Malumbano ya hoja ITV:Siwapendi wapiga debe

Malumbano ya hoja ITV:Siwapendi wapiga debe

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,633
Reaction score
7,021
Nimekuta mjadala uliokuwa ukizungumzia changamoto ya usafiri na abiria hasa nyakati kama hizi za mwisho wa mwaka.
Mojawapo ya hoja ya kutaabika kwa abiria wakipandishiwa nauli hovyo ni kutokana na kuwepo watu wanaoitwa wapiga debe.Nasikitika kutangaza rasmi kuwa nawachukia sana.
Katika mjadala kulikuwa na watu watatu ambao ni mzee Mrutu(Taboa),Mwakilishi wa Sumatra,na mwakilishi wa chama cha kutetea abiria.
Nimemkubali sana mzee mrutu kwa mawazo yake ya kutowataka kabisa hao wapiga debe.Na ameomba serikali isaidie kwa kutoa tamko tu kuwa haiwahitaji hao wapiga debe na hivyo wasiwepo vituo vya mabasi.
Hata hivyo inavyoonesha Sumatra ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa.Hii ni kutokana na msemaji wao leo akikwepa jukumu analoombwa na mwakilishi wa wamiliki kushirikiana kuwang'oa kabisa wapiga debe.Wengi ni matapeli na wasumbufu sana.Mf. juzi wanangu wamekwenda stand pale msanvu majira ya saa 12 asb.,lakini walikatiwa basi la kwenda Dodoma la saa saba mchana huku wakiwa wamedanganywa kuwa basi lipo asubuhi ile.Niliudhika sana ila kwa vile sikuwa karibu nigechukua hatua.
Mwakilishi wa chama cha kutetea abiria alichangia huku akionekana kuwatetea wapiga debe.Huenda kwa vile ofisi yake ipo hapo getini Ubungo,ameshajenga mazoea nao kiasi wala
Nashauri kama serikali inadhamira ya kuondoa usumbufu wanaopata abiria,itoe tamko tu na wizara ya mambo ya ndani ishughulikie
 
Hawahitajiki kabisa wa kokote wapiga debe hata kwenye vyama vya siasa
 
Mimi ndiyo nawachukia wapiga debe sana. Nilishuhudia siku moja kwenye stendi ya Geita. Kwanza ukiwa na gari lazima uliingize stendi. Pili mwenye gari akiishajaza lazima wapewe Tshs.10,000 wakisema ni kazi yao kuleta abiria kwenye gari ndo maana umejaza. Nikawauliza mlinisaidia kununua gari kwa nini niwape Tshs.10,000?. Kwa kweli wapiga debe wapigwe MARUFUKU kwenye vituo vyote vya mabasi nchi nzima. Kwanza wanaleta kero, wizi na hata kazi ya upigaji debe sioni ni kazi ya halali. Wafukuzwe wakalime huko vijijini.
 
Back
Top Bottom