Mahakama yapukutisha mali za Bilionea Mrema, yaamuru kupigwa mnada

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Mahakama kuu kanda ya Arusha,masijala ndogo ya kazi imetoa hati ya kukamata kwa jenereta kubwa mbili aina ya Katapila mali ya Hotel ya Ngurdoto ambaye ni mdaiwa kwenye shauri la madai namba 98/2018 ili kufidia deni linalotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.

Akitoa amri hiyo mahakamani hapo msajiri wa mahakama hiyo, John Mkwabi alisema mahakama imepokea maombi ya upande wa mashtaka na kutoa hati ya kukamatwa kwa jenereta hizo ili kufidia malipo ya Tsh. Milioni 231,000,000 yanayotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.

Awali afisa kazi mkoa wa Arusha,Emmanuel Mweta alisema kuwa awali mali zilizokuwa zimeombwa kukamatwa ni magari mawili ambayo yamebainika kutokuwepo kwenye kumbukumbu ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA kama ni Mali za mdaiwa.

"Mheshimiwa msajiri tunaiomba mahakama tubadilisha mali za kukamatwa kwa mdaiwa baada ya magari mawili tuliokuwa tumeomba kutokuwemo kwenye kumbukumbu ya TRA na hivyo tunapendekeza Mali nyingine ambayo ni jenereta mbili aina ya katapila lenye ukubwa wa umeme wa KV 400 ambayo ni mali ya mdaiwa" Alisema Mweta.

Pia Mweta alitoa maombi ya kupata hati ya kuvunja sehemu ya jengo la hotel ya Ngurdoto iliyokuwa imejengewa jenereta hilo ili liweze kutolewa .

Hata hivyo msajili Mkwabi aligoma kutoa hati mara mbili na kutoa Maelezo ya kuendelea na zoezi hilo na kama kutakuwa na tatizo mdaiwa atapaswa kufika Mahakamani .

Shauri hilo limeahirisha hadi litakapo tajwa tena tarehe 27,Oktoba mwaka huu ,hata. Hivyo msajiri aliagiza utekelezaji wa ukamataji wa jenereta hizo uwe umekamilika ifikapo Oktoba 20 mwaka huu.

Wakati huo huo mahakama hiyo imeamuru kuuzwa kwa mali za mdaiwa ambaye ni Hotel ya Naura Spring zinazoshikiliwa na dalali wa mahakama na zoezi hilo liwe limekamilika ifikapo Novemba 17,mwaka huu.

Aidha mahakama hiyo imetoa oda ya kukamatwa kwa jenereta na gari moja aina ya Noar lenye Namba T 991 BWD Mali ya mdaiwa ili kufidia deni la sh,milioni 32,000,000/linalotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.

Maombi ya kukamata Mali hizo yametolewa mahakamani hapo na afisa kazi, Emmanuel Mweta ambaye aliiambia mahakama katika shauri la madai namba 83/2019 kwamba Mali zilizokuwa zimeombwa hapo awali zinathamani kubwa na hivyo kuiomba mahakama hiyo kukamata Mali zingine.

Pia Mweta aliiomba mahakama hiyo kumpangia tarehe ya mnada wa kuuza magari matatu yanayoshikiliwa na dalali wa mahakama .

Wakili anayemwakilisha mdaiwa,Herode Biliamutwa alidai hana pingamizi na maombi hayo,ndipo msajiri wa mahakama hiyo John Mkwabi alipoamuru ifikapo novemba 12,mwaka huu Mali zilizokuwa zimepatikana ziwe zimeuzwa.

Shauri hilo limeahitishwa hadi novemba 3, 2020 mwaka huu litakapotajwa tena.
 
Ombi langu kwa waleta taarifa hapa JF.
Nimeshuhudia hawa wana JF wakikosea kutoa taarifa za kiasi cha hela kinachotajwa katika nyuzi zao mara kwa mara.
Ushauri wangu ni kuwa, usitaje kwa maneno, mfano elfu au milioni, wewe andika tarakimu tu na msomaji ataelewa.
Uzi huu inataja shilingi milioni 231,000,000, huu ni upotoshaji kwa kuwa maana nzima inageuzwa na kuwa ni uongo.
 
Hivi busara zooooooooote zimeshindakana hadi mambo yanafikia huku? Dah!
Busara ilikuwa ngumu, ndugu wanagombania kugawana, wanasahau kuna gharama za uendeshaji ka kulipa mishahara, beberu mara nyingi mwenye mali akifa, board of trustees wanaendelea wakati wana ndugu mnajipanga.

