Mama Kilango apiga Kambi Moshi mjini; kumng'oa Ndesamburo?

ukweli ni kwamba huyu mama anaweweseka,sijui ni kwa sabsabu ya siri ya ufisadi wake aliyoitoa mama simba???
na huyu lazima wataendelea kumlipua..ameshawashindwa kina LA sasa anahamia kwingine ambako hamna maslahi kwa wananchi...huyu katumwa
 
Sophia Simba aipasua CCM
• Kilango apania kumburuza mahakamani

na Janet Josiah

amka2.gif

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba, amekigawa chama tawala katika makundi makubwa mawili.
Kundi la kwanza ni la vigogo wa chama wanaompinga vikali, wakiwamo Mbunge wa Same, Anna Kilango-Malecela, Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Mzee John Malecela (Mtera), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), ambao miongoni mwao, Anna Kilango ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Malecela, amemwekea mawakili maarufu 10 kumburuza mahakamani kwa madai ya kumdhalilisha na kumchafulia jina.
Kundi jingine linamkingia kifua, likiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, ambaye jana alimtetea Waziri Simba akisema, ‘hana hatia.'
Mtafaruku unaomzunguka Waziri Simba unatokana na hatua yake ya ‘kusema hovyo' kwenye kikao cha Kamati ya Usuluhishi inayoongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, siku chache zilizopita, alipowashambulia kwa maneno makali wabunge wapambanaji wa ufisadi.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata, zinasema kuwa katika kesi hiyo ambayo bila shaka itavuta hisia za watu, itafunguliwa wakati wowote sasa, baada ya Sophia Simba kukaidi notisi ya siku 14 aliyopewa na mawakili hao kumuomba radhi mbunge mwenzake.
Wakati wa kikao kilichopita cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake (UWT), baadhi ya wajumbe walihoji kama Waziri Simba amepata notisi ya kusudio la kufunguliwa kesi. Yeye alikiri kupata notisi hiyo ya siku 14, zilizomalizika jana.
Hata hivyo, Baraza Kuu halikuweza kujadili suala hilo ndani ya kikao hicho kwa vile Mama Kilango si mjumbe.
Hivi karibuni, kwenye kikao cha Kamati ya Mzee Mwinyi mbele ya wabunge wa chama hicho tawala, wakati akichangia hoja kuhusu chanzo cha wabunge kulumbana wao kwa wao, Waziri Simba alimshambulia Mama Kilango kwamba si msafi kiasi cha kuwatuhumu wenzake kwamba wanahusika na ufisadi.
Waziri Simba alimtuhumu Mama Kilango kuwa si msafi, na kwamba baadhi ya watu anaowaita mafisadi leo ndio waliofadhili harusi yake na Mzee Malecela.
Alienda mbali kwa kusema bila juhudi za Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mama huyo asingeolewa na mkongwe huyo wa siasa nchini.
Waziri Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya Kilango na makamu huyo wa zamani wa CCM ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.
Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuchota takribani sh bilioni 11 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu pia Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya pili, kwamba wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu alimpa sh milioni 200 kwa ajili ya kampeni zake.
Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwa nguvu ya Mkapa, hata bila kujadiliwa na vikao.
Akizungumza kwa kujiamini na ujasiri, Simba alimtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya kuukosa ‘ufesti ledi' (kuwa mke wa rais).
Naye Kilango alisema alishuhudia wakati makombora hayo yakirushwa, akaeleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.
Mbali na Mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.
Pia alimshambulia Mbunge wa Kyela, Dk. Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.
Waziri Simba alisema hata tuhuma dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.
Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba, hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu. Wakati Kilango akijiweka sawa kufungua kesi, ndani ya CCM, hatua hiyo imezua mjadala mkubwa. Baadhi ya wanachama wanataka mahasimu hao wawili wapatanishwe ndani ya vikao na wengine wanataka suala hilo litinge kortini ili haki itendeke.

