Wananchi wanataka usimame hadharani juu ya mambo mawili makuu ambayo yamegeuka mateso makubwa na fedheha kwa jiji:
Tunasisitiza pia usimame na kusikiliza wananchi uso kwa uso katika maeneo haya: Buhongwa, Mkolani, Nyegezi Stend, Mkuyuni na Mabatini.
- Maji – Takribani mwezi mzima chanzo cha Butimba kimeharibika. Ulizindua mradi huu kwa matumaini, lakini hali imeendelea kuwa mbaya zaidi:
- Hata mgao wa siku mbili kwa wiki uliokuwepo awali haupo tena.
- Juzi, baada ya kelele nyingi za wananchi, maji yalirudi lakini kwa spidi sifuri (0).
- Wananchi wanateseka sana: wananunua maji kwa shilingi 2,000, wengine hawana kabisa. Hii ni hali ya fedheha na mateso yasiyo na kifani.
- Mama, uliza hadharani: Hii ni uzembe wa makusudi au kuna wanaokuhujumu? Huu ni wakati wa kutoa kauli kali ya utenguzi – wananchi hawawezi kuendelea kuvumilia mateso haya.
- Piga marufuku mradi wa uuzaji maji kwa magari unao fanywa na Mwauwasa hi ndo iadsbsbisha wazembee kutoa maji ili watu wanunue.
- Barabara – Hali ya Mabatini na Mkuyuni ni aibu kubwa. Ni vipande vidogo tu, lakini mkandarasi hafanyi kazi kwa uharaka. Foleni zimekuwa mateso ya kila siku, watu wanasota masaa barabarani. Hii ni barabara kuu ya jiji, haiwezekani ikakaa mwaka mzima bila kukamilika.
- Mama, ukifika Mkuyuni, simama hadharani na utembelee vipande hivyo. Wananchi wanataka majibu ya papo kwa papo.
Tunasisitiza pia usimame na kusikiliza wananchi uso kwa uso katika maeneo haya: Buhongwa, Mkolani, Nyegezi Stend, Mkuyuni na Mabatini.