Mama Kilango ingekuwa vyema kama pia ungepigia kelele ufisadi unaotokea katika mahospitali yetu, kuna watu wanakufa kwa kukosa elfu tano ya kumpa nesi ili aongezewe damu, kuna watu wanafia hospitali kisa hawana vifaa vya kujifungulia, wananchi wanashindwa kusafirisha mazao yao kwa ajili ya kukosa miundombinu bora itakayowaunganisha na masoko ya mazao yao mijini, Je hili sio la kulipigia kelele kuliko hilo suala la EPA? Je hii ni nguvu ya soda kutuzuga wadanganyika tunyamaze kusema kuhusu mengine?
Nilidhani hapatakalika pale ambao bajeti ilionekana ina mapungufu mengi na sana waziri wa fedha kuonekana incompetent hadi asaidiwe? Je mama hili kwake lilikuwa halina haja ya kupigiwa kelele?
Well said! wenye access naye wamwambie kuwa we are sensing fishy here! Bajeti yenyewe haituondoi steji moja toka hapa tulipo, inazidi kutudidimiza. Hii bajeti ameiunga mkono asilimia mia. Jiulize, hii bajeti imeongeza shilingi ngapi kwa watanganyika wanaofanya kazi katika mazingira magumu! Kwanini hakusema kuwa hapatatosha kama mishahara ya walimu haitaongezwa? Kwanini asiseme hapatoshi kama barabara zetu hazitajengwa kwa kiwango kinachochochea maendeleo? Kama haridhiki na CCM kwanini asiseme hi;lo wazi na anaendelea kumsifu Jakaya ambaye kila mtu anmwona kuwa ni msanii!!!!?