Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,759
- 699,085
Chawa ni nani?
Hilo ni jina la Kiswahili, kiingereza ni lice na kwa jina la kitaalam ni Phthiraptera
Kiasili chawa ni aina ya wadudu wadogo tambazi wanaopenda kuishi kwenye miili ya binadamu wachafu na baadhi ya wabyama wafugwao wasiotunzwa kwenye mazingira safi
Chakula chake rasmi ni damu anayonyonya toka kwenye mwili wa binadamu au mnyama (hawa wa kufugwa) na akifanikiwa kupenya kwenye vidole vya miguu michafu hujichimbia kwenye ile ngozi laini na kugeuka funza na kutaga mayai humo
Funza ana mzio na watu wasafi! Kamwe hawezi kuweka makazi yake kwa watu safi wanaoishi kwenye mazingira safi.. Pepo yake ni kwenye mwili, mchafu wenye nywele chafu, kucha chafu,nguo chafu, humo hufanya makazi yake na kutaga mayai yake! Hufyonza damu kwa ajili ya chakula, na huwasha ngozi.. Ule muwasho wake ukijikuna upele hufuata.. Huleta na magonjwa mengine pia!
Kwa kifupi chawa si mdudu mwema maana ana hasara nyingi kuliko faida na mtu kufananishwa ama kuitwa chawa kama sio sifa mbaya basi ni dhihaka kubwa ama ni tusi au ni kejeli
Wahenga wana usemi wao kwa kutumia lahaja wanapotaka kumuelezea mtu mbaya.. Usemi huu asili yake ni chawa mwilini... Unasema hivi! Kikulacho ki nguoni mwako!
Nilipomsikia bi mkubwa akisema ana chawa wake niligutuka kwa mshtuko na fadhaa kubwa, maana kila kinachoonekana kwa macho ya nyama kina replica ya kiroho!
Happy new year BELOVED TANGANYIKA