Mama Killango Jitoe Ccm Kama Wewe Ni Mkweli!

Mama Kilango ingekuwa vyema kama pia ungepigia kelele ufisadi unaotokea katika mahospitali yetu, kuna watu wanakufa kwa kukosa elfu tano ya kumpa nesi ili aongezewe damu, kuna watu wanafia hospitali kisa hawana vifaa vya kujifungulia, wananchi wanashindwa kusafirisha mazao yao kwa ajili ya kukosa miundombinu bora itakayowaunganisha na masoko ya mazao yao mijini, Je hili sio la kulipigia kelele kuliko hilo suala la EPA? Je hii ni nguvu ya soda kutuzuga wadanganyika tunyamaze kusema kuhusu mengine?

Nilidhani hapatakalika pale ambao bajeti ilionekana ina mapungufu mengi na sana waziri wa fedha kuonekana incompetent hadi asaidiwe? Je mama hili kwake lilikuwa halina haja ya kupigiwa kelele?

Well said! wenye access naye wamwambie kuwa we are sensing fishy here! Bajeti yenyewe haituondoi steji moja toka hapa tulipo, inazidi kutudidimiza. Hii bajeti ameiunga mkono asilimia mia. Jiulize, hii bajeti imeongeza shilingi ngapi kwa watanganyika wanaofanya kazi katika mazingira magumu! Kwanini hakusema kuwa hapatatosha kama mishahara ya walimu haitaongezwa? Kwanini asiseme hapatoshi kama barabara zetu hazitajengwa kwa kiwango kinachochochea maendeleo? Kama haridhiki na CCM kwanini asiseme hi;lo wazi na anaendelea kumsifu Jakaya ambaye kila mtu anmwona kuwa ni msanii!!!!?
 
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!

JMushi1 nadhani statistically kusema kuna mwamko tofauti kwa wananchi kwa kutumia kipimo cha mijadala ya JF sio sahihi. Kungekuwa na mwamko unaousema then CHADEMA walikuwa na kila sababu ya kushinda Kiteto kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katikati ya kashfa kibao zinazohusu utendaji wa serikali. Nadhani wewe ndio unahitaji kufanya uchunguzi juu ya hali halisi.
 
Mama Kilango anaweza yote kuunga bajeti kusema kutajaa lakini hawezi kujaribu kujiondoa CCM.Hili hakuna wa kulipinga maana she just can't .

Swala la yeye kuunga bajeti mia kwa mia hilo nalo mie limeniacha hoi kabisa .
 
Mafisadi hawafai kushirikishwa katika kujadili mustakabali wa taifa and they belong in prisons lakini ni muhimu kupata jibu la swali hili: who is fisadi? the notion that being out of CCM is being non-fisadi is something I just cant agree.

Wote wale waliochota fedha kwa niaba ya chama.
Mzee Iddi Simba,lukaza na malegesi ndio connection ya chama na UFISADI..Wote hao wana ccm wenye uhusiano na hao niliowataja hapo juu wangeshafukuzwa uanachama.

Wote hao waliozianzisha zile kampuni feki ni ccm na makampuni hayo ya kijambazi ni ya ccm na viongozi wao flani flani ambao wana nguvu kiasi cha kwamba ndani ya chama huwezi waambia kitu hata iweje!

Narudia tena...Tafadhali soma kwa makini sababu nilizotoa ni kwanini hawezi kutenda mema akiwa ccm!
Na listi ni defu tu kiasi cha kwamba kama wakianza kamata kamata matajiri wote wa chama watakwenda ndani na ccm inaweza kufa!
Huo ni woga wa chama na si wa maslahi ya taifa!
Watanzania HUU NI WAKATI WA MUNGU...WAKE UP PLZZZZ!
 
Mama Kilango anaweza yote kuunga bajeti kusema kutajaa lakini hawezi kujaribu kujiondoa CCM.Hili hakuna wa kulipinga maana she just can't .

