Malinzi ahofia Karume kupigwa Mnada

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (pichani kushoto) amesema kwamba ana wasiwasi Uwanja wa Karume, unaweza kupigwa mnada na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hiyo inafuatia TRA kukamata magari matano ya TFF kutokana na deni la kodi Sh. Bilioni 1 Milioni 118 ambazo ni malimbikizo tangu mwaka 2010, wakati TFF ikiwa chini ya Rais Leodegar Tenga.

“Kwa kweli hali mbaya, na sitashangaa hata kesho Uwanja wa Karume nao ukipigwa mnada, kwa sababu magari waliyokamata thamani yake haifiki deni wanalodai,”amesema Malinzi leo Dar es Salaam.

Ofisa wa TRA, Richard Kayombo amesema wamekamata magari hayo ili kuwapa shinikizo TFF waweze kulipa madeni hayo.

Amesema deni hilo la Sh. Bilioni 1 na Milioni 118 ni malimbikizo ya kodi mbalimbali kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, zikiwemo za VAT na mishahara
ya wafanyakazi wake.

“Ikumbukwe awali tulikamata akaunti zao kwa sababu deni lilifikia Bilioni 1. 6 na baada ya kupunguza deni tukawaachia akaunti zao, lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano,”amesema Kayombo.

Ofisa huyo wa TRA amesema magari yote yaliyokamatwa, likiwemo basi la wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars yapo kwenye kampuni minada ya Yono.
 
Kwani wanasubiri nini kukamata yeye Malinzi na kumpiga mnada? Huyo ndo wangeanza nae, apigwe bei maisha yakwende, tumechoka na kulialia kwake!
 
TFF nalo ni jipu ambalo linatakiwa litumbuliwe.
Nnashauri maafisa na wachunguzi wa CAG na ikiwezekana na TAKUKURU wahamie hapo hapo kukagua na kuchunguza kila aina ya matumizi na mapato.
 
Rais wa Simba changamkia deal hilo tununue karume Simba ikiupata huyo uwanja itakuwa safi sana vyura fc magufuli ana mpango wa kubomoa Bondeni huko
 
Rais wa Simba changamkia deal hilo tununue karume Simba ikiupata huyo uwanja itakuwa safi sana vyura fc magufuli ana mpango wa kubomoa Bondeni huko
Simba hamna hela...hadi mlipwe hiyo ya Okwi tutakuwa tushamaliza malipo yote na tutasubiri makanidhiano siku tukiwa tunakabidhia kombe la klabu bongwa africa....chezea Yanga wewe
 
Hahahaha basi la Taifa stars ? Usikute ile ndege ya raisi nayo inadaiwa kodi ,hebu TRA wafanye kuifuatilia .....
 
FIFA walitoa Bilioni Moja na nusu kwa Tanzania kwa ushirii wake kwenye mashindano ya kombe la dunia...hatua ya mtoano.....Hizo pesa zimefanya nini?

TFF inachangiwa na wanachama .hzo pesa zinafanya nini?

TFF inachukua mapato ya mlangoni...hizo pesa zinafanya nini?

TFF inanufaika na mkataba wa Vodacom...hizo pesa zinafanya nini?
 
FIFA walitoa Bilioni Moja na nusu kwa Tanzania kwa ushirii wake kwenye mashindano ya kombe la dunia...hatua ya mtoano.....Hizo pesa zimefanya nini?

TFF inachangiwa na wanachama .hzo pesa zinafanya nini?

TFF inachukua mapato ya mlangoni...hizo pesa zinafanya nini?

TFF inanufaika na mkataba wa Vodacom...hizo pesa zinafanya nini?
Watu wanajengea Magholofa na kununulia mashangingi ya kutembelea hapo Mjini.
 
Kipindi anagombea alipambana sana kupata hiyo nafasi. Lakini kuna watu walizungumza hii "pichu!" ya TFF ni kubwa mno kwa Malinzi, yeye akang'ang'ania! "Ooooooh ntaifunga na pini itanitosha!" sasa pini imefunguka kazi kwake! Sijui sasa hivi atatumia "stepler pin!":D:D
 
...msimkaange sana Malinzi,kama na yeye alikuta TFF wanadaiwa sio kosa lake,cha muhimu waweke mkazo kwenye kulipa hayo madeni,pesa wanazopokea kutoka FIFA zinawatosha kabisa kulipa,wajipange.
 
Kwenye hili la kujaribu kuuza uwanja wa karume ili kufidia deni la kodi wadau wa michezo hatuta kuelewa Malinzi!!
 
Malinzi TFF amefanya yake tuu hakuna kinachoendelea sema wajumbe wengi sio watu wa mpira ndio maana wanatuchagulia magarasha haya.
 
Back
Top Bottom