Mama Killango Jitoe Ccm Kama Wewe Ni Mkweli!

Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!

Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.

Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!

Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.

Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.

Ni hayo tu kwasasa...

Jmushi, kumbe wewe ni kati ya wale wanaokimbia matatizo! Mama Kilango anatakiwa abaki humo humo ili aweze kumwaga Nyuki wengine tule asali kama anavyofanya sasa Bunge.

Kwa mfano, akahamia NCCR MAGEUZI unafikiri masuala ya EPA na mengineyo utayasikia wapi?

Cha msingi ni kumuombea kwa Mungu, akiwemo na Mhe. Mwakyembe waendeleze libeneke na kama inawezekana wapatikane wengine humo humo chamani kuyaweka haya sawa.
 
Mushi,

Siasa za Tanzania huzijui, kama ungezijua vizuri na kwa umakini, ungemuelewa Bubu.

Mtikila alikuja na hoja nzuri sana, akapata wafuasi wengi sana, kisha kama mshumaa kwenye tufani ukazimika, mwangaza uliporudi, umahiri wake ukaonekana batili na hata sasa pamoja na kuwa kaongea mengi ya maana, anaonekana kama Mwendawazimu.

Mzee Cheyo wa Mimose, alikuja mputa na moto wa kifuu, akasikilizwa, akabanwa kende, sasa ni mgombea binafsi (chama chake ni dhaifu mno) haishi kuandamana na kauli za chama Tawala.

Utakapoelewa uimara wa CCM, labda unaweza kupata ufunuo kujua kuwa kazi ya kuing'oa CCM si kazi rahisi.

Wengine tunachofanya sasa si kukimbilia CCM kama Chama, bali ni kukata vichwa viwili vitatu ambavyo viko CCM ili magonjwa yasitambae.
 
Mkuu Bubu Bravo, hapa tupo ukurasa mmoja bro! Saafi sana ni kuchapa fimbo tu!

FMES Kama ulimpigia mama simu na kuwa ukweli najua anaweza akawa anafuatilia huu mjadala...Naona message ni ALUTA CONTINUA!
Najua ulisita kusema kitu hadi usikie kutoka kwake...Na kwasababu mimi nina kipaji nilichopewa na Mungu..Ni wazi kuwa amekataa kutoka ccm...Haya sasa mjadala umeanza RASMI...Na tutaona utakapoishia maana every second of every minute of every hour matters like never before!
 
Mushi,

Siasa za Tanzania huzijui, kama ungezijua vizuri na kwa umakini, ungemuelewa Bubu.

Mtikila alikuja na hoja nzuri sana, akapata wafuasi wengi sana, kisha kama mshumaa kwenye tufani ukazimika, mwangaza uliporudi, umahiri wake ukaonekana batili na hata sasa pamoja na kuwa kaongea mengi ya maana, anaonekana kama Mwendawazimu.

Mzee Cheyo wa Mimose, alikuja mputa na moto wa kifuu, akasikilizwa, akabanwa kende, sasa ni mgombea binafsi (chama chake ni dhaifu mno) haishi kuandamana na kauli za chama Tawala.

Utakapoelewa uimara wa CCM, labda unaweza kupata ufunuo kujua kuwa kazi ya kuing'oa CCM si kazi rahisi.

Wengine tunachofanya sasa si kukimbilia CCM kama Chama, bali ni kukata vichwa viwili vitatu ambavyo viko CCM ili magonjwa yasitambae.

Mimi si mtikila wa mwanzo...Mimi ni Jmushi ambaye labda ni kama mtikila mpya aliyegundua haki ni SHERIA!
MAFISADI WAKAMATWE...SHERIA INASEMA!
 
To be honest, I find it really strange and utterly naive to dismiss Mama Kilango's point of view on the basis that he did not oppose the parliament's move to punish Zitto. People on this side of the debate are using a wrong premise and therefore their conclusion is definetely flawed.

Sanasana naona mnajaribu kuwagombanisha wabunge wetu "mahiri" kwa wananchi pasipo sababu za msingi. Kazi ya msingi ya mbunge ni kutetea wananchi na nchi yake pale serikali inapojaribu kwenda kinyume na majukumu yake ya msingi. Hivi ndivyo alivyofanya Zitto na ndivyo alivyofanya Mama Kilango na wabunge wengine kadhaa hivi karibuni. Sasa kwa nini tuhoji dhamira ya mama Kilango? Viongozi wa kisiasa wanapimwa kwa maneno na matendo yao; hatuwezi kuwapima kwa yale wanayoyafikiria maana kamwe hatuwezi kuyajua. Ningeelewa hoja hizi kama mama Kilango ali-flopflip. Yaani kama kuna wakati alitetea wizi wa EPA na sasa anapinga. Otherwise, tusije tukajikuta nasi tunaanza kuwashindanisha wabunge wetu kwa umaarufu. Huo utakuwa ni uhuni maana wanayoyafanya akina mama Kilango ndivyo wanavyopaswa kuwa wanafanya siku zote.

Tatizo ninaloliona mimi hapa ni kwamba hatujazoea viongozi wetu, wakiwemo wabunge, wakitekeleza wajibu wao kiasi kwamba siku wakifanya wajibu wao inakuwa taabu kiasi cha kuwa news na kuzaa threads na threads kwenye mitandao ya internet. Yaani viongozi wametufikisha mahala ambapo sasa tunaona kwamba kutekeleza wajibu wao imekuwa ni upendeleo kwa wananchi unaostahili tuzo na pongezi kemukemu. Katika hali ya kawaida hatupaswi kuwa tunajadili na kupongeza au kuhoji dhamira ya mbunge kuibana serikali bungeni maana kwa kweli hii ndio kazi yao. Kwa utaratibu huu itafika mahala wanafunzi watakuwa wanaandamana kumpongeza mwalimu wao kwa kukumbuka kuingia darasani kufundisha kipindi chake!

Mkuu Mushi,

Heshima mbele bro, soma hapa uone maan ya kitu tunaita kichwa, yaani points mwanzo mpaka mwisho, vyama nyuma taifa mbele!

Ahsante Mkuu
 
Mkuu Mushi,

Heshima mbele bro, soma hapa uone maan ya kitu tunaita kichwa, yaani points mwanzo mpaka mwisho, vyama nyuma taifa mbele!

Ahsante Mkuu

Mama na kikwete lao moja tu!

MASLAHI YA ccm YAMEZIDI YALE YA TAIFA!

Zitto naye honestly namshauri awe extremely careful!

Mama na kikwete walimpa kazi kwenye kamati iliyokuwa na MAFISADI kwa utaratibu ule ule wa kuchanganya wachafu na wasafi ili kuuwa soo!
Tushaona looong time!

Naomba unieleze mshahara na marupurupu ya hao wanakamati halafu ujue ni kwanini offer ilikuwa ni too nzito kuikataa!

KAMATI AMABYO SASA TUNAJUA ILIKUWA NI UFUJAJI WA PESA ZA WATANZANIA KWA KUNYAMAZISHANA NA KUTEGANA!

Ripoti ya kamati ya madini kwa sinclair nayo hatujui nani alimpekea huko sijui ni canada au wapi!

Narudia tena...NI MUHIMU KUWA MAKINI!

Kikwete alitegwa,katega na mchezo unaendelea...Ila tunafuatilia kwa karibu..Ushauri wangu waje na plan B kwani najua lazima ipo!
 
Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kama ninakuelewa ni kwamba ili mama aweze kuwa kiongozi mzuri ni lazima afuate masharti yako Mushi, ama sivyo anakuwa hafai sawa sawa mkuu nimekusikia sana!
 
Kama ninakuelewa ni kwamba ili mama aweze kuwa kiongozi mzuri ni lazima afuate masharti yako Mushi, ama sivyo anakuwa hafai sawa sawa mkuu nimekusikia sana!

Hapana...Mjadala uendelee tu huku nnyie mkitafakari PLAN B kwani najua ipo!
Ila mki get personal mtazidi kujishushia hishma!
Sijaweka masharti...Nimeweka hoja ya kuwa ni kwanini HAWEZI KUSAFISHA UCHAFU WASIOUONA AMBAO WANACHI WANAUONA!
 
Hapana...Mjadala uendelee tu huku nnyie mkitafakari PLAN B kwani najua ipo!
Ila mki get personal mtazidi kujishushia hishma! Sijaweka masharti...Nimeweka hoja ya kuwa ni kwanini HAWEZI KUSAFISHA UCHAFU WASIOUONA AMBAO WANACHI WANAUONA!

Kwa hiyo kwa maoni yako mkuu mama akitoka tu ndio atakuwa kiongozi safi, au? Labda kuna something I am missing?
 
Kwa hiyo kwa maoni yako mkuu mama akitoka tu ndio atakuwa kiongozi safi, au? Labda kuna something I am missing?

Huu mpango wa ccm kusafishana mbele za macho ya mtanzania haukuanza leo...Hii ni post kwenye ile thread yangu ya kuwataka wakamatwe na si kututega na kutugawa kama ilivyo wazi hapa jf...Jambo ambalo nilitabiri na nikaanzisha thread waaay befoe!
Mkuu fwatilia thread zangu utaona kama wazalendo hawatashinda!

Chenge: Nimezushiwa

na Jane Kajoki, Bariadi



MBUNGE wa Bariadi Magharibi aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni kwa kashfa ya kukutwa na fedha zinazohusishwa na ufisadi, Andrew Chenge amewataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumwamini kwa kuwa yeye ni mtu safi na asiye na hatia yoyote kwani tuhuma dhidi yake ni za kuzushwa.
Mbali ya hilo, Chenge alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu zaidi ya wiki mbili zilizopita si kwa sababu ya kukiri makosa, bali ili kutoa fursa kwa taasisi zinazochunguza kashfa yake kufanya kazi yake kwa uwazi.
Chenge ambaye jana alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Bariadi Mjini, Ramadi, Nyakabimbi na Kapiwi, alisema wakazi wa Dar es Salaam ndio ambao wamekuwa wakimuona kuwa mtu asiyefaa kutokana na kubebeshwa tuhuma zisizo za ukweli, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa kifo.
“Dar es Salaam wanasema sifai labda kwa sababu ya sura yangu...Pamoja na watu wa Dar es Salaam kupiga kelele kuwa sifai, naamini sina hatia yoyote, na ndiyo maana nilijiuzulu. Ninyi wakazi wa jimboni kwangu ndio mnajua kama sifai au nafaa.
“Haya mambo yaliyotokea ni ajali ya kisiasa. Ni mambo ya kupikwa na watu, lakini kwa tuhuma hizi wacha tuwape nafasi waendelee na uchunguzi. Sitakiwi kuzungumzia hilo kwa sasa, nimekuja nyumbani kuhimiza shughuli za maendeleo katika jimbo letu katika nyanja zote za barabara, elimu, afya na maji,” alisema Chenge ambaye alivuta umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimshangilia kila alipokuwa akihutubia.
Alisema pamoja na kujiuzulu uwaziri, aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na akasema anaamini ifikapo mwaka 2010 atakuwa ametekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.
“Walio na ndoto za ubunge tukutane kwenye hoja za utekelezaji wa ilani mwaka 2010. Mmeona tulivyojenga shule za sekondari, barabara, mabwawa, visima, vituo vya afya vyote hivyo ni katika jimbo letu. Pamoja na habari ya kuzushiwa kifo, nawaomba mtulie, tushirikiane kwa kutembea kifua mbele kufanya kazi na kujiletea maendeleo,” alisema Chenge ambaye anatembelea jimbo lake kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu.
Akiwa katika Kijiji cha Dutwa alisema alitaja vijisenti si kwa nia ya kukejeli bali akiwa na mtazamo wa Kisukuma ambao wao wanapoongelea ng’ombe 100 kwa mfano wanasema ‘vijing’ombe’.
Hii ni mara ya pili kwa Chenge kuzungumzia kauli yake ya vijisenti ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo inayoonekana kuwa iliyokuza tuhuma alizokuwa akihusishwa nazo.
Kwa mara ya kwanza, Chenge alizungumzia kauli yake hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, ambapo aliwaomba radhi Watanzania ambao walikwazika au kuumizwa na kauli yake hiyo ya vijisenti.
Alisema halikuwa lengo lake kuwakera wananchi kwa kauli hiyo iliyozua mjadala kiasi cha baadhi ya makundi ya watu wa kada tofauti kutoa maoni yao wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.
“Mimi siyo Mzaramo. Hiki ni Kiswahili. Sisi wengine kule Usukumani kusema vijimambo, au vijisenti, vijitoto hivi ni kawaida kwa desturi zetu...ndiyo maana napenda kusema wazi kwamba iwapo kuna Watanzania niliwaumiza kwa kauli ile niliyoitoa kwa nia njema kabisa na wala si kwa lengo la kuwakejeli, naomba radhi kwa hilo,” alisema Chenge wakati huo.
Tuhuma dhidi ya Chenge ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza likikariri taarifa kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini humo (SFO).
Gazeti hilo liliandika kuwa, uchunguzi wa SFO uligundua akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.
Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ilikuwa ikitarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zilikuwa na uhusiano na zile zinazoaminika kuwa zilitolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.
The Guardian katika habari yake hiyo liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo,” alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.
“Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa,” alisema mwanasheria huyo wa Chenge. Hata hivyo, gazeti hilo liliandika uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa. Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu, na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.

Ndugu wana JF...Kama si kuwagawa wananchi.."Then kuwa mtu wa Dar es Salam, ama kuwa mtu wa Mara...Kuwa Mzaramo ama kuwa Msukuma"

Vinahusiana vipi na yeye kutuhumiwa na Taifa kuwa ni FISADI?

MWENYE JIBU NAOMBA ANIPE TAFADHALI!

NB: Je Muungwana anakubaliana na Chenge kuwa eti ni "Ajali ya Kisiasa?"

Na kama si hivyo..then mbona hakamatwi?

WAPI BALALI?
 
Plani ya chenge na mkapa ilipokwama...kuliwaka moto kwani watu walishangazwa sana...ccm na kina CHENGE,MKAPA,KIKWETE,LOWASSA,MRAMBA,KILLANGO NA WENGIENEO Wakaamua wakakutane huko kwenye kaburi la mwalimu.

Wakaja na PLAN...Mara uchawi,mara habari kibao kwenye vyombo vyetu ambazo hata hazigusii ufisadi tena utafikiri watu tayari wako jela...

Mkapa awasha moto



na Salehe Mohamed



UAMUZI wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanza kujibu tuhuma dhidi yake, umeibua malumbano ya hoja kutoka kwa wanasiasa kadhaa ambao wameeleza kushangazwa na majibu na hatua yake hiyo.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa maoni yao kuhusu kauli hiyo ya Mkapa, ni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumrushia makombora ya tuhuma rais huyo mstaafu, akifanya hivyo ndani ya Bunge.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kimaro alimtaka Mkapa kujibu tuhuma dhidi yake na kuacha kuwanyoshea kidole wengine kwa matatizo anayokabiliana nayo.
Katika kauli yake hiyo, Kimaro alisema alielekeza tuhuma kwa Mkapa si kwa sababu ya chuki au kwa kuwa alinyimwa nafasi yoyote ya kimadaraka serikalini kama alivyodai kiongozi huyo mstaafu, bali alifanya hivyo kutokana na kuwa na mapenzi ya dhati kwa taifa lake.
Alisema kuwa, alichokisema kilitokana na kuwa na moyo wa kuwaonya viongozi mbalimbali kutokana na kutumia madaraka yao vibaya na kwa masilahi binafsi.
Alisema ushahidi wa Mkapa kujihusisha na biashara akiwa Ikulu upo Mamlaka ya Usajili wa Leseni na Biashara (Brela), Tanesco na taasisi nyingine zinazohusika na mambo ya biashara, hivyo alichokisema si jambo la kutunga au kumzushia kiongozi huyo kwa sababu ya chuki binafsi au nyinginezo.
“Mimi sitarajii uongozi serikalini, nilishafanya kazi huko nikaamua niendelee na mambo mengine, nitakuwa muwazi siku zote… kamwe sitaki unafiki na yoyote anayefikiri nilifanya hivyo kwa ajili ya kumlenga Mkapa anakosea… nilifanya vile kwa sababu ya kuisimamia serikali na viongozi wengine wasielekee kule kusikofaa,” alisema Kimaro.
Alisema tabia ya viongozi kusema kuwa nchi ina amani, utulivu na rasilimali nyingi haina mantiki kwa wananchi, iwapo hawataona uwajibikaji wa viongozi na matumizi sahihi ya rasilimali zao katika jitihada za kuwakomboa katika lindi la umasikini.
Kimaro alisema hatarajii kufanya siasa za kumchafua mtu, bali anachokifanya hivi sasa ni kile alichotumwa na wananchi wake, hivyo si vema mtu kumhusisha na dhana mbaya dhidi ya viongozi anapotimiza wajibu wake aliotumwa na wapiga kura wake wenye kiu ya maendeleo.
Wakati wa kikao kilichopita, Bunge lilipokuwa likijadili Muswada wa Sheria ya Nishati, Kimaro alimtuhumu Mkapa kwa kutumia vibaya madaraka yake kujinufaisha wakati akiwa madarakani.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe, alisema mtindo alioutumia Mkapa kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake unaweza kuzaa matatizo mengine na kusababisha malumbano yasiyokwisha.
Akitoa ushauri wake, Wangwe alisema kwa kuwa Mkapa anaonekana kuwa ameamua kuanza kujibu tuhuma hizo, anatakiwa kujitofautisha na watu wanaoonekana kujitafutia huruma kupitia kuwachafua watu wengine.
Alisema ili aaminike, Mkapa anapaswa kutoa utetezi wake chini ya kiapo cha mahakama kuhusu kutohusika kwake na ufisadi, ili kuwawezesha wapinzani na wananchi kufuatilia mali zake, badala ya kujitetea mkoani kwake.
Akizungumza na waandishi kuhusu utetezi wa Mkapa alioutoa mwishoni mwa wiki iliyopita, Wangwe alisema kuwa, kauli hiyo ya rais huyo mstaafu haina uzito wowote kwa Watanzania, bali kama kweli ana nia ya kusafisha jina lake akale kiapo mahakamani kuhusu kile anachokisema.
Alisema baada ya hapo, ufuate uchunguzi dhidi yake, ufanyike kulingana na kiapo hicho na kama atabainika kufanya biashara akiwa Ikulu, kiapo hicho kitumike kama ushahidi dhidi yake.
“Leo hii Mkapa hawezi kusema mambo kirahisi rahisi namna hii… anapaswa akale kiapo mahakamani na serikali ifanye uchunguzi juu ya kile alichokisema na kama itathibitika kuwa kafanya ufisadi akiwa madarakani, basi kiapo kile kiwe sehemu ya ushahidi,” alisema Wangwe.
Wangwe alisisitiza kuwa Mkapa hawezi kuepuka dhambi ya ufisadi, kwani wasaidizi wake wengi akiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wake, Andrew Chenge, wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimsaidia kugeuzageuza mikataba mbalimbali kwa lengo la kujinufaisha.
Alisema ni jambo lililo wazi kuwa Mkapa alikuwa akifanya biashara akiwa Ikulu na kibaya zaidi alikuwa akitumia anwani ya Ikulu kwa masilahi binafsi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya maadili ya watumishi wa umma na viongozi, lakini kwa sababu ya tamaa za madaraka aliamua kupindisha sheria hiyo.
Katika mtazamo mwingine, Wangwe aliliunganisha tukio la Mkapa kujitetea akiwa kijijini kwake na matukio yanayofanana na hayo yaliyopata kufanywa kwa nyakati tofauti na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Chenge.
Wangwe aliutumia mlolongo huo wa matukio kuonya kuwa inaelekea nchi sasa inamezwa na ukabila kwani haiwezekani mtu atuhumiwe kitaifa, halafu atumie jukwaa la kijijini kujibu tuhuma hizo.
Alionya kuwa matukio hayo yanaipeleka nchi pabaya zaidi, kwani watu wanaotumiwa kwa ufisadi wameanza kugeuza ajenda hizo kwa ukabila kwa kukimbilia vijijini kwao kujitetea.
“Kila mtu hivi sasa anakimbilia jimboni au mkoani kwake kujisafisha, mara leo utasikia huyu yupo Monduli, kesho utasikia yule yupo Bariadi, hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi kwani wanataka Watanzania wasahau kuhusiana na vita ya ufisadi na badala yake wajikite katika ukabila,” alisema Wangwe.
Aidha, alisema hoja ya Mkapa kuwa wanaomtuhumu hivi sasa wanafanya hivyo kwa husuda baada ya kuwanyima vyeo, haina maana kwani wanaopiga kelele hizo wengi wao ni wapinzani ambao kwa mfumo wa sasa wa utawala, hawawezi kujumuishwa serikalini.
Alisema kama Mkapa anao ushahidi wa kuombwa nafasi za uongozi na kambi ya upinzani, ajitokeze hadharani na kuwataja watu hao, ili hoja yake iweze kuwa na nguvu, kuliko anavyodai hivi sasa kuwa aliwanyima nafasi za uongozi na wanamuonea wivu.
Wangwe alisema Mkapa ni mmoja kati ya watu waliotajwa na wapinzani akituhumiwa kwa ufisadi kati ya viongozi wakubwa 11, lakini hajawahi hata siku moja kujitokeza na kukanusha jambo hilo au kwenda mahakamani kuwafungulia kesi wale wanaomhusisha na ufisadi. Alisema Mkapa alikingiwa kifua na baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kuwa ni msafi na kweli alipoanza kazi miaka mitatu ya mwanzo, alikuwa akifanya kazi vizuri, lakini aligeuka mara baada ya kifo cha Nyerere na kuanza kuinadi nchi kama vile haina mwenyewe sambamba na kukithiri kwa rushwa na kufikia viwango vikubwa. Alisema katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, rushwa kubwa imeimarika zaidi ambapo miaka mitano ya mwisho wa uongozi wa rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ndipo ilipoanza na miaka yote kumi ya awamu ya tatu chini ya Mkapa rushwa iliimarika mara dufu na miaka miwili ya Rais Kikwete hali iliendelea kuwa ile ile.
 
Plani ya chenge na mkapa ilipokwama...kuliwaka moto kwani watu walishangazwa sana...ccm na kina CHENGE,MKAPA,KIKWETE,LOWASSA,MRAMBA,KILLANGO NA WENGIENEO Wakaamua wakakutane huko kwenye kaburi la mwalimu.

Wakaja na PLAN...Mara uchawi,mara habari kibao kwenye vyombo vyetu ambazo hata hazigusii ufisadi tena utafikiri watu tayari wako jela...

Mkapa awasha moto



na Salehe Mohamed



UAMUZI wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanza kujibu tuhuma dhidi yake, umeibua malumbano ya hoja kutoka kwa wanasiasa kadhaa ambao wameeleza kushangazwa na majibu na hatua yake hiyo.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa maoni yao kuhusu kauli hiyo ya Mkapa, ni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumrushia makombora ya tuhuma rais huyo mstaafu, akifanya hivyo ndani ya Bunge.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kimaro alimtaka Mkapa kujibu tuhuma dhidi yake na kuacha kuwanyoshea kidole wengine kwa matatizo anayokabiliana nayo.
Katika kauli yake hiyo, Kimaro alisema alielekeza tuhuma kwa Mkapa si kwa sababu ya chuki au kwa kuwa alinyimwa nafasi yoyote ya kimadaraka serikalini kama alivyodai kiongozi huyo mstaafu, bali alifanya hivyo kutokana na kuwa na mapenzi ya dhati kwa taifa lake.
Alisema kuwa, alichokisema kilitokana na kuwa na moyo wa kuwaonya viongozi mbalimbali kutokana na kutumia madaraka yao vibaya na kwa masilahi binafsi.
Alisema ushahidi wa Mkapa kujihusisha na biashara akiwa Ikulu upo Mamlaka ya Usajili wa Leseni na Biashara (Brela), Tanesco na taasisi nyingine zinazohusika na mambo ya biashara, hivyo alichokisema si jambo la kutunga au kumzushia kiongozi huyo kwa sababu ya chuki binafsi au nyinginezo.
"Mimi sitarajii uongozi serikalini, nilishafanya kazi huko nikaamua niendelee na mambo mengine, nitakuwa muwazi siku zote… kamwe sitaki unafiki na yoyote anayefikiri nilifanya hivyo kwa ajili ya kumlenga Mkapa anakosea… nilifanya vile kwa sababu ya kuisimamia serikali na viongozi wengine wasielekee kule kusikofaa," alisema Kimaro.
Alisema tabia ya viongozi kusema kuwa nchi ina amani, utulivu na rasilimali nyingi haina mantiki kwa wananchi, iwapo hawataona uwajibikaji wa viongozi na matumizi sahihi ya rasilimali zao katika jitihada za kuwakomboa katika lindi la umasikini.
Kimaro alisema hatarajii kufanya siasa za kumchafua mtu, bali anachokifanya hivi sasa ni kile alichotumwa na wananchi wake, hivyo si vema mtu kumhusisha na dhana mbaya dhidi ya viongozi anapotimiza wajibu wake aliotumwa na wapiga kura wake wenye kiu ya maendeleo.
Wakati wa kikao kilichopita, Bunge lilipokuwa likijadili Muswada wa Sheria ya Nishati, Kimaro alimtuhumu Mkapa kwa kutumia vibaya madaraka yake kujinufaisha wakati akiwa madarakani.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe, alisema mtindo alioutumia Mkapa kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake unaweza kuzaa matatizo mengine na kusababisha malumbano yasiyokwisha.
Akitoa ushauri wake, Wangwe alisema kwa kuwa Mkapa anaonekana kuwa ameamua kuanza kujibu tuhuma hizo, anatakiwa kujitofautisha na watu wanaoonekana kujitafutia huruma kupitia kuwachafua watu wengine.
Alisema ili aaminike, Mkapa anapaswa kutoa utetezi wake chini ya kiapo cha mahakama kuhusu kutohusika kwake na ufisadi, ili kuwawezesha wapinzani na wananchi kufuatilia mali zake, badala ya kujitetea mkoani kwake.
Akizungumza na waandishi kuhusu utetezi wa Mkapa alioutoa mwishoni mwa wiki iliyopita, Wangwe alisema kuwa, kauli hiyo ya rais huyo mstaafu haina uzito wowote kwa Watanzania, bali kama kweli ana nia ya kusafisha jina lake akale kiapo mahakamani kuhusu kile anachokisema.
Alisema baada ya hapo, ufuate uchunguzi dhidi yake, ufanyike kulingana na kiapo hicho na kama atabainika kufanya biashara akiwa Ikulu, kiapo hicho kitumike kama ushahidi dhidi yake.
"Leo hii Mkapa hawezi kusema mambo kirahisi rahisi namna hii… anapaswa akale kiapo mahakamani na serikali ifanye uchunguzi juu ya kile alichokisema na kama itathibitika kuwa kafanya ufisadi akiwa madarakani, basi kiapo kile kiwe sehemu ya ushahidi," alisema Wangwe.
Wangwe alisisitiza kuwa Mkapa hawezi kuepuka dhambi ya ufisadi, kwani wasaidizi wake wengi akiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wake, Andrew Chenge, wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimsaidia kugeuzageuza mikataba mbalimbali kwa lengo la kujinufaisha.
Alisema ni jambo lililo wazi kuwa Mkapa alikuwa akifanya biashara akiwa Ikulu na kibaya zaidi alikuwa akitumia anwani ya Ikulu kwa masilahi binafsi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya maadili ya watumishi wa umma na viongozi, lakini kwa sababu ya tamaa za madaraka aliamua kupindisha sheria hiyo.
Katika mtazamo mwingine, Wangwe aliliunganisha tukio la Mkapa kujitetea akiwa kijijini kwake na matukio yanayofanana na hayo yaliyopata kufanywa kwa nyakati tofauti na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Chenge.
Wangwe aliutumia mlolongo huo wa matukio kuonya kuwa inaelekea nchi sasa inamezwa na ukabila kwani haiwezekani mtu atuhumiwe kitaifa, halafu atumie jukwaa la kijijini kujibu tuhuma hizo.
Alionya kuwa matukio hayo yanaipeleka nchi pabaya zaidi, kwani watu wanaotumiwa kwa ufisadi wameanza kugeuza ajenda hizo kwa ukabila kwa kukimbilia vijijini kwao kujitetea.
"Kila mtu hivi sasa anakimbilia jimboni au mkoani kwake kujisafisha, mara leo utasikia huyu yupo Monduli, kesho utasikia yule yupo Bariadi, hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi kwani wanataka Watanzania wasahau kuhusiana na vita ya ufisadi na badala yake wajikite katika ukabila," alisema Wangwe.
Aidha, alisema hoja ya Mkapa kuwa wanaomtuhumu hivi sasa wanafanya hivyo kwa husuda baada ya kuwanyima vyeo, haina maana kwani wanaopiga kelele hizo wengi wao ni wapinzani ambao kwa mfumo wa sasa wa utawala, hawawezi kujumuishwa serikalini.
Alisema kama Mkapa anao ushahidi wa kuombwa nafasi za uongozi na kambi ya upinzani, ajitokeze hadharani na kuwataja watu hao, ili hoja yake iweze kuwa na nguvu, kuliko anavyodai hivi sasa kuwa aliwanyima nafasi za uongozi na wanamuonea wivu.
Wangwe alisema Mkapa ni mmoja kati ya watu waliotajwa na wapinzani akituhumiwa kwa ufisadi kati ya viongozi wakubwa 11, lakini hajawahi hata siku moja kujitokeza na kukanusha jambo hilo au kwenda mahakamani kuwafungulia kesi wale wanaomhusisha na ufisadi. Alisema Mkapa alikingiwa kifua na baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kuwa ni msafi na kweli alipoanza kazi miaka mitatu ya mwanzo, alikuwa akifanya kazi vizuri, lakini aligeuka mara baada ya kifo cha Nyerere na kuanza kuinadi nchi kama vile haina mwenyewe sambamba na kukithiri kwa rushwa na kufikia viwango vikubwa. Alisema katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, rushwa kubwa imeimarika zaidi ambapo miaka mitano ya mwisho wa uongozi wa rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ndipo ilipoanza na miaka yote kumi ya awamu ya tatu chini ya Mkapa rushwa iliimarika mara dufu na miaka miwili ya Rais Kikwete hali iliendelea kuwa ile ile.

