Mama Janeth Magufuli agoma kukampeni, acharuka

Status
Not open for further replies.

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kutokana na kutoonekana kwenye kampeni za mumewe, Dr. John P. Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametumiwa ujumbe na CCM ili ajiunge kwenye kampeni za Dr. Magufuli. Ujumbe huo wa kichama ulitumwa kupitia wanamama manguli chamani ili kwenda kumpigia kampeni mumewe na kufanya ayafanyayo Mama Regina Lowassa, mke wa mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa.

Katika kikao hicho cha kichama na kirafiki ili aafiki, Mama Magufuli aligoma kujiunga kwenye timu kampeni za mumewe zinazoendelea kurindima nchi nzima. Mama Magufuli, aliyesemekana kuwa mkali, alisema kuwa aachwe aendelee kufundisha wanafunzi wake wa Mbuyuni Primary School kwakuwa yeye si mwanasiasa. Mama Magufuli amewadokeza wapeleka ujumbe kuwa amekubaliana na Dr.Magufuli juu ya uamuzi wake wa kutoambatana naye kwenye kampeni.

Wajumbe waliopeleka ujumbe wa chama walibaki kimya na kurudisha majibu hayo ya mgomo. Turufu ya mwisho ya kumshawishi Mama Magufuli kujiunga kwenye kampeni imebaki kuwa Mama Maria Nyerere ambaye anatajwa kuwa na uwezo wa kumshawishi Mama Magufuli. Mama Magufuli atakutanishwa hivi karibuni na Mama Nyerere nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere Dar es Salaam ili kuyaweka sawa mambo hayo.

Inampasa Mama Magufuli aige mfano na awe kama Mama Regina Lowassa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Yaani ninyi, mnataka ccm iwe UKaWA?

Magufuli hawezi kuwa Lowasa hata mkimwita M4C.

Janeth hata angejiloweka kwenye magadi haji kuwa Regina.

Kama hamna vya kwenu, mkalale, maigizo hayasaidii!
 
Huyo Mama Ndo Mwenye Akili,anajijua Yeye Si Mwanasiasa Hataki Kuingilia Fani Za Wengine,wanasiasa Fanyeni Yenu Na Yeye Afanye Yake.Hatutamchagua Rais Just Because Anatembea Na Mke Wake Au Mke Wake Anamsaidia Kukampeni,kama Ni Hivo 2005 Lipumba Asingeambulia Hata Nusu Ya Kura Alizopata......
 
Magufuli ni player mzuri sana kwa Wanawake, huyu mama wametengana kwa sababu ya Magufuli kuzidisha michepuko...ikiwa Magufuli atashinda Urais basi ndoa yake itakuwa km ile ya Benjamin Mkapa na Anna Mkapa!
 
Mama Janet Magufuli ni mtu "Kiona mbali" sana!! ameshagundua kwamba safari ya mumewe "is on a road to nowhere"
!! Aachwe aendelee na kazi yake ya wito, UALIMU.

VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
Hawa CCM kweli ni vichwa maji, wanamkumbuka Mama Maria Nyerere wakati wanapokwama.
 
Kutokana na kutoonekana kwenye kampeni za mumewe, Dr. John P. Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametumiwa ujumbe na CCM ili ajiunge kwenye kampeni za Dr. Magufuli. Ujumbe huo wa kichama ulitumwa kupitia wanamama manguli chamani ili kwenda kumpigia kampeni mumewe na kufanya ayafanyayo Mama Regina Lowassa, mke wa mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa.

Katika kikao hicho cha kichama na kirafiki ili aafiki, Mama Magufuli aligoma kujiunga kwenye timu kampeni za mumewe zinazoendelea kurindima nchi nzima. Mama Magufuli, aliyesemekana kuwa mkali, alisema kuwa aachwe aendelee kufundisha wanafunzi wake wa Mbuyuni Primary School kwakuwa yeye si mwanasiasa. Mama Magufuli amewadokeza wapeleka ujumbe kuwa amekubaliana na Dr.Magufuli juu ya uamuzi wake wa kutoambatana naye kwenye kampeni.

Wajumbe waliopeleka ujumbe wa chama walibaki kimya na kurudisha majibu hayo ya mgomo. Turufu ya mwisho ya kumshawishi Mama Magufuli kujiunga kwenye kampeni imebaki kuwa Mama Maria Nyerere ambaye anatajwa kuwa na uwezo wa kumshawishi Mama Magufuli. Mama Magufuli atakutanishwa hivi karibuni na Mama Nyerere nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere Dar es Salaam ili kuyaweka sawa mambo hayo.

Inampasa Mama Magufuli aige mfano na awe kama Mama Regina Lowassa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Wwe nyumbu hebu acha mihemuko, Magufuli ni mwenyewe ni timu ya watu mia, anapiga mzigo mwenyewe, na atamaliza mwenyewe. Hii inatuambia pia kuwa hata akiingia ikulu hatayumbishwa na mke wake, maana kazi anapiga mwenyewe. Kwa lowassa ni wazi kabisa maamuzi mengi ya nchi yatakuwa yanatolewa na mama lowassa, maana kampen wamefanya woten
 
Magufuli ni player mzuri sana kwa Wanawake, huyu mama wametengana kwa sababu ya Magufuli kuzidisha michepuko...ikiwa Magufuli atashinda Urais basi ndoa yake itakuwa km ile ya Benjamin Mkapa na Anna Mkapa!

Mkuu unamaana mh Jp nimdau wa njia za vumbi..
sasa siatakua anapigwa stuli kama besti yake mzee lod.lofa..
 
Magufuli ni player mzuri sana kwa Wanawake, huyu mama wametengana kwa sababu ya Magufuli kuzidisha michepuko...ikiwa Magufuli atashinda Urais basi ndoa yake itakuwa km ile ya Benjamin Mkapa na Anna Mkapa!

hivi watu mnapata wapi mamlaka ya kuzungumzia maisha ya ndan ya mtu?.
Huko ni kukosa hoja ukiona mtu anaanza kuchambua maisha ya chumban ya mtu.

Mbona hujamuuliza baba yako alivyobambikiwa mimba na mama yako?
 
Yaani kila kitu mnaiga tuuuu heeeee.
Pandeni daladala basi, maana Mama Lowasa anapiga kampeni na nyie mwataka Mke wa Magufuli
 
Kuna tatizo na idara ya usalama. Ilibidi hiyo itilafu itatuliwe kabla hata kamati kuu kumpitisha. Ni aibu kwa ccm. Kama ameshindwa kumamliza mgogoro wa ndani ataweza wa nje?
 
Yaani March Yeye ni Muajiriwa halali kabisa anapokea Mshahara kwa halali kupitia Kufundisha... Sasa Ninyi CCM Mnataka Mama aache Kazi yake Akaambatane na Mtu ambaye Hata Raisi wa Libya humjui, kwa Kazi gani... Halafu Huyo Mama akiondoka watoto wetu Watafundishwa na Nani...

Hebu fikirieni Marambili Bana HUYO MAMA NI MFANO WA KUIGWA KWANI ANAIPENDA KAZI YAME, ANAITHAMINI NA ANAITENDEA HAKI.... SIKU NIKIMUONA KWENYE CAMPAIGN NITAMTOA KASORO NYINGI SANAAAAA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom