalamiko yake ameshayapeleka kwa DPP, AG, IGP, Waziri wa Sheria, Dkt Mwakyembe na sehemu mbalimbali ambazo aliona zitamsaidia lakini hakuna lolote mpaka sasa.

Mama huyo alienda mbali zaidi na kueleza kuwa imefikia wakati anatumiwa ujumbe wa vitisho vya kuuawa ambapo ujumbe huo aliupeleka polisi na kumtumia Rais Magufuli ili aone namna ambavyo anatishiwa maisha.

“Mheshimiwa rais mimi ni mjane, kuna watu wamefanya mbinu za kunidhulumu mali zangu ambazo nilitafuta na mume wangu, wamevuruga wosia wa mirathi na hata niliposhtaki sikutendewa haki kwani kuna mawakili wamehusika katika kutengeneza mbinu ili nidhulumiwe.

“Hakimu aliyesimamia kesi hiyo ametoa nakala tofauti ya huku ya kesi hiyo, kwangu na kwa mdaiwa.

“Jambo hili DPP, AG, IGP na Waziri Mwkyembe wanafahamu.

“Imefikia wakati ninatumiwa ujumbe wa kuuawa kwenye simu, au kwa kuwa watu hao wanapesa za kuuza madawa ya kulevya? Ninawajua kuwa wanafanya hizo biashara za drugs (madawa ya kulevya) hata picha za ushahidi ninazo,” alisema mama huyo huku akilia kwa uchungu.

“Ninakuomba mheshimiwa rais unisaidie nipate haki yangu, nimeteseka vya kutosha, nina nyaraka zote za ndoa kutoka BAKWATA, Wizara ya Mambo ya Nje ambayo nilipewa kwenye Ubalozi wa Kenya,” alisema mama huyo.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimsimamisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu ambaye alikiri kuifahamu kesi hiyo na kuelekeza kuwa inashughulikiwa na mahakama ya wilaya jijini Tanga.

Aidha Rais Magufuli amewaagiza DPP na AG kuhakikisha wanaishughulikia kesi hiyo ili mama huyo aweze kupata haki yake haraka iwezekanavyo kwani suala hilo liko ndani ya uwezo wao.

Kutokana na kutishiwa maisha, Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi wampe ulinzi mjane huyo mpaka atakapopata haki yake.


"
 
Mkuu amefanya kazi ya suleiman Mwana wa daudi.
Ila huyo mjane ni mpambanaji kweli kweli inaonekana hapo ni kilele cha mapambano yake amewahi kumtext jpm, AG anajua, mkuu wa police anajua issue yake. Amenikumbusha kisa cha kadhi dhalimu mfano wa mjane uliotolewa na yesu jinsi yule mama alivyokomaa hadi akapata haki yake. Wajane waache unyonge wakomae
 
Hawezi kudhuriwa labda hawajipendi. Amewaambia asidhuriwe kwa hali yyte ile.
 
Hakika ni ujasiri wa hali ya juu, sijui kwa sababu ni mkenya? Watanzania wengi wako tayari Kuacha haki take ipotee kisa hataki usumbufu.
 
kisa cha mama huyu ni kielelezo cha wengi kupokwa haki zao. Kwa namna alivyoeleza amepigania sana haki yake. Lakini katika muda wote hakupata haki anayoidai. Binafsi nimehuzunika sana namna wanaadamu tulivyo na roho mbaya. Nadhani kwa kuwa jambo lake limefika moja kwa moja kwa Mheshimiwa Rais na kalisikiliza na tayari katoa maagizo, bila shaka haki yake ataipata.
 
Back
Top Bottom