Hivi huyu kimaro naye anaendelea vipi?
Ama wamesha msIdeline..Maana huko BUTIAMA HUKO KWENYE KABURI LA MWALIMU MAFISADI WALIENDA KUMWULIZA CHA KUFANYA MTU ALIYEKO KABURINI AMA NI MITAMBIKO?
Halafu ccm na wapambe wake ni watu wenye kuwageuza watu vichaa machoni pa wananchi!
Kimaro PAMBANA NDUGU YANGU!
JITOE MUHANGA KWA NIABA YA TAIFA KWENYE VITA HII MPYA!
Ila na wewe angalia ushauri...Mlishajaribu mkashindwa kwani MKAPA ALIKAZA ROHO AKAENDA BUTIAMA MARA BAADA YA MAKONGORO NYERERE KUDAI KUWA HAWAWEZI KUMTOA KWENYE FAMILIA YA MWALIMU...see?
Interests ni nyingi..Hata wale kina BUTIKU NA WARIOBA NAONA WESHAPEWA CHAO WAPIGE KIMYA..Kwasababu kuna mtu alishawahi ku sugest kuwa kelele za Butiku ni njaa kwani hakupewa chochote na mkapa na akaunti ya Mwalimu Nyerere Foundation ilikuwa MUFLIS!
 
Kwenye ile thread yangu ya madai ya MAFISADI KUKAMATWA ILI WASITUGAWE...Niliandika hili kwenye posting yangu ya kwanza...Hili ambalo linaendelea sasa na ambalo nililisoma toka mwanzo kuwa ndio mbinu ya ccm na mimi nimejitolea kupambana nayo!

Nimeshangazwa sana na vitendo vya watuhumiwa wa ufisadi wakienda mikoani kwa kile kinachoitwa kujisafisha!

Ni gharama za nani wanatumia?

Kwanini sheria isifuate mkondo then wananchi wenyewe ndio wajiamulie kama ni kweli ni mafisadi ama la?

Serikali iko wapi ili kuwakinga na kuwaprotect wananchi na ulaghai wa mafisadi na propaganda!?

Serikali haiwajali wananchi wake ambao wengi wao ni masikini na wasio na uelewa wa kutosha kutokana na lack of education?

Kama kweli Serikali iko upande wa wanchi kwenye vita vya ufisadi..

Then kwa nini isiwalinde dhidi ya propaganda za mafisadi ambazo ndio walizitumia ili kuweza kuingia madarakani na kufanya ufisadi?


Je wanataka kuexploit ignorance ili wawatumie wananchi kama ndio kinga ya kujisafisha na hivyo kupelekea migawanyiko!?

Wananchi wapelekewe kesi ya "kujisafisha" baada ya sheria kuchukua mkondo na kuwasafisha na si vinginevyo!

Hawa kamwe kujisafisha hawawezi! Kivipi?

Mambo ya siasa ni next time..Hawa watu ni watuhumiwa!

Wana pesa nyingi za ufisadi hivyo wasipewe nafasi ya kuwarubuni wananchi hivyo haki kutotendeka hence machafuko na umasikini!

Maoni yangu ni kuwa hawa watu wawe under uangalizi kwa sasa then waruhusiwe kwenda kuelezea kesi yao mara baada ya sheria kuchukua mkondo wake!

Kikwete hawezi kukaa na kuwaangalia wakiwarubuni wananchi huku wakiwatisha wale wenye kuwanyooshea vidole!

MUUNGWANA UKO UPANDE WETU AMA WAO?

Walijiuzulu kwasababu ya tuhuma na si propaganda za kisiasa!

Ni tuhuma zilizowafanya wajiuzulu na wala si wananchi!

Ni tuhuma wanazotakiwa wazijibu na si eti "kujisafisha"

Ni tuhuma hizi hizi zitakazowasafisha mara baada ya mahakama kutoa uamuzi!


Hivyo wajiandae kisheria na si kuwavaa wananchi!

Kama ni kujisafisha waende ndani kwenye vyama vyao husika na ijulikane wazi kwamba wanawaelezea wana CCM na wala siyo Taifa zima!

Ni maoni tuu!
 
Without an empty rhetorics from the ccm politicians we can move forward because we all know what should be done!
Badala ya kurudisha pesa tunajua alitakiwa aseme wakamatwe mara moja!

Watanzania msipodai ripoti ya EPA..Ni wazi mtakuwa mmekubali kupigwa bao!

Natoa ushauri musome ripoti ya EPA, Taarifa za kaguzi zote pamoja na sources mbali mbali ili tuanze kuwabana wale wote waliotenda kinyume na kaziwakamatwe..Halafu wahojiwe na sisi wananchi tusikilize kauli na majibu yao halafu tuoanishe na ripoti zote za uchunguzi kuona kama ni kweli waliyosema yana make sense...

SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE!

Marekani waliwaambia KIKWETE KAKATAA KUMLETA BALLALI WATU WAKAPINGA SANA HAPA JF NA BALLALI KAPOTELEA MBALI!

MAREKANI WANASEMA TENA TUKITAKA HAKI TUDAI RIPOTI..BADALA YAKE VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO KUSEMA KWELI VINATIA MASHAKA..VINAWAPOTOSHA WANANCHI MAKUSUDI BILA KUJALI!

Sijawahi kuona siku za karibuni ripoti ya EPA ikidaiwa licha ya ushauri huo wa wamarekani ambao tunawasumbua karibia kila siku ya MUNGU!
__________________
 
Mimi na Lunyungu tulipishana kuhusu kauli ya kikwete ya kuwapa moyo mafisadi...Nilishawasoma ccm kitambo sana na hao hawajua nimeamua kupambana nao hadi kieleweke!
Quote:
Originally Posted by Lunyungu
Kwa heshima na taadhima naomba link ya ushahidi wa maneno ya JK .Ni mazito na yana maana pana na kuwa na nzito .Naomba link plizi .

Ngoma hii hapa Mh Lunyungu! Kazi kwako!
Wakandarasi wababaishaji sitaki -Kikwete

2008-05-04 10:45:16
Na Lucy Lyatuu, Singida


Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.

``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aidha, aliwataka wizara ya ujenzi wanapotoa tenda wamchague yule aliyetoa hesabu kubwa na sio kuangalia mwenye hesabu ndogo kwani wao pia ukubwa wa kazi wanaijua.

``Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali!,`` alishauri.

Aidha, amesema yapo makampuni kadhaa hapa nchini ambayo kazi yao ni kudanganya pindi wanapokuwa wamepewa tenda za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizindua barabara ya Isuna hadi Manyoni yenye urefu wa kilomita 55 baada ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kushindwa kazi kwa visingizio.

Rais Kikwete yuko mkoani humu kwa ziara ya siku sita kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka 2005.

Rais Kikwete alisema awali barabara hiyo ya Isuna-Manyoni, ilikuwa ikijengwa na mkandarasi kutoka China ambaye alishindwa kukamilisha kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kilichotokea hapo iwe ni fundisho na kwamba tatizo la namna hiyo lisijitokeze tena.

Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Kuhusu makampuni yanayodanganya alisema hapa nchini yapo kadhaa na kazi yao ndio hiyo halafu badaye huhitaji majadiliano.

``Simamieni wataalamu mlio nao, makampuni yawe yanasema ukweli kuepusha hasara katika nchi,`` alisema.

``Nchi hii ni maskini, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za wananchi, epukeni kuingia gharama mara mbili, kwani wanaofanya hivyo wanakuwa wanyonya damu,`` alisema.

Pia aliwataka kukasirika na kuwachukulia hatua makampuni yanayokiuka utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwaambia kwa herini (byebye) wakatafute tenda nyingine nje ya nchi.

Rais aliongeza kuwa mhandisi mshauri naye hatakiwi kulipwa malipo yake endapo ujenzi hautakuwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwani wasipofanya hivyo Tanzania itakuwa shamba la wajinga.

Lazima Watanzania waone uchungu na kutekeleza miradi ya wananchi katika kiwango kinachotakiwa, alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Bw. Omar Chambo alisema barabara hiyo itagharimu kiasi cha Sh. bilioni 30.43 na ujenzi wake ulisainiwa Desemba 11, mwaka 2007.

Alisema barabara hiyo ilisainiwa kati ya TANROADS na Kampuni ya China Geo Engineering kutoka nchini China na kwamba sehemu ya barabara hiyo inatarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2010.

Alisema mradi huo unasimamiwa na mhandisi mshauri Black &Veatch kutoka Afrika Kusini akishirikiana na Kampuni ya Mak Consult ya Tanzania kwa gharama ya Sh. milioni 857.23.
  • SOURCE: Nipashe
 
Mimi pia nashauri Mama Kilango atoke CCM, lakini sishauri aende chama chochote cha siasa kilichopo. Shauku yangu ni kuona CCM inagawanyika vipande viwili, kundi la mafisadi dhidi ya waadilifu. Mama Kilango atoke na waadilifu wenzake humo kwenye Bunge na kutuundia chama kingine. Imani yangu ni kuwa CCM imejiwekea mizizi sana kiasi kwamba njia pekee ya kukibomoa ni kukigawa.

Kwangu mimi chama ni tatizo kubwa na si tabia za watu walioko ndani yake. Kama ilvyoonekana hivi karibuni NEC ikigeuzwa mtetezi wa ufisadi mnafikiri kweli tutafika?. Tokeni humo, akina Kilango, Sendeka, Kimaro, Mwakyembe, Seleii, Manyanya, na wengine ambao hata hatuwafahamu, mtuundie chama kingine kitakachoibomoa CCM, hapo ndipo mtakapopata support ya wananchi, lakini kama mmo humo humo siju?
 
Kutoka CCm sio dawa. Ni muhimu sana kuwapinga ukiwemo humohumo ndani kuliko ukiwa nje.

Mama bakia humu humu. Tunakusapoti.
 
Salehe Mohamed

MVUTANO mkubwa unaoonekana hivi sasa kwa baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea hivi sasa mjini Dodoma, unaonyesha wazi namna watu wanavyoanza kujipanga kwa ajili ya kuwania uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao unaotabiriwa kuwa mgumu.

Kurushiana ‘madongo' baina ya wabunge hao, ni ishara tosha kuwa CCM sasa makundi yamerejea, tena kwa kasi kubwa bila ya kificho, na kiu ya waliopo kwenye makundi hayo ni kupata madaraka kwa gharama zozote zile. Kasi hii ya vitisho na majibizano ndani na nje ya Bunge vinaashiria mambo mengi. Kwanza, ni kuchoshwa na kulindana kunakofanywa ndani ya CCM, hasa kwa wanachama ambao wameliingiza taifa katika matatizo, lakini chama kinaonekana kuwakingia kifua.

Pili, inajidhihirisha wazi kuwa baadhi ya wanachama wanataka kulipa kisasi kwa kukosa nafasi za uongozi walizozitaka katika chaguzi zilizopita ndani ya CCM na uchaguzi mkuu uliopita, ambapo kulikuwa na makundi kadhaa ndani ya chama hicho ambayo mpaka sasa yanaendesha harakati zao kimyakimya. Uvumilivu ni kitu muhimu kwenye siasa, lakini unaonekana kwenda harijojo kwa wanachama hao kiasi cha kutoleana matamshi ya chuki iliyopo ndani ya mioyo yao kwa muda mrefu sasa.

Wabunge wanaonekana hivi sasa kuwa wakali zaidi wakidai wanasimamia maslahi ya wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa na maisha magumu, hasa kutokana na rasilimali zao kutotumika inavyopaswa na viongozi waliopewa dhamana za kuzisimamia.

Anna Kilango Malecela (Same Mashariki)

Huyu mama hivi sasa ni mwiba mchungu na mkali kwa serikali, na wote waliotenda au kutuhumiwa kushiriki kwenye ufisadi na ameainisha wazi wakati wa wabunge kuwa mihuri ya kupitisha mambo ya wakubwa umepita, na hivi sasa ni wembe wa kuwanyoa wanaokwenda kinyume. Ujasiri wa kusimama bungeni na kutaja hadharani na kuionya serikali na chama chake kuchukua hatua kwa watu wanaohujumu nchi, kumeonekana kuwachoma na kuwaudhi baadhi ya vigogo waliozoea kulindana kwa misingi kuwa aibu ya chama isitolewe nje.

Kilango kwenye mkutano wa 10 wa Bunge uliokabidhiwa taarifa ya kamati teule iliyoundwa kuchunguza zabuni iliyoipa ushindi kampuni ya kufua umeme wa dharuala ya Richmond aliongea kwa ukali na kutaka kuwajibishwa kwa wote waliohusika na kuliingiza taifa katika hasara baada ya kubainika kuwa kampuni hiyo ilikuwa hewa.

Alipata nafasi ya kuwa mchangiaji wa kwanza ambaye aliitumia nafasi hiyo vema kuonyesha ushahidi kuwa baadhi ya viongozi walitoa baraka za kuharakisha utiaji saini wa makubaliano ya kampuni hiyo kukabidhiwa zabuni hiyo sambamba na kuanza kupewa fedha kutoka serikalini, kiasi cha sh milioni 152 kwa siku. Kikao hicho ambacho kiliweka historia kilishuhudia mawaziri watatu wakijiuzulu nyadhifa zao akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na hivyo Rais Jakaya Kikwete kulazimika kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri.

Majeraha ya kikao hicho mpaka hivi sasa bado hayajakauka vizuri na ndiyo lilikuwa anguko kubwa la wanamtandao ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliofanya kazi ya kuhakikisha Rais Kikwete anapata nafasi ya kuliongoza taifa hili, huku wao wakiwa pembeni yake wakimuelekeza njia na wanavyotaka.
Moto wa Mama Kilango unaendelea kushika kasi baada ya juzi kuitaka serikali kuwabana wote waliokopa sh bilioni 216 kupitia Mpango wa Uagizaji Bidhaa (Import Support) pamoja na urejeshwaji wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kiasi cha sh bilioni 133 zilizoibwa na wajanja kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kilango ameionya serikali kuwa iwapo fedha hizo hazitarejeshwa hadi Julai mwaka huu, basi Bunge litawaka moto na yupo tayari kufa (haogopi) kwa kukisimamia na kutetea kile anachoamini kwa dhati ndiyo msaada au mkombozi kwa wananchi. Kimsingi kauli za mama huyo ni nzito ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa anatumiwa na watu waliokosa nafasi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, ambapo kulikuwa na makundi mabalimbali ambayo hivi sasa yameonekana kuanza kujitokeza. Pamoja na hayo, lakini swali linabaki palepale. Je, Kilango ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge na CCM ataendelea na moto huo au ndiyo akitimiza malengo yake atafunga mdomo kama wanavyofanya baadhi ya waliomtangulia?

Peter Serukamba (Kigoma Mjini)

Huyu ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM). Ni miongoni mwa damu changa zilizopo bungeni, ambaye anaonekana kuwa na matarajio fulani katika siasa kiasi cha kuwakemea wenzake, hasa Mama Kilango, wasigeuze ufisadi kuwa agenda ya kubomoana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama.
Inavyoeleka amesahau kuwa wapigakura wake wana matatizo makubwa yanayotokana na ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi, ambao wengi wao ni wanachama wa chama chake ambao waliapa kuzilinda rasilimali za nchi na kutetea masilahi ya wananchi ili waondokane na umasikini.
Damu changa hii kwa bahati mbaya ama kwa kujua au kwa kutojua, imejikuta inaingia katika mtego wa kulindana na kuficha maovu, ambao kwa muda mrefu ulizoeleka ndani ya chama chake bila ya kujua kuwa mtego huo kwa sasa unaonekana kushtukiwa na watu wengi na wanafanya kila njia kuukwepa.

Siku za hivi karibuni, mwanasiasa huyo mchanga ameingia kwenye malumbano na mwanasiasa mkongwe, Anna Kilango Malecela anayeijua nchi na chama vilivyo, ambaye kwake mafisadi wanamchefua kupindukia na yupo tayari kufa ili kuhakikisha wote wanatokomea. Kauli ya Serukamba ndiyo iliyomsababishia matatizo kiasi cha kudai kuwa anatishiwa maisha na Kilango ambaye hivi sasa moto wake wa kutaja bayana mambo ya kifisadi unaonekana kuzidi kukolea na unaanza kuwaunguza wale wote wenye mawazo ya kulindana na kutafuna rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi.
Swali linaloendelea kusumbua vichwa vya watu hivi sasa ni je, Serukamba ataweza kuendelea kung'ang'ania kuwa ufisadi usifanywe ajenda na kutaka kuwekana sawa ndani ya CCM na kuhimili mawimbi ya wanasiasa wakongwe kama kina Kilango?

Lazaro Nyarandu (Singida Kaskazini)

Yeye ni Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM). Ameshindwa kuvumilia, uoga wake ulikwisha na kutamka bayana kuwa nchi imeuzwa. Sababu ya kauli ya Nyarandu, ni viongozi kuuza rasilimali nyeti na zenye msaada kwa wananchi kwa utashi binafsi badala ya kufanya hivyo kwa maslahi ya wananchi wenye kiu ya kuona rasilimali zao zinawakwamua kiuchumi. Anaamini kuwa hasira ya wananchi hivi sasa dhidi ya viongozi wao ni kubwa, na kama viongozi hawatajirekebisha na kuanza kuwa makini na kutoa haki wanapoingia mikataba na wawekezaji, kuna hatari kubwa hasira hizo zikavuka mipaka na kuwa balaa zaidi.

Nyarandu anasema kuwa, uuzaji wa hoteli katikati ya mbuga, mikataba isiyofaa, uuzaji wa kampuni zenye tija kwa wananchi, ni miongoni mwa kero zilizowafanya wananchi waendelee kuwaona viongozi wao wasaliti na wenye kujali masilahi binafsi kuliko wale waliowapa dhamana ya kuongoza na kusimamia rasilimali wanazoziuza kiholela. "Wawekezaji wanaokuja hapa nchini wanakuja na mikoba yao na kupewa dhamana na mikopo ya benki za hapa nchini na kwenda kuwekeza katika sekta ya utalii na katika kipindi kufupi huwa matajiri sana ilihali kuna Watanzania walioomba nafasi hizo, lakini walinyimwa. Sasa kama mambo haya yatendelea hivi huko tunakokwenda itakuwa hatari zaidi," anasema Nyarandu.

Alikwenda mbali zaidi pale alipodai kuwa na nia ya kupeleka hoja binafsi akiitaka serikali irejeshe hoteli za mbugani ilizoziuza kwa bei ya kutupa na kuziuza tena kwa njia ya ushindani (mnada/zabuni), kwa bei itakayokuwa na manufaa kwa taifa.

Anna Margeth Abdallah (Viti maalum-Masasi)

Ni miongoni mwa wanasiasa waliokomaa, na alishashika nyadhifa mbalimbali serikalini. Si mzungumzaji sana awapo bungeni ila anapozungumza mambo huwa mazito zaidi, hasa hufanya hivyo unapotokea utata ambao unahitaji wakongwe kudhibiti au kuutatua. Amepewa ridhaa ya kuingia bungeni na Rais Jakaya Kikwete. Ameonekana kama vile anatuliza joto la kisiasa linaloendelea kupanda hasa kwa matamshi yake ya juzi kuwa hakuna mbunge muoga au anayetishiwa maisha kwa kuongea na kutetea maslahi ya wananchi bungeni. Kauli ya mbunge huyo inaelekea kama majibu kwa Kilango ambaye alibainisha kuwa haogopi vitisho anavyovipata kutoka kwa watu kadhaa wakiwamo wabunge kuhusu kuzungumzia masula ya ufisadi, yakiwemo ya EPA ambayo hivi sasa yanaelekea kuwachanganya baadhi ya vigogo wa chama tawala.

Abdallah anapozungumzia kuwa kila mbunge ana nia ya kukemea ufisadi ila tofauti yao inakuja kwenye uzungumzaji wengine wanafanya kwa mbwembwe na wengine wanazungumza kwa utulivu, anakosea sana kwani kuna baadhi ya wabunge hawapendi kusikia wimbo huo ukiimbwa bungeni na kwingine kwa sababu unawagusa na wanafaidika. Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya watu walioshiriki kufanya ufisadi huo ni wanachama wa CCM na baadhi yao ni wabunge, hivyo si rahisi kujitokeza hadharani kuupinga kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kujichimbia wenyewe kaburi jambo ambalo hawawezi kulifanya hata kidogo.

Kuna baadhi yao wanadiriki hata kuwanunua baadhi ya wabunge ili wasiweze kuzungumzia suala hilo ambalo pia kwenye vikao vya CCM hivi karibuni lilileta mtafaruku mkubwa ambapo baadhi ya watu walitaka wanaohusika na vitendo vya ufisadi watengwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tatizo ambalo mpaka sasa lipo kwa baadhi ya wabunge hasa wa CCM ni kutokubali mageuzi na kuwajibishana sambamba na kutopenda kumuona mwenzao akipata sifa kwa kusimama kidete kupinga maovu ambayo yanawahusisha wanachama wa chama hicho. Kufanya kazi au siasa kwa mazoea kulishapitwa na wakati, na kila Mtanzania angependa kuona uhai wa Bunge na serikali katika kuwajibishana na si huyu leo amezungumza hiki kesho anatokea mwingine anampinga au kutoa kijembe kwa lengo la kumkatisha tamaa.
Malumbano yanayotokea hivi sasa bungeni ni dalili nzuri ya kuelekea kwenye kutibu kero za wananchi ingawa ndiyo mwanzo wa mgawanyiko wa wanachama wa chama tawala ambao hapo kabla walikuwa na utaratibu wa kuwa anachokisema mwenyekiti wao ndiyo sahihi (zidumu fikra za mwenyekiti).

Hakuna ubishi na wala haihitaji wataalamu kujua kuwa hivi sasa kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM na inaelekea makundi yameanza kufufuka upya huku lile kundi kuu la wanamtandao likikosa nguvu ile ya awali iliyowafanya wamwezeshe Rais Kikwete kutwaa madaraka. Baadhi ya wana mtandao hasa waliotemwa kwenye uongozi bado haijajulikana wazi wamehamia katika kundi gani, lakini ni dhahiri kuwa kuna kundi watajiunga nalo ili kutimiza ndoto zao ambazo zimeyeyuka kama barafu kwenye jua kutokana na dhoruba mbalimbali walizokutana nazo. Muda si mrefu kutoka sasa taifa litaingia kwenye uchaguzi wa madiwani na bado ule wa wabunge na urais, hivyo wenye makundi yao hivi sasa ndiyo kumekucha, wanaanza kupanga mikakati ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho huku wakitafakari sababu zilizowafanya wakose nafasi za uongozi katika uchaguzi uliopita.

Mambo hayo ndiyo kwa kiasi kikubwa yatakayozidisha ugumu wa uchaguzi ujao ndani na nje ya CCM ambayo siku za hivi karibuni imeamua kuwatakasa wanachama na viongozi wanaohusihwa na tuhuma za ufisadi.


salehe_mohamedi@yahoo.com
 
Last edited by a moderator:
Kutoka CCm sio dawa. Ni muhimu sana kuwapinga ukiwemo humohumo ndani kuliko ukiwa nje.

Mama bakia humu humu. Tunakusapoti.

Kwasababu unelekea kufikiri kuwa maoni yangu kuwa Killango hawezi kusafisha ccm akiwa humo unnless MAFISADI WAMEKAMATWA NA KUTUPWA NJE...Then asome makala pamoja na nyinginezo...Hii hapa..


CCM na ufisadi ndoa yao itadumu milele!

ban.nundu.jpg
Deus Bugaywa

NI wazi sasa kwamba kile kinachosemwa kuhusu CCM na hatima yake kutokuwa ya kutia matumaini si tena habari za mitaani, ni suala ambalo liko wazi na dhahiri hata kaka wenye chama chao hawataki kuuikiri ukweli huo. Na zaidi sana kutokiri kwao kwamba mambo si shwari ndani ya chama chao ni moja ya dalili za wazi kwamba huu ni mwanzo wa mwisho wa chama hicho kikongwe katika historia ya siasa ya nchi hii na bara la Afrika.

Ukiangalia kwa makini taarifa zilizotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari tangu kuanza kwa kikao kinachoendelea cha Bunge na fununu kwamba kwamba lipo kundi la wanachama wakongwe wa chama hicho waliokuwa na mkakati wa kushawishi wabunge wa chama hicho wawasafishe watuhumiwa wa Richmond. Pia kuibuka kwa tuhuma za ushirikina bungeni na yaliyojiri kwenye kikao cha NEC ya CCM na wabunge wake, na habari zilizoandikwa kama matokeo ya kikao hicho, haihitaji kuwa Thomaso kujua kwamba uko mkono unaoiandikia CCM ukutani kwamba ‘Mene mene tekeli na peres' yaani ufalme wake sasa umekwisha.

