mama anataka harusi na wakati sijawa tayari...

hizi mada za mama anataka nioe ni nyingi huku jamvini.nafikiri wanaume wa siku hizi wengi wameshikiwa akili na mama zao ypung ang foolisly mistaken

Ndo hivyo kaka wazazi wanafosi harusi as vijana hatueleweki kila siku mchuchu mpya
 
Heshima kwenu brothers an sisters

Nimebanwa sana na my best friend kutoa ushauri hadi kichwa kinauma naombeni msaada wa mawazo,

My best ni kjana (me) age yupo mid 20's ni graduate na ameajiriwa katika mojawapo ya big 4 auditing firm as auditor,

Jamaa anakaa na mama yake as mtoto wa pekee, baba yake alifarik mapema sana baada ya yeye kuzaliwa some years ago so amelelewa na kusomeshwa na mama yake peke yake na hadi leo bado anaish nyumban kwao na mama japokuwa ameanza kazi toka 2010 after university na mama yake hakutaka ahame as atakuwa mpweke na amemzoea sana mwanae, na mama ana maisha ya middle class as nyumba inapendeza na miradi midogo midogo mingi so hela za kubadilisha magari ya kijapan haimpigi chenga,na kwa kipindi kirefu toka tupo first year mama yake anaumwa umwa sana as alipataga ajali na toka hapo kichwa hakipo sawa as alifanyiwa surgery kichwan.. Sasa mama ameanza kelele anataka kucheza harusi ya mtoto wake wa pekee na kuona mjukuu au wajukuu kabla hajafariki na jamaa ajajiandaa kuoa kisaikolojia as he still enjoy bachelors life, b mkubwa amekomaa na maneno yake toka mwaka jana na kila siku anaongea anataka mkamwana na mjukuu but jamaa anashindwa afanyeje?

So ndo katushtua watu wake wa karibu tufanyeje as anadai yeye hayupo tayari na kila mdada anakutana nae anaona hawaendan as ana dream ya kuoa msichana aliye kama mama yake as mchapakaz na smart darasan like her mom as hata yeye bahat mbaya akiondoka dunian watoto wasitetereke kama yeye alivyopata mahitaj yote hata baada ya mzee kufariki, so anashindwa afanyeje na mama anataka acheze harusi mapema as ana imani mwanae anajimudu kwa kipato na hata yeye hatoshindwa kulea wajukuuu kama mwanae akikwama. Na hata asipopata mtoto basi amwone mkamwana kabla hajafa

Wadau mtu kama huyu nimshauri vp?

Sijaelewa Mkata Kiu
Ushauri unaotaka ni upi?
ni:-
  1. Aoe au asioe? kwa maana amsikilize dying mother wake au asimsikilize.
  2. Apataje huyo smart and hard working girl?
  3. Azae au asizae?

1. At 25 anafaa kuoa, na sio mbaya. Kwa hilo ni bora amsikilize mama yake, kwani anamuongoza kwenye yaliyo mema; unless aniambie hafanyi uasherati (sex before ndoa) which is dhambi kwa madhehebu mengi.
2. Atapataje huyo smart girl, aombe sana na Mungu atampa. Mwambie asi-look so hard kwani akifanya hivyo atapata fake. Amwambie mama machaguo yake na amsaidie kusali na kutafuta. Apate marafiki wengi wenye sifa kama hizo, na katika hao ataweza kupick. Aangalie wapi anatafutia, kutokana na choices zake atapata kwenye mazingira hayo hayo.
3. Kuzaa tu sikushauri, mtoto anahitaji uwepo wa wazazi wote wawili; hivyo hakikisha utakaye zaa naye ndio mkeo.

Mwisho nakutakia kila lenye heri!
 
Back
Top Bottom