Mama afurahia kifo cha mwanaye aliyeuawa na wananchi wenye hasira kali

Mwanamke Mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ndilikuli Matupa Mkazi wa kijiji cha Mkangaula Kata ya Namalenga wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ameshukuru wananchii wenye hasira Kali kwa Kumchoma Moto Kijana wake Abdallah Hussein Mahona kwa Tuhuma za Kuhusika na matukio Kadhaa ya Ukabaji,Unyang'anyi na Mauaji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 12 asubuh mwanzoni mwa wiki hii ambapo marehemu alihusishwa na kuwajeruhi watu wawili ndipo wananchi wenye hasira wakamtafuta na kumchoma moto mpaka kifo chake.

Akiongea katika eneo la Tukio ambalo Marehem Abdallah Hussein amechomwa mama yake Mzazi Bi Ndilikuli Matupa anasema alilazimika kulala nyumba za stareh {Disco}ili kuepuka kuuawa na Mwanae ambapo mara kadhaa amekuwa akimtishia Kumuua. “Sina Masikitiko yoyoyote Mzazi Mimi,Nimepona kwa chukuchuku kila siku Mwenye disko mtu mkubwa kama Mimi nilikuwa nawaacha wajukuu wangu Mmoja wa Marehem Mmoja wa kaka yake mimi nakwenda kwenye disco ilihali mimi sio mtu wa disco yaan kukimbia Kifo”alisema Bi Ndilikuli Matupa ambaye ni Mama wa marehem.

Hata Hivyo Bi Ndilikuli ameongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa Marehem mwanae Kumtishia kumuua kwa kumtuhumu kuwa ni Mchawi kutokana na Mtoto wa Marehemu Kuumwa kwa kipindi cha Muda Mfupi.

Huyo Mama alipata ujasiri wakuongea hayo maneno kwa wakati huo, ila akija akakaa na kutulia na kufikilia tukio atakuwa anahudhunika na kulia mwenyewe, mzazi mzazi tu tumbo la uzazi likimrudi uchungu ataupata
 
Kbsa mkuu kuna1 yupo hpa mtaani kwetu kwenye makuzi yake alikua mtundu muhuni sana kibaka ukimpiga mama yake anakuja juu kama moto wa nyikani, lkn mambo yamekua tofauti now amekua wa kumrudi uyo mzazi wake tena kwa kichapo hevi, mwizi wa kuvunja maduka pombe na yeye yeye na pombe majirani walishamkamata wakataka kupiga kiberiti, lkn polisi waliwai alipelekwa jela, mama yake amefanya bidii zote amerudi uraiani hivi ninavyo andika hpa j3 hii kampiga tena Mama yake kichapo cha haja mchana kweupe majirani walisimama wote pembeni hkna aliesogea
Inasikitisha sana.

Malezi ya kudekeza hasa kina mama kwa watoto yana athari mbaya kitabia.

Nami nilikuwa na ndugu yangu mtoto wa mama mdogo huko mkoani.
Mtoto najua ni kibaka.

Basi mama mdogo akanipigia simu mdogo wako (kinaka) ana hamu ya kukutembelea huko Dar.
Nikamwambia mama mdongo wangu mbona mdokozi?

Mama mdogo akaniambia alishaacha sasa hivi amekua, ule ulikuwa utoto.

Nami nikampokea mdogo kwa furaha.
Alikaa siku hiyo hiyo moja.
Siku ya pili asubuhi nikaenda kazini , niliporudi ,.....lahaula!

Jamaa kaingia chumbani, kabeba sanduku na nguo, nilikuwa na redio digital kabeba, nilikuwa na baiskeli sports hapo ndo akapata na usafiri kabisaa!
Na akapotea.

Nikamkumbuka mama mdogo na kumchukia sana, alinidangaya!
Bado alikuwa anamtetea kijana wake kibaka.
To cut the story short, kibaka yule alikuja kuwa pickpocket watu kwenye msiba.
Aliugua ki ajabu na kuishia.
 
Sasa mama angeenda kutoa ushahidi gani wa kuweza kumfunga mwanae kifungo cha maisha jela? Maana akijua umemshtaki na Akaja kuachiwa baadaye basi anakuja kukumaliza! Sometimes inabidi ukae kimya!
Mama wa watu alikuwa alitumia busara sana
 
Hata mimi hainiingi akir kabisa unawezaje kufurahia kifo cha mtoto wako alimbebea mimba miez 9 ,mm nimezaa naujua uchungu sidhani kama mama huyu ni mama mzazi kwa mtoto huyo,hata iweje kufurahia kifo ni ngumu sana hizo ni tabia za kichawi
Jaribu kugeuka upande wa pili ,mama alijisikiaje mtoto aliyembeba miezi tisa tumboni akitaka kumuua !
 