Baadhi ya wanaomsakama Simba wamefika mahali pa kumshauri Rais Jakaya Kikwete amtimue kazi.
Hata hivyo, Msekwa alisema jana kuwa, Waziri Simba hakukosea, na kwamba alikuwa sahihi kutumia uhuru wake ndani ya chama kuibua hoja ambazo zilipaswa kuwa siri.
"CCM haiwezi kumchukulia hatua Mheshimiwa Simba kwa kusikiliza maneno ya uvumi, ambayo yamekuwa yakiandikwa na kusikika katika vyombo vya habari," alisema Msekwa.
Kwa sababu hiyo, Msekwa alisema chama hakiwezi kuchukua hatua zozote dhidi yake.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya miaka mitano ya ushirikiano kati yake na Chama Cha Kikomonisti cha Cuba (CPC) ambapo Cuba iliwakilishwa na Balozi wake nchini, Ernesto Gomez Diaz.
Msekwa ambaye alikuwa mjumbe katika kamati ya watu watatu ya kutafuta chanzo cha mgogoro wa wabunge wa CCM na mawaziri, alisema anayeona Waziri Simba amekosea kutokana na kauli yake, anapaswa kupeleka ushahidi wa maneno na wa kisheria ili CCM iweze kuchukua hatua na si kuzungumza tu.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini wanasema, mgawanyiko huu wa makundi ya vigogo kuhusu kauli za Simba, unaongeza ufa katika chama ambacho kwa miaka miwili mfululizo kimekuwa kinahaha kujinusuru na tuhuma za ufisadi zinazowakabili makada wake wakuu, ambazo kwa mara ya kwanza zilirushwa na viongozi wa vyama vya upinzani mwaka 2007. Wanadai kwamba kwa kuwa Rais Kikwete ndiye alimteua Simba kuwa mbunge na waziri, na kwa kuwa amegoma kumchukulia hatua kutokana na jinsi alivyowasilisha kauli zake, naye anaingizwa katika kundi linalombeba Simba, akiwa upande wa makamu wake, Msekwa. Na ingawa Mzee Malecela, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM kabla ya Msekwa, ni mjumbe wa kudumu wa Halmashauri Kuu ya CCM, mashambulizi haya dhidi yake na mkewe yanamfanya kuwa katika kundi linalomtetea Kilango na kumsakama Simba
 
Sophia Simba aipasua CCM
• Kilango apania kumburuza mahakamani

na Janet Josiah

amka2.gif

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba, amekigawa chama tawala katika makundi makubwa mawili.
Kundi la kwanza ni la vigogo wa chama wanaompinga vikali, wakiwamo Mbunge wa Same, Anna Kilango-Malecela, Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Mzee John Malecela (Mtera), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), ambao miongoni mwao, Anna Kilango ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Malecela, amemwekea mawakili maarufu 10 kumburuza mahakamani kwa madai ya kumdhalilisha na kumchafulia jina.
Kundi jingine linamkingia kifua, likiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, ambaye jana alimtetea Waziri Simba akisema, ‘hana hatia.’
Mtafaruku unaomzunguka Waziri Simba unatokana na hatua yake ya ‘kusema hovyo’ kwenye kikao cha Kamati ya Usuluhishi inayoongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, siku chache zilizopita, alipowashambulia kwa maneno makali wabunge wapambanaji wa ufisadi.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata, zinasema kuwa katika kesi hiyo ambayo bila shaka itavuta hisia za watu, itafunguliwa wakati wowote sasa, baada ya Sophia Simba kukaidi notisi ya siku 14 aliyopewa na mawakili hao kumuomba radhi mbunge mwenzake.
Wakati wa kikao kilichopita cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake (UWT), baadhi ya wajumbe walihoji kama Waziri Simba amepata notisi ya kusudio la kufunguliwa kesi. Yeye alikiri kupata notisi hiyo ya siku 14, zilizomalizika jana.
Hata hivyo, Baraza Kuu halikuweza kujadili suala hilo ndani ya kikao hicho kwa vile Mama Kilango si mjumbe.
Hivi karibuni, kwenye kikao cha Kamati ya Mzee Mwinyi mbele ya wabunge wa chama hicho tawala, wakati akichangia hoja kuhusu chanzo cha wabunge kulumbana wao kwa wao, Waziri Simba alimshambulia Mama Kilango kwamba si msafi kiasi cha kuwatuhumu wenzake kwamba wanahusika na ufisadi.
Waziri Simba alimtuhumu Mama Kilango kuwa si msafi, na kwamba baadhi ya watu anaowaita mafisadi leo ndio waliofadhili harusi yake na Mzee Malecela.
Alienda mbali kwa kusema bila juhudi za Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mama huyo asingeolewa na mkongwe huyo wa siasa nchini.
Waziri Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya Kilango na makamu huyo wa zamani wa CCM ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.
Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuchota takribani sh bilioni 11 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu pia Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya pili, kwamba wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu alimpa sh milioni 200 kwa ajili ya kampeni zake.
Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwa nguvu ya Mkapa, hata bila kujadiliwa na vikao.
Akizungumza kwa kujiamini na ujasiri, Simba alimtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya kuukosa ‘ufesti ledi’ (kuwa mke wa rais).
Naye Kilango alisema alishuhudia wakati makombora hayo yakirushwa, akaeleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.
Mbali na Mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.
Pia alimshambulia Mbunge wa Kyela, Dk. Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.
Waziri Simba alisema hata tuhuma dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.
Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba, hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu. Wakati Kilango akijiweka sawa kufungua kesi, ndani ya CCM, hatua hiyo imezua mjadala mkubwa. Baadhi ya wanachama wanataka mahasimu hao wawili wapatanishwe ndani ya vikao na wengine wanataka suala hilo litinge kortini ili haki itendeke.

Baadhi ya wanaomsakama Simba wamefika mahali pa kumshauri Rais Jakaya Kikwete amtimue kazi.

Hata hivyo, Msekwa alisema jana kuwa, Waziri Simba hakukosea, na kwamba alikuwa sahihi kutumia uhuru wake ndani ya chama kuibua hoja ambazo zilipaswa kuwa siri.
“CCM haiwezi kumchukulia hatua Mheshimiwa Simba kwa kusikiliza maneno ya uvumi, ambayo yamekuwa yakiandikwa na kusikika katika vyombo vya habari,” alisema Msekwa.
Kwa sababu hiyo, Msekwa alisema chama hakiwezi kuchukua hatua zozote dhidi yake.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya miaka mitano ya ushirikiano kati yake na Chama Cha Kikomonisti cha Cuba (CPC) ambapo Cuba iliwakilishwa na Balozi wake nchini, Ernesto Gomez Diaz.
Msekwa ambaye alikuwa mjumbe katika kamati ya watu watatu ya kutafuta chanzo cha mgogoro wa wabunge wa CCM na mawaziri, alisema anayeona Waziri Simba amekosea kutokana na kauli yake, anapaswa kupeleka ushahidi wa maneno na wa kisheria ili CCM iweze kuchukua hatua na si kuzungumza tu.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini wanasema, mgawanyiko huu wa makundi ya vigogo kuhusu kauli za Simba, unaongeza ufa katika chama ambacho kwa miaka miwili mfululizo kimekuwa kinahaha kujinusuru na tuhuma za ufisadi zinazowakabili makada wake wakuu, ambazo kwa mara ya kwanza zilirushwa na viongozi wa vyama vya upinzani mwaka 2007. Wanadai kwamba kwa kuwa Rais Kikwete ndiye alimteua Simba kuwa mbunge na waziri, na kwa kuwa amegoma kumchukulia hatua kutokana na jinsi alivyowasilisha kauli zake, naye anaingizwa katika kundi linalombeba Simba, akiwa upande wa makamu wake, Msekwa. Na ingawa Mzee Malecela, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM kabla ya Msekwa, ni mjumbe wa kudumu wa Halmashauri Kuu ya CCM, mashambulizi haya dhidi yake na mkewe yanamfanya kuwa katika kundi linalomtetea Kilango na kumsakama Simba

huyu simba hawajui wapare wanapenda kesi hao...yaani hapa huyu mama kilango ndio yupo uwanja wa nyumbani leh!!
 
Ina maana Mpare anaweza kuwa tayari kumuuza hata mumewe ili ashinde kesi?

Mama Simba, changamkia tenda hiyo, Mgogo John itabidi auzwe, Mpare ashinde kesi ..... hahaaaa Shemeji zangu Wapare.
 
Hivi mama Kaboyoka yupo wapi, kilichosababisha yeye kutopata nafasi ya kugombea 2005 ni kutokuhonga tu, yule mama inaelekea hana longo longo, akipata ubunge labda walau kutakuwa na maendeleo...

kuna wakati huwa na lazimika kuamini kwamba kinachomfanya mama Kilango alie lie na mafisadi ni kisirani cha mumewe kunyimwa kugombea urais 2005...
 
Huyu mama kilango sasa wenzake wanampelekesha manake kitendo cha kumvamia Ndesamburo ili hali jimboni mwako hajafanya kitu chochote ni sawa na kumcheka nyani wakati kun**lo hulioni. kwanza jimbo lake ndilo la mwisho kimaendeleo kuliko yote kilimanjaro kwanza barabara mbovu.,wananchi wanateseka manake hawajawahi kupata mbunge mzuri toka kipindi cha nyuma. kwanza alikuwa na Mgonja .huyu mgonja hajaleta chochote..akaja YONA huyu ndio kabisa fisadi.sasa kaja huyu mama kwa vile magazeti yanamuandika andika basi anaona kila kitu kipo shwari. hivi ana habari kuwa jimbo lake halina barabara ya lami nyingine yoyote ukiondoa ile barabara ya kwenda Arusha???? hivi amesahau kuwa hata barabara ya kwenda kwao haina lami??hivi anajua kuwa wananchi wa same walikuwa wanategemea zao la kahawa ambalo limeshazikwa????halafu amewasaidia nini wananchi wa same kuleta/kuanzisha zao mbadala?amewasaidia nini wananchi wa same hasa wa milimani kuwatafutia soko zuri la tangawizi zao??anataka kufananisha maendeleo aliyoyaleta Ndesamburo jimboni kwake na ya jimboni kwake same??

Nonsense...nonsense... nonesense comments!!! Hizo sio kazi za mbunge... Ni serikali.... hii inaonyesha jinsi ccm ilivyoshindwa....
 
Siasa game chafu sana, Hapa Mama Kilango anatafuta cheap popularity itakayomponza.

Wakati yeye anapiga kambi Moshi mjini, watu kule Same wanajenga kabisaaa, by the time anarudi kila kitu kimeshatwaliwa.

Mama Kilango hapo unapoenda umekosea, wrong political move.
 
Unajua , Ngoma ikilia sana hupasuka.

Ndiyo ya mama huyu. Amelewa sifa kidogo aliPEwa nazo, anaona sasa anaweza kuhamisha milima!

Nao wananchi wa Moshi kweli watakubali kumwangusha mtu ambaye wanamjua kawasaidia, kisa domokaya la huyu mama?, idont think so.

Wachagga wana uelewa wa kutosha, sidhani kama watadanganyika!
 
Nadhani mama amegundua kuwa hatima yake kisiasa iko shakani come year 2010.

Si ni kweli ili uwe mbunge ni lazima upitishwe na chama chako, na chama chake kimeshikwa na mafisadi sasa anafanyaje ili aonekane kwamba bado anakipenda chama katiza zama hizi ambazo yeye anatuhumiwa kusaidia upinzani kukidhoofisha chama kwa kukihusisha na ufisadi...ni kujiunga na kampeni ya kina Kilewo ya kugomboa majimbo ya kilimanjaro kutoka mikono ya upinzani.

Anataraji kwa kufanya hivyo ataweza kupata sympathy ya wazee wa chama ambao pengine watamsaidia itakapofika siku ya kukutana na kisu cha mafisadi kwenye uteuzi wa wagombea ubunge wa ccm. Na hii inadhihirisha kuwa si mpiganaji bali ni political opportunist wa kawaida kabisa ambaye kwa kuwa ameshaingia mjengoni hayuko radhi kutoka ima fa imma. Angekuwa mpiganaji wa kweli angekuwa tayari kukutana na kisu cha mafisadi...akipata ubunge hewala akikosa sio mwisho wa dunia wala mapambano.

Ni good pre-emptive move ingawa ni vigumu kujua kama itamsaidia kwa sasa maana hata hao wazee wameshajua kuwa hawana chao ndani ya ccm zaidi ya kulipia kadi zao kila mwaka na kuvaa mashati ya jembe na nyundo wa kati wa mikutano ya chama, kwani ni rasmi sasa kuwa chama ni cha EL na RA.

Kwa kweli hali imefika patamu sana na 2010 tutaona mengi..tuombe uhai..

ni mtazamo tu....
 
Mkuu,unamaanisha hata waliopiga kambi kipindi cha uchaguzi wa busanda walikuwa wanalinda majimbo yao au???!!!

Mama Kilango anatapatapa na anajua wazi kuwa watamfyatua tu kwenye kupitisha majina ..si alisema patachimbika huyu sasa analo eti jimbo lake ...kuna mtu ana jimbo hapa
 
Jambo moja ambalo halifichiki ni mahitaji ya elimu kwa wapiga na wapigiwa kura, na kwa hali ilivyo sasa wapiga kura wana nafuu kuliko wapigiwa kura. Nia kama ni njema kujenga nchi...hivi mtu makini katika siasa anatafutaje kumuondoa mbuge anayelifanyia kazi jimbo lake kwa vile tu ni mpinzani badala ya kuwatoa wenzie wanaoipeleka nchi pabaya? Mama Kilango anataka kujaribu kuvaa viatu over size tena high heels! utauweza huo mji? Mama, Chunga pua yako maana ndio itakuwa ya kwanza kufika chini.
 
Mtemi.
Hii haijatulia kabisa. Hawezi kushinda na Ndesamburo,akapige kambi kwenye jimbo lake,yeye mwenyewe kwake amekalia kuti kavu ndo ataweza Moshi Mjini. Asijidanganye kwamba anakubalika kila sehemu.Mi namshauri aende akapige kambi Mtera kwa mumewe.
 
Siasa game chafu sana, Hapa Mama Kilango anatafuta cheap popularity itakayomponza.

Wakati yeye anapiga kambi Moshi mjini, watu kule Same wanajenga kabisaaa, by the time anarudi kila kitu kimeshatwaliwa.

Mama Kilango hapo unapoenda umekosea, wrong political move.

FairPlayer
Heshima mbele.Hii imekaa vizuri.
 
Unajua , Ngoma ikilia sana hupasuka.

Ndiyo ya mama huyu. Amelewa sifa kidogo aliPEwa nazo, anaona sasa anaweza kuhamisha milima!

Nao wananchi wa Moshi kweli watakubali kumwangusha mtu ambaye wanamjua kawasaidia, kisa domokaya la huyu mama?, idont think so.

Wachagga wana uelewa wa kutosha, sidhani kama watadanganyika!

PakaJimmy
Heshima mbele.Hii imekaa vizuri
 
Mama Kilango kama walivyo wanasiasa wengi wa bongo anajua kuuma na kupuliza. Unafiki kwenye siasa zetu ni sehemu ya maisha ya kila siku ya wanasiasa wetu. Nakumbuka pia alivyoanza kudandia hoja za ufisadi zilizokuwa zikiibuliwa na upinzani Bungeni. Alisema wazi kuwa hawezi kukaa kimya awaachie akina Zitto kujizolea umaarufu dhidi ya Chama chake.
 
Re: Kilango kuwa chambo kwa kuja Moshi,
Nadhani mtandao wa serikali ni mpana sana. kuja kwa Kilango Moshi naona ni mtego kwake yeye Kilango kujimaliza kisiasa. Kuna mambo kadhaa yanaashiria niyasemayo hapo juu kama,
1) Ndesa amefanya mengi Moshi ni pamoja na kuboresha mtandao wa maji sehemu ya Kiboriloni, Kuboresha barabara ya Mbokom, Kujenga soko la wamachinga Kiborilon, kusaidia vkundi vingi tuu vya wakaazi wa Moshi, Kuwa nguzo kamili kutetea ufufuaji wa uchumi Moshi na mengine mengi tuu.
2) Maswala ya ujinsia nao umewekwa mbele sana Moshi. Mkuu wa mkoa, mbunge, mkugenzi wa manispaa wote ilitakiwa wawe wanawake. Na sasa tena, ameletwa Kilango kuongeza maswali. hii yote ni kuongeza msongo wa mawazo kwa wakaazi wa Moshi ambao wanamfumo dume anzia enzi za ujima.
3) Kilango anajifanya kuwa mpiganaji vita vya mafisadi. Ameanza kuumbuliwa na Sofia sasa Moshi ndo watamzika. Akileta mambo ya utani wa kikabila hata jimboni kwake atanguka
4) Naona anataka kujishika na CHADEMA ila ameanzia pabaya. Aombe CHADEMA msaada wa kusaidia waadhirika wa maporomoka ya ardhi jimboni kwake ajazie hizo za kampeni ya kukomboa jimbo la Moshi ziwasaidie
Mungu amsaidie aachane na sisism labda atarudi bungeni mwakani.
 
Huyu mama nashindwa kuwelewa vile. Yeye anajifanya mpambanaji, sasa anasema anataka kumngoa Ndesa, je ndesa ni fisadi? Watu wa moshi mjini na sehemu nyingene nchini wanafahamu wazi kuwa huyu mzeewatu Ndasamburo ni mmoja wa viongozi wachache sana tulionao hapa nchini.
Ningemshauri huyu mama arrudi jimboni mwake akajipange vizuri maana yawezekana Mafisadi wakamngoa, na si kuja moshi kupambana na Ndesamburo. Ataaibika bure.
Na kama anataka, maana naona same yanamshinda,basi aje moshi agombbe pamoja na ndesamburo,tuone umaarufu wake.
 
Mwe,Mwe,Mwe...Mama kawachokoza wachagga na Chadema yao,angepiga kambi Monduli angesifiwa kuwa ni kamanda wa makamanda lakini kwa sababu ni moshi kwa Chadema mama atatukanwa leo..mwe..mpaka Tanzania Daima gazeti la Chadema limemwandika mama.Tuliambiwa anataka kuja Kyela vilevile tunamkaribisha,nondo za mama SS zitammaliza.Kama ndoa iliendeshwa na pesa za kifisadi kwahiyo hiyo ni ndoa ya kifisadi..mweeeeeeeeeeee.
 
Mama kilango siyo mpiganaji, kwa nilijua hayo wakati wamijadala ya bungeni.
Hajawahi kuiprement issue yoyote zaidi ya kuchangia ya wenzake.
Na mara kwa mara ni ile inayo husu makosa furani.
Sema tu anauwezowa kutoa sauti au kupanua midomo.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom