Malinzi acha kutudanganya , tena acha.

Jamal malinzi rais wa tff mwenye mageuzi kama david moyes wa man utd tunahitaji majibu ya maswali yenye ukakasi ukianza kuweka taasis kubwa kama TFF kwenye mfuko wako na wadau wako napata kuumwa kichwa kidogo.

Inanifanya niamini kuwa hata kukiwa na ubadilifu wa hela hapo kwenye taasis yako na wadau wako usiulizwe hii n zaidi ya tanzania tuijuavyo.

Najiuliza ivi taasis yako hii na wadau wako mkifikisha mwaka itakuwaje kama hii miezi minne mmeanza kuiweka mfukoni mwenu jaman mbona huruma hakuna.

Sitaki kuamini kuwa na huku kwenye taasis ya malinzi na wadau wako kuna watu wamekuja kuchuma ili wakamalizie nyumba zao,haya malizeni hata icho mlichoachiwa na wenzenu alafu tuone itakuwaje.

Haya maswali kila mpenda michezo hasa soka anatakiwa kujiuliza maana tunarudi kwenye mabasi ya railways enzi zileeee badala ya kuelekea mbele.

Ivi kweli ata Sepp Blattler na yy huwa anaotoa hela mfukoni kwake na wadau wake daah kichwa kinauma kwelii
 
Kiuhalisia kabisa kulikuwa hakuna haja ya kuvunja mkataba na Kim kama TFF walikuwa hawajiandaa kulipa gharama za kuvunja mkataba. Mkataba wa Kim ulikuwa umebaki mwaka mmoja tu uishe, kulikuwa na haja gani ya kuvunja mkataba sasa?
Tatizo la Soka la Tanzania haliko moja kwa moja kwa makocha bali lipo kwenye mfumo, kama Malinzi ndiye Rais wa TFF na hajui namna ya kutatua changamoto ya Soka letu basi tumekwisha!
Hii ya kumlipa kocha kutoka mfukoni kwake nikuwafanya wajumbe wamwogobe na kukabaliana na chochote atakachosema. Huyu jamaa anaweza hata akaitisha mkutano wa wajumbe na kuwalipia wote gharama za usafiri na Malazi kwa madai kuwa TFF haina hela au anaweza hata akagharamia kambi ya Timu ya Taifa kwa madai hayo TFF haina hela.
Kama kweli TFF haina hela alitakiwa aanze kubuni miradi na kutafuta wadhamini ambao watasaidia na kama yeye alikuwa anatamani kuwa mfadhili wa TFF alikuwa na haja gani ya kugombea urais?
Kiongozi wa TFF anatakiwa awe na vision na mission na kuinua mpira wetu na kuliimarisha shirikisho kiuchumi kwa vyanzo endelevu ambayo vitadumu hata baada yaye kumaliza uongozi wake na si kuchangia kutoka mfukoni mwake.
 

Uko sawa kabisa
 

mzee unalipwa kiasi gani kumtetea Jamal Malinzi?
 
Wewe ndio uende tena shule kusudi uwache wivu wa kike.amesema ata cover hizo gharamma na washikadau wa soka wewe unakuja na mapovu kibao.

Mpira ni wa Watanzania wote na kila kitu kinapaswa kuwa transparent.
Hebu tuambie basi wewe ni kiasi gani cha pesd Malinzi ametoa ili kuvunja mkataba na Kim?
Halafu kwa nini mkataba uvunjwe kwa siri na sio kwa uwazi wakatueleza pros and cons of the matter?
Hebu tuambie basi na wewe!
 
mzee unalipwa kiasi gani kumtetea Jamal Malinzi?

Mimi silipwa chochote kile ujue hapa ni GT, siyo lazima kila unapoleta uzi wako hapa upate suport 100%, lazima kutokee watu wa kuchallenge na wengine wata suport.mimi binafsi sikubaliani na lawama kwa Malinzi kwani wazo lake naliona liko sahii.
 
Malinzi yuko sahihi kabisa! duh kweli ili suala zito hadi 'nyama.. laini' namuon anachangia!
 
Nionavyo:
1. Hakuna kipya ambacho kocha aliyesitishwa mkataba wake angeweza kutuletea. Kama alishindwa WC 2014, CONCAF, CECAFA CHALLENGE na CHAN tena kwa masafa marefu, nini kinatushawishi kwamba angeweza ndani ya mwaka mmoja ushei uliosalia?
2. Inawezekana wazo la kusitisha mkataba wake lilikuwa sahihi.
3. Kulihitajika mashauriano angalau ndani ya TFF kuona kama kocha asitishwe mkataba.
4. Umma ulipaswa angalau kujulishwa kuwepo kwa mashauriano hayo na hatma ya maamuzi kabla ya utekelezaji. Vinginevyo ni dharau kwa umma wenyewe. Inazidi kuwa hivyo pale wachache kama ShafiiDauda wanapokuwa na habari hizo mapema, japo waliziita fununu.
5. Kama ni swala la kuvunja mkataba kwa maridhiano, angalau wanahabari wangejua japo dondoo za makubaliano hayo.
6. Hata kwa wasiomuunga mkono Tenga, aliwacha akaunti nono TFF. Sio ya fedha, bali ya kuwa mwazi na mshirikishi kwa wadau. Utaratibu wa taarifa kutoka TFF za kila wiki umeanzia naye. Ulipaswa kutumika muda wote wa mchakato wa swala hili.
7. Taratibu za utawala wa kifedha hazikubaliani na kiongozi kutoa fedha zake mfukoni kwa shughuli za taasisi. Ilifanyika hivyo zama za kudai Uhuru kwa mazingira maalum ya harakati zenyewe.
8. Kwa hivyo kusitisha mkataba wa kocha kwa utaratibu huu hakukuwa sahihi, ingawa inaweza kuwa ni kwa nia nzuri. Njia ya jehanamu imejaa tele nia njema.
 
