Well Said mkuu - binafsi swala hili nilisha liona mapema sana - Serikali yetu isipo jitahidi kumaliza kero za ndugu zetu Waislaam sitashangaa siku moja Nchi hii ukakuta inagawanyika mara mbili kama ilivyo gawanyika Sudan - kusini Wakristo na Kasikazini Waislaam. Labda nieleweke kwamba sio kwamba nataka/pendekeza hilo litokee lakini tukumbuke binadamu wana kikomo cha kuvumulia, hamuwezi kuapuuzia malalamiko ya kweli ya kundi la madhehebu fulani miaka yote - tusije tukajidanganya hapa.
Historia inaonyesha hii si mara ya kwanza nchi moja kugawanyika kwa misingi ya Dini - India kwa mfano: Wakati India inatawaliwa na Waingereza hapakuwepo nchi inayo julikana kama Pakistani wala Bhangladeshi, katika harakati za kutaka kukomboa India, Kiongozi wa Kislaam aliye julikana kwa jina la Mohammed Ali Jinnah alimwendea rafiki na mwanaharakati mwenzake wa madhehebu ya kihindu aliyejulikana kwa jina la Mohandas Karamchand Gandhi (wote walisomea Sheria Chuo kikuu London kweye miaka ya mwishoni mwa 1800). Jinnah kamweleza kinaga ubaga Ghandi kwamba India ukinyakua uhuru basi nchi hiyo ingawane sehemu mbili - moja iwe kwa Wahindu na nyingine kwa ajili ya Waislaam, Gandhi alijitahidi sana kumsihi Jinna kwamba wawe kitu kimoja wasigawe nchi, Jinna alimkatalia akisema Waislaam wananyanyaswa sana hawewezi kukubali kuwa chini ya Wahindu, kapeleka swala lake UN na akakubaliwa kuhunda Taifa la Pakistani na yeye kuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Taifa jipya la Pakistani, kama sikosei tatizo hili limekuja kujirudia tena miaka ya hivi karibuni nchini Yugoslavia ilikuja kugawanywa kwa misingi hii hii.
Kwa hiyo ninapo toa tahadhali nafikilia vitu kama hivyo, lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya Watanzania wenzangu kwenye forum hii ambao aidha awanielewi au ni watu wenye dhalau zisizo na tija kwa kukosa kutafakali mambo kwa kina, oh yes kuna mmoja wao amediriki kusema mimi ni MPUMBAVU!!! - hizo ndio hulka za baadhi ya Watanzania wenzetu tulivyo, you can't blame 'em! Can U? inategemea walivyo kuwa brought UP - wana thrive kutokana na MATUSI waliyo ya-acquire utotoni.