Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

Ccm watu wazima na wakongwe hili linamalizwa mapema... Ila kijana Makonda usituchafulie hali ya hewa. Shame on you.... Mhamasishaji wa nn wewe? Peleka upuuzi wako huko

Ha ha ha kwi kwi magamba wakizidiwa wanaanza kuleta ngojera zao kama simba anae kula nyasi kwa kutingwa na njaa kali baada ya kukosa nyama.Nape na Kinana walipogundua kuwa serekali ya chama chao inaongozwa na mizigo walizunguka nchi nzima wakiitangaza mizigo yao bila ya kujali kuwa CCM ni chama kikongwe ambacho kinaweza kuwaita mizigo yao wakaihoji kwenye vikao vyao.
 
ccm imekufa ! Inalindwa na kiuzi chembamba sana kinachoitwa MADARAKA .
 
safi sana ngoma inogile!! na sasa ni burudani kwa kwenda mbele haya tunasubili sijui nani atafuata na mistari gani.¿
 
Si mda mrefu vitaanza kutokea vifo vya ajabu ajabu maana kuna mamafia ndani ya ccm hatari
 
Mpaka uchaguzi mkuu tutasikia mengi mola atupe uhai
 
CCM lazima ife na kujizika yenyewe kama ifuatavyo:-

Case I

Lazima ife kwa matendo ya mwenyekiti wa chama, katika uongozi wake anagawa madaraka....

-Ameendekeza sana undugu& urafiki, mke, watoto, wajomba, mashangazi, nyumba ndogo nk.

hawana uwezo anawabeba kimadaraka, na hili limejenga chuki kubwa miongoni wa wanaccm wazalendo.

Case II
Lazima ife kwa matendo na mikakati ya hovyo ya viongozi wa CCM

-Uchochezi wa kidini kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii. CCM hunena tena hadharani bila aibu eti

i-CUF ni cha waislam, wakristo wanatengwa-hakika ni Uwongo (baadhi ya viongozi ndani ya ccm hawakubali)

ii-CHADEMA ni cha wakristu, waislam wanatengwa-hakika ni uwongo (baadhi ya viongozi ndani ya ccm hawakubali)

-Uchochezi wa ukabila kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii.

i) ccm kwa propaganda ya kishenzi inawababuwa waziwazi wachaga (ndani ya ccm, wachanga wote + wapare nichukizo)


-Uchochezi wa kikanda kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii.

i- Ni aibu pale UVCCM wanapotamka waziwazi eti kiongozi ajaye hatatoka kanda ya kaskazin??
inamaana waliondani ya ccm na kutoka kaskazin hili ni chukizo kubwa.

Case III
-Matumizi ya vyombo vya dola kukandamiza wanyonge, (badhi ya wanaccm wanaumia kuliwa ndugu zao)

Arusha mauwaji

Iringa mauwaji (Daud Mwangosi)

Morogoro mauwaji ALLY ZONA

Zanzibar mauwaji, wanachama wa CUF

Mbeya,mwanza,Ruvuma, Mara nk kupigwa na kuumizwa watu

Case IV

Viongozi wa CCM kuendekeza utendaji wa kibaguzi (baadhi ya viongozi wa ccm inawaudhi)

i) Bandari kuu mpya kujengwa Bagamoyo, Tanga, Mtwara, Dar watajijuwa na vijibandari vyao.

ii) Gesi kutoka mtwara Bagamoyo, huko ni bandarini sinauhakika kama ndio kuipanua pwani kibiashara na nje

iii) Kila wakati barabara za lami kufumuliwa na kujengwa upya na zingine kuongezwa pwani- kwingine hakuna KITU!

iv) Bei ya petrol nikama ya mafuta ya taa, ni ajabu na kweli, baadhi ya wanaccm wanaumizwa na ujinga huu

Case VI
Ukosefu wa nidham ndani ya ccm, kila mmoja anandevu, baba, mama, watoto na marafiki
 
Wakati tuko busy na operation pamoja daima, majirani wameanza kugombea fito chache zilizobaki.

CCM vipande-vipande
 
Hawa ndio baadhi ya Waanzilishi wa CCJ;


  1. Samuel Sitta (sh 500,000)
  2. Harrison Mwakyembe (sh 300,000)
  3. Anne Kilango (sh 400,000)
  4. James Lembeli (sh 400,000)
  5. Amina Katemi (sh 300,000)
  6. Alex Kisumo (sh 300,000)
  7. Baraka Seif (sh 300,000)
  8. Sospeter Banigwa (sh 300,000)
  9. Saleh Omari (sh 300,000)
  10. Asma Watosha (sh 300,000)
  11. Sarah Patrick (sh 200,000)
  12. Daniel Mwaijojeli (sh 200,000)
  13. Dk. Ngonyani (sh 300,000)
  14. Elisha Eliya (sh 200,000)
  15. Emanuel Magonja (sh 200,000)
  16. Hamad Ferej (sh 200,000)
  17. Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000)
  18. Innocent Makala (sh 200,000)
  19. Jacob Msambya (sh 200,000)
  20. Kipute (sh 200,000)
  21. Joseph Kashindye (sh 200,000)
  22. Kamala Ng’ombe (sh 200,000)
  23. Gumbo (sh 150,000)
  24. Ishelula (sh 150,000)
  25. Nape Nnauye (sh 100,000)
  26. Paul Makonda (sh 100,000)
  27. Hamadi Maduku (sh 100,000)
  28. Flavian Nkya (sh 100,000),
  29. Masudi Kangi (sh 100,000)
  30. Idd Kiriwe (sh 100,000)
  31. Kulwa Lulelema (sh 50,000)
  32. Ally Harun (sh 50,000)
  33. Daniel Malongo (sh 50,000).
 
MALUMBANO ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanayoonekana dhahiri kuchagizwa na makundi ya urais yameendelea kushika kasi ndani ya chama hicho.

Baada ya jana Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda, kumshambulia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwamba anawatumia watu kusema hovyo kupitia vyombo vya habari juu ya kazi na juhudi zinazofanywa na sekretarieti, kada mwingine, Richad Kiabo, jana aliibuka kuanika majina ya waasisi wa chama cha siasa cha CCJ kilichokufa hata kabla ya kupata usajili.

Makonda alidai Lowassa anafadhili mikakati ya kupingana na juhudi za sekretarieti ya chama hicho na alipongeza kazi zinazofanywa na sekretarieti chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana na wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, akijibu mapigo ya Makonda, Kiabo aliyekuwa mwenyekiti wa CCJ kabla ya kurejea CCM, aliyataja majina 37 na michango waliyoitoa kwa ajili ya kufanikisha maandamano ya amani ya chama hicho ya kupinga uonevu wa aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini wakati huo, John Tendwa.

Kiabo ambaye amekoleza malumbano hayo, alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, kuwachukulia hatua wasaliti hao.

Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000), Samuel Sitta (sh 500,000), Anne Kilango (sh 400,000), Nape Nnauye (sh 100,000), Paul Makonda (sh 100,000) na James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.

Wengine ni Amina Katemi (sh 300,000), Alex Kisumo (sh 300,000), Baraka Seif (sh 300,000), Sospeter Banigwa (sh 300,000), Saleh Omari (sh 300,000), Sarah Patrick (sh 200,000), Daniel Mwaijojeli (sh 200,000), Dk. Ngonyani (sh 300,000), Elisha Eliya (sh 200,000), Emanuel Magonja (sh 200,000) na Asma Watosha (sh 300,000).

Pia wamo, Kulwa Lulelema (sh 50,000), Hamadi Maduku (sh 100,000), Flavian Nkya (sh 100,000), Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000), Hamad Ferej (sh 200,000), Ally Harun (sh 50,000), Masudi Kangi (sh 100,000), Gumbo (sh 150,000), Idd Kiriwe (sh 100,000), Innocent Makala (sh 200,000), Jacob Msambya (sh 200,000), Ishelula (sh 150,000), Kipute (sh 200,000), Joseph Kashindye (sh 200,000) Kamala Ng’ombe (sh 200,000) na Daniel Malongo (sh 50,000).

Kiabo alisema anashangaa kuona ndani ya CCM bado kuna wanachama na viongozi waandamizi wenye kadi mbili, yaani kadi ya CCJ na CCM na wameshindwa mpaka sasa kuzirudisha na hata kukana, ikiwemo kuwaomba radhi wanachama kwa kitendo cha usaliti.

“Nawashangaa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu na wasaliti wa chama baadhi yao wameanza harakati za kugombea urais 2015 ili wapewe ridhaa na chama ambacho tayari walikwisha kisaliti, nami nitakishangaa chama wakati ukifika kama kitawakubalia na kuwapitisha kuwa wagombea watu wenye kadi za vyama viwili,” alisema.

Kiabo alisema watu wenye uwezo wa kuwasema viongozi wenzao mara kwa mara na wao wasijisahau kuwa hawana usafi wowote wa kusema na kuwanyoshea vidole wenzao kwa usaliti walioifanyia CCM.

Aidha, alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015 ni vizuri kikaanza kusafisha nyumba yake ili mamluki waumbuke na wasipewe nafasi ya kugombea wakati ukifika.

Kutoka jijini Morogoro, inaripotiwa kuwa UVCCM Mkoa wa Morogoro imemtaka Makonda kumwomba radhi Lowassa kwa kauli za kichochezi zinazoweza kukigawa chama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii jana, wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia kundi la vijana, Jonas Nkya na Ramadhani Kimwaga, walisema kauli ya Makonda ni yake binafsi wala haihusiani na UVCCM.

Nkya alisema vijana wa Mkoa wa Morogoro wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda akimshutumu Lowassa kuwa hafai kuwa kiongozi wa nchi hii, wala kuwa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa CCM taifa.

Nkya alisema kuwa umoja huo hautaki kuingizwa katika masuala binafsi ambayo yanaweza kusababisha na kuchangia kukigawa chama na jumuiya zake.

Mnyukano wa sasa miongoni mwa makada wa CCM umekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kuwarejesha madarakani mawaziri mizigo waliopendekezwa na chama chake watoswe.

Baada ya uteuzi huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alitoa kauli ya kuunga mkono uteuzi huo, lakini akisisitiza chama kitaendelea kuwashughulikia mawaziri mizigo na safari hii wataelekeza mapambano hayo ndani ya Bunge na kwenye mabaraza ya halmashauri.

Kauli hiyo ilimuibua mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ambaye alimtukana Nape kwamba ameteuliwa kimjombamjomba na hawezi kumchagulia rais majina ya uteuzi.

Kauli ya Guninita ikamuibua Makonda na sasa Kiabo, ambao duru za siasa zinasema wote wamepewa hela kwa malengo ya urais mwaka 2015.

- The mburulazzz kama kweli Lowassa anafanyiwa kampeni za urais na watu kama huyu basi ndio maana hatakuwa, what is this? Hili tu ndio tatizo kubwa la Kambi ya Lowassa ni kuamini kwamba wanaweza kutumia ubabe na pesa kuapta urais what is CCJ? Kwani kuanzisha CCJ kama ni kweli ilikuwa a Crime against the State? au ilikuwa a Crime aganist CCM?

- I mean nyie watu wa Lowassa kama kweli mnataka Urais mnatakiwa kuachana na wajinga wajinga kama huyu mtu, so haya ndio majibu ya Ile hotuba ya Makonda? Kweli yale maneno ya Makonda unaweza kuyajibu na foolishness kama hizi?

Le Mutuz
 
- The mburulazzz kama kweli Lowassa anafanyiwa kampeni za urais na watu kama huyu basi ndio maana hatakuwa, what is this? Hili tu ndio tatizo kubwa la Kambi ya Lowassa ni kuamini kwamba wanaweza kutumia ubabe na pesa kuapta urais what is CCJ? Kwani kuanzisha CCJ kama ni kweli ilikuwa a Crime against the State? au ilikuwa a Crime aganist CCM?

- I mean nyie watu wa Lowassa kama kweli mnataka Urais mnatakiwa kuachana na wajinga wajinga kama huyu mtu, so haya ndio majibu ya Ile hotuba ya Makonda? Kweli yale maneno ya Makonda unaweza kuyajibu na foolishness kama hizi?

Le Mutuz
Pasco sema neno moja tu hapa na roho yangu itapona.
 
Last edited by a moderator:
Mama ako wa kambo ni muasisi wa CCJ hata baba ako naye yuko upande wa kina Sitta so familia nzima uelekeo wenu ni ule ule.
 
Pasco sema neno moja tu hapa na roho yangu itapona.
Usisikilize kelele za waganga njaa na muflisi wa kisiasa!, rais wa Tanzania, 2015 ni yule tuu aliyeandikiwa na Mungu na sio anayetajwa na binadamu dhaifu!.

Mungu amepanga kuwadhihirishia Watanzania utukufu wake kwa kulifanya "Jiwe walilolikaa waashi, litafanywa jiwe kuu la pembeni!". Kuna mtu ameisha ambiwa "Wewe ni mwamba!, na juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!"
Kwa wanaodhani hili haliwezekani, nawahakikishia, "Lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu, linawezekana!.
Pasco.
 
Kwa mwendo huu hali itazid kuwa mbaya sana ndan ya chama usiku na mchana
 
Usisikilize kelele za waganga njaa na muflisi wa kisiasa!, rais wa Tanzania, 2015 ni yule tuu aliyeandikiwa na Mungu na sio anayetajwa na binadamu dhaifu!.

Mungu amepanga kuwadhihirishia Watanzania utukufu wake kwa kulifanya "Jiwe walilolikaa waashi, litafanywa jiwe kuu la pembeni!". Kuna mtu ameisha ambiwa "Wewe ni mwamba!, na juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!"
Kwa wanaodhani hili haliwezekani, nawahakikishia, "Lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu, linawezekana!.
Pasco.

Hawa mimi nawajuwa vyema, nchi ilisimama miaka miwili kwa ulaghai wa Sitta na Mwakyembe, finally Obama amekuja kuibariki Richmond na sasa tunawalipa Wamarekani.

Harusi ya Malecela na Anne Kilango Jeetu Patel aliwapa milioni 200 hawa wanafki wazazi wa Le Mutuz, na kinachomuuma huyu hopeless oldman ni Anne Kilango kupigwa chini na Sofia Simba UWT sasa anadhani watanzania ni mazuzu wa kulishwa chuki zao binafsi, tunajitambuwa vizuri sana.

Hii familia ya Malecela ni political losers family.
 
Mzee Philipu Mangula uko wapi mbona kimya? Hebu wakemee hawa wanaojifanya miamba ya kupasho wanakuharibia sifa ya chama chako. Maana katika viongozi wewe ndiye mkongwe.
Mwenyekiti alishasema wanaoutaka uraisi waanze kujipitisha pitisha ... hii ndio style yenyewe ya kujipitisha
 
Back
Top Bottom