Mimi silipwa chochote kile ujue hapa ni GT, siyo lazima kila unapoleta uzi wako hapa upate suport 100%, lazima kutokee watu wa kuchallenge na wengine wata suport.mimi binafsi sikubaliani na lawama kwa Malinzi kwani wazo lake naliona liko sahii.
Mmawia samahani mkuu je kilicho sahihi ni nini kati ya haya
  1. kutoa pesayake mfukoni kwa ajili ya taasisi ya uma au
  2. kuvunja mkataba wa kocha bila kutoa maelezo ya kwa nini kafanya uamuzi huo
  3. kushirikisha rafiki zake a.k.a wadau katika mambo ya kifedha ya taasisi
 
Last edited by a moderator:

Kwa mtazamo wangu nikuwa Malinzi kama yeye anavyosema wadau, inamaana ndefu.Inawezekana hata tbl, sbl na makampuni ya simu ambao ni wafadhili wa taifa stars.Inawezekana hawakutaka kutajwa hadharani, pili kuvunja mkataba mie naona ni sawa kwani huyo kocha kashindwa angalau kutufikisha tulipo achwa na Maximo.Hivyo mie nampa 5 Malinzi 100%.
 
Last edited by a moderator:

Lazima kichwa kikuume mkuu, eti malinzi ni good samaritan kumbe kimeo
 
Wapi TAKUKURU?
Mshughulikieni huyu , kuzuia ni bora kuliko kuponya... au mnataka mpaka apige hizo hela kabisa?
 

Tatizo kubwa la Malinzi ni kulipa kisasi kwa uongozi wa kina Tenga,kila waliloanzisha wenzake anataka kuliondoa,ameteua kamati nyingi lakini sidhani kama anazipa nafasi na uhuru hizo kamati kufanya kazi zao.
Kama mkataba wa kocha umebakiza mwaka mmoja kulikuwa hamna haja kuuvunja wangesubiri uishe,sidhani kwa mwaka mmoja hata ukimleta Guardiola atabadilisha soka la Tanzania.TFF ni taasisi sio mahali pa kufanya maamuzi binafsi.Tangu ameingia TFF kuna mambo ameyafanya kwa kukurupuka

1.Kuvunja mikataba ya waajiriwa wa TFF ambayo ilikuwa inakaribia kwisha(Osiah,Polsen,Marsh)

2.Ameteua kamati nyingi ambazo nyingi hakuna kazi wanayofanya

3.Electronics tickets ambazo tayari zilifeli vibaya

3.Kuajiri mtu ambae hana vigezo kutokana na job description waliotangaza mwenyewe(Mwesigwa)

4.Kuteua timu ya Taifa wakati yeye sio kocha
 

Mkuu Mmawiasorry lakini ndo maana nilikwambia RUDI SHULE, msingi wa makampuni makubwa kama TBL, SBL au makampuni ya simu kudhamini au hata kutoa pesa katika taasisi ni MARKETING STRATEGY, na hii ni makusudi ili wapate publicity as well to strengthen public relation, appriciation, and touch. Sasa usitegemee hata siku moja eti MAKAMPUNI hayo yatatoa msaada kimya kimya, bila kuita vyombo vya habari na kuhakikisha wananchi wanajua hilo.

Hao WADAU wake ni watu BINAFSI tena wenye malengo ovu, ndo maana hawataki kutajwa wala kutaja kiwango walichotoa.

sorry kama imekuumiza but ndo ukweli
 
Last edited by a moderator:
mi sioni shida kwa Malinzi kuipa pesa TFF. Hata mwingine yeyote akitaka akatoe. Ninachotaka ni kwa Malinzi na wengieo wasije hata siku moja kudai pesa hizo na TUNATAKA KUONA SOKA LA TANZANIA LINAKUA PHYSICALY na si kwa uongo uongo. Tff si taasisi ya biashara.
 

Mimi siwezi kuumia kwa sababu ya mchango wako hata dkd 1, la msingi ni jee hizo lawama na shutuma unazo mtupia Malinzi zinajenga au zinadidimiza? Unataka kusema alivyotoa wazo hilo uongozi husika (wizara) hawajui? Mbona hatujasikia wao wanalikemea hilo? Au unataka kusema wizarani watu hawajui wajibu wao?Kukaa kwa wizara kimya ina maana imebariki hayo mambo yaendelee kwa kuwa yana maslahi kwa taifa.Utapiga sana kelele lakini kama wizara imebariki hakuna postive changes utaiona ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:
Nitoe hoja gani tena mleta Uzi kamaliza kila kitu? Mi nilichofanya hapo ni kuchangia hoja kwa kuiunga mkono,vp mkuu machoko mchuzi nn?

Nimekwambia usitoe derogatory language sasa unanitukana kwa nini. mimi sijakutukana. Nimesema usitumie derogatory language. Mimi ni Mfuasi wa Yesu, nakugeuzia na shavu la pili utukane!
 

Uongozi kweli unahitaji moyo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…