Mali za aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Mfanyabiashara Mkoa wa Mara zapigwa mnada

Roho Mbaya

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
777
670
Katika pita pita zangu kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na Tangazo la mnada kwa mali zilizokuwa za Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa zamani wa Zamani wa CCM (Zembwela).

Mali zinazopigwa mnada ni pamoja na hotel yake ndani ya mji wa Musoma (Afrilux Hotel) pamoja na vituo vya mafuta vilivyokuwa vikimilikiwa na tajiri huyo.

Nimeamini kweli pesa ni maua tu.

Screenshot_20220223-091913_Instagram.jpg
Screenshot_20220223-091846_Instagram.jpg
 
Usishangae kusikia sehemu kubwa ya mapato alipeleka kuimarisha chama akidhani watamsaidia asilipe deni, mwisho wa siku wamekamua kila kitu wamemtelekeza
 
Ooh! Mbwa kala mbwa, hakika hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata Mathayo (mbunge wa musoma mjini) hotel yake ya Matvilla anauza sasa najiuliza mji huu matajiri wake wamekosea wapi?
 
Ooh! Mbwa kala mbwa, hakika hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata Mathayo (mbunge wa musoma mjini) hotel yake ya Matvilla anauza sasa najiuliza mji huu matajiri wake wamekosea wapi?
Na wewe tajiri uchwara umepatia wapi?
 
Hizo sheli zinazouzwa zitakuwa za mbunge wa sasa wa Musoma Mjini (Vedastus Mathayo)

Zembwela shell zake zilishapigwa mnada muda mrefu kwa sasa zinamilikiwa na GBP
Screenshot_20220223-162002_Instagram.jpg
 
Ooh! Mbwa kala mbwa, hakika hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata Mathayo (mbunge wa musoma mjini) hotel yake ya Matvilla anauza sasa najiuliza mji huu matajiri wake wamekosea wapi?
anauza Tsh ngapi nijipige pige hapa😅 ila huyo jamaa alikuwa na pesa sana
 
anauza Tsh ngapi nijipige pige hapa😅 ila huyo jamaa alikuwa na pesa sana
Anaiuza Matvilla kwa milioni 700 tu najiuliza ni kipi hasa kilichomkuta huyu Tajiri Vedastus Mathayo Mbunge wa Musoma mjini..

4B3D4DBE-C83E-4777-8218-509E27296B46.jpeg
 
Hapo inategemea hela zake alizipataje?

Ova
Alikuwa na vituo vya mafuta pia vya HASS na kiwanda cha maziwa mara milk bado najiuliza imekuaje ukwasi umeyeyuka fasta ama mikopo ya benki imemlaza na viatu
 
Back
Top Bottom