Malisa GJ: Rais Samia anawakaanga MATAGA

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,799
18,218
Dig Deeper-Hotuba ya Mama

Na Malisa GJ

Kimsingi mama anaisuka Tanzania mpya, lakini hataki sindano iwaume sana wale chawa wa mwendazake, hivyo anachoma halafu anawapuliza kwa kuwaambia kuwa yeye na mwendazake ni kitu kimoja.

Wakishangilia anaongeza sindano nyingine. Wakishtuka anapuliza tena anawaambia mwendo ni uleule alioacha mwendazake. Wanabwatuka tena kushangilia, anaongeza sindano nyingine. Yani mama ana akili sana.

#Mosi; Ameahidi kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kufungua balozi mpya kwenye nchi mbalimbali. Uhusiano wetu kimataifa uliingia doa kwa miaka 6 ya mwendazake. Tulifeli ktk diplomasia. Yeyote aliyekua na mawazo tofauti na sisi tulimuita beberu. Hatukutaka kuchangamana na dunia hata vikao vikubwa kama WEF au UN hatukutaka kushiriki. Tulikosa exposure nyingi ambazo zingetusaidia kupiga hatua.

Mama kasema uhusiano utaimarishwa. Hakuna tena "blahblah" za mabeberu. Tutashirikiana na mataifa mengine kwa maslahi mapana ya Tanzania yetu. Dunia inasogea sisi hatuwezi kubaki nyuma. Kwa hiyo lazima tushirikiane na dunia lakini kwa kulinda maslahi yetu, bila kukubali masharti yatakayoharibu utu wetu. Yeyote anayetaka kushirikiana na sisi aheshimu misingi yetu ya utaifa.

Hiki ni kitu ambacho tumeshauri kwa muda mrefu lakini mwendazake hakutaka kabisa kushauriwa. Leo mama amefanya yaleyale ambayo tulishauri, lakini ili kuwapooza "chawa" akasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja. Wakashangilia.

#Pili; Mama ameahidi kuukuza demokrasia na utawala wa sheria. Na katika kuonesha anamaanisha AMEOMBA WATANZANIA WAIKOSOE SERIKALI. Hili ni jambo kubwa sana. Yani Rais wa nchi anawaomba wananchi mkosoe serikali. Haijawahi kutokea. Mama kaweka rekodi. Mwendazake hajawahi kukubali kukosolewa, achilia mbali kuomba wananchi wamkosoe. Hiyo kwake ilikua "future imposible tense".

Ukosoaji ulikua ni dhambi kubwa hata kama unakosoa kwa nia njema. Muulize mdogo wangu Kumbusho Dawson alipokosoa ujenzi wa mabweni baada ya kupata nyufa nini kilimtokea? Kuna watu wamefungwa wengine wamepigwa, na kufanyiwa vitendo vya kikatili kwa sababu tu ya kukosoa serikali.

Leo Mama kasema kukosoa ruksa. Hii ni ishara kwamba anapenda mawazo mbadala. Kwahiyo wakosoaji tumepewa ruksa ya kujiachia ili mradi tusivunje sheria za nchi. Tukosoe kwa misingi ya kujenga (constructive critisism). Hii ni sindano kali kwa chawa lakini ili kuwapooza akawaambia mimi na mwendazake ni kitu kimoja. Wakashangilia.

#Tatu; Mama kaonesha nia ya maridhiano kwa kukubali ombi la viongozi wa upinzani kukutana nae. Amesema atakutana nao muda mfupi kuanzia sasa. Hii ni habari njema maana nchi hii ni yetu sote na inahitaji mawazo ya kila upande ili kupiga hatua. Wakati wa mwendazake kuna watu walijimilikisha nchi. Wakajiona wao ni wenye nchi na wengine ni wapangaji. Wakaamini wao ndio wenye haki ya kutoa maoni, na si mtu mwingine yeyote.

Sasa Mama kasema atakutana na viongozi wa upinzani kwa ajili ya maridhiano, ili tusonge mbele tukiwa wqmoja. Nachowashauri kwenye meza ya maridhiano wasisahau Katiba mpya. Mchakato uendelee pale kwenye rasimu ya Warioba. Akifanya hivyo ataacha legacy kubwa sana kwa taifa hili. Katiba mpya pia itatupa Tume huru ya uchaguzi na mengine mengi kwa maslahi ya taifa letu.

Mwendazake hakutaka maridhiano kabisa na hata viongozi wa upinzani walipomuomba kukutana nae aliwapuuza. Chawa wakatukana upinzani eti mlizoea kuitwa Ikulu kwenda kunywa juice wakati wa JK lakini JPM hana muda huo, yuko busy kujenga SGR. Sasa mama kasema SGR itajengwa na Ikulu tutaitwa. Na safari hii hatutakunywa juice tu, hadi futari tutakula. Na tukitoka tutawaambia mama na mwendazake ni kitu kimoja ili mpige nduru 🤣.

#Nne; Mama amevihakikishia vyombo vya habari uhuru wao. Mambo ya waandishi kukamatwa, kupigwa, kutekwa, yamefika mwisho. Vyombo vipo huru kuandika na kuripoti habari yoyote yenye maslahi kwa taifa ili mradi vinafuata sheria za nchi. Mwendazake alizika kabisa uhuru wa vyombo vya habari, tangu alipowaambia "hamna freedom to that extent". Mama kafungua huo mnyororo rasmi kuanzia leo.

#Tano; Mama ameahidi kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, kwa kupandisha vyeo na mishahara. Huu ni mfupa uliomshinda mwendazake. Kwa zaidi ya miaka 6 watumishi hawakupandishwa madaraja wala kuongezewa mshahara. Kila walipolalamika walijibiwa kwa kejeli kama hawataki kazi waache.

RC mmoja akasema eti angewachapa viboko. Unamchapaje viboko mtu anayedai haki yake ya kisheria? Nyongeza ya mshahara sio huruma ya kiongozi ni matakwa ya kisheria. Lakini watumishi wamedhulumiwa haki hiyo kwa miaka 6 bila huruma. Sasa mama amesema imetosha. Ameamua kuwafuta machozi.

Sambamba na hilo mama pia ameahidi ajira mpya. Katika ajira hizo walimu ni 6,000. Hapa ningependa nimshauri kidogo. Kwanini serikali inataka kuajiri walimu 6,000 wakati mahitaji ni 40,000? Idadi ya walimu waliohitimu tangu mwaka 2015 hadi sasa ni 45,000, deficit ya walimu ni 40,000. Sasa kwanini ajira 6,000? Si waajiriwe tu wote?

#Sita; Kuhusu uwezeshaji kwa vijana mama amesisitiza halmashauri ziendelee kutenga 10% ya bajeti yake kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wenye ulemavu. Hapa ningemshauri aunde timu ya ufuatiliaji. Je halmashauri ngapi hufanya hivyo? Na je hufanya kwa kiwango kinachotakiwa? Kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2019/20 halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilipitisha bajeti ya Bilioni 48, ambapo Bilioni 4.8 zilipaswa kutengwa kwa ajili ya vijana. Lakini kiasi kilichotengwa kwa ajili ya vijana hakifiki hata 500M. Kuna haja ya ufuatiliaji.

#Saba; Kuhusu ATCL mama amekubali kuwa shirika linajiendeaha kwa hasara, sawa na ripoti ya CAG inavyosema. Hii ina maana zile story za mwendazake kwamba ATCL inapata faida hadi inatoa gawio serikalini zilikua drama tu. Mama ameahidi kuliwezesha shirika kwa kuliongezea mtaji, na kulifutia baadhi ya madeni ili lijiendeshe kwa tija.

Hii ndio sifa ya kiongozi bora. Unakubali penye mapungufu na unaweka mipango ya kusolve mapungufu hayo. Sio unatupiga sound kwamba shirika linatoa gawio wakati lipo hoi bin taaban.

#Nane; Mama amezungumzia kifo cha Magufuli. Amesisitiza tena kwamba kilitokana na tatizo la moyo na si vinginevyo. Amesema kuna watu wanaotoa taarifa za uchonganishi mitandaoni kuhusu kifo cha Magufuli. Amewataka watu hao waache mara moja uchonganishi huo.

Wengi tumesikia wachonganishi hao ambao wamejirekodi sauti na kusambaza kwenye mitandao wakitunga "hadithi" kuhusu hicho. Bila shaka watu hao ni wale waliomtumaini JPM kwa moyo na akili zao zote na kudhani hawezi kufa. Wakasahau kwamba nae ni mwanadamu kama sisi.

Watu hao kwa sasa wapo kwenye "denial" na ndio wanahaha kutunga story za kuchonganisha viongozi. Mama amewaomba muache. Kumbukeni ombi la mama ni amri. Sasa kama hamtaki kusikia msije kujilaumu. Achaneni na hizo drama. Ukurasa wa JPM umeshafungwa na sasa ni zamu ya Samia. Tumpe nafasi!
 
Rais Samia mara zote anasema anaendeleza yale yaliyofanywa na Hayati Magufuli na katika kukazia hilo akasisistiza kwa kusema kwa Yeye na JPM ni wamoja. Kama ndivyo huyu kijana wa mwenyekiti asiyepingwa anapata wapi ujasiri wa kusema hayakuwepo enzi za Magufuli? Nilichogundua ni kwamba Magufuli alikuwa hapendi siasa za choko choko mchokonoe akikugusa kakuonea akikuacha kakuogopa
 
naamini ukosoaji ukizidi kuliko uwezo wa kujirekebisha na kuficha makosa ya kukosolewa.

Watu watabinywa tu kwa kuchoma sindano na kupuliza kama awamu za nyuma kabla ya Baba lao.

Hakunaga nchi kila mtu anabwabwaja tu alafu anaangaliwa. Tofauti ni jinsi anavyonyamazishwa tu. Hata snowden na assange walishughulikiwa na baba la demo
 
Mwendazake hakutaka maridhiano kabisa na hata viongozi wa upinzani walipomuomba kukutana nae aliwapuuza. Chawa wakatukana upinzani eti mlizoea kuitwa Ikulu kwenda kunywa juice wakati wa JK lakini JPM hana muda huo, yuko busy kujenga SGR. Sasa mama kasema SGR itajengwa na Ikulu tutaitwa. Na safari hii hatutakunywa juice tu, hadi futari tutakula. Na tukitoka tutawaambia mama na mwendazake ni kitu kimoja ili mpige nduru 🤣.
Hii ndio para iliyochekesha :cool: :cool:
 
jamani nisa

Watu hao kwa sasa wapo kwenye "denial" na ndio wanahaha kutunga story za kuchonganisha viongozi. Mama amewaomba muache. Kumbukeni ombi la mama ni amri. Sasa kama hamtaki kusikia msije kujilaumu. Achaneni na hizo drama. Ukurasa wa JPM umeshafungwa na sasa ni zamu ya Samia. Tumpe nafasi.!
jamani nisaidieni nakusudia kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani, na na neno nitakutana nao yote ni sawa?.pia kuhusu ukosoaji aliosema Mama kama sikosei katoa angalizo kuwa msivunje sheria nadhani maneno haya yanafanana na yale aliyosema JPM hakuna democrasia isiyo na mipaka.hebu mnisaidieni.
 
Malisa amemaliza kila kitu! Ushamba na ujinga ni Tatizo sana Kwa mataga
 
Ivi unajua mmeazima wangapi toka CDM, mawaziri na sasa Covid 19. Halafu unasemà hakuna rasilimali watu!
Ni wenyewe walikimbia na kwenda kwingine (mimi sio mwachama wa upande huo, ni shabiki tu kama nilivyokuwa upande ule enzi za Dr. W.Slaa)
 
Mwendazake hakutaka maridhiano kabisa na hata viongozi wa upinzani walipomuomba kukutana nae aliwapuuza. Chawa wakatukana upinzani eti mlizoea kuitwa Ikulu kwenda kunywa juice wakati wa JK lakini JPM hana muda huo, yuko busy kujenga SGR. Sasa mama kasema SGR itajengwa na Ikulu tutaitwa. Na safari hii hatutakunywa juice tu, hadi futari tutakula. Na tukitoka tutawaambia mama na mwendazake ni kitu kimoja ili mpige nduru .

#Nne; Mama amevihakikishia vyombo vya habari uhuru wao. Mambo ya waandishi kukamatwa, kupigwa, kutekwa, yamefika mwisho. Vyombo vipo huru kuandika na kuripoti habari yoyote yenye maslahi kwa taifa ili mradi vinafuata sheria za nchi. Mwendazake alizika kabisa uhuru wa vyombo vya habari, tangu alipowaambia "hamna freedom to that extent". Mama kafungua huo mnyororo rasmi kuanzia leo.

#Tano; Mama ameahidi kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, kwa kupandisha vyeo na mishahara. Huu ni mfupa uliomshinda mwendazake. Kwa zaidi ya miaka 6 watumishi hawakupandishwa madaraja wala kuongezewa mshahara. Kila walipolalamika walijibiwa kwa kejeli kama hawataki kazi waache.

RC mmoja akasema eti angewachapa viboko. Unamchapaje viboko mtu anayedai haki yake ya kisheria? Nyongeza ya mshahara sio huruma ya kiongozi ni matakwa ya kisheria. Lakini watumishi wamedhulumiwa haki hiyo kwa miaka 6 bila huruma. Sasa mama amesema imetosha. Ameamua kuwafuta machozi.

Sambamba na hilo mama pia ameahidi ajira mpya. Katika ajira hizo walimu ni 6,000. Hapa ningependa nimshauri kidogo. Kwanini serikali inataka kuajiri walimu 6,000 wakati mahitaji ni 40,000? Idadi ya walimu waliohitimu tangu mwaka 2015 hadi sasa ni 45,000, deficit ya walimu ni 40,000. Sasa kwanini ajira 6,000? Si waajiriwe tu wote?

#Sita; Kuhusu uwezeshaji kwa vijana mama amesisitiza halmashauri ziendelee kutenga 10% ya bajeti yake kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wenye ulemavu. Hapa ningemshauri aunde timu ya ufuatiliaji. Je halmashauri ngapi hufanya hivyo? Na je hufanya kwa kiwango kinachotakiwa? Kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2019/20 halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilipitisha bajeti ya Bilioni 48, ambapo Bilioni 4.8 zilipaswa kutengwa kwa ajili ya vijana. Lakini kiasi kilichotengwa kwa ajili ya vijana hakifiki hata 500M. Kuna haja ya ufuatiliaji.

#Saba; Kuhusu ATCL mama amekubali kuwa shirika linajiendeaha kwa hasara, sawa na ripoti ya CAG inavyosema. Hii ina maana zile story za mwendazake kwamba ATCL inapata faida hadi inatoa gawio serikalini zilikua drama tu. Mama ameahidi kuliwezesha shirika kwa kuliongezea mtaji, na kulifutia baadhi ya madeni ili lijiendeshe kwa tija.

Hii ndio sifa ya kiongozi bora. Unakubali penye mapungufu na unaweka mipango ya kusolve mapungufu hayo. Sio unatupiga sound kwamba shirika linatoa gawio wakati lipo hoi bin taaban.

#Nane; Mama amezungumzia kifo cha Magufuli. Amesisitiza tena kwamba kilitokana na tatizo la moyo na si vinginevyo. Amesema kuna watu wanaotoa taarifa za uchonganishi mitandaoni kuhusu kifo cha Magufuli. Amewataka watu hao waache mara moja uchonganishi huo.

Wengi tumesikia wachonganishi hao ambao wamejirekodi sauti na kusambaza kwenye mitandao wakitunga "hadithi" kuhusu hicho. Bila shaka watu hao ni wale waliomtumaini JPM kwa moyo na akili zao zote na kudhani hawezi kufa. Wakasahau kwamba nae ni mwanadamu kama sisi.

Watu hao kwa sasa wapo kwenye "denial" na ndio wanahaha kutunga story za kuchonganisha viongozi. Mama amewaomba muache. Kumbukeni ombi la mama ni amri. Sasa kama hamtaki kusikia msije kujilaumu. Achaneni na hizo drama. Ukurasa wa JPM umeshafungwa na sasa ni zamu ya Samia. Tumpe nafasi!

Kwani hao mataga ni chama gani?
Na huyo Malisa ana matumaini na nani kutoka chama gani? Hivi chadema wanategemea Samia hataacha kulinda maslai ya CCM na ya kwake?
 
Rais Samia mara zote anasema anaendeleza yale yaliyofanywa na Hayati Magufuli na katika kukazia hilo akasisistiza kwa kusema kwa Yeye na JPM ni wamoja. Kama ndivyo huyu kijana wa mwenyekiti asiyepingwa anapata wapi ujasiri wa kusema hayakuwepo enzi za Magufuli? Nilichogundua ni kwamba Magufuli alikuwa hapendi siasa za choko choko mchokonoe akikugusa kakuonea akikuacha kakuogopa
Mataga naona sindano zinawaingia
 
Back
Top Bottom