Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

Hii bado ni 'trela' ama 'picha' ndio lishaanza

mahindi yangu ya kubanika ninayo tayari, kinachofuata ni kufaidi 'picha'
 
Jamani mbona yeye Kiabo ni yaleyale ya nyani kumcheka mwenzie. Kawataja waliochangia CCJ lakini yeye hakutuambia mchango wake kwenye hicho chama!!!!!
 
Vita vya panzi, furaha ya kunguru. Waendelee kusigana tu huku sisi tukijenga chama! Dhambi ya usaliti waliyotaka kuipandikiza chadema inaanza kuwatafuna wenyewe taratiiiiiiiibu!
Mkuu, hiyo haiandikwi hivyo kama ulivyoandika. Ni Tartiiiibuu
 
Kiyabo ni mke wa mtu,amemwaga mboga,wenzake watamuanika yeye ni mke wa nani,subiri tuone.
 
Hii bado ni 'trela' ama 'picha' ndio lishaanza

mahindi yangu ya kubanika ninayo tayari, kinachofuata ni kufaidi 'picha'

Mi nimeshakunywa kahawa ya kutosha. Halali mtu hapa mpaka hili muvi la komando kipensi liishe. Raha si raha jama??
 
Mi nimeshakunywa kahawa ya kutosha. Halali mtu hapa mpaka hili muvi la komando kipensi liishe. Raha si raha jama??


Nahofia tu lisije kuwa ni 'li muvi' halafu tujipate tukiangalia tamthilia. Itaboaje!
 
Samuel Sitta : 500,000
Anne Kilango : 400,000
James Lembel : 400,000

Hawa jamaa walikuwa na Chuki na Hasira na CCM ndiyo maana wakachangia zaidi

CCM wangewaacha wakaondoka! Kuna siku watajuta kwanini hawakuwaachia,msaliti ni msaliti huwa haachi usaliti!
 
CCM lazima ife na kujizika yenyewe kama ifuatavyo:-

Case I

Lazima ife kwa matendo ya mwenyekiti wa chama, katika uongozi wake anagawa madaraka....

-Ameendekeza sana undugu& urafiki, mke, watoto, wajomba, mashangazi, nyumba ndogo nk.

hawana uwezo anawabeba kimadaraka, na hili limejenga chuki kubwa miongoni wa wanaccm wazalendo.

Case II
Lazima ife kwa matendo na mikakati ya hovyo ya viongozi wa CCM

-Uchochezi wa kidini kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii. CCM hunena tena hadharani bila aibu eti

i-CUF ni cha waislam, wakristo wanatengwa-hakika ni Uwongo (baadhi ya viongozi ndani ya ccm hawakubali)

ii-CHADEMA ni cha wakristu, waislam wanatengwa-hakika ni uwongo (baadhi ya viongozi ndani ya ccm hawakubali)

-Uchochezi wa ukabila kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii.

i) ccm kwa propaganda ya kishenzi inawababuwa waziwazi wachaga (ndani ya ccm, wachanga wote + wapare nichukizo)


-Uchochezi wa kikanda kwa watanzania, sasa wengi wanaifaham mbinu hii ndani ya ccm na hawako radhi tena kuishiriki dhambi hii.

i- Ni aibu pale UVCCM wanapotamka waziwazi eti kiongozi ajaye hatatoka kanda ya kaskazin??
inamaana waliondani ya ccm na kutoka kaskazin hili ni chukizo kubwa.

Case III
-Matumizi ya vyombo vya dola kukandamiza wanyonge, (badhi ya wanaccm wanaumia kuliwa ndugu zao)

Arusha mauwaji

Iringa mauwaji (Daud Mwangosi)

Morogoro mauwaji ALLY ZONA

Zanzibar mauwaji, wanachama wa CUF

Mbeya,mwanza,Ruvuma, Mara nk kupigwa na kuumizwa watu

Case IV

Viongozi wa CCM kuendekeza utendaji wa kibaguzi (baadhi ya viongozi wa ccm inawaudhi)

i) Bandari kuu mpya kujengwa Bagamoyo, Tanga, Mtwara, Dar watajijuwa na vijibandari vyao.

ii) Gesi kutoka mtwara Bagamoyo, huko ni bandarini sinauhakika kama ndio kuipanua pwani kibiashara na nje

iii) Kila wakati barabara za lami kufumuliwa na kujengwa upya na zingine kuongezwa pwani- kwingine hakuna KITU!

iv) Bei ya petrol nikama ya mafuta ya taa, ni ajabu na kweli, baadhi ya wanaccm wanaumizwa na ujinga huu

Case VI
Ukosefu wa nidham ndani ya ccm, kila mmoja anandevu, baba, mama, watoto na marafiki
Aisee, wewe si bure, utakuwa geneous
 
1.jpg


SIKU moja baada ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kutoa tamko la kumtaka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuacha kukigawa chama kwa madai kuwa hana sifa kuwa rais, mambo mazito yamezidi kuibuka huku ikitolewa orodha ya wanachama wa CCM wakiwemo mawaziri, wabunge na makada maarufu wanaodaiwa kukisaliti chama hicho.
Hatua hiyo imeenda sambamba na kumtaka Katibu wa Umoja wa Vijana Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda, kuacha kuwanyooshea vidole wenzao, wakati ndani ya chama hicho kuna wasaliti wakubwa na wasiokuwa na usafi wowote wa kuwasema wenzao.


Hayo yamewekwa hadharani Dar es Salaam jana na aliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, Richard Kiyabo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO).

Kiyabo aliitaka CCM kusafisha wanachama wasio waaminifu ambao ni mamluki wakiwemo mawaziri, wabunge machachari na makada maarufu kutokana na kushiriki kwao kuanzisha Chama Cha Kijamii (CCJ) huku bado hawajarejesha kadi za chama hicho.

Kiyabo alisambaza kwa waandishi wa habari orodha ya wanachama wa CCM 37 anaodai walishiriki kutoa michango ya fedha kwa ajili ya kufanikisha maandamano ya amani ya CCJ yaliyolenga kupinga uonevu wa msajili wa vyama vya siasa nchini.

Alisema tayari ameshamwandikia barua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula kukiomba chama kichukue hatua za kinidhamu na kimaadili kwa wanachama ambao si waaminifu na tayari walikwishapoteza sifa za kuwa wanachama, kutokana na kushirikiana nao kuanzisha CCJ, huku wakiwa wanachama wa CCM.

"Kitendo cha kuwa wanachama wa vyama viwili kwa wakati mmoja ni kosa kubwa na ni usaliti ndani ya chama, kosa hili halipishani na kosa la uhaini ndani ya chama, lakini kwa masikitiko yangu makubwa watu hawa hadi sasa hawajaitwa na vikao vya chama wala hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa au kujadiliwa kwa makosa ya kukisaliti chama na kuamua kuwa mamluki ndani ya chama," alisema Kiyabo.

Alisema mwanzoni mwa mwaka 2010 walipokubaliana kuanzisha CCJ malengo makuu ilikuwa chama hicho kushiriki uchaguzi mkuu na kusimamisha mgombea wa kiti cha urais na wabunge, pamoja na madiwani kama wangekidhi matakwa ya kisheria.

"Nashangaa ndani ya CCM bado kuna wanachama na viongozi waandamizi wana kadi mbili za CCJ na CCM na wanashindwa kuzirudisha na hata kukana, ikiwemo kuwaomba radhi wanachama kwa kitendo cha usaliti," alisema na kuongeza kuwa anawashangaa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu ndani ya chama.

Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000), Samuel Sitta (sh 500,000), Anne Kilango (sh 400,000), Nape Nnauye (sh 100,000), Paul Makonda (sh 100,000) na James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.

Wengine ni Amina Katemi (sh 300,000), Alex Kisumo (sh 300,000), Baraka Seif (sh 300,000), Sospeter Banigwa (sh 300,000), Saleh Omari (sh 300,000), Sarah Patrick (sh 200,000), Daniel Mwaijojeli (sh 200,000), Dk. Ngonyani (sh 300,000), Elisha Eliya (sh 200,000), Emanuel Magonja (sh 200,000) na Asma Watosha (sh 300,000).
Pia wamo, Kulwa Lulelema (sh 50,000), Hamadi Maduku (sh 100,000), Flavian Nkya (sh 100,000), Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000), Hamad Ferej (sh 200,000), Ally Harun (sh 50,000), Masudi Kangi (sh 100,000), Gumbo (sh 150,000), Idd Kiriwe (sh 100,000), Innocent Makala (sh 200,000), Jacob Msambya (sh 200,000), Ishelula (sh 150,000), Kipute (sh 200,000), Joseph Kashindye (sh 200,000) Kamala Ng'ombe (sh 200,000) na Daniel Malongo (sh 50,000).
Alisema ni vyema wakati huu kuelekea uchaguzi CCM ianze kujisafisha ili wale mamluki waumbuke na wasipewe nafasi ya kugombea wakati ukifika
Makonda alipoulizwa kuhusiana na madai hayo alijibu kuwa anaelewa kuwa mchezo huo unachezwa na vibaraka kwani suala hilo halina uzito ndani ya chama.

Alidai kuwa suala la kuondoa watu wanaotumiwa na Lowassa kukihujumu chama hicho halijibiwi. Alisema ni muhimu kuelewa kuwa wapambe wote wa Lowassa watatoka na watakapomalizika atashughulikiwa yeye kichama kwani ndiye tatizo.

"Wapambe wote watoke na watakapoisha tutashughulika na bosi wao anayewatuma... ninajua hawajajipanga ndiyo maana wamekurupuka na kuja na hoja rahisi," alisema.

Alisema wanamtaka Lowassa akanushe kuwatumia hao watu. Kwa Nape, alisema yalishajadiliwa na mjadala kufungwa ndani ya chama, hivyo madai hayo si mapya hawezi kuyazungumzia.


source : http://masamaentertainment.blogspot.com/2014/01/balaa-muasisi-wa-ccj-ataja-majina-ya.html?spref=fbmapya hawezi kuyazungumzia.
 
haya sasa kumekucha mapka 2015 ikifika ccm mtakuwa mmekwisha nyakanyaka, picha ndo kwanza inaanza
 
Lowassa yuko imara,
Lakini pia ccm iko imara zaidi.

2015 Ikulu bado ni ya ccm no matter what....
 
Mwisho wa CCM umefika. Mungu ibariki CDM Mungu ibariki Tanzania
 
orodha ya wanachama wa CCM wakiwemo mawaziri, wabunge na makada maarufu wanaodaiwa kukisaliti chama hicho.
Hayo yamewekwa hadharani Dar es Salaam jana na aliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, Richard Kiyabo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO).
Kiyabo alisambaza kwa waandishi wa habari orodha ya wanachama wa CCM 37 anaodai walishiriki kutoa michango ya fedha kwa ajili ya kufanikisha maandamano ya amani ya CCJ yaliyolenga kupinga uonevu wa msajili wa vyama vya siasa nchini.


Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000),
Samuel Sitta (sh 500,000),
Anne Kilango (sh 400,000),
Nape Nnauye (sh 100,000),
Paul Makonda (sh 100,000) na
James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.


Wengine ni
Amina Katemi (sh 300,000),
Alex Kisumo (sh 300,000),
Baraka Seif (sh 300,000),
Sospeter Banigwa (sh 300,000),
Saleh Omari (sh 300,000),
Sarah Patrick (sh 200,000),
Daniel Mwaijojeli (sh 200,000),
Dk. Ngonyani (sh 300,000),
Elisha Eliya (sh 200,000),
Emanuel Magonja (sh 200,000) na
Asma Watosha (sh 300,000).

Pia wamo,
Kulwa Lulelema (sh 50,000),
Hamadi Maduku (sh 100,000),
Flavian Nkya (sh 100,000),
Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000),
Hamad Ferej (sh 200,000),
Ally Harun (sh 50,000),
Masudi Kangi (sh 100,000),
Gumbo (sh 150,000),
Idd Kiriwe (sh 100,000),
Innocent Makala (sh 200,000),
Jacob Msambya (sh 200,000),
Ishelula (sh 150,000),
Kipute (sh 200,000),
Joseph Kashindye (sh 200,000)
Kamala Ng'ombe (sh 200,000) na
Daniel Malongo (sh 50,000).


NAPE ANA KADI MBILI?
 
Kuchangia CCJ ni kwenda na kinyume cha KATIBA YA CHAMA?
 
Back
Top Bottom