Swala la yeye kuunga bajeti mia kwa mia hilo nalo mie limeniacha hoi kabisa .

kwa sisi wananchi shida zetu zingepungua sana pale ambapo angepiga zile kelele kwa ajili ya bajeti mbofu mbofu kama aliyoitoa Mkullo: Sio wanahistoria lakini nadhani this is the most incompetent minister of finance we have ever had kwenye bunge letu, mbona mama alimpigia makofi. Ningekuwa na confidence na Mama Kilango kama angeweka kura ya no kwenye kuipitisha ile bajeti, whats so special with EPA wakati alijua fika report yake iko karibuni kutolewa?
 
JMushi1 nadhani statistically kusema kuna mwamko tofauti kwa wananchi kwa kutumia kipimo cha mijadala ya JF sio sahihi. Kungekuwa na mwamko unaousema then CHADEMA walikuwa na kila sababu ya kushinda Kiteto kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katikati ya kashfa kibao zinazohusu utendaji wa serikali. Nadhani wewe ndio unahitaji kufanya uchunguzi juu ya hali halisi.

Sio based on jf trust me!

Nenda makanisani na misikitini ambapo wapiga kura wanakutana kila mara...mamilioni ya wananchi..Sasa kama wewe hujui wananchi wana mawazo gani then sitashangazwa.

We unafikiri wananchi humo wana raha na ccm?

Especially this time ambapo wanaweza ku link njaa zao,magonjwa yao,ukosefu wa huduma za afya na matatizo ya umeme aliyosababishwa na RICHMOND!

Si tu kuwa taifa letu bado linaendelea kuwalipa mafisadi fidia...Bali pia limepoteza mabilioni mengine kwa kutukosesha umeme ambao ulipelekea uchumi kulala hence matatizo zaidi kwa mtanzania masikini...Mtanzania masikini aliyegundua kuwa yeye ni tajiri na umasikini wetu ni wa kifikra na utawala bora wa kizalendo wenye kujali maslahi ya taifa na watu wake kwa ujumla!
 
Nashukuru kwa maoni yako lakini this time around there is an EXTREMELY DIFFERENT SITUATION HENCE DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY AND MAYBE THE WORLD!
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!

Huu mwamko wa tofauti uko wapi? Umejiuliza ilikuwaje Chenge na Lowassa wakapokelewa kwa Shangwe kama Wafalme katika majimbo yao? Hivi unafikiri na hoja zote za kuwatuhumu Chenge, Lowassa, Mkulo, Karamagi, Msabaha leo kukifanyika uchaguzi mkuu wakakosa kura za kuwarudisha Bungeni?

Umeulizwa swali zuri sana, kuwa kama nyakati hizi ni za mwamko na mageuzi, ilikuwaje Upinzani ukapigwa ngwala Kiteto?

Be realistic my friend. Hizi kelele za kufoka "kamata mafisadi" zinanikumbusha wakati Lyatonga alipokaribia kuondoka CCM na hata alipoondoka.

Kama ulikuwa mdogo miaka 16 iliyopita, nitakupa kilichotokea na huyo Lyatonga ambacho kilifikia mahali kuanguka vibaya katika siasa za Tanzania.

Mrema alipojitoa CCM baada ya kuvuliwa Uwaziri, alianza kuhangaika kama malaya akitaka ukuu kwa kuwa alijiona kuwa ule umaarufu wake ndio ngao pekee.

Mind you this is typical political behaviour ya Wanasiasa Tanzania ambao wana umashuhuri kujiamini kuwa wao ni Alpha na Omega.

Alikwenda Chadema akamwambia Mtei ampishe Uenyekiti kama sharti la yeye Mrema kujiunga Upinzani. Mtei akamwambia, kwanza inabidi uwe mwanachama, pili itabidi upitie kila ngazi zinazotakiwa ukisubiri wakati Chadema ifanye mkutano mkuu ugombee uenyekiti, na kama ni kutaka kuwa mgombea wa Uraisi kwa Chadema, basi ni shurti upitie mchakato kama wengine. Mrema akalikataa hili, akaenda NCCR ambako wale wanausalama wenzake Mabere Marando, Lamwai na wengine ambao walikuwa ni viongozi, wakampa Uenyekiti harakaharaka ili NCCR kipate umaarufu.

Kilichofuata ni mtiririko wa vurugu ndani ya NCCR mpaka akafukuzwa akaenda TLP ambako nako bado hakujawa na salama.

Una lengo zuri kutaka mabadiliko yafanyike, lakini jifunze kuwa Historia inatuambia nini?

Kama unafikiri kujitoa CCM na kukimbilia Upinzani ni kazi rahisi, waulize wazee makini kama Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, John Malecela na hata Edward Lowasa wa 1995, kwa nini walibakia CCM na hawakukimbilia huko unakosema ndiko kwenye njia pekee.

Unaposema CCM ni mafisadi, je una maana CCM nzima au sehemu ya CCM ina mafisadi? Maana kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa CCM ni chama pekee chenye wanachama wengi kuliko vyama vyote vya upinzani vikijiunga. CCM imejijenga mijini na vijijini kiasi kuwa kila mtu anavuta pumzi inaitwa CCM.

Je unafikiri kuhama CCM ndio suluhisho pekee? Mwanasiasa makini wa CCM kamwe hawezi kufanya kosa la kujidhuru na kujitia kitanzi kama alivyofanya Mrema au Tambwe Hiza!
 
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!

Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.

Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!

Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.

Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.

Ni hayo tu kwasasa...

Ushauri wa bure tu ambao unahitaji wewe kujiandaa kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimboni kwake. kwi kwi kwi ..............
 
Mchungaji mwulize kakobe waumini wake wana maoni gani na ccm!

Hivi hawa kina kilaini unafikiri wamejiamulia wao wenyewe kuzungumza?

Nimeshawapa ushauri wangu viongozi wa dini na kama wasipoufuata...wasishangazwe na waumini wao kuyumba imani dhidi yao!

Wanajua kuwa waumini wao wameshaelewa UFISADI wa ccm na hata hao watumishi wa Mungu wenyewe ambao wengi wao ni ccm hawawezi kuitetea tena ccm kwani haiteteeki!

Unafikiri kwanini wabunge wengi na viongozi wa serikali wanatembea mtaani kwa tabu na wananchi hawataki hata kuwaona?

Vyombo vya habari tayari kuna vilivyonunuliwa...Haya mambo ya chenge kwenda huko kijijini kwake na kuutangazia umma kwa mbwembwe kuwa alipokelewa vyema JIMBONI ni propaganda za wazi wazi!

Na pia kuna wana ccm wengine ambao hawakupendezwa na vitendo vya wanakijiji hao wazembe wasio na uelewa ambao labda nao wamerogwa!

Mkapa alivyoona hivyo na yeye akaenda na kuongea nao lugha ya kitoto..."Uongo uongo uongo"

Unafikiri ni kwanini kuna wabunge waliotamka wazi wazi kuwa wananchi wana hasira?

Mchungaji hata kama hauishi bongo...Jaribu kufuatilia mambo bila kuwa na bias na utaujua ukweli!

Huyu Kigoma naye ndiye yule mbunge wa huko kigoma wa ccm nini?

Maana michango ake yote inaelekea elekea huko...Na pia anaonekana ni mtu mwenye kuzijua nyeti na msomi!
Jitokeze tu kigoma tukate issue.

NB:Naomba pia ujifunze na historia...SADDAM HUSSEIN BADO ANAPENDWA SANA HUKO KIJIJINI KWAKE..INA MAANA ALIKUWA SAFI?
WAPI BAATH PARTY...CHAMA KILICHOSHIKA UTAMU KWA MIAKA ZAIDI HATA YA HII ccm?
 
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!

Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.

Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!

Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.

Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.

Ni hayo tu kwasasa...