Kbsa mkuu kuna1 yupo hpa mtaani kwetu kwenye makuzi yake alikua mtundu muhuni sana kibaka ukimpiga mama yake anakuja juu kama moto wa nyikani, lkn mambo yamekua tofauti now amekua wa kumrudi uyo mzazi wake tena kwa kichapo hevi, mwizi wa kuvunja maduka pombe na yeye yeye na pombe majirani walishamkamata wakataka kupiga kiberiti, lkn polisi waliwai alipelekwa jela, mama yake amefanya bidii zote amerudi uraiani hivi ninavyo andika hpa j3 hii kampiga tena Mama yake kichapo cha haja mchana kweupe majirani walisimama wote pembeni hkna aliesogea
Huyuu me namuwekea Sumuu walahii...
 
Inasikitisha sana.

Malezi ya kudekeza hasa kina mama kwa watoto yana athari mbaya kitabia.

Nami nilikuwa na ndugu yangu mtoto wa mama mdogo huko mkoani.
Mtoto najua ni kibaka.

Basi mama mdogo akanipigia simu mdogo wako (kinaka) ana hamu ya kukutembelea huko Dar.
Nikamwambia mama mdongo wangu mbona mdokozi?

Mama mdogo akaniambia alishaacha sasa hivi amekua, ule ulikuwa utoto.

Nami nikampokea mdogo kwa furaha.
Alikaa siku hiyo hiyo moja.
Siku ya pili asubuhi nikaenda kazini , niliporudi ,.....lahaula!

Jamaa kaingia chumbani, kabeba sanduku na nguo, nilikuwa na redio digital kabeba, nilikuwa na baiskeli sports hapo ndo akapata na usafiri kabisaa!
Na akapotea.

Nikamkumbuka mama mdogo na kumchukia sana, alinidangaya!
Bado alikuwa anamtetea kijana wake kibaka.
To cut the story short, kibaka yule alikuja kuwa pickpocket watu kwenye msiba.
Aliugua ki ajabu na kuishia.
Aisee alishakufa???
 
Hata mimi hainiingi akir kabisa unawezaje kufurahia kifo cha mtoto wako alimbebea mimba miez 9 ,mm nimezaa naujua uchungu sidhani kama mama huyu ni mama mzazi kwa mtoto huyo,hata iweje kufurahia kifo ni ngumu sana hizo ni tabia za kichawi
Haya mambo kuna wakati tunatakiwa kuyahusisha na maisha ya watu wanaotuzunguka na usiyafikirie kwa uzoefu binafsi hususani kama hujawahi kupitia magumu au kushuhudia wanaopitia magumu. Kuna mambo yanaonekana abnormal lakini yanatokea kila uchao mitaani/vijijini mwetu. Pengine ungeshangaa kivingine pia kama mama angeuawa na huyo mtoto wake.Kuna watu wanabeba mimba miezi tisa na kuwauwa watoto wao na wengine kuua mimba.Kwa hiyo mama huyu alikuwa ktk hali ngumu na kwa maisha ya vijijini naamini alikuwa anaona uwepo hai wa mtoto wake ni hatari kwake.
 
Mama naye hajapata sehemu nyingine ya kwenda kujisitiri ila disco?

Hahahaa si ndo hapo, na Masasi penyewe hizo kumbi za disco ziko ngapi? Sana sana pale kwa Adam Viazi, nako disco sio kila siku
 
Haya mambo kuna wakati tunatakiwa kuyahusisha na maisha ya watu wanaotuzunguka na usiyafikirie kwa uzoefu binafsi hususani kama hujawahi kupitia magumu au kushuhudia wanaopitia magumu. Kuna mambo yanaonekana abnormal lakini yanatokea kila uchao mitaani/vijijini mwetu. Pengine ungeshangaa kivingine pia kama mama angeuawa na huyo mtoto wake.Kuna watu wanabeba mimba miezi tisa na kuwauwa watoto wao na wengine kuua mimba.Kwa hiyo mama huyu alikuwa ktk hali ngumu na kwa maisha ya vijijini naamini alikuwa anaona uwepo hai wa mtoto wake ni hatari kwake.
Mmh ok bas ila kijana yaweza kuwa alikuwa ni zaid ya mafia

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom