Mali kale ( Tunnu za Kale ) na Umaskini wetu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mali kale ( Tunnu za Kale ) na Umaskini wetu !

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by The Fixer, Apr 16, 2012.

 1. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wadau;
  Mimi ni mmoja kati ya Watanzania wenye hamu kubwa ya maendeleo kiuchumi katika Taifa letu, Nimeskia kuwa Wakoloni wa Kijerumani wakati wanaondoka nchini baada ya kushindwa vita na Waingereza walifukia kwenye mahandaki & kanisani na mahala pengi tu tofauti tofauti na kuficha mali nyingi sana zikiwemo Vinoo vya Dhahabu, Mabonge ya Almasi, Mapande makubwa ya Lulu, Madumu ya Mercury, Viroba vya Uranium,Makasha ya Sarafu na Noti za Rupia na madini mengi sana mbali mbali !
  Kwanini Serikali ya Tanzania wasiingie ubia na Wajerumani na kuvuna hizi Mali kale zoote na kunufaisha nchi hizi mbili na yale maisha bora yaonekane ! Huu Umaskini wa Watanzania kwani hauwakeri watu wa Magogoni ? Zipo site zaidi ya 5,320 kwa kumbukumbu za Wizara ya mali asili na Utalii ! Kinachotokea sasa hivi ni hawa Wajerumani mmoja mmoja kuja na kuwalaghai Viongozi wetu na Familia zao na hatimaye kunufaika wao wenyewee tena wanakuwa Mabilionea wa kutishaa sana ! Watanzania wengi
   
 2. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa nakumbuka niliwai kutembelea mbuga ya Serengeti eneo moja linaitwa Fort Ikoma watu wa huko wanadai Mjerumani alificha mali nyingi sana.Lakini wanachodai ni kwamba mali hizo zinaambatana na imani za kishirikina so ni ngumu sana kuzipata
   
 3. kiagata

  kiagata Senior Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  \

  Wazo lako ni zuri kwa haraka haraka,la serikali kuchukua au kufichua hazina ambazo zimefichwa kwa maslahiya watanzania. Ila tatizo mambo mengine ya rupia yanahusishwa sana na ushirikina. mfano,utapata taarifa kuwa lazima mtu anayeenda kuchukua mali akae kwa mganga muda fulani na mali itakayopatikana lazima igawanwe sawa bila dhuruma.
  Halafu toka wajerumani waondoke mwaka 1919 na kumwacha mwingereza ni muda mrefu sana hata hayo madumu yaliyofukiwa ardhini lazima yatakuwa yameharibika na sarafu itakuwa imeshapata kutu.Ukizingatia teknolojia ya utunzaji vitu ilikuwa ipo chini.
  Kwa kweli kama mali ipo eneo fulani,mimi naadhani watu wangeelewa wasingeacha tu,lazima wangechimba.Wasingeshindwa kuchimba wakati Geita watu wanachimba mashimo ya karibu mita 300 chini ya ardhi sembuse kanisani ambapo hata ulinzi hakuna?. Chamsingi taarifa hizi huenda zinasambazwa na hao hao wakoloni ili kuleta mitafaruku,maana nchi hii waliondoka wanaipenda.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hivi vitu vipo sana, Ila hukohuko Serengeti kuna mahali walifukia hadi magari yao na yakaja kupatikana yakiwa yameoza kwa kutu, Ila hao hao wajerumani nilisikia mahali fulani sitaki kupataja jina walukija kwa gia ya kuwasaidia wananchi wa hapo kujenga barabara, kumbe wale wajerumani walikuwa na ramani ya mahali babu zao walifukia mali, walicho fanya walichora mchoro wa barabara na cha kushangaza waliforce barabara ipite katikati ya mlima, kumbe kwenye ule mlima ndo ilikuwa tageti yao na baada ya kulima barabara hadi kwenye huo mlima walichimbua mali zao wakaondoka na kuacha magreda pale pale na hawakurudi tena
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuiondowa CCM madarakani ni lazima kwanza tupambane na watu wajinga kama huyu mleta hii thread, hawa ndio maadui wa nchi yetu kuliko umaskini tulionao, ni mppuuzi na mpumbavu pekee ndiye anayeweza kusadiki kwamba kuna binadamu anaweza akazifukia mali chini wakati ana uwezo wa kuzipeleka anakotaka.
  Ningekuwa mimi ni Rais ningeamuru watu wote wenye mawazo mgando kama haya wakamatwe na wanyongwe hadi kifo, maana ni hasara kwa Taifa.
   
 6. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Viongozi ambao wamenufaika na Mali kale hizi ni pamoja na Mzee Mkapa maana hata ile Nyumba yake ya Lushoto pia kuna site kubwa sana amejimilikisha pale,Mboma naye amenufaika, Komandoo wa Zanzibar naye alinufaika, JK na familia yake maana msione tu ni Billionea mkadhani ni FISADI watu wamepiga mali kale hizo.Shida yenu ninyi mnataka mpaka mtu ajitokeze mbele yenu na kusema kuwa mimi nimenufaika na mali kale. Ingekuwa ni uzushi na ujinga hata pale Wizarani ya Mali asili na Utalii wasingesumbuka kuweka Idara kusimamia ujinga huu. Matola don't under estimate kila kitu ! Matengenezo ya Ocean Road mwaka 1995 yalitoka makontena zaidi ya 20 ya Dhahabu na madini mbalimbali na wakubwa walinufaika na mchakato huo ! QUOTE=Matola;3704375]Kabla ya kuiondowa CCM madarakani ni lazima kwanza tupambane na watu wajinga kama huyu mleta hii thread, hawa ndio maadui wa nchi yetu kuliko umaskini tulionao, ni mppuuzi na mpumbavu pekee ndiye anayeweza kusadiki kwamba kuna binadamu anaweza akazifukia mali chini wakati ana uwezo wa kuzipeleka anakotaka.
  Ningekuwa mimi ni Rais ningeamuru watu wote wenye mawazo mgando kama haya wakamatwe na wanyongwe hadi kifo, maana ni hasara kwa Taifa.[/QUOTE]
   
 7. F

  FemaraFe Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I am very appreciated
   
 8. majay86

  majay86 Member

  #8
  Dec 27, 2013
  Joined: Aug 30, 2013
  Messages: 83
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  uwepo wa mali kale katka taifa letu c wa kubuni ni kweli na hakika 100% na c taifa letu tu ni mataifa mengi yana hazina za kale, tatizo moja kubwa na ni janga la kitaifa katika nchi yetu watu hawana elimu ya kuvumbua mali hizi,kwanza kabisa kuna alama za siri ambazo zilibuniwa na secret societe ambao kwa jina lingine tunawaita free masons na hao masons waliobuni alama hizo wanaitwa the masonic church of 33 degrees ambao ni totaly evils, kabla hujafikiria kutafuta hazina za kale lazima ujifunze kutafsiri alama nembo na vipimo ili uweze kufanya kazi zenye mafanikio.
   
 9. a

  antimatter JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2017
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 444
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Author wa post #5 ni jipu lililoiva !
   
Loading...