Mama afurahia kifo cha mwanaye aliyeuawa na wananchi wenye hasira kali

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,096
Hasira.PNG

Mwanamke Mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ndilikuli Matupa Mkazi wa kijiji cha Mkangaula Kata ya Namalenga wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ameshukuru wananchii wenye hasira Kali kwa Kumchoma Moto Kijana wake Abdallah Hussein Mahona kwa Tuhuma za Kuhusika na matukio Kadhaa ya Ukabaji,Unyang'anyi na Mauaji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 12 asubuh mwanzoni mwa wiki hii ambapo marehemu alihusishwa na kuwajeruhi watu wawili ndipo wananchi wenye hasira wakamtafuta na kumchoma moto mpaka kifo chake.

Akiongea katika eneo la Tukio ambalo Marehem Abdallah Hussein amechomwa mama yake Mzazi Bi Ndilikuli Matupa anasema alilazimika kulala nyumba za stareh {Disco}ili kuepuka kuuawa na Mwanae ambapo mara kadhaa amekuwa akimtishia Kumuua. “Sina Masikitiko yoyoyote Mzazi Mimi,Nimepona kwa chukuchuku kila siku Mwenye disko mtu mkubwa kama Mimi nilikuwa nawaacha wajukuu wangu Mmoja wa Marehem Mmoja wa kaka yake mimi nakwenda kwenye disco ilihali mimi sio mtu wa disco yaan kukimbia Kifo”alisema Bi Ndilikuli Matupa ambaye ni Mama wa marehem.

Hata Hivyo Bi Ndilikuli ameongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa Marehem mwanae Kumtishia kumuua kwa kumtuhumu kuwa ni Mchawi kutokana na Mtoto wa Marehemu Kuumwa kwa kipindi cha Muda Mfupi.
 
Kama hii stori haijapindishwa iko sawasawa na kilichokuwa kinatokea, mama yuko sahihi hata mimi namsapoti. I could feel the same at her place
 
Hii Nimeshuhudia kesi kama hii usiku saa tisa, mtoto kaiba kakimbizwa na aliowaibia kimya kimya kafika getini anagonga analia 'wananiuaaa'
Mama akajibu kama mmemfikisha kwangu muacheni kichapo kinamtosha ila kama mnataka kuua kamuueni mbali mtoeni getini kwangu sitaki usumbufu.
Nkasema kweli mama kachoka na hajali tena.
 
Huyu mama anasema alikuwa analala disco bila kupenda kwa kuogopa vitisho vya mwanae....mpaka anafikia hatua hiyo hakuviona vituo vya polisi? Kwa hali Kama hiyo Kama ni kweli polisi wasingemuacha kijana kaka jambazi mtaani...
 
Marehemu hakuwepo eneo la tukio walipojeruhuwa watu wawili, raia wakajadiliana wakasema atakua ni huyu, wakaenda kumchomoa kwake wakamsomea hukumu ya kesi yake na adhabu. Alipopiga kelele akaambiwa maamuzi ya raia hayana rufaa.

Tough on crime society.
 
Kwanini siku zote anatishiwa kifo hakwenda kuripoti kwa usalama wake?
Huyu mama naye siyo mzima hata kidogo! Haiwezekani mzazi kufurahi kifo cha mwanae hata kama alikuwa mbaya vipi. Kwanini hakuchukua hatua za kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama au hata kuhusisha ndugu katika familia? Yaani mtoto wa kumzaa mwenyewe afe kifo kile halafu afurahie?! Huyo hawezi kuwa mama hata siku moja labda ni mama fake!
 
Huyu mama anasema alikuwa analala disco bila kupenda kwa kuogopa vitisho vya mwanae....mpaka anafikia hatua hiyo hakuviona vituo vya polisi? Kwa hali Kama hiyo Kama ni kweli polisi wasingemuacha kijana kaka jambazi mtaani...
Sasa mama angeenda kutoa ushahidi gani wa kuweza kumfunga mwanae kifungo cha maisha jela? Maana akijua umemshtaki na Akaja kuachiwa baadaye basi anakuja kukumaliza! Sometimes inabidi ukae kimya!
 
Back
Top Bottom