Mama Kilango apiga Kambi Moshi mjini; kumng'oa Ndesamburo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Kilango apiga Kambi Moshi mjini; kumng'oa Ndesamburo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtemi, Nov 23, 2009.

 1. m

  mtemi Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Daniel Mjema (mwananchi),Moshi

  MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametangaza rasmi kupiga kambi Moshi Mjini hadi mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa CCM inanyakua jimbo hilo, uamuzi ambao unamuingiza kwenye vita kali na mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo.

  Katika kuonyesha kuwa Ndesamburo hana nguvu kwenye jimbo hilo, Kilango aliwaambia wanachama na viongozi wa CCM kuwa mbunge huyo kutoka Chadema ameshinda mara mbili mfululizo kutokana na matatizo ya wanaCCM wenyewe na kuwataka wajisafishe.

  Kilango, ambaye amekuwa akilalamika kuwa mafisadi wanataka kuchukua jimbo lake la Same Mashariki, alitangaza mkakati huo jana wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi, ikiwa dalili za wazi kwamba, CCM sasa imeanza kujipanga kufanya mashambulizi mkoani hapa ambako vyama vya upinzani vinaonekana kuwa na nguvu kubwa.

  “Nitapiga kambi hapa... kwanini tupate madiwani 12 na Chadema watatu halafu tushindwe ubunge,” alihoji Kilango. “Nitakaa hapa mpaka nimfahamu mchawi ili nimshike mkono nimwambie Rais (Jakaya) Kikwete huyu ndiye anayetufanya tushindwe na Ndesamburo.”

  Mbunge huyo aliongeza kusema:”Hatuwezi kukubali kuwa na wanaCCM ambao mchana wamevaa kijani, lakini usiku wamevaa nguo nyingine…nimeongea na Ndesamburo ananiambia wanaompa ubunge ni wanaCCM wenyewe… hili halikubaliki”.

  Alisema kuwa suala la Jimbo la Moshi Mjini kuwa chini ya upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 linampa tabu sana na hilo ndilo lililomsukuma kupiga kambi katika jimbo hilo hadi uchaguzi mkuu wa 2010.

  “Leo nimebisha hodi hapa tutakuwa wote mpaka Oktoba 2010 na kama tunakosa naomba wananchi mtuambie mapema nini na ndio maana nitakuja kila siku hapa, lakini na nyinyi viongozi na wanaCCM mjitazame inakuwaje tuna madiwani 12 tukose mbunge,” alisema mbunge huyo wa Same.

  Hata hivyo, alisema katika kipindi cha siku mbili tu alizokaa Moshi Mjini ameambiwa kuwa moja ya kero inayoinyima CCM ushindi ni vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga.

  Kilango alifafanua kuwa hakuna mtu muhimu kama anayejitafutia riziki yake, lakini ni jambo baya kama mtu huyo anakwamishwa na kuapa kuwa kwa suala hilo la machinga, ikibidi kulifikisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, basi atafanya hivyo.

  “Sisi tuna njia zetu pale bungeni unaweza kuuliza maswali ya kawaida au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na ikibidi kumuuliza, nitamuuliza,” alisema Kilango.

  Katika hali iliyodhihirisha kuwa suala hilo la machinga linagusa mioyo ya wananchi wengi wa mji wa Moshi, mara tu baada ya Kilango kulitaja, umati wa wananchi na wafuasi wa CCM ulilipuka kwa furaha.

  Mbunge huyo aliamua kumsimamisha katika hadhara hiyo mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi Kuu ya Moshi, Vicent Asenga kuelezea kile kinachowakwaza hadi waamue kutoipa CCM kura katika vipindi vitatu mfululizo.

  Asenga alisema waliingia makubaliano na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwamba kama wanataka kutoa huduma ya biashara kwenye stendi hiyo, wawe na vitambulisho na sare jambo ambalo walilitekeleza kikamilifu.

  Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema walishangaa siku moja wakivamiwa na kukamatwa na kupelekwa ofisi ya kikosi cha usalama barabarani na kutozwa faini ya kati ya Sh20,000 hadi Sh40,000 kana kwamba wao wamefanya makosa yanayohusiana na usalama barabarani.

  “Sisi hatuna upinzani na CCM lakini tuna upinzani na wanaotukwamisha,” alisema Asenga huku akishangiliwa na wananchi waliofurika katika mkutano huo na kuhoji kama makosa ya kufanya biashara yana uhusiano wowote na kikosi cha polisi wa usalama barabarani.

  Kutokana na maelezo hayo na kuwepo wafanyabiashara wengine waliojitokeza kutaka kuzungumza, Mama Kilango aliwataka wafanyabiashara hao kuteua wawakilishi watano ambao angekutana nao jana jioni kupata picha halisi ya kero hiyo.

  Suala la Machinga limekuwa kete ya kisiasa na Ndesamburo aliwahi kununua eneo kwa ajili ya kuanzisha soko la wafanyabiashara hao wadogo, lakini inadaiwa kuwa aliwekewa vizingiti na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, uamuzi ambao unadaiwa kuzidisha hasira ya wafanyabiashara dhidi ya CCM.

  Jimbo la Moshi Mjini limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 1995 likianzia kwa Joseph Mtui wa NCCR (1995-2000) na Philemon Ndesamburo wa Chadema ambaye ameshikilia Jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo (2000-2005 na 2005 hadi 2010).

  Mwaka 1995, CCM ilimsimamisha mkuu wa Itifaki, kapteni mstaafu, Abubakar Nkya ambaye alishindwa vibaya na Mtu wa NCCR kabla ya kumsimamisha wakili Elizabeth Minde 2000 na 2005 ambaye hata hivyo hakufua dafu kwa Ndesamburo. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika mwezi uliopita, CCM iliibuka na ushindi wa asimia 65 ikinyakua mitaa 39 huku CHADEMA ikichukua mitaa 21.

  Maoni yangu:
  Huyu mama naona anakoelekea ni kutapatapa ili ccm wamsamehe asingolewe jimboni kwake same, maana anarukia hata miti asiyoweza eti anapiga kambi moshi mjini ili 2010 ndesamburo aanguke

  wadau hii imekaaje????
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh, mafisadi wana kazi kubwa sana kusambaza udaku!..Hata hivyo Watanzania sii wajinga tena wanazisoma alama za wakati na wakati wenu umefikia kikomo.
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu,unamaanisha hata waliopiga kambi kipindi cha uchaguzi wa busanda walikuwa wanalinda majimbo yao au???!!!
   
 4. m

  mtemi Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wamtuma Anne Kilango kumwangusha Ndesamburo Moshi[​IMG]Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ametangaza mapambano Moshi Mjini.[​IMG]Daniel Mjema,Moshi

  MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametangaza rasmi kupiga kambi Moshi Mjini hadi mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa CCM inanyakua jimbo hilo, uamuzi ambao unamuingiza kwenye vita kali na mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo.

  Katika kuonyesha kuwa Ndesamburo hana nguvu kwenye jimbo hilo, Kilango aliwaambia wanachama na viongozi wa CCM kuwa mbunge huyo kutoka Chadema ameshinda mara mbili mfululizo kutokana na matatizo ya wanaCCM wenyewe na kuwataka wajisafishe.

  Kilango, ambaye amekuwa akilalamika kuwa mafisadi wanataka kuchukua jimbo lake la Same Mashariki, alitangaza mkakati huo jana wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi, ikiwa dalili za wazi kwamba, CCM sasa imeanza kujipanga kufanya mashambulizi mkoani hapa ambako vyama vya upinzani vinaonekana kuwa na nguvu kubwa.

  “Nitapiga kambi hapa... kwanini tupate madiwani 12 na Chadema watatu halafu tushindwe ubunge,” alihoji Kilango. “Nitakaa hapa mpaka nimfahamu mchawi ili nimshike mkono nimwambie Rais (Jakaya) Kikwete huyu ndiye anayetufanya tushindwe na Ndesamburo.”

  Mbunge huyo aliongeza kusema:”Hatuwezi kukubali kuwa na wanaCCM ambao mchana wamevaa kijani, lakini usiku wamevaa nguo nyingine…nimeongea na Ndesamburo ananiambia wanaompa ubunge ni wanaCCM wenyewe… hili halikubaliki”.

  Alisema kuwa suala la Jimbo la Moshi Mjini kuwa chini ya upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 linampa tabu sana na hilo ndilo lililomsukuma kupiga kambi katika jimbo hilo hadi uchaguzi mkuu wa 2010.

  “Leo nimebisha hodi hapa tutakuwa wote mpaka Oktoba 2010 na kama tunakosa naomba wananchi mtuambie mapema nini na ndio maana nitakuja kila siku hapa, lakini na nyinyi viongozi na wanaCCM mjitazame inakuwaje tuna madiwani 12 tukose mbunge,” alisema mbunge huyo wa Same.

  Hata hivyo, alisema katika kipindi cha siku mbili tu alizokaa Moshi Mjini ameambiwa kuwa moja ya kero inayoinyima CCM ushindi ni vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga.

  Kilango alifafanua kuwa hakuna mtu muhimu kama anayejitafutia riziki yake, lakini ni jambo baya kama mtu huyo anakwamishwa na kuapa kuwa kwa suala hilo la machinga, ikibidi kulifikisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, basi atafanya hivyo.

  “Sisi tuna njia zetu pale bungeni unaweza kuuliza maswali ya kawaida au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na ikibidi kumuuliza, nitamuuliza,” alisema Kilango.

  Katika hali iliyodhihirisha kuwa suala hilo la machinga linagusa mioyo ya wananchi wengi wa mji wa Moshi, mara tu baada ya Kilango kulitaja, umati wa wananchi na wafuasi wa CCM ulilipuka kwa furaha.

  Mbunge huyo aliamua kumsimamisha katika hadhara hiyo mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi Kuu ya Moshi, Vicent Asenga kuelezea kile kinachowakwaza hadi waamue kutoipa CCM kura katika vipindi vitatu mfululizo.

  Asenga alisema waliingia makubaliano na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwamba kama wanataka kutoa huduma ya biashara kwenye stendi hiyo, wawe na vitambulisho na sare jambo ambalo walilitekeleza kikamilifu.

  Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema walishangaa siku moja wakivamiwa na kukamatwa na kupelekwa ofisi ya kikosi cha usalama barabarani na kutozwa faini ya kati ya Sh20,000 hadi Sh40,000 kana kwamba wao wamefanya makosa yanayohusiana na usalama barabarani.

  “Sisi hatuna upinzani na CCM lakini tuna upinzani na wanaotukwamisha,” alisema Asenga huku akishangiliwa na wananchi waliofurika katika mkutano huo na kuhoji kama makosa ya kufanya biashara yana uhusiano wowote na kikosi cha polisi wa usalama barabarani.

  Kutokana na maelezo hayo na kuwepo wafanyabiashara wengine waliojitokeza kutaka kuzungumza, Mama Kilango aliwataka wafanyabiashara hao kuteua wawakilishi watano ambao angekutana nao jana jioni kupata picha halisi ya kero hiyo.

  Suala la Machinga limekuwa kete ya kisiasa na Ndesamburo aliwahi kununua eneo kwa ajili ya kuanzisha soko la wafanyabiashara hao wadogo, lakini inadaiwa kuwa aliwekewa vizingiti na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, uamuzi ambao unadaiwa kuzidisha hasira ya wafanyabiashara dhidi ya CCM.

  Jimbo la Moshi Mjini limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 1995 likianzia kwa Joseph Mtui wa NCCR (1995-2000) na Philemon Ndesamburo wa Chadema ambaye ameshikilia Jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo (2000-2005 na 2005 hadi 2010).

  Mwaka 1995, CCM ilimsimamisha mkuu wa Itifaki, kapteni mstaafu, Abubakar Nkya ambaye alishindwa vibaya na Mtu wa NCCR kabla ya kumsimamisha wakili Elizabeth Minde 2000 na 2005 ambaye hata hivyo hakufua dafu kwa Ndesamburo. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika mwezi uliopita, CCM iliibuka na ushindi wa asimia 65 ikinyakua mitaa 39 huku CHADEMA ikichukua mitaa 21.
   
 5. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ningemshauri Kilango aende Moshi Mjini, sio kumg'oa Ndesa pesa, bali kumwomba amsaidie ili ateuliwe mgombea wa Chadema huko huko Same Mashariki ccm watakapom ditch.
   
 6. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh ni kweli jamani?

  A WOMAN CAN BE STRONG,CONFIDENT AND SEXY

  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yake anayajuwa???
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Namuheshim mama Killango lakini naona anatumika vibaya hapo na inabidi awe mwangalifu. Kama alishawahi kuwa mkazi wa Moshi mjini nitashangazwa sana kama atakuwa haijui Moshi na wakazi wake vizuri.
  Wananchi wa jimbo la Moshi si wajinga,wanajua haki zao na pia hawapendi haki zao kimsingi ziminywe ama hata kufinyangwa....Kitendo cha kutotaka Ndesamburo asaidie wananchi wake ni ufinyangwaji wa haki zao.

  Kama halmashauri walimkatalia Ndesamburo kuwasaidia hao wafanyabiashara ndogo ndogo kwasababu yeye ni mbunge wao ambaye hatoki CCM halafu waje kufanya the same thing alichotaka kufanya mbunge wao huyo kipenzi na kutegemea kuwa wata win hearts and minds basi wameliwa.Mama Killango angekuwa mjanja na mwenye kuwafahamu watu wa Moshi basi angeanza na kulaani vitendo vyovyote vya kinyanyasaji ikiwemo Ndesamburo kunyimwa haki ya kuwasaidia wanajimbo wake. Lakini notion kwamba Ndesamburo ambaye wananchi wana imani naye,haruhusiwi kuwasaidia wananchi kwasababu yeye si CCM itawacost no matter nani kaenda kupiga kambi hapo Moshi,Mwalimu mwenye palimshinda wakati ule akijaribu kutusokomezea Mkapa as Mr clean,nakumbuka kwenye uwanja wa mashujaa watu walizomea pale alipong'ang'ana na kutoa picha ya Mkapa,akasema taka msitake huyu ndo rais wenu. Jimbo la Moshi mjini lishapotea long time na CCM hawatalipata tena hadi watakapoacha kuwafanya wananchi ni wajinga.

  Wananchi wa Moshi mjini hawana mawazo ya kichangudoa kama CCM wanavyodhani,kwasababu hata kama ni manyanyaso walishapambana nayo lakini hawajawahi kubadili msimamo,wanajua haki zao na hawataki danganya toto,pia siyo watovu wa fadhila kiasi kwamba wamtupe mtu mwenye moyo wa kuwasaidia eti kwasababu CCM wanataka iwe hivyo.
  CCM ikibadilika kiukweli wananchi wa Moshi watajua. Kiutaratibu unaweza kuona hata wapiganaji nao ni wasanii na hawana nia ya kweli ya kuumaliza ufisadi ama kuyashughulika matatizo ya wananchi in a honest way.Kwasababu ufisadi bado haujamalizwa humo CCM,basi ni bora ange concentrate humo ndani ya chama then waje kutuambia kuwa wamebadilika,lakini kama siasa ni za danganya toto,basi hawatampata mtu hapo Moshi. Kwamba madiwani ni wengi zaidi na hivyo ni lazima washinde na ubunge hilo halina corelation yoyote na the way people of Moshi thinks,tena inamaanisha kuwa wakazi wa Moshi wanafanya reasoning na si ushabiki na ndio maana matokeo kama hayo yamekuwa possible,na ndio maana hata yeye mwenyewe mama Killango anadai Ndesamburo kasema wanaompigia kura ni CCM,hapo ndo atajuwa wananchi wanafanya reasoning na si ushabiki na utaratibu wa kwenye makabrasha,wakifanya tathmini zao za kwenye vitabu,reality on the other hand inakuja kuwaumbua,kwa mfano nina uhakika kuwa kuna majimbo ambayo rais wa CCM kachaguliwa lakini mbunge ni wa upinzani.

  Kwa maoni yangu,Mama Killango na CCM wanachezea hizo pesa zao bure tu,badala ake kama kweli wangetaka kuwa win watu wa Moshi,basi hizo pesa wangezipeleka kuwasaidia na si kuzitumia kwa style ya "Tume" ambapo pesa nyingi zinazotumika kwenye tume zimezidi hata kile kilichopotea kabla ya uundaji wa tume,yani costs zinazidi benefits.
  Ndesamburo aliona hilo,wakati CCM wanatumia pesa zao kuhonga pilao,kanga nk,yeye anatumia pesa zake kuwasaidia wananchi,hapo kuna tofauti kubwa sana ambayo wananchi wa Moshi mjini wanaiona lakini viongozi wakuu wa CCM hawaioni.
  Kaazi kweli kweli.
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Mama kilango tulizani ni mpiganaji wa kweli wa haki za wanyonge kumbe geresha? Kutaka umaarufu kunamponza. Tunasubiri ajibu tuhuma alizotupiwa na Sofia za kuvuta m200 kutoka kwa mtuhumiwa wa ufisadi. Ni haki yetu kupokea maelezo kutoka kwake kwani 1-aliahidi kufanya hivyo akiisha kujua kilichomsukuma Sofia kutoboa siri. 2-Alijipambanua kuwa ktk kundi la wasafi na kupewa tuzo hivyo tunataka tujirizishe. Ni kiongozi aliyepewa dhamana. Kuna watu wanaofanyia siasa kila kitu, majibu yao kwa kila swali ni siasa hata kama gari ikipata ajali watasema ni kwa sababu ilikuwa inapita kwenye kipande cha barabara kilichopo kwenye eneo la wapinzani. Au ndio tuseme mama kilango ndio anarudi kundini kiaina? Maana Sofia aliwaweka ccm wote kwenye pipa moja la watu waliokwisha chafuka. Tulitarajia kilango kupiga kambi kwa watu wake wa Same waliofurikishwa na mvua na kukosa makazi mpaka watakapokuwa wamepata hospitali, shule maji safi,makazi nk. Badala yake ati Moshi kwa Ndesa pesa! Kama utakuwa moshi kweli tumia hiyo fursa kuitisha harambee Ndesa utakupiga tafu kwa ajili ya maafa ya Same!!!!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Bado yuko CCM na bado anapokea amri,naona mafisadi wamemlengesha,watampa kila aina ya misaada ili apige kambi hapo,kiukweli hii ni mbinu ya ndani kwa ndani ya CCM ambayo hata hivyo inaweza kum cost mama wa watu pamoja na wale wote wenye kujiita "wapiganaji" Crabs in a bucket,the will keep on pulling each other down.
  Eventually Ndesamburo will prevail i can bet my 2 cents.
   
 11. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ........Halafu wakishatwaa jimbo inakuwaje?.....Kumng'oa Ndesamburo ndio kutaleta maendeleo Moshi Mjini?....Kutafuta sifa kwingine hakuna maana yoyote....
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hakuna kiongozi yoyote Tanzania anayemiliki jimbo, kata, au tarafa licha ya mkoa ni haki ya kila mwananchi kushirki katika siasa za taifa hili na mahali popote pale, sio a crime againts Jamhuri,

  - However, hapa Mama Kilango anachemsha tena sana, Ndesamburo ni aina ya kiongozi tunayemuhitaji sana wananchi wa Tanzania kwa sababu anajali masilahi ya taifa. Ninasema hayo kwa sababu ninakumbuka mimi mwenyewe binafsi kuzunguka naye majuu akifuatana na mtoto wake wa kike ambaye ni hakimu kule Kibaha, akitafuta malori ya kuzima moto kwa ajili ya jimbo lake na aliishia kununua malori mawili na ni kwa hela zake za mfukoni na kuyapeleka jimboni kwake kwa ajili ya wanachi wake,

  - Pamoja na kwamba ni haki ya kila mwananchi kugombea popote pale katika taifa letu kwa sababu sio a crime, tunasema kwamba hapa mama anachemsha na hata CCM wanajua sana kwamba hilo jimbo politically ni la Ndesamburo, wala hakuna ubishi.

  - Na Ndesamburo ni lazima achaguliwe hapo kwenye hili jimbo kwa sababu anatufaa kwa masilahi ya taifa, mambo mengine hayahitaji hata kufikiri mara mbili au hata kuwa careful kuyasema ni one, two, three Ndesamburo ni lazima achaguliwe hapo.

  Respect.

  FMEs!
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hii Moshi mjini ilimshinda Mkapa, mkewe na mihela yao ya kifisadi leo tu maneno ya wana CCM hata kama wanapigana na ufisadi kweli yatasaidia kuirudisha mikononi mwa CCM ambayo BADO inaongozwa na mafisadi? Let us wait and see!
   
 14. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Upinzani si uadui, wapinzani wanahitajika sana nchini kwetu katika kuisukuma Serikali kuwatumikia watu....
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Jasusi unajua kuna mzee mmoja mshikaji hivi na mjanja mjanja sana alikuwa Mkurugenzi huko UN kwa muda mrefu sana, na yeye alirukia hilo jimbo nikamwambia kwamba hao CCM wanakuchuuza upoteze hela zako bure, tena nakumbuka Mkapa, kumuahidi kumpa uwaziri through ubunge wa bure iwapo yule mzee angeshindwa kumtoa Ndesamburo,

  - Maskini mzeee wa watu akaliwa hela kibao na kuishia kupata kura yake tu, uchaguzi kuisha Mkapa hataki hata kumsikia, ila kwa vile yule mzee ni mjanja mjanja akaishia kuanzisha NICO na sasa yuko sawa na zile hela zake zote alizopoteza kwenye ile kampeni alishazirudisha, si unajua bongo tena akili mukichwa!

  Respect.

  FMEs!
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mie nadhani huyu mama ana kazi kubwa ya kufanya, ila nguvu yake anaielekeza mahali pasipokuwa na tija kwa Watanzania. Kwanini asielekeze nguvu zake kwa Kina Chenge, Serukamba, Karamagi na wengine wa aina hiyo? Hapa itatufanya tushindwe kuamini kile anachodai kukisimamia. Ina maana anataka kuingiza kina Serukamba na chenge wengine kwa kuwa kina Slaa, Ndesamburo, Mpendazoe, Kilango etc walipotoka katika malengo na msimamo wa maslahi ya taifa?

  Kweli siasa ni mbaya
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  Huyu mama kilango sasa wenzake wanampelekesha manake kitendo cha kumvamia Ndesamburo ili hali jimboni mwako hajafanya kitu chochote ni sawa na kumcheka nyani wakati kun**lo hulioni. kwanza jimbo lake ndilo la mwisho kimaendeleo kuliko yote kilimanjaro kwanza barabara mbovu.,wananchi wanateseka manake hawajawahi kupata mbunge mzuri toka kipindi cha nyuma. kwanza alikuwa na Mgonja .huyu mgonja hajaleta chochote..akaja YONA huyu ndio kabisa fisadi.sasa kaja huyu mama kwa vile magazeti yanamuandika andika basi anaona kila kitu kipo shwari. hivi ana habari kuwa jimbo lake halina barabara ya lami nyingine yoyote ukiondoa ile barabara ya kwenda Arusha???? hivi amesahau kuwa hata barabara ya kwenda kwao haina lami??hivi anajua kuwa wananchi wa same walikuwa wanategemea zao la kahawa ambalo limeshazikwa????halafu amewasaidia nini wananchi wa same kuleta/kuanzisha zao mbadala?amewasaidia nini wananchi wa same hasa wa milimani kuwatafutia soko zuri la tangawizi zao??anataka kufananisha maendeleo aliyoyaleta Ndesamburo jimboni kwake na ya jimboni kwake same??
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  shame on her,nilimpenda kama mpiganaji lakini amejidhihilishia wazi kuwa nae ni fisadi alotumwa na mafisadi kummaliza mpiganaji mwenzake Ndesamburo japo vyama tofauti.Kwa hili hapana sijakubaliane nae,Ataondoka kichwa chini.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  serious huyu mama sio mpiganaji manake sasa anapigana na Ndesamburo au na mafisadi au anapigania wananchi wake???? mimi sijaelewa intention yake...kwamba yeye anataka ccm wawe na majimbo mengi ili iweje? wakati wananchi wake wanateseka.
   
 20. m

  mtemi Member

  #20
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli ni kwamba huyu mama anaweweseka,sijui ni kwa sabsabu ya siri ya ufisadi wake aliyoitoa mama simba???
   
Loading...