Baada ya kikao cha NEC na wabunge kila aliyekuwa na shaka na ukali wa wabunge wa CCM wakati wa kujadili ripoti ya kamati ya Mwakyembe sasa amethibitihsa hofu yake hiyo, kwamba hizo zilikuwa ni mbio za sakafuni ambazo mkiambiaji wake hata awe na kasi kama ya mwanga, jeuri yake inaishia ukingoni - haifiki mbali. Msomaji mmoja wa safu hii aliwahi kuniandikia wakati wa vurugu hilo lililosababisha waziri mkuu wa wakati huo kujiuzulu kwamba ‘ndugu mwandishi hiki kinachosemwa na wabunge wa CCM sasa ni ngoma ya watoto haikeshi, ufisadi siku hizi ndiyo mhimili wa CCM, kujidai wanaupiaga vita ni kama wanajipiga vita wenyewe, wataweza?' Wakati huo nilimwambia kila kitu lazima kiwe na mwanzo na mapinduzi yanapoanza huwa kuna mstari mwembamba sana katikati ya hali ya zamani iliyozoeleka na hali mpya ya kimapinduzi inayoanza kuzaliwa, kiasi kwamba unaweza usione tofauti, kwa hiyo huo huenda ukawa mwanzo wa CCM kujivua gamba lake.

Kokote aliko msomaji huyu najua wala hakushangaa kusikia matokeo ya kikao cha chama kinaamua kurejea kwenye jadi yake na kuwatakasa watuhumiwa wa ufisadi, kwamba kuitengeanisha CCM na ufisadi unaoendelea nchini ni kazi kubwa. Tunaambiwa hata wale ambao tuhuma zao wala hazihitaji kuwa mhitimu wa kilichokuwa chuo cha kijasusi cha Patrice Lumumbe huko Urusi, kujua kwamba kulikuwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kukiuka maadili ya kawaida kabisa uongozi.
Na hapo ndiyo ule mwisho unapokaribia, kwamba kikao hicho kama vilvyokuwa vilivyotangulia vilivyokuwa na lengo la kuleta mshikamano katika chama, kimesaidia kuongeza uadui miongoni mwa wanachama wake wakongwe na viongozi waandamizi kiasi kwamba nyufa zilizopo sasa sina shaka hata mweyekiti wake, Rais Kikwete, anaweza kuzuia zisiendelee kukua na kupanuka achilia mbali kuziziba kabisa.

Inapofika mahali chama kikongwe chenye viongozi wazoefu, kama viongozi wake wa ngazi ya mwenyekiti wa kamati ya maadili ya chama ya taifa, anamwambia Spika wa Bunge lenye wabunge wengi wa CCM na Spika huyo anatoka CCM, kwamba ni mzushi anaongoza Bunge kizushi, ujue anguko kuu haliko mbali. Na hizi tunazoziona hadi huku nje ni ishara chache tu kwamba sasa hivi kuna CCM mbili, bila kujali wennyewe wanafunika kombe vipi, hata kama watasingizia kwamba ndio kukomaa kwa demokrasia, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mambo ndani ya chama hicho yanakwenda msege mnege.

Kama tulivyojuzwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba pamoja na mvutano uliotokea ndani ya kikao hicho cha NEC na wabunge juu ya nini chama kifanye kwa watuhumiwa wa ufisadi, na mwenyekiti kuishia tu kutoa kauli laini ambazo kila kundi linaitafsiri kwamba ilikuwa ni kijembe kwa upande mwingine, si ishara nzuri ya kiuongozi, hii inatoa mwanya kwa watu kuanza kuamini kwamba hata mwenyekityi wake sasa kuna watu au kundi analoliogopa ndani ya chama.

Hakuna ubishi kwamba kusafishwa au (kujisafisha?) kwa watuhumiwa wa kashfa za Richmond na EPA ndani ya CCM, si suala ambalo limekuja kibahati bahati, huo ni makakati ambao umeandaliwa na wahusika siku nyingi, kwa ujuzi mkubwa na gharama kubwa. Kwa hiyo, ndiyo kusema kwamba CCM mengine ya chama hicho sasa hayategemei sana itikadi yake na mfumo wake wa kutendaji au kimaadili, isipokuwa ujanja wa baadhi ya wanachama wake wanaoweza kufanya ‘maarifa' na kuwafanya wajumbe wawaunge mkono katika kile wanachokitetea hata kama kinasigana na maadili na miongozo ya chama hicho. Wanaoshinda kwa ‘mbinu' na maarifa yao katika hoja moja wanatoa mwanya kwa kundi lililoshindwa nalo kujiandaa na kupanga mikakati ya kuja kuwapiku wengine, ilimradi ni mashindano ya madaraka na kunyemelea nani atakuwa mpangaji anayefuata wa mambo pale Magogoni.

Kwa kufanya hivi viongozi wa chama hiki wamewasahau wananchi, wako bize wanapigana vikumbo vya kuwania ukubwa, katika vikao vyao vingi vya hivi karibuni kwenye kila hoja nyeti, mwananchi na mwanachama hana nafasi ukisikia ametajwa ni katika hali ya kujihami kwamba ‘wananchi wameamka' kwa hiyo mwaka 2010 chama kinaweza kuwa na kazi kubwa kushinda. Kusahauliwa huku kwa wananchi ndiko kunakopaswa kutumiwe na Watanzania kuona na kukijua hasa chama hiki kinachoitwa cha mapinduzi, kina sura gani na viongozi wake wana mweleko na malengo gani na watu wa taifa hili.

Kwa kuamua kuwakumbatia mafisadi, CCM inatuma salamu kwa wananchi kwamba chenyewe kinaangalia watu wake kwanza, ikumbukwe CCM ina wenyewe na wenyewe ni wao, na chama hakiko tayari kuwaona ‘wanapata tabu' hata kama wanatuhumiwa na nini. Ni jukumu la wananchi kuamua kusuka au kunyoa - chama ndiyo hivyo kimeamua kufunga pingu za maisha na ufisadi, kwa kwamba yaliyounganishwa na NEC, wananchi kwa maana ya Bunge lao lisiyatengue.

Mbele ya CCM hata Bunge si lolote si chochote, kwamba hata kama Bunge limejiridhisha kwamba kweli hawa ni watuhumiwa, lakini kwa kuwa wanachokifanya ni kile kinachoitikadiwa na chama chao, acha Bunge lisema na ‘lizushe linavyoweza kuzusha', lakini ndoa ya CCM na watu wake hata kama ni watuhumiwa hawana ruksa kuivunja. Chama (kipande kimoja cha chama) ndiyo hicho kimeamua kuchukua ufisadi, je, kundi la wakereketwa linalodhani mwenendo wa mambo ndani ya chama hicho si wenyewe litakwenda njia ipi? Ni suala la kusubiri na kuona.

Lakini kitu kimoja ni dhahiri kwamba kwa kila kitendo na kila neno wanalosema CCM linashabikia mtu ambaye machoni pa umma anaonekana hana sifa hata za kuwa balozi wa nyumba kumi, kwa kukosa nidhamu na uadilifu wa kiuongozi, ni hatua moja ya taratibu lakini yenye nguvu na ya uhakika kuelekea kwenye kaburi lake.
Mungu ibariki Tanzania!

drbugaywa@yahoo.com
0734 449 421


h.sep3.gif
 
Last edited by a moderator:
Waseme hao....Miye....

Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM

ban.maswali.jpg
Ansbert Ngurumo

STAILI ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetumia kujisafisha inavutia, inashangaza, inachekesha na kutafakarisha kidogo. Ni staili inayozua maswali yasiyo na majibu au yenye majibu yasiyoridhisha. Lililo dhahiri ni kwamba, kwa kitendo cha kujisafisha, kwa kutumia kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), CCM imekiri kile ilichokuwa inakikataa kwa muda mrefu - kwamba imechafuka.

Lakini staili yake ya kujisafisha inatufanya tuhoji upya: Uchafu ni nini? Umeingiaje CCM? Umeingizwa na akina nani? Umeingia lini? Na unaondolewaje? Labda CCM wangejiuliza maswali haya na kuyatafutia majibu ya kina, wangepiga hatua kidogo. Majibu ya maswali haya yanatosha kuandika kitabu ambacho kitaandikwa siku moja na kuwa marejeo ya vizazi vijavyo kuhusu historia ya ukombozi wa nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni weusi waliojipa haki ya kutafuna matunda ya uhuru wa Watanzania bila ridhaa yao.

Ikumbukwe kwamba zilipoibuliwa tuhuma dhidi ya CCM, hadi baadhi ya watani wake kisiasa wakakiita Chama Cha Majambazi; Chukua Chako Mapema; Chama Cha Majangili; Chama Cha Mafisadi na kadhalika. Viongozi wakuu wa wanachama walipinga, waling’aka, kuwakebehi na hata wakawatisha waliotoa tuhuma hizo. Katika hali ya kutapatapa na kukata tamaa, na kama ilivyo kawaida ya CCM kufanya propaganda katika masuala ya msingi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitamka hadharani kwamba tuhuma dhidi ya CCM ni kelele za mlango zisizoweza kumzuia yeye (akajiita mwenye nyumba) kulala! Wiki hii ni yeye aliyeongoza kikao cha NEC kujaribu kujisafisha, kwa staili aliyochagua yeye na viongozi wenzake. Viongozi wenzake, naye akiwamo, pamoja na wastaafu, wamefunikwa na kashfa nzito mno kichwani hadi miguuni.

Hawaonekani! Hata waliotishia kwenda mahakamani baada ya kuhusishwa na ufisadi wameshindwa kwenda kwa sababu dhamiri zao zinawaeleza ukweli kwamba hizi si kelele za mlango, bali sauti za wanyonge, wenye mali ya nchi hii, ambao hatimaye wamegundua mnyonyaji wao ni nani. Watuhumiwa hawa wanaogopa yasifumuke mengine wakiwa kule mahakamani. Na licha ya ushahidi wote uliopatikana hata bila kwenda mahakamani, vyombo vya dola vimeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.

Polisi wetu wameamua (bila shaka kwa maagizo ya kisiasa) kufanya kazi ya kisiasa. Wanakimbizana na vibaka na wezi wakuu mitaani; wanawabambikia kesi wananchi maskini wanaotafuta kwa jasho. Wakati mwingine wanawanyonga ili kuwanyang’anya walicho nacho. Wanashindwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wanaotuhimiwa kwa wizi mkubwa unaofilisi hata maisha binafsi ya polisi wenyewe. Maana kama watuhumiwa walishindwa kwenda wenyewe mahakamani kuwashitaki waliowatuhumu, Jeshi la Polisi lingetusaidia kwa kuwakamata watuhumiwa ili haki itendeke.

Kimsingi, hata wanasiasa makini wanaotaka kujisafisha matope ya ufisadi, walio na dhamiri ya kuonyesha kwamba hapa kuna ari mpya, wangepaswa kuchukua hatua za kisheria ili kujisafisha au kuwasafisha watuhumiwa au kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria. Huo ndiyo ungekuwa usafi wa CCM na serikali yake. Hapo ndipo rais angeanzia kuisafisha na kuwasafisha wenzake. Angechanganya hatua hiyo na zile fursa kadhaa zilizojitokeza, akabadilisha sura na mfumo wa utawala; akaondoa wachafu na kuweka wasafi; akafukuza wazembe na kuingiza wachapakazi.

Angepata pa kuanzia upya; na tungemsikiliza. Mara zote alizobahatika kufanya mabadiliko madogo na makubwa katika Baraza la Mawaziri zilikuwa fursa muhimu za kutuonyesha nia yake ya kusafisha serikali na CCM. Alishindwa kuzitumia. Akawahamisha mawaziri kutoka wizara moja hadi nyingine; akawapunguza wachache wasio na tuhuma nyingi; akawabakiza wale wanaotuhumiwa kila siku. Ni sawa na mtu anayefagia nyumba yake halafu akakusanya uchafu wote akaulundika chumbani anakolala; kisha akawatangazia wana familia na majirani kwamba nyumba yake ni safi.
Harufu ya uchafu inayowakera hao, inamburudisha yeye, maana yeye na wao wana tafsiri tofauti ya usafi na uchafu. Tusisahau kuwa kabla aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu, rais alikuwa ameunda Tume ya Profesa Rwekaza Mukandala kumsaidia kuwachunguza mawaziri wake na kumpa ushauri juu ya nani mbovu, nani ana nafuu, nani aondolewe na nani abaki.

Kwa bahati mbaya, hakuunda tume kabla ya kuwateua, ili kubaini ubovu wao. Lakini wengi wa wateule wake ni wale ambao yeye na wao wamekuwa pamoja serikalini kwa zaidi ya miaka 17. Haiwezekani kwamba hakuwajua. Wala hakuhitaji ushauri wa tume. Wananchi wenyewe walionyesha wasiwasi juu ya baadhi yao. Iweje wananchi wajue udhaifu wa mawaziri, yule aliyewateua, tena mwenye vyombo vya kiutawala vya kumsaidia kuwajua, ajidai kwamba hawajui hadi aletewe taarifa na tume ya ‘kisomi’! Ajabu ni kwamba, hata tume ilipoleta majibu, hakuyatumia. Akawateua wale wale, tena wengine wakamkejeli kwenye vyombo vya habari. Andrew Chenge ni mfano hai. Alipoteuliwa kuongoza Wizara ya Miundombinu, wanahabari wakamhoji kwanini amerudi akasema “muulize rais aliyeniteua. Ndiye anajua sababu.” Chenge alikuwa sahihi.

Na hata baadaye alipoondoka kwa kashfa za kuficha nje mabilioni ya shilingi ambazo hazijajulikana alivyozipata, alitoa kauli nyingine kwamba ameondoka ili kumwondolea ugumu rais. Maana yake, kama si kwa ajili ya rais, Chenge asingeondoka. Lakini maana kubwa zaidi inayopatikana kwenye kauli yake ni kwamba kama asingeondoka, rais asingemfukuza! Kauli kama hii ilitolewa pia na Lowassa alipojiuzulu uwaziri mkuu, akasema amefanya hivyo si kwa kuwa ana mkono kwenye Kampuni ya Richmond, bali kwa kuwa alitaka kulinda heshima ya chama na serikali.

Baadhi yetu tuliandika kumsahihisha Lowassa, tukasema alijiuzulu kulinda heshima ya rais kwa kuwa wote walikuwa washiriki wakuu katika mradi wa Richmond. Kuna jambo lilitokea wakati ule ambalo lipo hadi sasa. Ile heshima ya chama na serikali haikurejea. Kwa hiyo, kujiuzulu kwa Lowassa hakukusaidia kurejesha heshima ya serikali na CCM. Na sababu mojawapo iliyosababisha heshima hiyo isirejee ni kwamba mafisadi wale wale wameendelea kuwa viongozi wa CCM na serikali. Wao walitaka tuamini kwamba fisadi ni Lowassa; akiondoka serikali inakuwa safi. Wapi! Sasa NEC ya CCM imekaa na kumsafisha rasmi Lowassa kwa kusisitiza kauli yake ya awali.
Maana yake ni kwamba CCM na serikali hii ya Kikwete inamhitaji sana Lowassa. Na imegundua kwamba inahitaji kumlinda. Inajua, kwamba tunavyojua, kwamba alipokuwa waziri mkuu, Lowassa hakutenda jambo lolote zito kwa uamuzi wake pekee.

Yote aliyatenda kwa idhini na ushauri wa rais. Ndiyo maana yalipomtokea yaliyosababisha ajiuzulu, rais alikuwa wa kwanza kumtetea, akasema amepatwa na ajali ya kisiasa; kwa kuwa Lowassa ni kiongozi mchapakazi, mwadilifu na mzalendo wa kweli. Aliyasema hayo huku akijua kuwa umma wa Watanzania unamzomea Lowassa na kumwona fisadi wa kutupwa, maana katika sakata hili la Richmond, jina la Lowassa limetajwa mno kuliko hata la wamiliki halisi wa Richmond. Hili ndilo ambalo CCM imejaribu kupambana nalo. Na kitendo cha NEC kumsafisha Lowassa sasa, ni uthibitisho kwamba CCM imesisitiza kauli ya Rais Kikwete juu ya ‘uadilifu na uzalendo’ wa Lowassa. CCM na Serikali ya Kikwete inamuogopa Lowassa. Na haikuanza leo.

Lakini woga huu uliongezeka pale walipoona Lowassa anawekewa zulia jekundu kwao Monduli! Woga ulizidi walipoanza kusikia akijitetea hadharani. Wakajua wasipofanya kitu, atalipuka na kulipua mambo. Wakaamua kumlipua yeye kwa njia mbili. Kwanza, wakawa wanamtumia wajumbe wa kumpa pole na kumfariji kwa yaliyompata. Pili, walipogundua bado ana kinyongo na kwa hulka yake atazidi kusema mengine wasiyotaka aseme - maana alishaamua kujitetea asife kibudu - wakaingiza nguvu ya dola. Wakamuonya. Akaufyata! Hadi leo najiuliza. Kuna kitu gani serikali inaogopa kwa Lowassa? Kitu gani waliogopa asiseme? Na hapa walipofikia, inawezekana hatasema tena; maana wamemsafisha. Wamemziba mdomo.

Lakini usafi huu wa Lowassa una maana gani pana? Wamemsafisha Lowassa kumlinda mwingine. Na ulinzi huu ndiyo sababu ya NEC kuwatisha wabunge na kuwawekea ‘gundi’ mdomoni wasijadili masuala ya ufisadi wa EPA bungeni.
Huu ni uchafu ambao wakubwa hawataki kuondokana nao. Uchafu huu ndiyo asili ya nyadhifa zao. Uchafu huu ndiyo ulaji wao. Ukizungumzwa kwa uwazi, ukaanikwa, hakuna mmoja wao atakayebaki. Hakuna atakayemfukuza mwingine. Na ndiyo maana wamekuwa wakilindana na kuogopana hata mambo yanapokuwa yameharibika waziwazi.

Na ndiyo maana wengine tunatilia shaka hizi harakati za CCM na serikali kujisafisha kwa kuwatoa kafara wachache na kuwakumbatia wengi. Wanataka kutumia ‘usafi’ wa Lowassa kuisafisha CCM na serikali. Lakini wanashindwa kuchukua hatua za dhati kwa mafisadi wa EPA. Hakuna atakayewaelewa. Hata Richmond (sasa Dowans) bado inaendelea kulipwa mamilioni wasiyostahili (sh 152,000,000 kila siku). Matendo haya ya NEC huku serikali ikishindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi, ni sawa na CCM kujisafisha kwa kunawa matope. Sote tunajua matokeo yake.

Inavutia kufuatilia mchakato wa namna hii; inashangaza CCM wasivyojua maswali ya msingi yanayowakabili; inachekesha kwamba watawala wameamua kufanya maigizo mbele yetu; na inatafakarisha kwamba vita dhidi ya ufisadi inahitaji watawala mbadala na vyombo mbadala. Si hawa tulio nao.


ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com
+447853850425
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom