Malisa GJ: Kuhusu muswada wa Novatus Igosha

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,041
Juzi nikiwa Dodoma nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni afisa mwandamizi serikalini. Akanionesha muswada uitwao FINEST VALOR.

Kwanza nikataka kumjua mwandishi. Nikaona ni Novatus Igosha. Japo hatujawahi kuonana lakini nafahamu umahiri wake katika masuala ya diplomasia na siasa za kimataifa. Ni moja ya vijana waliobarikiwa ubongo wenye uwezo mkubwa.

Nikapitia Dibaji nikakuta imeandikwa na mzee Pius Msekwa. Nikapitia sura kadhaa kujua maudhui, nikaona amefanya narrative analysis ya utawala wa Magufuli kwa miaka mitano iliyopita na dira yake kwa miaka mitano ijayo. Amechambua strength, challenges na opportunities na kushauri mambo kitaalamu na kwa weledi.

Amemtafsiri Rais Magufuli kama VALOR yani mtu jasiri asiyeogopa vitisho hata katikati ya hatari. Amejaribu kuonesha Magufuli alivyochukua hatua katika mambo ambayo alitarajiwa angesita kuchukua hatua.

Amechambua kuhusu diplomasia ya kimataifa akifanya historical reflection tangu enzi za Mwalimu. Ametoa ushauri wa kitaalamu wa mambo ya kufanya kuimarisha diplomasia yetu.

Kwa kifupi ni moja ya reflective analysis bora kabisa. Akifanikiwa kuchapa muswada huu kuwa kitabu basi atakua ameipa serikali "road map" ya kule wanakotaka kwenda.

Lakini nikasikia wapo watu ndani ya serikali wamezuia muswada huu kuchapwa. Nikauliza hofu inatoka wapi mbona hakuna baya? Mbona haujaandikwa na mpinzani? Mbona kachanbua kwa kuonesha changamoto na suluhisho?

Nikaambiwa kuna watu wanahofia muswada huu ukiwa kitabu kitasomwa sana kwa sababu kimetoa majawabu ya mambo mengi. Hivyo watakua wamevuliwa nguo, maana wataulizwa kwanini mambo hayo hawakuyaona wao hadi yaonekane na kijana mdogo asiye na wadhifa wowote serikalini? Hiyo ndio vita?

Nikaambiwa aliwahi kuwekwa "mahabusu" na Naibu Katibu wa wizara kwa sababu ya muswada huu. Yapo madai kuwa wanataka kumuibia muswada huu wauchapishe kwa jina la wizara. Hivyo kufanikiwa kuzika juhudi zake. Nilimhoji @novatusigosha nikasikitika sana.

Kwa nchi zilizoendelea angepaswa kutumika vizuri kwa maslahi ya taifa. Thadei Ole Mushi huwa anasema akili kubwa zote ni mali ya Rais. Lakini huku kwetu ni vice versa. Yericko Y. Nyerere aliwahi kusema ukiwa akili kubwa Afrika sio sehemu salama kwako. It's either uipumzishe ili uishi vizuri, au uitumie uishi kwa mashaka.!
 
Mbona hajatuambia ameandika nini kuhusu hivyo vitu?

Mbona sijaelewa Malisa kusifia kusifiwa kwa Magufuli? Na anashadadia kabisa kitabu kitolewe?
 
Ameandika kwa mukhtasari kuhusu huo muswaada husika. Sasa angeandika yote yaliyomo si angekuwa anaweka hadharani kila kitu ambacho kwa sasa kimezuia kuchapishwa?

Na hata huu mukhtasari aliouandika kwa maoni yangu unaweza kumuweka hatarini Novatus na pia hata kufukuzwa kazi.
Mbona hajatuambia ameandika nini kuhusu hivyo vitu?

Mbona sijaelewa Malisa kusifia kusifiwa kwa Magufuli? Na anashadadia kabisa kitabu kitolewe?
 
He is right
Hii ni afya kufikiri.

Maana ametuchanganya kitabu cha kumsifia Magufuli kuwa ni jasiri halafu Malisa anapiga kelele kitoke?

Inafikirisha.
Melissa hapingi maandishi ya watu kama unavyojiaminisha. Mtu yeyote mwelevu hawezi pinga mawazo mazur ya mtu hujasema na kujua mazuri na mabaya yaliyopo. Fumbua macho
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
😂😂😂😂😂 sasa unadhani kama kinamsifia tu huyo anayejiita mwendawazimu kwanini kinaleta utata?
He is right
Hii ni afya kufikiri.

Maana ametuchanganya kitabu cha kumsifia Magufuli kuwa ni jasiri halafu Malisa anapiga kelele kitoke?

Inafikirisha.
 
Nyazifa nyingi zimekaliwa na wasaka tonge ,wasio na dira yeyote endelevu na yenye tija wanachokijua ni kucopy na kupest,wanawaza maslahi yao tu na posho za vikao vya majungu ,wao ni kujadili na kulinda nafasi tu hakuna negative thought
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hongera Novatus sio kitu rahisi kufanya publication yeyote na ikapata Kusifiwa na watu wa kudurusu.
Hongera sana Mallisa GJ kwa kuchambua na kudurusu kwa faida ya wengi ambao hatuja pata bahati kukisoma. Hongereni.

Naongeza heshima yangu kwa Mallisa hasa kutambua strength ya mpinzani wako, sio kitu rahisi na hii imeniashiria kuwa unatambua kuwa kuna macho, miguu, mikono miwili miwili na hata pua ina matundu mawili. Na muono wa kila tukio au uendeshaji wa Taifa haukosi mazuri na mapungufu.

Mapungufu ndio ungeyaweka tukaya soma na kuyaelewa, kwa sababu mazuri kama yapo tayari tumekwisha kuyaona.

TUNAKISUBIRI KITABU KITUONGEZEE UFAHAMU NA UELEWA WA MKULU NA UTAWALA HUU.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom