Mama Mjane amlilia Rais Magufuli mbele ya Waziri wa Sheria

Hii ishu hata mimi nikifikiria naona kama kuna kitu.
Aliingia kama nani pale ndani ?
Lazima kutakuwa na mtu aliyempa sapoti kuingia pale , je mtu huyo ni nani ?
Hii inanikumbusha mikutano ya uponyaji ya akina nanihii
 
ninawezekana ni kweli ukimuangalia vizuri mlizi aliyekaa na magufuli pembeni ni kama kuna kitu kinaendelea
 
Ni kweli tukio limetokea na mama amefanikiwa kufikisha ujumbe. Lakini hapa kuna funzo tunalipata haswa kwa walinzi wa Rais. Kwa kweli inasikitisha sana kama iwapo yule mama alipenya na kufika kwenye tukio. Hili tukio limeacha maswali mengi kichwani mwangu.
Najiuliza je ile shughuli ilikuwa ya wazi, au iliruhusu watu wote wafike au ilikuwa ni ya watu mahsusi yaani waalikwa pekee? Na pia kama ilikuwa ya watu mahsusi yule mama alifanikiwa vipi kupenya mpaka akafika kwenye eneo la tukio? Au ina maana kuna sehemu iliteleza katika kufanya wa ukaguzi na mshika bango akafanikiwa kupenya? Au alikuwa mualikwa?
 
Penye utata mkuu ni kwamba tayari alisha kua na mawasiliano na mkulu tena ya sms.pia kwakua walisha kua na mawasiliano ilikuaje maamuzi hayakufikiwa kabla ya pale mkutanoni?

Swala la yule mama kuwa na bango pekeyake na kupenya msitu wa wanausalama hadi kufika pale mbele nalo sio la kupuuza hasa ukizingatia wanausalama wetu kiutendaji wakazi zao.
Sio jambo baya swala la huyo mama kupatiwa ufumbuzi.ila yatupasa iamshe akili zetu juu ya uwezo na utashi wa vyombo vyetu vinavyo husika na haki za raia.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mama mmoja ambaye ni mjane amefika mbele ya Rais kulilia haki yake, hakika kuna uwezekano hili suala linaenda na mtu

Kesi ya msingi hasa ni mirathi, hili jambo limekuwa likifanyika sana kwa watu wa hali ya chini.

Hii kesi inapande mbili ukimsikiliza IGP alivoulizwa na Mkuu wa Nchi, kwanza marehemu anamke zaid ya mmoja, pili kesi imeshughulikiwa na mawaziri zaid ya wawili na bado kesi ipo mahakamani.

Kwa mujibu wa mama kesi imefanyiwa judgements za aina mbili mama kapewa yake na hao nduguze pia, hii maana yake nini ?

Nilifungua huu Uzi ili nijue jinsi JPM alivyo " stage manage" hiki kituko sikuona.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mama mmoja ambaye ni mjane amefika mbele ya Rais kulilia haki yake, hakika kuna uwezekano hili suala linaenda na mtu

Kesi ya msingi hasa ni mirathi, hili jambo limekuwa likifanyika sana kwa watu wa hali ya chini.

Hii kesi inapande mbili ukimsikiliza IGP alivoulizwa na Mkuu wa Nchi, kwanza marehemu anamke zaid ya mmoja, pili kesi imeshughulikiwa na mawaziri zaid ya wawili na bado kesi ipo mahakamani.

Kwa mujibu wa mama kesi imefanyiwa judgements za aina mbili mama kapewa yake na hao nduguze pia, hii maana yake nini ?

Haliwezi kwenda na mtu
 
Jitahidi hivyo hivyo waweza kuukwaa uDC you know? Shida ni Mara nyingi Bendera Bin Peperuka wanakuwa na IQ ya single digits, dont you think so?
Mokili, achana na huyu Belo, jibizana na magreat thinkers wenzako. Huyu kapaniki ndiyo maana ameishia kutukana na kubwabwaja badala ya kutoa hoja kinzani ili tuipime.
Mimi binafsi natoa challenge hapa. Hebu mmoja wetu siku moja avamie mkutano wa rais bila taarifa kutoa malalamiko yake uone kipondo utakachokipata! Wataaminije nia yako ni njema hadi uruhusiwe kumvamia rais hadharani? Na ikitokea ukizungumza maneno ya aibu mbele ya kadamnasi na kumuaibisha rais? Ndio maana ninaamini kabisa kwamba ni wazi kwamba hili jambo lilikuwa linajulikana kinagaubaga na rais na walinzi wake na yule mama alisndaliwa na pia kufanyiwa upekuzi na rehearsal ya kutosha! Yule mama sliandsliwa na ikulu lunogesha ile event!
 
Hatimaye hukumu imetokaa jana mama anaejiita mjane ameshindwa vibaya mno.Haki itabaki kuwa haki hatautoe machozi ya simba.yaan raisi magufuli alipotoa amri ya suala hili nilijua mama mjane fake hatoboi na akifanya mchezo atafungwa ili iwe fundisho kwa wengine
 
Mkuu ongezea nyama basi, ikibidi anzisha Uzi mpya kabisa! Utapeli ni kipaji maza alikuwa anatembea na "Masijara" nzima kumbe yote mangumashi.
 
Back
Top Bottom