Hana sababu yoyote ya kutoka CCM, wakati mwngine ni rahisi kuleta mabadiliko ndani ya chama kama ukiendelea kuwemo ndani na siyo ukiwa nje. Akitoka atakuwa amewapa ushindi mkubwa mafisadi. Muasisi wa Chama Mwalimu Nyerere alikuwa anawachamba viongozi mbali mbali ndani ya CCM na sirikali na hakutoka CCM.

Mbona akina Mwinyi, Butiku, Warioba, Kawawa, Msuya na wengineo ambao wamewasemea hovyo mafisadi ndani ya chama na serikali hamuwaambii wajiengue ndani ya Chama? Kulikoni?

Mama Kilango huu ni mwanzo tu, endelea na juhudi zako za kupambana na mafisadi ndani ya chama na serikali, Watanzania wengi tuko nawe bega kwa bega katika hili. Uwe makini mno katika movement zako za kila siku na Mungu atakulinda.
 
JAY EFU PATAMU...OK atueleze atakavyoibadilisha ama kuisafisha ccm wakati yeye na mwenyekiti wake wanaamini haina mafisadi na wala haina uchafu wowote ule!

Wachawi na wauwaji wako naye meza moja!Na yeye bila aibu..Ameshirikiana nao kupitisha BAJETI YA KIFISADI Huku akiwaambia warudishe pesa walizodokoa ambazo labda hadi sasa zisharudishwa ama karibia zote.

Wamewatreat MAFISADI kama vile ni watoto wadokozi waliokubali kurudisha kile walichodoka kabla ya kukila...Usaniii!

Bubu unataka wasafishe uchafu ambao wanasema HAUPO?

Mwalimu alipokufa ccm ilikufa naye..TRUST ME!

Kaburini walipoenda haikusaidia lolote!

Kusafisha chama ni KUWASAFISHA MAFISADI...WHERE AS WANANCHI NOW KNOWS THAT KUWAKAMATA MAFISADI IS THE NEEDED JUSTICE...KINDA JUSTICE THAT THE PEOPLE NEED IT DESPARATELY...ITS A DEFING MOMENT NA NINAWAOMBA WASCRATCH OFF PLAN "A" KUTOKA KWENYE KILE KIKAO CHAO CHA SIRI MKAPA ALICHOHUDHURIA!

Waje na plan B lakini wawe makini kuna JMUSHI1 PIA!
 
JAY EFU PATAMU...OK atueleze atakavyobadilisa ccm wakati yeye na mwenyekiti wake wanaamini haina mafisadi!

Mpe muda!!!! Ameshatamka mara chungu nzima kwamba si sawa kundi la watu wachache kuhodhi utajiri mkubwa wa nchi wakati asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi maisha ya dhiki. JK alipoingia madarakani tulimpa muda wa kutosha kuyafanya yale aliyotuahidi Watanzania kwenye kampeni, na baada ya muda wengi wetu tukasema kwamba kumbe jamaa ni msanii tu.

Tumpe muda huyu mama tuone juhudi zake alizoanzisha za kupambana na mafisadi ndani ya chama na serikali zinafikia wapi, halafu hapo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuhititimisha kama juhudi hizo zilikuwa ni za kweli au ni usanii tu.
 
Mpe muda!!!!

Kwa uelewa wetu..Ameshakubaliana na mwenyekiti wake na MAFISADI kwa kupiga kura ya ndiyo kwenye bajeti yao ya KIFISADI PAMOJA NA KUKUBALI KAULI ZA M/KITI KUWA CHAMA NI SWAFI..YEYE LOWASA,CHENGE NA WENGINEO WALIPIGA KURA YENYE MWELEKEO WA KIFISADI FISADI...SASA HAPO KUNA HAJA GANI YA KUINGIA KWENYE KICHWA CHA MTU...EVERYTHING NI WAZI NDUGU!
 
Kwa uelewa wetu..Ameshakubaliana na mwenyekiti wake na MAFISADI kwa kupiga kura ya ndiyo kwenye bajeti yao ya KIFISADI PAMOJA NA KUKUBALI KAULI ZA M/KITI KUWA CHAM NI SWAFI...SASA HAPO KUNA HAJA GANI YA KUINGIA KWENYE KICHWA CHA MTU...EVERYTHING NI WAZI NDUGU!

