wangapi wanaweza haya maisha?
This is a very special case and unique in itself. Kwa hiyo hakuna sababu ya kudhani kwamba kuna watu wengine wanaweza kuiga. Hata hivyo ndoa zote ni unique. Hata ukiachana na mkeo au mumeo wa sasa na kuoa/kuolewa na mtu mwingine usitegemee kuendelea na mambo yetu ya sasa. Tunachoweza kujifunza hapa ni kuwa endapo watu wamechokana basi wapeane nafasi na muda ili kijitathmini kama kweli uamuzi wa awali ulikuwa sahihi. Time heals and unaweza kuona jamaa sasa wanaanza kujenga uhusiano ambao ni imara sana kuliko ule wa kwanza ambao ulikuwa na aina fulani ya usanii.
Hata hivyo naanza kujiuliza kama vijana wa kizazi cha sasa wana balanced hormones. Je wanaume wanazo testosterone (http://en.wikipedia.org/wiki/Testosterone#Physiological_effects) za kutosha na wanawake wanazo estrogen (http://en.wikipedia.org/wiki/Estrogen) za kutosha? Naona kama kuna michanganyiko inayofanya watu waanze kuwa na vitabia vya ajabu ajabu! Mwanamke mwenye estrogen ya kutosha atakuwa mwenye kuvutia na ku-attract mpezi wake wakati wote na siyo kumfanyia jeuri. Pia mwanamume mwenye testosterone za nguvu anataka kumwonesha mke wake kuwa ni mwanamume kweli. Siyo mwanamume wa kulia lia na kukimbia matatizo madogo madogo. I think the biology is messing up things!
ni kweli kila ndoa ni unique mzee, hao nakubali mia kwa mia
nadhani maisha ya isasa nayo ni tatizo. yanaonekana kuwalemea kwanza wanawake na kisha wanaume wanaathirika sawia. ni kwamba mwanamke anajaribu sasa kupitia harakati mbalimbali za kijamii na kisiasa kuondoka kwenye nafasi yake ya asili (natural)na kuisogelea nafasi ya mwanaume. hali hii inammpunguzia unyenyekevu na natural gestures na badakla yake anapata hard orientations kumwelekea mumewe ambaye hutarajia soft orientations. matokeo yake ndo unakuta watu wamo ndani ya ndoa kuheshimu sheria au kutunza watoto tu basi. motives zote za awali wakati wa urafiki wao kabla ya ndoa wanazicompromise kwa mambo haya.
naamini hawa ndugu zangu kwa sasa wako katika mchakato wa kujenga ndoa imara zaidi kuliko ile waliyovunja mahakamani. kwani hii ya sasa inasimama katika mioyo zaidi kuliko sheria. mchakato huu wa ujenzi wa ndoa mpya utakapokamilika hizo talaka watazichana wenyewe tena usishangae hata mbele ya waandishi wa habari! kwani kilicho ndani yao kitakuwa mature enough kushinda hata kifo. tusbiri tuone
natoa ushauri kwa wanawake kupuuza harakati zisizo na maana hasa zile zinazopelekea vi-ubishiubishi na ungangaringangari wa wanawake kwenye ndoa zao kwani hizi sio hulka za asili za mwanamke. pia havisaidii kitu zaidi ya kumpunguzia mwanmke mvuto kwa mumewe na hata mume akikubali ujue ni kama anafunika kombe mwanaharamu apite tu. mwisho wa yote nyumba ndogo zitatamalaki huku wanawake wakijidanganya kuwa zinasababishwa na tamaa za wanaume kumbe ni ujeuri wao ndani ya ndoa
vipi bro salama? au tuite ambalesi? naona umejiquote mwenyewe na kujijibu mwenyewe hapo juu. au jamaa kaiba pasiwadimmmh
Hi All,
Eneo la ndoa ni nyeti sana,na unapopata nafasi ya kuwa mshauri usiwaanike wenzako hadharani,Hii ni sehemu nyeti sana.
Kama wewe ni mshauri jifunze kutunza siri za watu,kwenye ndoa tunaongozwa na confidentiality(usiri wa kutatua mambo)
Kuwa mwangalifu kwa hili
Elisante Yona
vipi bro salama? au tuite ambalesi? naona umejiquote mwenyewe na kujijibu mwenyewe hapo juu. au jamaa kaiba pasiwadi
katika mchango wangu leo kwenye thread moja nilitoa kisa hiki cha kweli kama mfano wa kile nilichochangia. kutokana na utata wake nimeona niweke hapa kama thread inayojitegemea ili great thinkers wa JF wapate fursa ya kuijadili kwa kina kwani inatugusa sote na hususani ndoa zetu tunazozienzi daima.
kisa chenyewe ni hiki:
kuna jamaa yangu mmoja mkewe alikuwa jeuri sana hadi akampiga talaka. kwa sababu ya mtoto, jama hakumwondoa nyumbani mara moja bali alimtegea aondoke mwenyewe kwa hiyari yake na wakati wote alimpa mtaumizi kamili bila kukosa. haukupita muda yule bwana alimhurumia kwa kumwona hana raha, akamhakikishia kuwa kama hataondoka kwa hiyari yake, kamwe yeye hatamfukuzza na kumtaka aondoe mawazo, waheshimiane na kulea mtoto wao mpendwa. mama akaanza kupata amani moyoni, mume akajiona hana tena uhalali na wife kwani alishamkana. akapata nyumba ndogo, na wife akabaki kulea mtoto tu. yalipomshinda wife aliomba na anaendelea kuomba kila anapotaka na sasa ni mwaka wa pili na majuzi wamebarikiwa mtoto mwingine! wanmpenda na kumlea kwa furaha.
wasipokuambia habari yao, kamwe huwezi kujua kuwa wana talaka mikononi mwaao.
kuna wengine alifikiri ni hadithi na wengine wakasema inafafanana na filamu moja ya kihindi, lakini ni kisa cha kweli na mimi niliyekileta si tu nilichangia na kushiriki kwa hali na mali katika harusi yao bali pia nimekuwa mshauri wao mkubwa katika maisha yao ya ndoa ndio maana ni mmoja wa watu wachache sana wanojua habari hii hapa duniani.
kweli ndoa zina mambo. leteni maoni yenu tuwasaidie wenzetu na tujimulike nasi wenyewe tuko salama kiasi gani.
Mungu zibarki ndoa zetu.
HIVYO SUALA LA MWANAMKE MIMI KUNIAMBIA ETI LEO ANATAKA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA SAUTI YAKE NITAMSHANGAA SANA. ANACHOTAKIWA NI KUONYEDSHA DALILI TU. MFANO KULE TANGA, MWANAMKE AKIVAA KANGA MOJA BABA UNAJUA LEO MAMA ANATAKA KULA CHAKULA CHA WAWILI "TULE NA BWANA" SIYO MCHELE ULE WA SHAMBANI HAPANA HUO NI MCHELE MWEINGINE. KWA HERINI
wanawake wakifuata ushauri huu hakuna ndoa itakayovunjikakwa kifupi wote wawili wana kazi, tena kazi ya mama stable zaidi! wote wamesoma vizuri wana elimu ya juu!
nadhani tatizo la ndoa za siku hizi ni maadili zaidi, na sioni kama ni uchumi. mwanamke anajitahidi kuondoka kwenye nafasi yake anasogelea nafasi ya mwanamme, matokeo yake anaonekana jeuri na anapoteza mvuto kwa mwanamme. anapoanza unyenyekevu kwa mumewe, mapenzi nayo yanarudi taratibu. kumbuka kwenye tread ya msingi nilisema mahali, mwanamme alipomwona mkewe anakuwa mnyonge alimhurumia akamhakikishia kuwa hana mpango wa kumfukuza ndipo mwanmke alipopata amani.
kuna haja ya mwanamke ku-revisit nafasi yake ndani ya ndoa, wanaume naona wako tayari kuendelea kuwapenda wake zza ama watahesimu nafasi zao
wanawake wakifuata ushauri huu hakuna ndoa itakayovunjika
...............................
HIVYO SUALA LA MWANAMKE MIMI KUNIAMBIA ETI LEO ANATAKA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA SAUTI YAKE NITAMSHANGAA SANA. ANACHOTAKIWA NI KUONYEDSHA DALILI TU. MFANO KULE TANGA, MWANAMKE AKIVAA KANGA MOJA BABA UNAJUA LEO MAMA ANATAKA KULA CHAKULA CHA WAWILI "TULE NA BWANA" SIYO MCHELE ULE WA SHAMBANI HAPANA HUO NI MCHELE MWEINGINE. KWA HERINI
Kiufupi mama kajirekebisha na hapo ndoa yake itapona,wanawake wengi hudhani tendo la ndoa lazima liombwe na mmewe na kamwe yeye hawezi omba hata mkae miezi mingapi,hii inaleta ugomvi mkubwa,maana mwenzio anavumilia akidhani labda ikipita week moja utakuwa tayari,kumbe siku anayoomba ndo wewe hauko vizuri na kusababisha ugomvi,mi nadhani wamama wakigundua siri ya kuwa wao waanzishe mchezo hakuna mwanaume wa kugoma na hii inalinda ndoa.nakubaliana nawe mkuu, baada ya obligation kuondoka , wameanza kuishi kama wapenzi japo taratibu bila wao kujua. sikumoja mama alinidokeza kuwa siku hizi baba nae taratibu na kwa uangalifu ameanza kuomba mara mojamoja! penzi limeanza upya na nyumba ndogo karibu inakufa sasa. kubwa zaidi tangu wameanza maisha yao haya mapya sijawahi kuwasuluhisha ugomvi wowote tofauti na kabla ya talaka ambapo kila siku hata usiku wa manane unagongewa, ugomvi tena!