grndossy
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 311
- 80
Mzizi Mkavu, picha hii inaweza kuleta taswira nyingi isivyokusudiwa na mleta mada.
Hivi Kikwete huwa ana muda wa kutulia ofisini pale magogoni kama huyu Obama anavyofanya? Kiwete ofisi imehamia angani sijui anapohitaji kuchomoa faili kutoka sehemu ofisini huwa anampigia simu ps wake!
Hivi ni kweli kabisa kwamba hakuna jema lolote ambalo JK ameitendea nchi hii? Siku moja tuseme basi na mazuri yake? Kwa wale wanaosoma Neno la Mungu mtagundua kila neno tunaloongea au kumsemea mtu au nchi yetu linaumbika na kuwa roho inayotenda kazi. Ndio maana tulipoiita hii nchi nchi ya bongo, imekuwa nchi ya bongo kweli!! Mwenye nafasi ya kusoma biblia soma Mithali 23:7(a) na Mithali 18:21. Tuinenee nchi yetu maneno mema tusiifunge nchi yetu kwa kuinenea maneno mabaya kila wakati.