Hayo ni mawazo yako lakini kwa maoni yangu bado ana nafasi kubwa ya kupambana na ufisadi, hii si vita ya siku moja eti katika bunge lenye wabunge zaidi ya 250 wa CCM Anna Kilango akipiga kura ya kutosupport bajeti basi ndiyo atakuwa ameshinda katika vita hivyo.

Lazima awe na strategy kali na siyo kukurupuka tu!!! Sasa kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa hajafanya lolote katika vita dhidi ya mafisadi bali angekuwa amevuruga mikakati na si ajabu baadhi yetu tungemkejeli sasa hiyo kura yako ya hapana ndiyo imesaidia nini katika kupambana na ufisadi? Mambo hayaendi pupa kaka...mpe mama muda kabla hujaanza kumzodoa!!!
 
KIKAO CHA SIRI CHA ccm ALICHOSHIRIKI YEYE NA KINA MKAPA NA CHENGE HUKO KWENYE KABURI LA NYERERE NA KWENDA KUMALIZIA KWA KUJIPONGEZA NA KURA YA NDIYO YA KIFISADI HUKO BUNGENI NDIO MWANZO WA MWISHO WA UMAARUFU WAKE HUU WA MOTO WA KIFUU KAMA AKIBAKI ccm TRUST ME ON THIS...THE RESOLVE IS CERTAINLY AT THE HIGHEST LEVEL EVER!
 
KIKAO CHA SIRI CHA ccm ALICHOSHIRIKI YEYE NA KINA MKAPA NA CHENGE NA KWENDA KUMALIZIA KWA KUJIPONGEZA NA KURA YA NDIYO YA KIFISADI HUKO BUNGENI NDIO MWANZO WA UMAARUFU WAKE HUU WA MOTO WA KIFUU KAMA AKIBAKI ccm TRUST ME ON THIS...THE RESOLVE IS CERTAINLY AT THE HIGHEST LEVEL EVER!

Haya mambo hukurupuki tu bila kuwa na mikakati na kuangalia na wale unaopambana nao wana mikakati gani, vinginevyo zitakuwa ni mbio za sakafuni....
Hebu tueleze kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa amefanikisha lipi katika vita dhidi ya mafisadi?
:confused:
 
Haya mambo hukurupuki tu bila kuwa na mikakati na kuangalia na wale unaopambana nao wana mikakati gani, vinginevyo zitakuwa ni mbio za sakafuni....
Hebu tueleze kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa amefanikisha lipi katika vita dhidi ya mafisadi? :confused:

Waulize wale ambao at least wali abstain!
Kwanini hakujiunga nao?
Niliazisha thread na kuwapa ushauri kuwa wasishirikiane na Mafisadi kuamua mustakabali wa nchi wakati hao watu walitakiwa kuwa rokapu aroo!
Tumia akili BUBU.
 
Miye sina akili, akili unazo wewe tu!!!
 
Hayo ni mawazo yako lakini kwa maoni yangu bado ana nafasi kubwa ya kupambana na ufisadi, hii si vita ya siku moja eti katika bunge lenye wabunge zaidi ya 250 wa CCM Anna Kilango akipiga kura ya kutosupport bajeti basi ndiyo atakuwa ameshinda katika vita hivyo.

Lazima awe na strategy kali na siyo kukurupuka tu!!! Sasa kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa hajafanya lolote katika vita dhidi ya mafisadi bali angekuwa amevuruga mikakati na si ajabu baadhi yetu tungemkejeli sasa hiyo kura yako ya hapana ndiyo imesaidia nini katika kupambana na ufisadi? Mambo hayaendi pupa kaka...mpe mama muda kabla hujaanza kumzodoa!!!

Mkuu Bubu Bravo, hapa tupo ukurasa mmoja bro! Saafi sana ni kuchapa fimbo tu! yees chapa bakora tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom