Mimi naona hii wizara ya Ardhi kuna ufisadi sana, hasa katika ngazi ya Halmashauri.
Kwenye Halmashauri ndo kwenye ardhi
Mifano michache, juzi juzi tu tulisikia uchakachuaji katika ugawaji viwanja Arumeru eneo la Burka. Watu walilalamika, magazeti yakaandika lakini bado hakuna kilichobadilika. Watu wamechakachua viwanja, vigogo wamechukua viwanja na kuwauzia makaburu wakati watanzania wenyeji wa hapo wamekosa viwanja na hawana makazi.
Sasa angalia hii nyingine. Ardhi ni ya Watanzania, wanastahili wagawiwe katika ada ndogo tu kwa ajili ya upimaji. Lakini sasa wajanja wachache wameamua kuteka ardhi ya watanzania na kufanya dili la kujipatia fedha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Tangazo la Kuuza Viwanja - Katika Mwananchi Paper page 17. Tarehe 20 Dec, 2011.
Arusha- TENGERU
Kabale Estates wanauza viwanja, je hawa kabale estate wametoa wapi hiyo ardhi? Nani amewauzia ardhi hao Kabale estates? Na huyo aliyewauzia kabale estate katoa wapi ardhi??
Kimsingi, hiyo ardhi ni mali ya watanzania wanaoishi maeneo hayo au wanaoishi na hawana makazi.
Sasa hawa viongozi wa Manispaa na afisa ardhi wanavyouza ardhi, je watanzania masikini wataweza, au mafisadi tu ndo watamiliki ardhi tanzania?
Hapa kuna harufu ya Rushwa sana...