Everyday is Saturday................................ :cool:
 
Hivi busara zooooooooote zimeshindakana hadi mambo yanafikia huku? Dah!
Busara ipi mkuu, hizi hotel Naura na Ngurdoto zimeyumba hakuna wateja.
Naura spring chumba siku hizi hadi 40,0000 unapata je utalipaje wafanyakazi? Hali ni ngumu sana
 
Yani hakuna hata wazee wa ukoo kuweza kuwapatanisha Hawa vijana mrema.Yani wamekuwa na tamaa ya kijinga utafikiri cyo wachagga
 
Ni Mara mwafrika kuzaliwa kwenye Mali akaziendeleza. Na kikwetu muitwe matajiri ni kuwa unaziendeleza pesa alizoacha babu Wa baba yako. Unamuona kama trump ama mo dewj ulizia Huo utajiri umetoka kwa kizazi cha ngapi.
Hapo wanauza magari machakavu namba A na B,hii familia imejaa wapumbavu tupu marehemu pamoja na kusomesha watoto kwa gharama kubwa ila wote viazi tu...wanazo assets ndogondogo nyingi za kuuza moja tu ikalipa madeni yote hayo
 
nilipita juzi nikaona majani yameota nje nikasema corona hii vipi imeadhiri hivi hadi kufunga kumbe wafanyakazi yao...
wakuu kama akaunti inasoma tarakimu 10 kachukue mjengo huo upo location nzuri
naura-spring-hotel.jpg
 
Hapo wanauza magari machakavu namba A na B,hii familia imejaa wapumbavu tupu marehemu pamoja na kusomesha watoto kwa gharama kubwa ila wote viazi tu...wanazo assets ndogondogo nyingi za kuuza moja tu ikalipa madeni yote hayo
Hii familia&watoto wa marehemu wanaweza wakaingia kwenye rekodi ya wap.mbv&wajinga wa kwanza Dunia

Ova
 
Sijui waafrika tunakwama wapi hapa. Naangaliaga makampuni makubwa ya familia kama samsung, yaani ndugu wanagombana ila kampuni inaendelea kupiga kazi bila kwikwi.
 
Jamaa lazima kaacha watoto wengi....mali za matajiri wengine zinapukutikaga sababu ya kuzaa zaa ovyo + malezi / maandalizi mabovu.....ku maintain mali even after ur deceased ni muhimu kwa kuweka strict family codes (hata ukizaa nnje, msort mtoto na mama yake nnje mapema...na iwe wazi hawahusiki kwenye main family bread)

Sijui mtazamo wangu tu.
Kitu kingine si wachagga sijui tuna nn....mtu unakuta kasomesha watoto hadi ulaya for thousands of pounds ila mtoto akirudi bongo anakua mgumu kumshirikisha kwenye biz zake game linavyochezwa (YES, WAPO VIJANA WENGI TU WANAJIELEWA) ila unakuta mzee anawakazia wengine hawataki kabisa watoto wawe involved kwenye biz zao. Mzee aki dunk ndio inakua mambo ya hivi.

Nitashangaa na kuhuzunika sana empire ya hawa jamaa ikianguka. Washasogea sanaa it will be awkward kuanza moja kila mtu kivyake. Nawaombea vijana wajielewe tu na waangalie kazi / stability kabla ya chochote. Wapo pazuri sana watulie tu.

N!gg*s ought to change big time.
 
Wengine wanakuwa na magendo mengi, nyuma unakuta ni jambazi, jangili, dhulumati mpaka anaua, hawawezi kushirikisha watoto, especially kama front, wanajidai ni innocent business personnel.

Mafanikio ya baadhi wengi yana siri kubwa nyuma ya pazia.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Wengine wanakuwa na magendo mengi, nyuma unakuta ni jambazi, jangili, dhulumati mpaka anaua, hawawezi kushirikisha watoto, especially kama front, wanajidai ni innocent business personnel.

Mafanikio ya baadhi wengi yana siri kubwa nyuma ya pazia.

Everyday is Saturday...............................

Huenda wengine walianzia huko (Hilo Hatuna Uhakika) Sasa hizi establishments kwann hamna vijana waku run prior ?? Hujui vijana watakomaa hata kifikra mapema ukiwashirikisha wakati mwenye mali akiwepo ??

Pia as a parent utajua majembe na bonkers on the process. Kuna vijana wamekosa channel tu ila ni mamba kinoma noma hata we mzazi unasubiri (nawajua madogo kibao wametoboa zaidi ya wazazi wao baada ya mzazi kukunjua channel)
 
Back
Top Bottom